Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
Habari wana JF. Juzi nilikuja na uzi nikimshambulia Flora Mbasha kwamba hana Mungu ndani yake maana anavunja ndoa yake mwenyewe misili ya mtu ambaye hajawahi kusoma hata fungu moja la Biblia, watu walinishambilia sana. Leo nimeona hii video ya Baba yake mbasha akisema Flora alimchoka mwanangu, inasikitisha sana nasikia kulia nikitafakari mke wako mwenyewe tena wa ndoa akikumaliza huku ukiona.
HITIMISHO
Mungu haabudiwi kwa style ya kuimba kwa kupiga makelele na kukata viuno bali tunamuita Mungu awe ndani yetu kwa kuimba nyimbo za kuabudu, ndio maana katika maisha yangu sijawahi kupenda nyimbo za huyu dada pamoja na Rose Mhando sidhani kama mungu atakua ndani kwa ujinga kama ule wa kupiga kelele na kukata viuno.
Inawezekana kweli Flora ana makosa kwa kuvunja ndoa yake.lakini hiyo haihalalalishi makosa ya Mbasha ikiwa kweli alibaka. Kwa kuwa suala liko mahakamani hebu acheni mahakama itende haki. baada ya hapo manaweza kutoa hayo majumuisho yenu.