Sokoine na Kolimba, vifo vyao vilimkera Mwalimu kiasi gani?

Katika kuonyesha kwamba hali si shwari sana ndani ya chadema kumekuwa na sintofahamu za hapa na pale kuhusu mbunge kijana machachari zitto kabwe ambapo safari hii tena ile Kauli yake kwamba wazo la chama chake kumuona Rais Jakaya Kikwete juu ya mabadiliko ya sheria ya katiba mpya lilitolewa na Regia Mtema, imepingwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, wazo hilo la kuzungumza na serikali na hata kumuona rais, lilitolewa na sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mara baada ya kifo cha Regia, tarehe 14 Januari mwaka huu, Zitto aliviambia vyombo vya habari kuwa ni yeye (Regia) aliyetoa wazo hilo kwenye kikao cha viongozi wakuu wa chama wakiwemo wabunge.

Regia ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum, alikutwa na mauti kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Ruvu mkoani Pwani. Lakini Zitto akizungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu alisisitiza, “…wazo hilo lilitolewa na Regia.”

Taarifa ya chama hicho inasema, sekretarieti ya CHADEMA iliibua wazo la chama kuwasiliana na serikali ili kutafuta njia bora ya kupatikana kwa katiba mpya.

“Wazo hilo lilitoka ndani ya sekretarieti na Mheshimiwa Regia Mtema hakuwa mjumbe wa sektarieti. Yeye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC),” anasema mmoja wa viongozi wa CHADEMA.

“Sasa mtu ambaye hakuwa mjumbe na ambaye hakualikwa kwenye mkutano wa sekretarieti anawezaje kuibua hoja kwenye kikao ambacho hakuwapo,” alihoji kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Amesema, “Sisi tumeamua kukaa kimya kwa kuwa hatutaki kuonekana tunaongelea marehemu; lakini kwa kweli tumesikitishwa na kauli ya mwenzetu…”

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya Zitto, naibu katibu mkuu wa CHADEMA, kueleza kuwa wazo la kutaka uongozi wa juu wa chama hicho kukutana na Rais Kikwete lililetwa na Regia Mtema.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alinukuliwa akisema, baada ya viongozi wake kutafakari wazo la Regia walilikubali.

Amenukuliwa akisema ushauri wa Regia haukupata upinzani katika majadiliano kwenye kikao cha Kamati Kuu ambapo hoja nzito zilijengwa kuuimarisha baada ya wajumbe kuona kuwa ni ushauri muhimu unaofaa kufanyiwa kazi.

Wakati Zitto akinukuliwa hivyo, waraka ambao gazeti hili limenasa unaonyesha wazo la viongozi wa CHADEMA kupanga kukutana na serikali lilianzia kwenye sekretarieti ambako Regia hakuwa mjumbe.

Waraka huo wenye kurasa 10 uliandaliwa na ofisa mmoja katika idara ya utafiti na sera, ambaye aliingiza hoja ya viongozi wakuu wa CHADEMA kuomba kuwasiliana na serikali.

Nyaraka zinaonyesha ofisa huyo aliteuliwa na kikao cha sekretarieti cha 15 Novemba 2011 jijini Dar es Salaam kilichoitishwa kuandaa kile kilichoitwa, “Mapendekezo ya mkakati endelevu wa kutafuta haki nje ya Bunge.”

Aidha, ofisa huyo aliwasilisha waraka wenye mapendekezo ya kuundwa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu kwenye mkutano wa CC uliofanyika 29 Novemba 2011.

Kikao cha sekretarieti kilichompa jukumu ofisa huyo kuandaa mapendekezo ya “mkakati endelevu,” kilifanyika saa chache baada ya wabunge wa chama hicho kutoka nje ya ukumbi wa bunge Dodoma, kupinga utaratibu uliotumika kuwasilisha muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Kwa mujibu wa waraka wa CHADEMA, kwenye ukurasa wa nane, “Sekretarieti inapendekeza njia ya kwanza ya kupata suluhisho ni majadiliano.”

Waraka unasema, “Baada ya pande mbili hizi – CCM/serikali na CHADEMA kutofautiana kwa hoja, sekretarieti inaona ni busara Kamati Kuu iunde timu ya watu wachache wataalamu ambayo itakuwa na wajibu wa kuandaa hoja zote ambazo CHADEMA inapingana nazo na kuzipeleka serikalini.”

Shabaha ya kazi hiyo ilikuwa “…kuangalia mambo ambayo angalau tunaweza kukubaliana nayo na yale ambayo chama kinaweza kukubaliana kutokubaliana nayo.”

Waraka unasema mapambano ya aina ya mjadala yana faida kubwa tatu. Kwanza, yataondoa dhana kwamba CHADEMA wanalalamika bila kuleta maandishi rasmi.

Unasema Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwahi kupotosha taifa kwamba hadi wabunge wa chama hicho wanatoka bungeni, alikuwa hajajua hoja zao.

Unasema Makinda alinukuliwa akisema hata pale ambapo kiongozi wa upinzani, Freeman Mbowe alipokutana naye, hakumweleza hoja za msingi ambazo chama hicho kinazisimamia, jambo ambalo umeliita “…uzushi uliopitiliza.”

Pili, waraka unasema kwa kutumia njia ya mjadala, jamii ya kimataifa, wanaharakati na wananchi wengine wataona kwamba CHADEMA haikufunga milango ya majadiliano na kwamba, kama serikali itaziba masikio, basi malalamiko yote yataelekezwa kwake.

Tatu, waraka unaeleza, “Lengo la mpango huu ni kuweka kumbukumbu sahihi, kwamba CHADEMA ni chama makini na kipo tayari kushika dola.”

Inaelezwa katika ukurasa wa saba wa waraka kwamba mjadala juu ya muswada wa sheria uliendeshwa kwa ushabiki na upotoshaji mkubwa.

Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema, waziri wa sheria, Celina Kombani na Rais Kikwete mwenyewe, wanatajwa kuendesha mjadala “kwa ushabiki.”

Waraka unapendekeza “…sekretarieti ya chama itoe elimu ya uelewa wa muswada kupitia mfumo wa chama kikatiba wa makongamano, mikutano ya hadhara na vyombo vya habari.”

“Majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA zinaweza kupata dondoo za ukweli, lakini majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CCM na vyama vingine, wataendelea kupotoshwa na hivyo kupunguza uungwaji mkono wa hoja zetu,” umeeleza waraka.

“Serikali na chama chake wametumia muda mwingi bungeni na kwenye vyombo vya habari, kuijadili na kuisema CHADEMA, wabunge na viongozi wake,” unalalamika waraka.

“Hali hiyo itaendelea sasa na hivyo ni muhimu kutafuta njia nzuri ya kueleza ukweli wa jambo hili kwa Watanzania,” unaeleza waraka.

Kama serikali itashindwa kuwasikiliza, unasema waraka, “…kukaa na hata kukabiliana na timu ya wataalamu ya CHADEMA… tutakuwa tumepata fursa adhimu ya kuandaa mchakato wa katiba na hatimaye kupata katiba mpya itakayoshindanishwa na ile inayoandaliwa na serikali.”

Wakati sekretarieti inapendekeza yote hayo, Zitto alikuwa kwenye matibabu India na kikao cha CC ambamo ulisomwa waraka huu, kilifanyika siku mbili baada ya Zitto kuwasili.

we umetumwa na ndo maana hamjadili kero za watu na jinsi ya kuzitatua badala yake mnajadili watu na kupiga umbeya usio na msingi!yapo mengi sana ya kushare na jamii lakini unaleta unafuiki wako wa kuchonganisha watu!ccm imekufa kabisaaaaaaaa unafanya nini ili ifufuke sio umbeya tuuuuuuuuu! f*ra mkubwa wewe!cdm ina watu wanaojua chama kinafanya nini?kiantakiwa kufanya nini, na nani atafanya nini sio ******* yameuza nchi yote na ubafiki mkubwa wenu mkijilimbikizia mali za nchi!ole wenu make mwisho wenu u karibu sana!snztyp!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Na wala sio secretarieti iliyoibua hoja hiyo Hoja hiyo imeibuliwa na Wilson Mukama ambaye ni undercover kutoka CCM. hivi awe ameibua regia au hata chacha wangwe inatusaidia nini ? hoja imeletwa ina impact wacha ifanyiwe kazi hata kama imeletwa na nani! sisi tunachoangalia ni matokeo sio nani ka creat. UPo!
Katika kuonyesha kwamba hali si shwari sana ndani ya chadema kumekuwa na sintofahamu za hapa na pale kuhusu mbunge kijana machachari zitto kabwe ambapo safari hii tena ile Kauli yake kwamba wazo la chama chake kumuona Rais Jakaya Kikwete juu ya mabadiliko ya sheria ya katiba mpya lilitolewa na Regia Mtema, imepingwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, wazo hilo la kuzungumza na serikali na hata kumuona rais, lilitolewa na sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mara baada ya kifo cha Regia, tarehe 14 Januari mwaka huu, Zitto aliviambia vyombo vya habari kuwa ni yeye (Regia) aliyetoa wazo hilo kwenye kikao cha viongozi wakuu wa chama wakiwemo wabunge.

Regia ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum, alikutwa na mauti kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Ruvu mkoani Pwani. Lakini Zitto akizungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu alisisitiza, “…wazo hilo lilitolewa na Regia.”

Taarifa ya chama hicho inasema, sekretarieti ya CHADEMA iliibua wazo la chama kuwasiliana na serikali ili kutafuta njia bora ya kupatikana kwa katiba mpya.

“Wazo hilo lilitoka ndani ya sekretarieti na Mheshimiwa Regia Mtema hakuwa mjumbe wa sektarieti. Yeye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC),” anasema mmoja wa viongozi wa CHADEMA.

“Sasa mtu ambaye hakuwa mjumbe na ambaye hakualikwa kwenye mkutano wa sekretarieti anawezaje kuibua hoja kwenye kikao ambacho hakuwapo,” alihoji kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Amesema, “Sisi tumeamua kukaa kimya kwa kuwa hatutaki kuonekana tunaongelea marehemu; lakini kwa kweli tumesikitishwa na kauli ya mwenzetu…”

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya Zitto, naibu katibu mkuu wa CHADEMA, kueleza kuwa wazo la kutaka uongozi wa juu wa chama hicho kukutana na Rais Kikwete lililetwa na Regia Mtema.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alinukuliwa akisema, baada ya viongozi wake kutafakari wazo la Regia walilikubali.

Amenukuliwa akisema ushauri wa Regia haukupata upinzani katika majadiliano kwenye kikao cha Kamati Kuu ambapo hoja nzito zilijengwa kuuimarisha baada ya wajumbe kuona kuwa ni ushauri muhimu unaofaa kufanyiwa kazi.

Wakati Zitto akinukuliwa hivyo, waraka ambao gazeti hili limenasa unaonyesha wazo la viongozi wa CHADEMA kupanga kukutana na serikali lilianzia kwenye sekretarieti ambako Regia hakuwa mjumbe.

Waraka huo wenye kurasa 10 uliandaliwa na ofisa mmoja katika idara ya utafiti na sera, ambaye aliingiza hoja ya viongozi wakuu wa CHADEMA kuomba kuwasiliana na serikali.

Nyaraka zinaonyesha ofisa huyo aliteuliwa na kikao cha sekretarieti cha 15 Novemba 2011 jijini Dar es Salaam kilichoitishwa kuandaa kile kilichoitwa, “Mapendekezo ya mkakati endelevu wa kutafuta haki nje ya Bunge.”

Aidha, ofisa huyo aliwasilisha waraka wenye mapendekezo ya kuundwa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu kwenye mkutano wa CC uliofanyika 29 Novemba 2011.

Kikao cha sekretarieti kilichompa jukumu ofisa huyo kuandaa mapendekezo ya “mkakati endelevu,” kilifanyika saa chache baada ya wabunge wa chama hicho kutoka nje ya ukumbi wa bunge Dodoma, kupinga utaratibu uliotumika kuwasilisha muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Kwa mujibu wa waraka wa CHADEMA, kwenye ukurasa wa nane, “Sekretarieti inapendekeza njia ya kwanza ya kupata suluhisho ni majadiliano.”

Waraka unasema, “Baada ya pande mbili hizi – CCM/serikali na CHADEMA kutofautiana kwa hoja, sekretarieti inaona ni busara Kamati Kuu iunde timu ya watu wachache wataalamu ambayo itakuwa na wajibu wa kuandaa hoja zote ambazo CHADEMA inapingana nazo na kuzipeleka serikalini.”

Shabaha ya kazi hiyo ilikuwa “…kuangalia mambo ambayo angalau tunaweza kukubaliana nayo na yale ambayo chama kinaweza kukubaliana kutokubaliana nayo.”

Waraka unasema mapambano ya aina ya mjadala yana faida kubwa tatu. Kwanza, yataondoa dhana kwamba CHADEMA wanalalamika bila kuleta maandishi rasmi.

Unasema Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwahi kupotosha taifa kwamba hadi wabunge wa chama hicho wanatoka bungeni, alikuwa hajajua hoja zao.

Unasema Makinda alinukuliwa akisema hata pale ambapo kiongozi wa upinzani, Freeman Mbowe alipokutana naye, hakumweleza hoja za msingi ambazo chama hicho kinazisimamia, jambo ambalo umeliita “…uzushi uliopitiliza.”

Pili, waraka unasema kwa kutumia njia ya mjadala, jamii ya kimataifa, wanaharakati na wananchi wengine wataona kwamba CHADEMA haikufunga milango ya majadiliano na kwamba, kama serikali itaziba masikio, basi malalamiko yote yataelekezwa kwake.

Tatu, waraka unaeleza, “Lengo la mpango huu ni kuweka kumbukumbu sahihi, kwamba CHADEMA ni chama makini na kipo tayari kushika dola.”

Inaelezwa katika ukurasa wa saba wa waraka kwamba mjadala juu ya muswada wa sheria uliendeshwa kwa ushabiki na upotoshaji mkubwa.

Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema, waziri wa sheria, Celina Kombani na Rais Kikwete mwenyewe, wanatajwa kuendesha mjadala “kwa ushabiki.”

Waraka unapendekeza “…sekretarieti ya chama itoe elimu ya uelewa wa muswada kupitia mfumo wa chama kikatiba wa makongamano, mikutano ya hadhara na vyombo vya habari.”

“Majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA zinaweza kupata dondoo za ukweli, lakini majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CCM na vyama vingine, wataendelea kupotoshwa na hivyo kupunguza uungwaji mkono wa hoja zetu,” umeeleza waraka.

“Serikali na chama chake wametumia muda mwingi bungeni na kwenye vyombo vya habari, kuijadili na kuisema CHADEMA, wabunge na viongozi wake,” unalalamika waraka.

“Hali hiyo itaendelea sasa na hivyo ni muhimu kutafuta njia nzuri ya kueleza ukweli wa jambo hili kwa Watanzania,” unaeleza waraka.

Kama serikali itashindwa kuwasikiliza, unasema waraka, “…kukaa na hata kukabiliana na timu ya wataalamu ya CHADEMA… tutakuwa tumepata fursa adhimu ya kuandaa mchakato wa katiba na hatimaye kupata katiba mpya itakayoshindanishwa na ile inayoandaliwa na serikali.”

Wakati sekretarieti inapendekeza yote hayo, Zitto alikuwa kwenye matibabu India na kikao cha CC ambamo ulisomwa waraka huu, kilifanyika siku mbili baada ya Zitto kuwasili.
 
Kila nikisikia Zitto namfananisha na Ismail Jussa kule Barza la wawakilishi.

Wote ni makini na wana hoja nzito sana na mara zote wanajipanga, kujiridhisha kabla kutoa hoja zao.

Hongereni sana
 
Ha ha ha hii ni JF ukileta za kuleta unapashwa mpaka basi zungumzia mambo ya muhimu kwa taifa letu sio watu huko tumetoka na hatutageuka nyuma mleta mada hovyooooooooooo
 
hoja yoyote huanza na mtu, kisha huingizwa kikaoni mwisho hutolewa maamuzi ya jumla ambayo tunaita maamuzi ya kikao halali, haijalishi nani alianzisha mada............. Mtamaliza visigino kufuatilia yasiyo wahusu, Hovyo.

428358_349718371729261_100000733047937_1110970_520880599_n.jpg

Nimeipenda sana hii PICHA ambayo inawakilisha na kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Eti bado kuna watu tunaishi katika nyumba hizi tena katika miji mikubwa Mfano DSM ambayo ni makao makuu ya Raisi wa Nji.

AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU.

TUKISEMA UKWELI......... ETI MNATUITA KUWA SISI NI CHADEMA!!!!!!!!!!!!!!!! KUMBE WALAAAAAH SISI NI WADANGANYIKA WALALAHOI!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
"Sasa mtu ambaye hakuwa mjumbe na ambaye hakualikwa kwenye mkutano wa sekretarieti anawezaje kuibua hoja kwenye kikao ambacho hakuwapo," alihoji kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Sasa hicho chanzo cha habari hii kama ni cha ukweli, KWA NINI ANAKATAA KUTAJWA HADHARANI JINA LAKE.

Ni habari ya ULONGO tu imetengenezwa kama walivyo fanya kesi ya kumpinga LEMA KULE ARUSHA. mashahidi wanajiumauma midomo.

Aangalie huyu naye asije kuwa kama wale wa Arusha!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Chadema ina watu wenye akili hawajadili watu wanajadili mada. Nyie endeleeni kujadili watu msishughulikie matatizo ya watz, jibu mtalipata 2015, vilaza wakubwa nyie.

Mlaaniwe kwa kuwahadaa watz kwa ajili ya matumbo yenu makubwa.

Viongozi ni nguzo muhimu katika jamii yoyote ile vikiwemo vyama vya siasa, kwa hiyo kujadili mstakabali wa ZITTO KABWE ndani ya CHADEMA si kuwahadaa viongozi...ni kweli kwamba wamemkana hadharani na penye ukweli tuwe tunakubali.
 
Kuna nchi walikuwa na Propaganda kama Urusi lakini ilifika mahala ikakatika vipande,CCM wenyewe wamefuta kitengo cha propaganda tunataka tuone nyie masalia katika nyakati hizi kama mutaweza kwa propaganda uchwara jipangani manake watanzania tumeamuka
 
Kuna jitihada kubwa za kuzua "migogoro ya 'kufikirika' ndani ya Chadema.Huo ni mwendelezo wa mafisadi na vibaraka wao kutapatapa baada ya hoja za UKABILA (UKANDA/UKASKAZINI) na ile ya UDINI kupuuzwa na Watanzania wengi wenye akili timamu.Sasa jitihada zimeelekezwa katika kuzua 'migogoro' isiyokuwepo na ****** mwingine kama huo.Kama hoja za ukanda na udini zilivyokufa kifo cha asili,hii ya uzushi wa migogoro feki nayo itajifia yenyewe.

Kosa la wazembe hawa ni kupuuza uwezo wa wanyonge kutambua nani yupo kwa maslahi yao na nani yupo dhidi ya maslahi yao.Priority ya mlalahoi kwa sasa sio kiongozi ni Mchaga au Mkristo bali atamkomboa vipi kutoka lindi la umsikini na ufisadi.
 
Chadema ina watu wenye akili hawajadili watu wanajadili mada. Nyie endeleeni kujadili watu msishughulikie matatizo ya watz, jibu mtalipata 2015, vilaza wakubwa nyie.

Mlaaniwe kwa kuwahadaa watz kwa ajili ya matumbo yenu makubwa.

haijawahi kutokea chadema ikawa na watu wabovu wabovu na ndio maana haina migogoro kwa hiyo usitegemee kuwagombanisha
 
mleta mada hajakosea kaleta mada mujadili sio kumtukana ushauri wa bure jamii forum sio ya chadema
 
Back
Top Bottom