Sokoine na Kolimba, vifo vyao vilimkera Mwalimu kiasi gani?

Nimejaribu kusoma kwa makini,japo bado inaendelea wiki ijayo,but so far naona Nyerere was a problem kwenye hii nchi,hasa baada ya kuondoka madarakani,sina tatizo nae alipokuwa madarakani,issue yangu ni alipokua nje ya madaraka aliutumia vibaya uzee wake kwa kujaribu kuiyumbisha serikali halali,inavyoonyesha kama sio huo uungwana wa rais wa wakati huu bwana mwinyi kama alivyokuwa akidai bwana "Alex Kowe",nyerere alitakiwa kuburuzwa kortini kwa uchochezi au uhaini.
 
Unaimba nyimbo ndefuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, Zaiko Langa Langa? Sisi tunataka chorus bana! Awilo Longomba - kwachuuu kwachuuuu
 
Nimejaribu kusoma kwa makini,japo bado inaendelea wiki ijayo,but so far naona Nyerere was a problem kwenye hii nchi,hasa baada ya kuondoka madarakani,sina tatizo nae alipokuwa madarakani,issue yangu ni alipokua nje ya madaraka aliutumia vibaya uzee wake kwa kujaribu kuiyumbisha serikali halali,inavyoonyesha kama sio huo uungwana wa rais wa wakati huu bwana mwinyi kama alivyokuwa akidai bwana "Alex Kowe",nyerere alitakiwa kuburuzwa kortini kwa uchochezi au uhaini.
Walijaribu kumburuza kortini lakini wakashindwa kumpata mtu ambaye atamfunga paka kengele. Soma Wikileaks uone jinsi akina Kikwete na Kapuya walivyokuwa wanamwogopa Waitara.
 
Nyerere kaiharibu vibaya sana Tanzania kuliko hata yule mkoloni aliyemchukia. Alikuwa hataki kabisaa mtu apingane na sera zake za ziwe mbaya au nzuri kwa wanachi. Kolimba alisema ukweli kuwa chama cha CCM hakina dira. maana wakati huo maendeleo yalikuwa hayaonekani ila sifa za nyerere tu katika kwaya na muziki wa danci. siajua kolimba alikufa namna gani mpaka leo.

Tusingekuwa na mtawala kama nyerere , tanzania hivi sasa tungekuwa tunaongea kiingereza vizuri, tungecheza AFCON Gabon,tungekuwa na viwanda vingi mikoa ya kusini na kutatuta kero za ajira,tungekuwa na wasomi mamilion kuliko kenya na uganda,wanamuziki wetu wangekuwa mabilionaire,tungekuwa na uhusiano mzuri na israel,tungeboresha utalii kupita nchi zote africa,Yanga na simba zingekuwa mabingwa wa soka Africa zaidi ya mara nne,ATC ingekuwa na safari za kimataifa kuliko nch yeyote barani africa, wapalestina wasingekuwa na maduka mjini dar, Tusingekuwa na mafisadi na Tanzania ingekuwa na heshima kubwa duniani.

Si unakumbuka serikali yake iliwafukuza Tambwe Leya na kamara mwaka 1976? wakati huo waziri wa michezo alikuwa Sarakikya mirisho? wewe hapo unapata picha gani?

Jamani watanzania wenzangu, kweli nyerere anastahili kuwa mtakatifu?
 
Utakatifu ni process za kanisa kama una hoja peleka kanisa Katoliki! Hata kutangazwa mwenye heri bado ndugu yangu.uadilifu wa uongozi Nyerere ni namba moja duniani whether ndoto zake zilifanikiwa au la!
 
mmempa Kikwete kifupisho maarufu cha Nyerere cha "JK" while alistahili kuwa JM(Jakaya Mrisho) sikuhizi Nyerere mnatumia JKN! Au mlidhani nyota ipo kwenye jina? Haya bana!
 
Kolimba alikaribia kumuweza nyerere na nyerere inaonekana alilijua hilo mapema,akaamua "kumdhibiti",angeendelea kuwepo leo Tanganyika ingewepo......nyerere alikua mbabe(dikteta)
 
Katika kuonyesha kwamba hali si shwari sana ndani ya chadema kumekuwa na sintofahamu za hapa na pale kuhusu mbunge kijana machachari zitto kabwe ambapo safari hii tena ile Kauli yake kwamba wazo la chama chake kumuona Rais Jakaya Kikwete juu ya mabadiliko ya sheria ya katiba mpya lilitolewa na Regia Mtema, imepingwa.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, wazo hilo la kuzungumza na serikali na hata kumuona rais, lilitolewa na sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Mara baada ya kifo cha Regia, tarehe 14 Januari mwaka huu, Zitto aliviambia vyombo vya habari kuwa ni yeye (Regia) aliyetoa wazo hilo kwenye kikao cha viongozi wakuu wa chama wakiwemo wabunge.


