Solar powe/umeme wa jua unahitajika

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Ndugu zangu,

Natafuta information za kampuni yeyote inayouza vifaa vya umeme wa jua kwa bei nafuu. Nataka nifunge umeme wa jua kijijini kwa sabau umeme wa TANESCO ni garama sana hasa seheu inayohitaji nguzo zaidi ya moja.

Vifaa vinavyotegemea kutumia umeme ni Taa 10 za WH zisizozidi 35, TV ndogo, kucharg simu, Redio na pasi siku moja moja.

Nitashukuru sana nikipata information za bei na vifaa vinavyohitajika. Mimi niko Dar es Salaam ila hata kama vitapatikana hapa Dar nitavisafirisha kwenda Kilimanjaro kijijini kuvifunga.

Natanguliza shukrani zangu kwa msaada wako
 
Hebu tuijadili TANESCO

Kuna wizi wa wazi unaofanywa na serikali kupitia shirika hili dhidi ya walalahoi wa nchi hii.
Utakuta mwananchi anahitaji kuunganisha umeme analipia application fee, halafu kama main line ipo mbali atalazimika kununua nguzo (hatozimiliki) kutoka tanesco kisha atalazimika kutoa rushwa au kusubiri muda mrefu aunganishiwe umeme. Kibaya zaidi utakuta kama anunua nguzo 10 kutoka main line halafu inbetween kuna mteja mpya, shirika bila ya kumhusisha aliyenunua nguzo watatumia zile alizolipia kumuunganishia huyu mpya. Na hii ni kutokana na kigezo katika sheria zao kwamba ukinunua nguzo kutoka kwao wanabakia na umiliki… Hapa nakosa jawabu la hesabu hii.
Utanunua MITA halafu wamiliki ni wao.

pamoja na mbwembwe za kupitisha mswada wa kupandisha gharama za uunganishaji wa umeme ambapo mahubiri yalikuwa kwamba itaongeza ufanisi na kupunguza ukiritimba, naona wameongeza uwiano wa kiwango cha rushwa ili uweze kuunganishwa kwa wakati.
Nadhani Badala ya kulalama kwa mbwembwe kuwa nchi itaingia gizani tusiponunua DOWANS kwanza safisha tanesco, toa huduma sahihi na muafaka kwa wateja. Haiingii akilini kung'ang'ania kununua maskrepa ya mitambo wakati hata kidogo kilichopo hakina uangalizi mzuri.
Wizi huu ni wa wazi tena umebarikiwa na BUNGE letu tukufu.

ANGALIZO
Mgao wa umeme umeanza nchini maana wamekuwa wakikata umeme bila sababu au taarifa kwa zaidi ya wiki mbili sasa. Na wakazi wa kigamboni kule Dar wamekuwa wakikatiwa umeme kila ifikapo saa moja usiku bila taarifa au sababu. Kama kunakuwa na hitilafu basi ni uungwana kuomba radhi kwa usumbufu.
 
Mimi nilikuwa na wafanyia wazee wangu hilo suala, kwanza inabibi uandae sh kama 1.5 M Kama unataka kitu kizuri amabcho kesho na keshokutwa hakitakukatiza,ila mimi nilikuwa na taa kumi na kila moja ilikuwa na watts tano
Hivyo nililazimika kununua Panel zenye watts 90, Na betri ndo ilikuwa ya garama zaidi nilitaka ninunue ambayo hata jua lisipowaka kwa siku tatu ifanye kazi na nilinunua kwa sh 500,000. Lakini kuna hata ndogo zake ambazo ni chini ya laki mbili.Ila nakushauri,uende duka fulani ckumbuki mtaa ila ni watu wa AFRICAN CABLES,LIPO kariakoo mtaa unaouza vifaa vya umeme nyuma ya tahafifu kama unaijua hiyo bookshop kubwa ya kariakoo,pita pembeni ya hilo duka na ingia kushoto mtaa wa kwanza na hilo duka lipo upande wako wa kulia,utaona tangazo lao la african cables, na vifaa mbali mbali. Kwa maelezo zaidi tuwasiline,Hili duka wanauza vitu durable na mii nina mwaka sasa na hamna matatizo na bei zao ni nzuri saana na unapewa na waranty
 
