Soma: Nguvu ya mmea wa "Isale" katika kusuluhisha jamii

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,597
1,071
Tangu enzi za Mababu inasemekana Wachagga wametumia "Isale" au (Dracaena afromontana) katika kuleta suluhu na kusameheana (forgiveness) katika jamii yao.

Mmea huu unatumiwa sana katika maofisi duniani kama mapambo (ornamental).

Mmea huu una nguvu za Kimungu (Goddess/ritual powers) kwani anayekataa suluhu hufikwa na mabalaa/ mikosi.

Je, jamii nyingine tunatumia njia gani za kimila kusuluhishana?.

Kwanini mbinu hizi zisitumike kuleta muafaka (reconciliation) na mapenzi mema katika Taifa letu linalofarakana?.
 
....

Adansonia digitata ....hapa hukatizi kama ukisema uwongo
Sensiveria robusta (Wasukuma wanajuwa hii kitu ...misambwa)
Bolongoja ukengeniensis ....huu unatumika kutega majangili ...jangili hupata mikosi kila kukicha

..niendelee?
 
mimi nakubaliana nawe mkuu!pia hutumika kugundua mahala bora kwa makazi.kwa mfano ukitaka kujenga nyumba yako mahala fulani halafu ukawa na wasiwasi napo,basi tangulia kupanda huo mmea wa ISALE kisha utapata majibu.kama kweli hapafai huo mmea utakauka,kama sio utachanua.nimeshuhudia mwenyewe wakuu!
 
kuonyesha ishara ya amani na upendo masale hupeperushwa juu kuwapokea viongozi wa kisiasa na kutumika kupamba mikutano ya kisiasa na nyumba za ibada!
 
Tangu enzi za Mababu inasemekana Wachagga wametumia "Isale" au (Dracaena afromontana) katika kuleta suluhu (forgiveness) katika jamii.

Leo mmea huu unatumiwa sana katika maofisi duniani kama mapambo.

Amini, mmea huu una nguvu za Kimungu (Goddess/ritual powers) kwani anayekataa suluhi hufukwa na mabalaa/ mikosi.

Je, jamii nyingine tunatumia njia gani za kimila kusuluhishana?.

Kwanini mbinu hizi zisitumike kuleta muafaka na mapenzi mema katika Taifa letu linalofarakana?.

Weka na picha ya huo mmea wa Kale! wenye Nguvu za Mungu wa Wachanagaa
 
......

........hapa ndo magamba walivyolaaniwa na kubakiza majengo. tupu bila wanachama.. Laana hii iliweza kusambaa Tanzania nzima!!!!

.....chezea isale wewe.....

.....Haya....mulamula or mutendere
.....Iraqw(Mbulu)......sansuli
......Pare,meru,chaga.....isale
 

Attachments

  • ACHADEMA 007.jpg
    ACHADEMA 007.jpg
    326.9 KB · Views: 731
Chini ya mlima meru linatumika kama kitenga mpaka kati ya shamba moja na lingine; na iliaminika kwa yeyote aliyejaribu kusogeza mpaka kwa kulirudisha isaale ndani alipata laana. Kuna ibada pia hufanywa na washili wakati wa kulipanda mpakani
 
Hili isathe huwa tunalipanda kwenye (Mbuho) sehemu inayotumika kuchinjia na kuzunguka mpakani na huwa ni mwiko kuyakata hovyo
 
Kitu msonge wa ukweli nimeshtuka nikadhani babu zake na babu yangu wamefufuka.Nani mtaalamu wa mila aniambie hayo mawe mawili mlangoni yanamaana gani?
Umenikumbusha wakati wa utafiti (research) wangu Mkuu.
Maandiko (literature) zinataja sehemu muhimu za nyumba (msonge);

1, Ukooyo= top apex
2. Kiwangowango= nafasi /kabati (vault) juu ya mlango
2. Ulii = sehemu ya kitanda cha mama
4. Kichi = Kitanda cha watoto
5. Kimolya = kistoo cha maziwa na chakuka.
6. Kayi = dari
7 Moondi = hori la ng'ombe
8. Koombe = eneo la ngome
9. ? = Sehemu ya mbuzi
10. Upuruni - matoleo ya mikojo ya wanyama (Matundilo kwa Kisukuma)
11. Mashigha/ rikonyi = jiko

Endeleeni

12.
13.
14.
15.
 
Back
Top Bottom