Regia ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum, alikutwa na mauti kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Ruvu mkoani Pwani. Lakini Zitto akizungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu alisisitiza, “…wazo hilo lilitolewa na Regia.”


Taarifa ya chama hicho inasema, sekretarieti ya CHADEMA iliibua wazo la chama kuwasiliana na serikali ili kutafuta njia bora ya kupatikana kwa katiba mpya.


“Wazo hilo lilitoka ndani ya sekretarieti na Mheshimiwa Regia Mtema hakuwa mjumbe wa sektarieti. Yeye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC),” anasema mmoja wa viongozi wa CHADEMA.


“Sasa mtu ambaye hakuwa mjumbe na ambaye hakualikwa kwenye mkutano wa sekretarieti anawezaje kuibua hoja kwenye kikao ambacho hakuwapo,” alihoji kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.


Amesema, “Sisi tumeamua kukaa kimya kwa kuwa hatutaki kuonekana tunaongelea marehemu; lakini kwa kweli tumesikitishwa na kauli ya mwenzetu…”


Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya Zitto, naibu katibu mkuu wa CHADEMA, kueleza kuwa wazo la kutaka uongozi wa juu wa chama hicho kukutana na Rais Kikwete lililetwa na Regia Mtema.


Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alinukuliwa akisema, baada ya viongozi wake kutafakari wazo la Regia walilikubali.

Amenukuliwa akisema ushauri wa Regia haukupata upinzani katika majadiliano kwenye kikao cha Kamati Kuu ambapo hoja nzito zilijengwa kuuimarisha baada ya wajumbe kuona kuwa ni ushauri muhimu unaofaa kufanyiwa kazi.

Wakati Zitto akinukuliwa hivyo, waraka ambao gazeti hili limenasa unaonyesha wazo la viongozi wa CHADEMA kupanga kukutana na serikali lilianzia kwenye sekretarieti ambako Regia hakuwa mjumbe.


Waraka huo wenye kurasa 10 uliandaliwa na ofisa mmoja katika idara ya utafiti na sera, ambaye aliingiza hoja ya viongozi wakuu wa CHADEMA kuomba kuwasiliana na serikali.


Nyaraka zinaonyesha ofisa huyo aliteuliwa na kikao cha sekretarieti cha 15 Novemba 2011 jijini Dar es Salaam kilichoitishwa kuandaa kile kilichoitwa, “Mapendekezo ya mkakati endelevu wa kutafuta haki nje ya Bunge.”


Aidha, ofisa huyo aliwasilisha waraka wenye mapendekezo ya kuundwa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu kwenye mkutano wa CC uliofanyika 29 Novemba 2011.


Kikao cha sekretarieti kilichompa jukumu ofisa huyo kuandaa mapendekezo ya “mkakati endelevu,” kilifanyika saa chache baada ya wabunge wa chama hicho kutoka nje ya ukumbi wa bunge Dodoma, kupinga utaratibu uliotumika kuwasilisha muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.


Kwa mujibu wa waraka wa CHADEMA, kwenye ukurasa wa nane, “Sekretarieti inapendekeza njia ya kwanza ya kupata suluhisho ni majadiliano.”


Waraka unasema, “Baada ya pande mbili hizi – CCM/serikali na CHADEMA kutofautiana kwa hoja, sekretarieti inaona ni busara Kamati Kuu iunde timu ya watu wachache wataalamu ambayo itakuwa na wajibu wa kuandaa hoja zote ambazo CHADEMA inapingana nazo na kuzipeleka serikalini.”


Shabaha ya kazi hiyo ilikuwa “…kuangalia mambo ambayo angalau tunaweza kukubaliana nayo na yale ambayo chama kinaweza kukubaliana kutokubaliana nayo.”


Waraka unasema mapambano ya aina ya mjadala yana faida kubwa tatu. Kwanza, yataondoa dhana kwamba CHADEMA wanalalamika bila kuleta maandishi rasmi.


Unasema Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwahi kupotosha taifa kwamba hadi wabunge wa chama hicho wanatoka bungeni, alikuwa hajajua hoja zao.


