Solved: App ya JamiiForums imeboreshwa (Android & iOS)..

Wakuu,

Mimi hii app sijaipenda bora hiyo iliyokuwa ya zamani nimeona tangazo la app mpya ya JamiiForums nikaingia play store fasta nikaiupdate lakini kilichotokea bora hiyo ya zamani. Niwaombe uongozi wa JamiiForums waiangalie upya sijaipenda kwakweli,sijui wadau nyie mnaionaje kwanzia mazingira yake, rangi yake blue hovyo kabisa yani.

Karibuni
 
Mbona kwenye likes bado inakwamia only 5 likes..? Yaani likes hata zikiwa mia, hapa kwenye app inaishia 5 tuu, kwanini..? Naona kwenye ile concern yangu nyingine ya kutokea na option ya app ya Jf unapotumiwa link ya Jf, mmeifanyia kazi.. Now inapokuja link ya uzi, ninapofungua inakuja na option ya Jf App..
 
Ujue kila sehem lazima kuwe na wakwamishaji..!!! Ni maoni yako lkn una uhuru wa kutoa maoni
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mbona kwenye likes bado inakwamia only 5 likes..? Yaani likes hata zikiwa mia, hapa kwenye app inaishia 5 tuu, kwanini? Naona kwenye ile concern yangu nyingine ya kutokea na option ya app ya JF unapotumiwa link ya JF, mmeifanyia kazi.. Now inapokuja link ya uzi, ninapofungua inakuja na option ya Jf App..
Mkuu Sosoliso, asante kwa feedback.

Tunakushukuru kwa kutambua baadhi ya maboresho na kuyaainisha. Tunaendelea kufanya maboresho zaidi kwenye baadhi ya maeneo machache yaliyosalia.

Pamoja!
 
Moderator kwenye App ya zamani kulikuwa na tatizo la kuonesha idadi ya waliopendezwa na Uzi au mchango/maoni ya mchangiaji (Likes) kukomea mwisho tano, vipi hili tatizo limeshashughulikiwa kwenye hii app mpya?
 
Mkuu,

Kuna uzi bwana moderator ameuanzisha.

Pitia pale kutoa maoni yako ikiwa mapendekezo yako.

Kwa maoni yangu..

App imekua bomba, friendly user features zake zinabaki kuwa soo for privacy.

Nasubiri audio attachment ifae.
 
Salaam,

Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kwamba hatimaye tumekamilisha maboresho tuliyokuwa tukiyafanya kwenye APP ya JamiiForums na sasa inapatikana ikiwa na muonekano mzuri zaidi pamoja na urahisi wa kutumia. Unaweza kuipakua sasa au kama tayari unayo tafadhali fanya Update ili kupokea maboresho hayo.

Kwa takribani siku 10, baadhi ya watumiaji wa device za mfumo wa Android mlikutana na changamoto ya kutoweza kuipata App ya JamiiForums kupitia Playstore; JamiiForums haipatikani Playstore. Nini tatizo?

Tunashukuru kwa uvumilivu wenu katika kipindi chote tulichokuwa tukiifanyia kazi.

Kuna swali lolote?

Karibu..

Notification ni shida sana. Zinakuja mara moja kwa wiki. Ningependa kujua tu huu mgao uko jumangapi ili siku zingine nisihangaike.

Hongera kwa maboresho ila fanyieni kazi notifications kwenye android na iOs .
 
Mkuu, itakuwa ni network error kwa upande wako.

Jaribu kuangalia tena. Ikibidi ifunge na uifungue upya App yako.


effc1c122cd0150c08cba924cf02b742.jpg
Ahsante Mod.

Kidogo niione password yako(jokes)
 
Dark Mode Master Race...

Jaribuni hii kitu wakuu.

The app is great by the way. Kudos. Kuna bugs flani flani zilikuwa zinanikera kama kujirudia kwa threads kwenye 'New Posts' na ugumu wa kwenda kwenye subscribed forums. Hapa naona mambo sawia.

Wazo: Anzisheni public issue tracker kama JIRA hivi ili atleast wale technically inclined tuwe tunavumbua issues zilizopo na kuwawekea urahisi wa kuzireproduce.
cf27df8a88fb2cb233fd408c396aad27.jpg
 
Bado nini mkuu? Tueleze kama kuna tatizo lolote tulifanyie kazi mara moja..

Karibu!
Moja siwrzi kufuta post nikiwa natumia jf app,'wekeni option ya kufutia, pili sioni subscribed and participated threads kama hapo awali, likes and dislikes options.
 
Back
Top Bottom