Solved: App ya JamiiForums imeboreshwa (Android & iOS)..

Moderator

Supervisor
Nov 29, 2006
698
1,131
Salaam,

Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kwamba hatimaye tumekamilisha maboresho tuliyokuwa tukiyafanya kwenye APP ya JamiiForums na sasa inapatikana ikiwa na muonekano mzuri zaidi pamoja na urahisi wa kutumia. Unaweza kuipakua sasa au kama tayari unayo tafadhali fanya Update ili kupokea maboresho hayo.

Kwa takribani siku 10, baadhi ya watumiaji hususan wa device za mfumo wa Android mlikutana na changamoto ya kutoweza kuipata App ya JamiiForums kupitia Playstore; JamiiForums haipatikani Playstore. Nini tatizo?

Tunashukuru kwa uvumilivu wenu katika kipindi chote tulichokuwa tukiifanyia kazi.

Kuna swali lolote?

Karibu.. Bonyeza HAPA kuupdate
=====================

UPDATES (March, 2018):

Ndugu WanaJF,

Tumepokea malalamiko kuhusu changamoto kadhaa ikiwemo kuchelewa au kutopokea kabisa notifications kwa watumiaji wa Android.

Wataalamu wetu wanazifanyia kazi changamoto hizo hivyo tunaomba uvumilivu wenu kidogo.

Asante.
 
Screenshot_2018-02-14-16-31-03-1.png
Salaam,

Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kwamba hatimaye tumekamilisha maboresho tuliyokuwa tukiyafanya kwenye APP ya JamiiForums na sasa inapatikana ikiwa na muonekano mzuri zaidi pamoja na urahisi wa kutumia. Unaweza kuipakua sasa au kama tayari unayo tafadhali fanya Update ili kupokea maboresho hayo.

Kwa takribani siku 10, baadhi ya watumiaji wa device za mfumo wa Android mlikutana na changamoto ya kutoweza kuipata App ya JamiiForums kupitia Playstore; JamiiForums haipatikani Playstore. Nini tatizo?

Tunashukuru kwa uvumilivu wenu katika kipindi chote tulichokuwa tukiifanyia kazi.

Kuna swali lolote?

Karibu..

Mkuu bado kuna issues..
Nimelog out... kuja kusign in kuna option ya kuweka user name na password ila option ya kuruhusu kuingia haipo.
 
Kitu kimoja.

Hii app iwekewe uwezo wa mtu kuupload chochote, sasa hivi unaweza kuupload picha na video audio haiwezekani.

Na kuweza kuedit profile info kutokea kwenye app kuongezwe.

Pia ile traditional color ya dark blue ni bomba sana
Asante mkuu kwa maoni.

Ni kweli kuna baadhi ya features bado tunaendelea kuzifanyia kazi ikiwemo hiyo inayohusisha MP3 files. Kwa sasa unaweza kupakia kwa kutumia browser (as an attachment).

Tutajitahidi kulifanikisha hilo ndani ya muda mchache kutoka sasa.
 
Kwanza pongezi kwenu mods kwa maboresho, tumeyaona japo inaweza kutuchukua muda kidogo kuyazoea.

Halafu cha pili muwe mnasikiliza na kero nyingine za members, mfano mimi ni siku nyingine nimelalamika kufuhu notifications kwa email sizitaki, nimejaribu ku-unsubscribe lakini bado e mail zinaingia, hebu mnisaidie na hilo kwangu ni kero
 
Asante kwa pongezi mkuu. Pole kwa changamoto hiyo.

Jaribu kujiondoa tena leo kisha utupatie mrejesho kama bado utaendelea kuzipokea..
 
Imeboreshwaje? Je maboresho yamehusisha kufuta thread za kipuuzi za Pro-CCM??? Kama hapana, basi maboresho yaliyofanyika yatakua ya kawaida sana. Hata hiyvo hongereni, kesho navaa T-shirt yangu ya JF
Mkuu Elli, maboresho yaliyofanyika ni ya kiufundi kwa upande wa APP..

Huko kwenye threads unaweza kuripoti hayo maudhui ili yapitiwe na mods kama yanakiuka sheria za JamiiForums yashughulikiwe!

Asante sana kwa kutuunga mkono kwa kununua tisheti zetu.

Tupo pamoja!
 
Back
Top Bottom