Unasema Makinda alinukuliwa akisema hata pale ambapo kiongozi wa upinzani, Freeman Mbowe alipokutana naye, hakumweleza hoja za msingi ambazo chama hicho kinazisimamia, jambo ambalo umeliita “…uzushi uliopitiliza.”


Pili, waraka unasema kwa kutumia njia ya mjadala, jamii ya kimataifa, wanaharakati na wananchi wengine wataona kwamba CHADEMA haikufunga milango ya majadiliano na kwamba, kama serikali itaziba masikio, basi malalamiko yote yataelekezwa kwake.

Tatu, waraka unaeleza, “Lengo la mpango huu ni kuweka kumbukumbu sahihi, kwamba CHADEMA ni chama makini na kipo tayari kushika dola.”

Inaelezwa katika ukurasa wa saba wa waraka kwamba mjadala juu ya muswada wa sheria uliendeshwa kwa ushabiki na upotoshaji mkubwa.


Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema, waziri wa sheria, Celina Kombani na Rais Kikwete mwenyewe, wanatajwa kuendesha mjadala “kwa ushabiki.”


Waraka unapendekeza “…sekretarieti ya chama itoe elimu ya uelewa wa muswada kupitia mfumo wa chama kikatiba wa makongamano, mikutano ya hadhara na vyombo vya habari.”


“Majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA zinaweza kupata dondoo za ukweli, lakini majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CCM na vyama vingine, wataendelea kupotoshwa na hivyo kupunguza uungwaji mkono wa hoja zetu,” umeeleza waraka.


“Serikali na chama chake wametumia muda mwingi bungeni na kwenye vyombo vya habari, kuijadili na kuisema CHADEMA, wabunge na viongozi wake,” unalalamika waraka.


“Hali hiyo itaendelea sasa na hivyo ni muhimu kutafuta njia nzuri ya kueleza ukweli wa jambo hili kwa Watanzania,” unaeleza waraka.


Kama serikali itashindwa kuwasikiliza, unasema waraka, “…kukaa na hata kukabiliana na timu ya wataalamu ya CHADEMA… tutakuwa tumepata fursa adhimu ya kuandaa mchakato wa katiba na hatimaye kupata katiba mpya itakayoshindanishwa na ile inayoandaliwa na serikali.”


Wakati sekretarieti inapendekeza yote hayo, Zitto alikuwa kwenye matibabu India na kikao cha CC ambamo ulisomwa waraka huu, kilifanyika siku mbili baada ya Zitto kuwasili.
 
Nimejaribu kusoma kwa makini,japo bado inaendelea wiki ijayo,but so far naona Nyerere was a problem kwenye hii nchi,hasa baada ya kuondoka madarakani,sina tatizo nae alipokuwa madarakani,issue yangu ni alipokua nje ya madaraka aliutumia vibaya uzee wake kwa kujaribu kuiyumbisha serikali halali,inavyoonyesha kama sio huo uungwana wa rais wa wakati huu bwana mwinyi kama alivyokuwa akidai bwana "Alex Kowe",nyerere alitakiwa kuburuzwa kortini kwa uchochezi au uhaini.

Hili hata mimi pia nimewahi kulifikiria,nyerere was a disaster kwa kweli!
 
Wewe unaonekana ni mtu wa hovyo sana.Unachokijua ni kuandika ****** kila siku kuhusu CDM na Zitto.Watu tumechoka na habari zako za udaku.

Mara ulete matusi yako kuhusu Mbowe na Slaa,mara ulete mambo ya kipuuzi kuhusu mgombea wa CDM jimbo la kibaha na sasa unaendeleza umbea wako usio na msingi.Kama unadhani CDM ni wajinga kama wewe unajidanganya sana.

Endelea kuropoka lakini mwisho wako na ******* wenzako unakaribia sana. Stay tuned!
 
Kuna kipindi alisema kuna watu wanaugonjwa uitwao ZITTOFOBIA labda nawe ni miongoni mwao

Ulicho kileta hapa si kipya kitoka Mwanahalisi tulijadili kuwa huu ni uchovu wa fikira kujadili mada ambayo haina madhara kama unavyo jarribu kuikuuuuza Kama hoja ni hii Chadema hakuna mgogoro
 
Namsikitikia Mleta Hoja Kuleta Habari ambayo Haina Mashika na ambayo Hamsaidii Mtanzania wa Kawaida Kujikwamua kwenye Lindi la Umasikini!!
 
Back
Top Bottom