Ila nakushauri,uende duka fulani ckumbuki mtaa ila ni watu wa AFRICAN CABLES,LIPO kariakoo mtaa unaouza vifaa vya umeme nyuma ya tahafifu kama unaijua hiyo bookshop kubwa ya kariakoo,pita pembeni ya hilo duka na ingia kushoto mtaa wa kwanza na hilo duka lipo upande wako wa kulia,utaona tangazo lao la african cables, na vifaa mbali mbali

Asante Audax kwa kuwa wa msaada kwa mwenzetu. Ila Dar na miji yetu inahitaji kuwa na physical addresses. Hatuwezi kukaa tu bila coordinates.

Ningependa mno kuachana moja kwa moja na TANESCO. Haiwezekani kuisha kwa furaha na huku unategemea umeme wa mambumbu wa TANESCO.

Nimeuliza hapa, siku za nyuma, na naomba kuuliza tena: kama kuna mtu amewahi kuweka nyumbani kwake umeme wa jua wa kutosha shughuli zote za kawaida za nyumbani, basi tafadahali atupe experience yake.

Au kama kuna mtaalamu anayeweza kutupa quotation (for discussion) ya vifaa vya meme wa jua wa kutosha taa za nyumba ya kawaida, TV, pasi, jiko, vifaa vya nyumbani kama blender, etc, basi tafadhal tusaidie.

Ni lengo langu kuachana permanently, na TANESCO. Najua initial costs zitakuwa kubwa, lakini ningependa some estimates.
 
Hii kitu nzuri sanaa. Maana huwa tunajitahidi kujenga nyumba kwa kujipiga piga na inamalizika nadhaki hii kitu ni muhimu sana na hasa kama mambo yenyewe ya Tanesco ndio hivii, na bei yao yenyewe kubwaa. Na ni njia mojawapo ya kupambana na ufisadi na watu wengi wakienda kwenye Solar Tanesco watapunguza bei tuu kwa ushindani. Ila hii kitu Solar Power) ni muhimu sanaaaaa.
 
Ndugu zangu,

Natafuta information za kampuni yeyote inayouza vifaa vya umeme wa jua kwa bei nafuu. Nataka nifunge umeme wa jua kijijini kwa sabau umeme wa TANESCO ni garama sana hasa seheu inayohitaji nguzo zaidi ya moja.

Vifaa vinavyotegemea kutumia umeme ni Taa 10 za WH zisizozidi 35, TV ndogo, kucharg simu, Redio na pasi siku moja moja.

Nitashukuru sana nikipata information za bei na vifaa vinavyohitajika. Mimi niko Dar es Salaam ila hata kama vitapatikana hapa Dar nitavisafirisha kwenda Kilimanjaro kijijini kuvifunga.

Natanguliza shukrani zangu kwa msaada wako

Kuna njia nyingine niliyojifunzia wakati wa shida ya umeme Bongo. Unanunua mashine hii;

power inverter, kwa matumizi uliyosema, waweza chukua inayozalisha 1000 watts tu, ambayo kwa bei ya mwaka jana ilikuwa approx shs laki tano, kisha unanunua na battery zako mbili/tatu za namna hii N90;

unaunganisha kwenye umeme nyumbani kwako, aah... (unatumia umeme wa battery) unawasahau Tanesco!

Unahitaji Battery mbili/tatu, sababu unatumia moja kila baada ya siku/tatu, nyingine unaipeleka ku chajiwa...na bei ya ku charge battery haizidi sh1000. Ukibahatika kupata Solar panels, hiyo adha ya kucharge battery kwa umeme wa Tanesco pia itaisha.

