huyu mama alimzaaje mwanae?
Hivi hakusikia uchungu? Au aliutuma kwa bluetooth kwa mama mwingine?
Mi kuna baba mmoja hivi nilishuhudia kwa macho yangu, amehangaika na mwanae tena kwa kufanya kazi za ulinzi, kuanzia mwanae anasoma shule ya msingi, mpaka anafaulu kwenda kidato cha kwanza, baba akahama na mwane,
baba hakukata tamaa, akawa tu analala nje kwa muda miaka minne ili tu amsomeshe mwanae huyu mmoja wa kiume kwa miaka hiyo minne, mwanae nae akaonesha bidii, akafaulu mtihani wake wa kidato cha nne, akachaguliwa kwenda kidato cha tano kwenda ihungo bukoba. Bado baba akasafiri na mwanae, anamsomesha tu hivyo hivyo kwa shida na raha.
Mwanae kaja kumaliza shule, kidato cha sita mwaka 2012 na akapata division 1 ya point saba! Furaha iliyoje kwa baba! Matatizo yakawa yamepungukia hapo! Sasa mwanae yuko mzumbe university, anasoma baf!
Sasa huyu mama imekuwaje mpaka anamtelekeza mwanae namna hii?
Je, siku akipata, ataunyoosha mkono wake na kusema njoo mwanangu?