Sokoine University of Agriculture (SUA) special Thread

Duh, mzee wa kuvalia suruali juu ya kitovu? Anaumwa nini? Pole zake mwalimu wangu wa annual crops, Mwenyezi Mungu na amponye mja wake!!
Kweli kabisa, huyu mwamba hajawahi kuvalia suruali kiunoni hata siku moja. Suruali zake alikuwa anavalia tumboni.
 
Dr. Sarwat alinifundisha notes zake nazikumbuka (course iliyohusianana na animal science). Nadhani mwamba yeye alikuwa anatafuta pesa tu make alikuwa anapesa sana yuke mzee.

Mwingine aliyekuwa habadilishi notes (naye ni marehemu mwenyezi Mungu amuweke mahali pema) ni Dr./Prof. Msumari wa idara ya soil science, tena alikuwa anatuambia kabisa someni notes zangu msisome chochote kingine. Ila hii haikuwa nzuri kwa sababu unam-discourage mwanafunzi kusoma vitabu vingine ili apanue uelewa zaidi ya notes zako tu!
 
Kweli kabisa mkuu; marehemu Prof Msumari alikuwa strict kwenye somo lake la soil biology. Kuna siku alitutungia maswali ya T/F halafu majibu yote akaweka TRUE, nikapasua yote. Pia kuna Prof mmoja wa irrigation engineering anaitwa Prof Thadei, huyu naye notes zake ni zile za miaka ya 70; naye amekariri hizo hizo hawezi kubadilisha kitu. Tatizo syllabus ya SUA imeorodhesha tu mambo ambayo wanafunzi wanapaswa kufundishwa lakini haiendi deep zaidi kama zile syllabuses za vyuo vidogo. Kwa hiyo, lecturer anafundisha kile anachojua tu. Lecturers wanaweza wakawa wanafundisha somo hilo hilo lakini utakuta kila mmoja anafundisha vitu tofauti kabisa. Ushahidi ni katika somo la botany ambalo lilifundishwa na Prof Temu na Prof Minjas katika madarasa tofauti. Notes za Temu zilikuwa deep wakati zile za Minjas zilikuwa shallow and narrow.
 
Dr. Sarwat alinifundisha notes zake nazikumbuka (course iliyohusianana na animal science). Nadhani mwamba yeye alikuwa anatafuta pesa tu make alikuwa anapesa sana yuke mzee.
Exactly. Alikuwa mtoro sana chuoni na alikuwa anafundisha ovyo ovyo tu ilmradi kutimiza lengo. Muda mwingi alikuwa akihangaikia miradi yake ya kuingiza pesa ndefu.
 
Dr shayo Ngowi yupogo?alikuwa soil science
 
Probably atakuwa kastaafu maana kipindi kile tulichosoma pale (zaidi ya miaka 20 iliyopita) umri ulikuwa umesogea sana. Hawezi akawa bado anaendelea kufundisha.
Kwa sasa ukisoma SUA unaweza kupata ajira Za serikali kozi ambayo Sio ualimu?
 
Hata upekue vipi SUA baadhi ya kozi ni Za kufuta inept na wakati kwenye Soko la ajira
Sijakuelewa vizuri mkuu. Ukisoma degree kwa mfano ya Veterinary Medicine unaweza kujiajiri mwenyewe kwa kuuza pembejeo za mifugo na kutibu. Kuna kozi nyingi zinatolewa SUA ambazo ukihitimu unajiajiri mwenyewe mkuu. Fuatilia vizuri kwenye mtandao.
 
Sijakuelewa vizuri mkuu. Ukisoma degree kwa mfano ya Veterinary Medicine unaweza kujiajiri mwenyewe kwa kuuza pembejeo za mifugo na kutibu. Kuna kozi nyingi zinatolewa SUA ambazo ukihitimu unajiajiri mwenyewe mkuu. Fuatilia vizuri kwenye mtandao.
Mbona Jaffo alishindwa kujiajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…