Muhimu, ni kuangalia genuine product ni ipi, feki ni ipi toka China.
 
Asante Mbu kwa kutoa somo litakalosaidia wale wanaohitaji umeme wa taa tu. Sidhani hiyo mashine itatosha matumizi YOTE (taa, pasi, fridge, TV, computer, hata kupika).

Kama kuna mmoja wetu hapa anayeweza kutoa somo kuhusu investment inayotakiwa so as to enable one to sever relations with TANESCO mpaka kiyama, basi tunamwomba afanye hivyo. Ni njia moja ya kujenga nchi.
 
Ahsante mwalimu kwa kuleta maada hii yenye akili.Kitu kimoja kinachoitia kichwa TANESCO ni ukiritimba na monopoly hii juu ya umeme Tanzania.

Sina hakika kwa wale wenye connection kwenye national grid ambao wameamua pia kuwa na altenative sources kama solar power, kama wanaweza kuuza umeme huo kwenye national grid.
 
KWakweli ni vema tukiamka na kujitafutia maendeleo wenyewe, wazo la umeme jua kwa nchi yetu ni mkombozi, na pia zaidi tufikirie upepo na gas ili tuweze kujikwamua, tunanishati za asili ambazo nadhani wangezipata wenzetu sijui wangekuwa wapi!! JUA JUA ni bure masaa zaidi ya manane kila siku bado tunalia na TANESCO:

kwa ufupi natumia solar kwa matumizi ya taa, computer, redio, blender, kuchaji simu, kunyoa, nk kwa miaka takriban 5 sasa, naishi Dar ila ninaposihi hakuna hata NGUZO ya TANESCO ( samahani si mkoani, ni DAR).

nina panel 2 za watt 75 kila moja, inverter 800 Watt, battery moja ya 100 N (solar battery ingawa pia unaweza kutumia ya gari), installation iligharimu kama millioni 2 kwa kipindi kile. sijawahi kulipa billi wa ku-service toka nimeweka,

kubwa katika solar ni wewe mwenyewe kujipangia matumizi na pia kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa ila kama unabattery za kutosha mfano betri 2 au 3 za 100 N utakuwa huna tatizo.
mfano kwangu nawasha mchana kama ninahitaji tu kama sihiaji ninazima source, hii inasaidia kutokuichosha inverter na pia kuhifadhi umeme, na pia usiku napunguza matumizi ya vifaa vingine ili nipate umeme wa kurosha kwa ajili ya taa, vifaa kama blender, computer, kunyoa huwa natumia au nachaji mchana,

kuhusu kupikia sijajaribu ila solar niliuliza kuhusu kupikia na pasi, wakasema inabidi ufanye investment kubwa kama unataka kupikia (kwaufupi ni unaffordable) ila fridge, freezer inawezekana tena kuwa safe zaidi unaweza fanya installation separate ya fridge au freezer,
ila suala la jiko kwa sasa hatuhitaji saaana umeme maana majigo ya gas hadi yenye oven yanapatikana, na gas ni wa kuaminika, pia gas ya siku hizi ni light na inaharufu hivyo ikiwa inavuja ni rahisi kugundua.

wataalam wa solar kwa sasa wapo wengi sikumbuki kwa majina ila hata chloride exide wanahuduma!
 
Asante Audax kwa kuwa wa msaada kwa mwenzetu. Ila Dar na miji yetu inahitaji kuwa na physical addresses. Hatuwezi kukaa tu bila coordinates.

Ningependa mno kuachana moja kwa moja na TANESCO. Haiwezekani kuisha kwa furaha na huku unategemea umeme wa mambumbu wa TANESCO.

Nimeuliza hapa, siku za nyuma, na naomba kuuliza tena: kama kuna mtu amewahi kuweka nyumbani kwake umeme wa jua wa kutosha shughuli zote za kawaida za nyumbani, basi tafadahali atupe experience yake.

