CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
Bwana Yesu asifiwe....
Asalaam Aleikum....
Tumsifu Yesu Kristu...
Story ya kweli kabisaaaa.....
Iko hivi, kuna mdada mmoja alitoka katika familia ya kifukara sana Usukumani (Bariadi) tumuite "Kija" Kija alikuwa msichana mrembo tu ila hali ya kiuchumi ya nyumbani kwao ilimsababisha aonekana kutokuwa na mvuto... Basi mama mmoja ambaye anatokea Bariadi lakini anaishi Jijini Mwanza tumuite "Mrs. Kombe" alikwenda Bariadi kutafuta msichana wa kazi. Kwa bahati nzuri.akampata Kija...Huyu mama hakuwahi kujaaliwa kupata mtoto hata wa dawa ingawa mumewe alikuwa na mali nyingi....
Wakaja mpaka Jijini Kija akaanza kazi, alifanya kazi kwa bidii sana mpaka Mrs. Kombe akafurahi na kumpenda sana Kija, kwa vile Kija alikuwa ameishia darasa la saba basi Mrs. Kombe akaamua kumsomesha Kija elimu ya Sekondari, alianza kidato cha kwanza mpaka cha nne akiwa "day scholar" anafanya kazi zote za nyumbani kisha anakwenda shule. Yule mama akawa anamuongezea pesa katika mshahara wake ili kulipia ada ya shule mpaka alipomaliza kidato cha nne....
Baada ya kumaliza alifaulu kwa kiwango cha kati na akapangiwa kwenda chuo cha Ualimu. Baada ya kumaliza chuo akapangiwa kufundisha shule fulani ya msingi jijini Mwanza.
Yule mama alimlea Kija kama mwanae wa kuzaa na baada ya muda ile hali ya "U-house girl" ilififia akaonekana kama mwanafamilia ya yule mama. Baada ya kupata elimu hiyo Kija alianza kuichukia familia yake ya kuleee Bariadi na kujiona kama alikosea kuzaliwa katila familia hiyo. Mawasiliano yakawa mabaya baina yake na familia yake ya Bariadi.
Basi baada ya kuanza kazi ya ualimu aliamua kuanza kujitegemea, ndipo akakutana na mkaka flan tumuite "Mabula". Walianza mahusiano hatimaye Mabula akamchumbia Kija....Wakapanga siku ya kwenda kwao Kija...Lahaula lakwata!!!!!! Badala ya Kija kumpeleka kwa mama yake (baba yake alikuwa keshafariki) alimpeleka kwa Mrs. Kombe. Basi siku ya siku Mabula akaieleza familia yake kuwa amepata mchumba na taratibu zote zikafuatia, Wazazi wa Mabula walikwenda kwa Mrs. Kombe kama walivyotambulishwa na Kija kuwa pale ndio kwao taratibu zote za kimila zilifanyika ila mama mzazi wa Kija alipewa taarifa na kuhudhuria kama ndugu tu kutoka kijijini na akawa "treated" kama mgeni.
Mahari ilitolewa na aliyeipokea ni Mrs. Kombe (kama mjuavyoa masikini hana haki) yule mama bila aibu alipokea mali na kumgawia mama mzazi wa Kija kwa kisingizio kuwa yeye ndiye amehusika sana na malezi ya Kija mpaka hapo alipofika. Basi send off iliandaliwa na Mrs. Kombe na aliplay party kama vile mama mzazi (Hapa sisemi kama alikosea, ila kumbuka mama mzazi hakushirikishwa hata kwa mawazo) mwisho akafanyiwa bonge la send off "as usual mama mzazi alikuja kama ndugu tu aliyealikwa"....
Wakati wa utambulisho mama mzazi alitambulishwa kama "mama yangu mwingine" Ilikuwa hivi " Kwanza Napenda kumtambulisha mama yangu (akamsimamisha Mrs. Kombe)" Pili.napenda kumtambulisha mama yangu mwingine (akasimamishwa mama mzazi) u can't believe".......... No way ndo ishakuwa hivyo, maisha yakasonga.
Basi sasa baada ya Ndoa Kija akahamia Shinyanga alipokuwa anaishi Mabula, baada ya muda Kija akapata ujauzito akajifungua watoto mapacha, wale watoto walipokuwa Kija alifunga safari moja kwa moja mpaka kwa Mrs. Kombe kuwapeleka watoto waonwe na bibi yao. "Kimila zaidi" Ingawa ilipaswa wale watoto waonwe na mama mzazi wa Kija. Kisha akarudi zake Shy maisha yakasonga.
Mpaka dakika hii Mabula anafahamu ya kwamba Mrs. Kombe na Mzee. Kombe ndio wazazi wa Kija. Ni miaka miwili na miezi kadhaa imepita...
Najiuliza ilitokea mama mzazi wa Kija afariki dunia Kija ataliaje?
Hivi kuna wanawake wapo duniani wana tabia kama hii?????
NOTE: Majina na mahali sio halisi.....
SAMAHANI KWA STORY NDEFU ILA.UNAWEZA UKAPATA KITU.......
Wasalaam
CL