Sokoine na Kolimba, vifo vyao vilimkera Mwalimu kiasi gani?


K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2009
Messages
352
Likes
1
Points
33
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2009
352 1 33
Wana JF naomba mchango wenu ili nielewe kuhusu harakati za kukabilina na wahujumu uchumi na reaction ya Mwalimu kuhusu vifi nyao.

Maswali ni haya:

1. Kama Sokoine na Kolimba walikuwa wanapinga ufisadi, je vifo vyao vilimkera kiasi gani Mwalimu?
2. Mwalimu alifanya nini kuakikisha kwamba vita vya kuhujumu uchumi (Sokoine) na mwelekeo wa chama unarudi kwenye mstakabili wake (Kolimba)?
Napata shida kuelewa kwanini vifo vya hawa ma gwiji wa uzalendo vinahusina na chama cha mapinduzi na wakati huo Mwalimu alikuwepo. Mwalimu alikua on the same page na hawa mashujaa wete kweli?
 
Companero

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Messages
5,497
Likes
224
Points
160
Companero

Companero

Platinum Member
Joined Jul 12, 2008
5,497 224 160
Kifo cha Sokoine kilimkera na kumtoa machozi Mwalimu!

Kolimba hakuwa kipenzi cha Mwalimu baada ya sakata la G55, rejea Kitabu cha Mwalimu cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
 
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2009
Messages
9,557
Likes
7,453
Points
280
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2009
9,557 7,453 280
Kifo cha Sokoine kilimkera na kumtoa machozi Mwalimu!

Kolimba hakuwa kipenzi cha Mwalimu baada ya sakata la G55, rejea Kitabu cha Mwalimu cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MKUU COMPANERO HESHIMA KWAKO
hivi unaweza kuwa na soft copy ya hicho kitabu, ukakiweka hapo ili tupate usia wa mzee kidogo?
 
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2009
Messages
3,383
Likes
140
Points
160
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2009
3,383 140 160
Kolimba tulimsurubu,
Na kusababisha ububu,
Ukweli kutohutubu,
Kauliye kuiharibu.

Hakustahili hukumu,
Wala kumshutumu,
Na kumfanya haramu,
Na kumrushia sumu

Ukweli aliusema,
CCM haina wema,
Imeipoteza neema,
Imeleta hujuma.

Imepoteza dira,
Kwa uongozi wa hira,
Imepitwa na majira,
Haina tena sura.

Mimi najiuliza,
Nani wa kunijuza,
Hivi kweli tunaweza,
Kuwaondoa hawa vilaza.

Mimi si mahoka,
CCM nimeichoka,
Nimeitupa kama taka,
Kuyaondoa mashaka.
 
Magulumangu

Magulumangu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
3,040
Likes
24
Points
135
Magulumangu

Magulumangu

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
3,040 24 135
nakuunga mkono,
bila hata ukono,
mwendo wa konokono,
CCJ ndo ngao yetu,


Wengi wao wanoko,
ng'ang'ania kama ukoko,
njoo kwetu kunako,
CCJ ndo ngao yetu,

Kwa baba tumefika,
machungu yetu kusikika,
hakuna kabisa unoko,
CCJ ndo ndao yetu,

Walimmwaga hata Kolimba,
Komba kaja kuimba,
hata Sokoine kamuimba,
CCJ ndo ngao yetu,

Njoo kusiko shobo,
Ya baba kwa mbali nembo,
Waijua hata Warembo,
CCJ ndo ngao yetu,

Nyaraka wanaiba,
kariakoo ndiko wamekomba,
wabakize kuimba,
CCJ ndio ngao yetu,

hapa ndo doti komu,
sitaki leta mabomu,
wao kama ma'lemu,
CCJ ndio ngao yetu,
 
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2009
Messages
3,383
Likes
140
Points
160
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2009
3,383 140 160
nakuunga mkono,
bila hata ukono,
mwendo wa konokono,
CCJ ndo ngao yetu,


Wengi wao wanoko,
ng'ang'ania kama ukoko,
njoo kwetu kunako,
CCJ ndo ngao yetu,.....
umo umo kama ulikwepo
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
nakuunga mkono,
bila hata ukono,
mwendo wa konokono,
CCJ ndo ngao yetu,


Wengi wao wanoko,
ng'ang'ania kama ukoko,
njoo kwetu kunako,
CCJ ndo ngao yetu,...
Nimeipenda sana hii!
 
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
KAMA kichwa cha habari cha makala hii kinavyojieleza kuwa namkumbuka aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hayati Horace Kolimba ambaye alifariki dunia mwaka 1997, ndipo ninapotaka kuelekeza hoja yangu ili kujadili hali ya kisiasa ya ndani ya chama hicho na mustakabali wake.
Swali la kujiuliza msomaji ni kwanini leo nasema namkumbuka Kolimba?

Namkumbuka Kolimba kwa sababu aliweza kuonyesha ushujaa wa kukiambia ukweli chama ambacho alikuwa Katibu Mkuu na kada wa ngazi ya juu, alithubutu kusema kile ambacho kilikuwa kikimkereketa kwenye nafsi yake kwa ajili ya kukinusuru chama.

Hayati Kolimba, alipata kukikosoa chama chake kwa kubainisha kuwa kimekosa dira na mwelekeo, kauli ambayo ilikiweka chama katika wakati mgumu, kauli kama hiyo hivi sasa imerudiwa kutiwa nakshi na aliyekuwa kada wa chama hicho na Mbunge wa jimbo la (Kishapu) Fred Mpendazoe.

Kwa wasiokumbuka historia, kwa ufupi Kolimba alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) na Waziri wa Mipango katika serikali ya awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Kauli ya Kolimba kuwa chama kimekosa dira na mwelekeo ilisababisha mtafaruku mkali kiasi cha kufanya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imuite kujieleza na baada ya kujieleza Kolimba alifikwa na mauti.

Ninamkumbuka Kolimba kwa sababu alikitumikia kwa muda mrefu chama hicho tawala enzi za uhai wake kwa lengo la kutaka kibadilike hasa kwa kuachana na mfumo mbaya wa uchaguzi wa viongozi ndani ya chama ambao unakiweka chama njia panda.

Kwa kiongozi wa nafasi yake kutamka kuwa chama hicho kimepoteza dira na mwelekeo ni dhahiri kauli hiyo ilikuwa chungu cha moto kwa chama hicho na kuweza kuwafungua macho Watanzania wengi ambao walikuwa hawajui undani wa yaliyomo ndani ya chama hicho tawala.

Wengi tunafahamu katibu mkuu wa chama ndiye mtendaji wa shughuli za kila siku akiwa na jukumu la kukiongoza chama kutimiza malengo yake,na inapofika mahala kunena maneno hayo si jambo la kubeza kwa sababu yeye ndiye mtu anayekijua chama kinagaubaga.

Katika nadharia ya kawaida katibu mkuu ndiye anayefahamu utaratibu wa kupata viongozi wa ndani ya chama kuanzia kwenye matawi hadi ngazi ya taifa na pia kujua taratibu na majukumu ya utendaji wa serikali kutokana unyeti wa nafasi yake.

Ni dhahiri Kolimba aliyanena haya akijua lile alilolisema litakuwa mwiba kwake, lakini akafanya hivyo pengine kwa kuzingatia kuwa ushauri wake aliokuwa akiutoa kwa viongozi wenzake ulikuwa haukubaliki na kuamua kuanika hadharani ukweli wa ndani ya chama ili wanachama na wananchi waweze kuamua hatima yake.

Naguswa na kauli ya Kolimba kwasababu ni sawa na baba ndani ya familia kuwaambia majirani mtoto wake ni mdokozi, katika akili ya kawaida ni lazima tuamini kuwa lililosemwa lina ukweli ndani yake na haliitaji kubezwa.

Kwanini kauli hiyo ya Kolimba haikulenga jumuiya yoyote ndani ya chama bali kukilenga chama chenyewe na hapo ndipo unapoona mpasuko uliokuwamo ndani ya chama ya wakati huo na hadi sasa.

Mfumo mbaya wa kuchagua viongozi ndani ya chama bila kuwahakiki kama ilivyokuwa wakati CCM ikiongozwa na Azimio la Arusha ndio unaondelea kukikagharimu chama hiki kuonekana kupoteza dira.

Tangu kuvurugwa kwa azimio la Arusha mwaka 1992 kule Zanzibar na kuacha siasa za taifa hili zikiendeshwa bila maadili na kanuni katika mambo mengi, hasa suala la fedha katika uchaguzi na kuendesha vyama vya siasa, CCM imejikuta ikikumbatia kila aina ya wanachama.

Kwa hoja hiyo ya kuacha wafanyabiashara kuvamia uongozi ndani ya chama hicho ndipo ninapoguswa na kauli nyingine iliyowahi kutolewa na kada mwingine wa chama hicho, Philip Mangula, kuwa itafika mahala uongozi ndani ya CCM utakuwa ukitolewa kwa njia ya zabuni.

Mangula ambaye alipokea kijiti cha ukatibu mkuu wa CCM kutoka kwa marehemu Kolimba, aliyanena haya wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa ambapo alikuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo lakini hakufanikiwa kushinda.

Si lengo la makala yangu kutonesha kidonda cha kauli za makada wa chama hicho bali na kujaribu kukumbusha viongozi wa chama kujitazama wapi wanakwenda.

CCM imefikia mahala hata kuwashawishi watu wengine kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kwa sababu ya nguvu ya fedha jambo ambalo ni hatari kwakuwa si wote watakaoingia katika mfumo huo watakuwa na sifa za uongozi.

Wagombea wa kipindi cha Azimio la Arusha walikuwa hawapimwi kwa uwezo wao binafsi katika kuongoza, isipokuwa kilichokuwa kinapimwa ni uanachama wao na ukaribu walionao kwa uongozi wa taifa na itikadi ya chama.

Inaweza kufikiriwa kwamba kuvunjika kwa kanuni na miiko ndani ya chama hiki kikongwe kumechangiwa zaidi na kuvamiwa na wafanyabiashara na hivyo dawa ya kurejeshwa kwa maadili au miiko hiyo ni kutenganisha siasa na biashara.

Lakini pia mvutano baina ya wabunge wa chama hiki na serikali yake unasababishwa na CCM yenyewekutoruhusu Demokrasia ichukue mkondo wake katika kuweka wazi masuala mbalimbali ya kitaifa.

Tumekuwa tukishuhudia chama hiki kwa kushirikiana serikali ikitunga sheria mbalimbali ambazo lengo lakeni kuvibana vyama vya upinzani na wapinzani waliopo nje na ndani ya chama hicho.

Nayasema haya nikikilenga chama kwa sababu kimekuwa kikiwabana wabunge na makada wake wasiikosoe serikali inayoongozwa na chama chao jambo ambalo katika ustawi wa demokrasia halina nafasi.

Katika hali ya kawaida ya kutaka kuwaweka kufuli wabunge wake imejikuta ikiumia hasa kwa kuibuka mgawanyiko baina ya makada wa chama hicho na wabunge wenyewe kwa wenyewe ambao mitizamo yao imekuwa ikinzania kiasi cha kufikia hatua ya kutisha.

Yanayoibuka leo kwa kada wa chama kutoa kauli ya kukishutumu kuwa kimekosa dira na mwelekeo ni dhahiri ina ukweli na wahusika wanapaswa waifanyie kazi badala ya kuanza kumbeza au kuangalia namna ya kumfunga mdomo.

Unapojaribu kumbana mwanadamu katika namna yoyote ile asiseme ukweli wa kuikosoa serikali yake ni lazima atatafuta pa kusemea kama ameona hana namna kubainisha lile linalomkereketa.

Hapa ndipo wanapoibuka kina Mpendazoe wakifuata nyayo za Horace Kolimba kwasababu chama kimegoma kujitazama pale kilipojikwaa ili kuweza kujirekebisha zaidi ya kutaka kuendelea na mfumo wa kutoambiana ukweli.

Hapa ndipo CCM ilipojisahau na haikutakiwa kumsimanga Mpendazoe zaidi ya kujitazama na kutafakari lile lililosemwa tena likiwa limetamkwa na kada wake wa ngazi juu na si kukurupuka kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kumbeza na kusema alikuwa mzigo.

Kwa kauli ya Mpendazoe ya kusema CCM imepoteza dira na mwelekeo hapa ndipo ninapomkumbuka Horace Kolimba kuwa kauli hiyo yeye ndiye alikuwa mwasisi wake lakini lengo likiwa ni kukiamsha chama ingawa ilikuwa ni fedheha kwa chama hicho.

Ni vyema CCM ikajitazama kwa jicho la pili kwanini kauli ya kupoteza dira na mwelekeo na inatolewa na makada wake wa ngazi juu na si watu wa kawaida au wapinzani wa chama hicho.
 
Mphamvu

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
10,712
Likes
1,015
Points
280
Mphamvu

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
10,712 1,015 280
Kwa mujibu wako, huyu bwana nikimfananisha na Makamba ni kifo na usingizi...
 
commonmwananchi

commonmwananchi

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
2,916
Likes
1,122
Points
280
commonmwananchi

commonmwananchi

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
2,916 1,122 280
Si Mpendazoe tu bali hata Butiku,Jaji Warioba na kwa ujumla ile ccm halisi.wako walioko ccm wakiwa mateka wa ccm makamanda.
hapa kuna mechi kali CCM makamanda V'S CCM makada,na refarii ni MAFISADI.Ukicheza rafu(kusema ukweli)unapigwa red card kama yaliyowakuta ma-striker mahiri Shelukindo na Selelii.
 
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
uchaguzi ujao kwa kamati kuu ya CCM kazi wanayo makundi hayo yote lazima zichapwe
Si Mpendazoe tu bali hata Butiku,Jaji Warioba na kwa ujumla ile ccm halisi.wako walioko ccm wakiwa mateka wa ccm makamanda.
hapa kuna mechi kali CCM makamanda V'S CCM makada,na refarii ni MAFISADI.Ukicheza rafu(kusema ukweli)unapigwa red card kama yaliyowakuta ma-striker mahiri Shelukindo na Selelii.
 
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2006
Messages
4,914
Likes
1,172
Points
280
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2006
4,914 1,172 280
Tunajadili mawazo ya marehemu kwani sisi tulio wazima leo hii hatuna tena mawazo? Akili zetu zimebadilishwa na mifumo ya Computer (Software)? Wewe mtoa mada ungesema CCM wamekwama wapi na nini wanatakiwa wafanye ili kujikwamua
 
L

Logician

Senior Member
Joined
Nov 5, 2010
Messages
175
Likes
6
Points
0
L

Logician

Senior Member
Joined Nov 5, 2010
175 6 0
Tunajadili mawazo ya marehemu kwani sisi tulio wazima leo hii hatuna tena mawazo? Akili zetu zimebadilishwa na mifumo ya Computer (Software)? Wewe mtoa mada ungesema CCM wamekwama wapi na nini wanatakiwa wafanye ili kujikwamua
!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????????

In explaining where you are we do not forget the past, in describing the future we can't forget where we are! along the way......

Don't react rather think positively to change the course!


God Bless Tanganyika
 
Lyimo

Lyimo

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,825
Likes
38
Points
145
Lyimo

Lyimo

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,825 38 145
This is one of the self-evidence why our leading party CCM is collapsing drastically. Is true that, the FISADI's and other business people has a big vote in the party mainly for their interest. This made the rulling party now/government to save for these people rather than the public. Another threat evidence is; Why excel/truthful/strong leaders that expected by the public are grouped to be enemies to this historical party? I am sure many limitations are well known by CCM members those with good will, but they dont have any ground to change the prevailing system ("Mafisadi wameshika Utamu"). If they will not force an internal revolution within the party, we will witnessed an historical shame fall of this sounded party.

Izwe letu..................
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,976
Likes
230
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,976 230 160
People????????????????????????????????? Power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
46
Points
0
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 46 0
.......Wewe mtoa mada ungesema CCM wamekwama wapi na nini wanatakiwa wafanye ili kujikwamua
Jibu Ni CCM wamekwama kwa kukosa dira na mwelekeo. Kwa sasa CCM kam cahama hakina dira vile vile hakina Priority ni mambo gani ya msingi na yapi si ya msingi.

Kila kitu kimegubikwa na siasa Mwanasia anapata mshahara na maslahi bora kuliko waendaji wengine muhimu.

Mfano 1.Mbunge anamzidi maslahi Mganga mkuu wa mkoa, RPC, Afisa Kilimo, Mhandisi mkuu wa mkoa Afisa Elimu wa mkoa, etc. Hivi mabadiliko ya kweli kwenye jamii yanaletwa na mbunge au afisa elimu? Ni mbunge au mganga mkuu. Hizi ni dalili za kukosa dira mwelekeo. CCM wanatengenza taifa la kisiasa na wanasisa na sio Kilimo kwanza kama wanavyosema kwenye makaratasi


Mfano 2.Mgao wa umeme.CCM kwenye hotuba wanasema ni changamoto. Hii sio tetemeko au tsunami kama ya japan inayokuja ghafla. Kududmu kwa mgao wa umeme kwa zaidi ya miaka 10 ni ishara tosha na kutokuwepo na dira.

CCM wanatakiwa kutofautsiha changamoto na failures. Wakubali mapungufu yao ndio wanaweza kwenda mbele zaidi ya tulipo sasa. Kila mwaka tunasikai kuna mgao sababu

  • kina kimepungua wakati wa kiangazi
  • bwawa limejaaa matope wakati wa masika
Sasa wataalamu wa hali ya hewa, mipango na sera, engineers kwenye idara mbali mbali wanotakiwa kuyaona mambo kabla hayajaleta madharan kazi wanayofanya ni nini. Changamoto ni mafuriko na matetemeko na sio mnago ualidumu kwa miaka 10

Viongozi wa kiisiasa na watendaji wa hawa wataaalam tuwaeleweje???

tatizo liko wapi . jibu short simple and clear ni Uogozi bora. na uongozi unatakiwa kutoa dira.

Haya kawaambie hao viongozi wajikwamue na mwazo yao mgando
 
M

mfuachuma

Member
Joined
Mar 9, 2011
Messages
18
Likes
0
Points
3
M

mfuachuma

Member
Joined Mar 9, 2011
18 0 3
Haa wewe wa wapi tena ndugu?
Hivi kweli huelewi umuhimu wa historia? Assumption zangu zilikua...yeyote anayeweza kugonga key-board ya computer bongo hii lazima awe amepitia somo la historia japo kwa kiwango cha primary school. Wew vipi tena? Nadhani hii platform imekuzidi kimo,tafuta nyingine basi itakayo kufaa au sio mwana?
Tunajadili mawazo ya marehemu kwani sisi tulio wazima leo hii hatuna tena mawazo? Akili zetu zimebadilishwa na mifumo ya Computer (Software)? Wewe mtoa mada ungesema CCM wamekwama wapi na nini wanatakiwa wafanye ili kujikwamua
 
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
mzee umewahi kusoma historia??
Tunajadili mawazo ya marehemu kwani sisi tulio wazima leo hii hatuna tena mawazo? Akili zetu zimebadilishwa na mifumo ya Computer (Software)? Wewe mtoa mada ungesema CCM wamekwama wapi na nini wanatakiwa wafanye ili kujikwamua
 
M

Matarese

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2009
Messages
523
Likes
15
Points
35
M

Matarese

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2009
523 15 35
KAMA kichwa cha habari cha makala hii kinavyojieleza kuwa namkumbuka aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hayati Horace Kolimba ambaye alifariki dunia mwaka 1997, ndipo ninapotaka kuelekeza hoja yangu ili kujadili hali ya kisiasa ya ndani ya chama hicho na mustakabali wake.
Swali la kujiuliza msomaji ni kwanini leo nasema namkumbuka Kolimba?

Namkumbuka Kolimba kwa sababu aliweza kuonyesha ushujaa wa kukiambia ukweli chama ambacho alikuwa Katibu Mkuu na kada wa ngazi ya juu, alithubutu kusema kile ambacho kilikuwa kikimkereketa kwenye nafsi yake kwa ajili ya kukinusuru chama.

Hayati Kolimba, alipata kukikosoa chama chake kwa kubainisha kuwa kimekosa dira na mwelekeo, kauli ambayo ilikiweka chama katika wakati mgumu, kauli kama hiyo hivi sasa imerudiwa kutiwa nakshi na aliyekuwa kada wa chama hicho na Mbunge wa jimbo la (Kishapu) Fred Mpendazoe.....
Weka rekodi sawa, Mangula alipokea toka kwa Mrehemu Gama sio Kolimba
 

Forum statistics

Threads 1,251,231
Members 481,615
Posts 29,763,388