Au kama kuna mtaalamu anayeweza kutupa quotation (for discussion) ya vifaa vya meme wa jua wa kutosha taa za nyumba ya kawaida, TV, pasi, jiko, vifaa vya nyumbani kama blender, etc, basi tafadhal tusaidie.

Ni lengo langu kuachana permanently, na TANESCO. Najua initial costs zitakuwa kubwa, lakini ningependa some estimates.

Mkuu AM,

Kama ningekuwa na uwezo basi binafsi nigeiua TANESCO ili tujue hatuna hilo zimwi. Ni matatizo matupu.

Kuhusu umeme wa solar kuna wachangiaji wametoa ushauri mzuri. Ila niliwahi kukutana rafiki yangu ambaye anaishi nchi moja ya Ulaya, anatumia umeme wa solar kwa matumizi mengi ikiwa ni pamoja na kupasha joto nyumba wakati wa majira ya baridi. Alinambia kuwa gharama ya vifaa vyote ilikuwa kama $5000 (karibia 6.5m). Nadhani tunahitaji mjadala zaidi ili tuweze kupeana mbinu za kuachana na Tanesco. Shida kubwa ni kuwa watu wengi wenye pesa wanatumia umeme wa kuiba kwa hiyo wanaongeza mzigo kwa walala hoi. Kuna uwezekano mkubwa kwamba hata viongozi wakubwa wanaiba umeme na ndio maana hawajali. Kwa hiyo, kwa wale wenye uzoefu tusaidiane. Tukiamua kuachana na Tanesco tutakuwa tumepata ushindi mkubwa kwa sababu sasa hivi hili shirika limefanywa bomba la kutolea pesa za ufisadi. Kuna uwezekano hata 2010 wakulu wakakimbilia huko.
 
Mkuu AM,

Niliwahi kukutana rafiki yangu ambaye anaishi nchi moja ya Ulaya, anatumia umeme wa solar kwa matumizi mengi ikiwa ni pamoja na kupasha joto nyumba wakati wa majira ya baridi. Alinambia kuwa gharama ya vifaa vyote ilikuwa kama $5000 (karibia 6.5m)

Asante sana Dark City. Nadhani tunahitaji uzoefu wa mtu aliyeweka umeme wa solar Dar, wa kutosha matumizi yote ya nyumbani. Je, umekuwa ukimtosha kweli au inabidi wakati mwingine aongezee wa Tanesco? Aliingia ghrama gani?

Gharama ya 6.5/= mil. inaonekana ni cost effective. Kama nyumba inatumia umeme wa laki moja kwa mwezi basi mtu unafikia hizo 6.5/= mil. baada ya miaka mitano na nusu tu. Na solar panels nadhani zinadumu hata miaka 20.
 
Kuna njia nyingine niliyojifunzia wakati wa shida ya umeme Bongo. Unanunua mashine hii;

power inverter, kwa matumizi uliyosema, waweza chukua inayozalisha 1000 watts tu, ambayo kwa bei ya mwaka jana ilikuwa approx shs laki tano, kisha unanunua na battery zako mbili/tatu za namna hii N90;

unaunganisha kwenye umeme nyumbani kwako, aah... (unatumia umeme wa battery) unawasahau Tanesco!

Unahitaji Battery mbili/tatu, sababu unatumia moja kila baada ya siku/tatu, nyingine unaipeleka ku chajiwa...na bei ya ku charge battery haizidi sh1000. Ukibahatika kupata Solar panels, hiyo adha ya kucharge battery kwa umeme wa Tanesco pia itaisha.

Muhimu, ni kuangalia genuine product ni ipi, feki ni ipi toka China.

kaka nimekupata ila najaribu kufungua hizo attachment hazifunguki,nifanyie mpango nitazisomaje?
ray_mauki@yahoo.com nahitaji kununua solar nikirudi TZ this summer
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom