Sokoine na Kolimba, vifo vyao vilimkera Mwalimu kiasi gani?

Kuna nchi walikuwa na Propaganda kama Urusi lakini ilifika mahala ikakatika vipande,CCM wenyewe wamefuta kitengo cha propaganda tunataka tuone nyie masalia katika nyakati hizi kama mutaweza kwa propaganda uchwara jipangani manake watanzania tumeamuka

Source : Froida
 
Huyu alikua katibu mkuu wa CCM. Mwanachama mwadilifu na msema kweli. Siku za mwisho za uhai wake alidiriki kusema waziwazi kua CCM haina dira wala mwelekeo na pia alikua tayari kukihama chama na kua mpinzani. Lakini baada ya kauli yake hiyo haukupita muda mrefu akapatwa na umauti katika mazingira ya kutatanisha. Kwa maelezo haya machache najiuliza maswali yafuatayo na naomba kwa yeyote mwenye kujua anisaidie kunielimisha:

1. Kwa nini watu wanaokipa changamoto chama (na serikali) hupoteza uhai wao?

2. Ni lini raia wa kawaida ataweza kupaza sauti yake bila kukumbwa na mkondo huu (kifo)?

3. (Kwa anaejua) kifo cha komba kilitokea vipi na kwa nini?

Mwisho natanguliza samahani kwa atakayekwazika maana nataka kujifunza ili niujue mfumo wetu wa kiuongozi na kiutawala. Asanteni, nawasilisha.
 
Wewe unaonekana ni mtu wa hovyo sana.Unachokijua ni kuandika ****** kila siku kuhusu CDM na Zitto.Watu tumechoka na habari zako za udaku.Mara ulete matusi yako kuhusu Mbowe na Slaa,mara ulete mambo ya kipuuzi kuhusu mgombea wa CDM jimbo la kibaha na sasa unaendeleza umbea wako usio na msingi.Kama unadhani CDM ni wajinga kama wewe unajidanganya sana.Endelea kuropoka lakini mwisho wako na ******* wenzako unakaribia sana.Stay tuned!

kwanini mnatumia nguvu nyingi sana kujaribu kushut down mijadala yoyote kuhusu chama cha kususa na kuandamana,kuna nini hapa hamtaki kijulikane kwani?halafu mgombea wa jimbo la kibaha ni nani huyo na kwa uchaguzi upi labda?
 
we umetumwa na ndo maana hamjadili kero za watu na jinsi ya kuzitatua badala yake mnajadili watu na kupiga umbeya usio na msingi!yapo mengi sana ya kushare na jamii lakini unaleta unafuiki wako wa kuchonganisha watu!ccm imekufa kabisaaaaaaaa unafanya nini ili ifufuke sio umbeya tuuuuuuuuu! f*ra mkubwa wewe!cdm ina watu wanaojua chama kinafanya nini?kiantakiwa kufanya nini, na nani atafanya nini sio ******* yameuza nchi yote na ubafiki mkubwa wenu mkijilimbikizia mali za nchi!ole wenu make mwisho wenu u karibu sana!snztyp!!!!!!!!!!!!!!!!!!

jamani hiyo kauli si imetoka jikoni lakini?tatizo nyie chadema yenu mnaifanyia kwenye kata hamko jikoni,nyie wote ni chadema kata ndio mana hamtaki kujadili kauli mnanijadili mimi tarishi..
 
Ha ha ha hii ni JF ukileta za kuleta unapashwa mpaka basi zungumzia mambo ya muhimu kwa taifa letu sio watu huko tumetoka na hatutageuka nyuma mleta mada hovyooooooooooo
mambo muhimu kwenu ni kufeli kwa mtoto wa mwenyekiti wa ccm taifa si ndio mnayoyapenda au sio mzee?
 
kwanini mnatumia nguvu nyingi sana kujaribu kushut down mijadala yoyote kuhusu chama cha kususa na kuandamana,kuna nini hapa hamtaki kijulikane kwani?halafu mgombea wa jimbo la kibaha ni nani huyo na kwa uchaguzi upi labda?

Shut up!
 
jamani hiyo kauli si imetoka jikoni lakini?tatizo nyie chadema yenu mnaifanyia kwenye kata hamko jikoni,nyie wote ni chadema kata ndio mana hamtaki kujadili kauli mnanijadili mimi tarishi..

Huna hata sifa ya kuwa tarishi.
 
Basi chadema ni untouchable humu jf,na hapo ndio hamjashika dola je mkishika dola mtakua na simile na watu wenye mawazo tofauti na yenu kweli nyie?ndio wananchi wanakiogopa chama chenu kutokana na kutawaliwa na ubabe ikiwemo kumwagia tindikali usoni wasiokubaliana nyie...

[h=3]KADA WA CCM ALIYEMWAGIWA TINDIKALI NA WAFUASI WATIIFU WA CHADEMA IGUNGA AREJEA NCHINI KUTOKA INDIA BAADA YA MATIBABU YALIYOGHARAMIWA NA CCM..[/h]
1.jpg

MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha aliyekuwa nchini India kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na wafuasi watiifu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADAEMA), wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo (Igunga) mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, baada ya kurejea nchini. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni humo.
 
mambo muhimu kwenu ni kufeli kwa mtoto wa mwenyekiti wa ccm taifa si ndio mnayoyapenda au sio mzee?
*Kufeli kwa mtoto wa first lady, ambaye proffesional yake ni ualimu.
*kufeli kwa mtoto ambaye baba yake ni Rais wa nchi.
Hiyo kwako unalioma jambo linalopaswa kunyamaziwa? Bali unaona ya zitto kabwe ndio habari kwako,Umetumwa na NANI.....?
 
Mimi nawapenda CCM ,imeshehena watu makini zaidi ya vyama vyote!!!!!!!!!!!!!! kasoro zilizopo naamini zitatatuliwa kidemokrasia....hata wale mafisadi watakubali kuambiwa ukweli na kukaa pembeni kama alivyofanya ROSTAM AZIZ bila kuharibu misingi yake!!!!!!!!!!!!!!!!! Pia nitagombea UBUNGE mwaka 2015 kuongeza nguvu na kuimarisha uchumi wa TAIFA langu.....Tunajenga CCM ya VIJANA ambao wataendana na kasi ya mabadiliko ya kitechnolojia na mfumo wa siasa za kisasa zaidi!!!!!!!!!!!!!!!!
 
*Kufeli kwa mtoto wa first lady, ambaye proffesional yake ni ualimu.
*kufeli kwa mtoto ambaye baba yake ni Rais wa nchi.
Hiyo kwako unalioma jambo linalopaswa kunyamaziwa? Bali unaona ya zitto kabwe ndio habari kwako,Umetumwa na NANI.....?
La hasha si la kunyamaziwa bali yote yapewe uzito unaostahili tu ndio ombi langu,yule mtoto kufeli ni kielelezo tosha kwamba babake hashiriki mchezo mchafu wa wizi wa mitihani kama watz wengi walivyozoea mtoto wa mkubwa huwa hafeli..
 
Basi chadema ni untouchable humu jf,na hapo ndio hamjashika dola je mkishika dola mtakua na simile na watu wenye mawazo tofauti na yenu kweli nyie?ndio wananchi wanakiogopa chama chenu kutokana na kutawaliwa na ubabe ikiwemo kumwagia tindikali usoni wasiokubaliana nyie...

[h=3]KADA WA CCM ALIYEMWAGIWA TINDIKALI NA WAFUASI WATIIFU WA CHADEMA IGUNGA AREJEA NCHINI KUTOKA INDIA BAADA YA MATIBABU YALIYOGHARAMIWA NA CCM..[/h]
1.jpg

MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha aliyekuwa nchini India kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na wafuasi watiifu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADAEMA), wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo (Igunga) mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, baada ya kurejea nchini. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni humo.
Kwanza nampa pole nyingi ndugu yetu huyu na kumtakia maendeleo mema kiafya.mungu amsaide ili aweze kurudi katika siha njema kama awali.

*Mkuu unapaswa kuheshimu mahakama,huna uthibitisho wa tuhuma hizi, na mpaka sasa bado jambo hili liko mlkononi mwa vyombo husika vya dola kwa uchunguzi kamili.hivyo hizi ni tuhuma tu,
Kama ubabe uko kwenu ccm ambao mnapanda kwenye majukwaa na bastola vibindoni mfano halisi ni mh,Rage.
Mnawafokea waheshimiwa bungeni bila heshima nas kuwaambia "wametumwa" mfano halisi
Ni Mh omar nundu, waziri wa uchukuzi.
 
Katika kuonyesha kwamba hali si shwari sana ndani ya chadema kumekuwa na sintofahamu za hapa na pale kuhusu mbunge kijana machachari zitto kabwe ambapo safari hii tena ile Kauli yake kwamba wazo la chama chake kumuona Rais Jakaya Kikwete juu ya mabadiliko ya sheria ya katiba mpya lilitolewa na Regia Mtema, imepingwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, wazo hilo la kuzungumza na serikali na hata kumuona rais, lilitolewa na sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mara baada ya kifo cha Regia, tarehe 14 Januari mwaka huu, Zitto aliviambia vyombo vya habari kuwa ni yeye (Regia) aliyetoa wazo hilo kwenye kikao cha viongozi wakuu wa chama wakiwemo wabunge.

Regia ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum, alikutwa na mauti kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Ruvu mkoani Pwani. Lakini Zitto akizungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu alisisitiza, “…wazo hilo lilitolewa na Regia.”

Taarifa ya chama hicho inasema, sekretarieti ya CHADEMA iliibua wazo la chama kuwasiliana na serikali ili kutafuta njia bora ya kupatikana kwa katiba mpya.

“Wazo hilo lilitoka ndani ya sekretarieti na Mheshimiwa Regia Mtema hakuwa mjumbe wa sektarieti. Yeye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC),” anasema mmoja wa viongozi wa CHADEMA.

“Sasa mtu ambaye hakuwa mjumbe na ambaye hakualikwa kwenye mkutano wa sekretarieti anawezaje kuibua hoja kwenye kikao ambacho hakuwapo,” alihoji kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Amesema, “Sisi tumeamua kukaa kimya kwa kuwa hatutaki kuonekana tunaongelea marehemu; lakini kwa kweli tumesikitishwa na kauli ya mwenzetu…”

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya Zitto, naibu katibu mkuu wa CHADEMA, kueleza kuwa wazo la kutaka uongozi wa juu wa chama hicho kukutana na Rais Kikwete lililetwa na Regia Mtema.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alinukuliwa akisema, baada ya viongozi wake kutafakari wazo la Regia walilikubali.

Amenukuliwa akisema ushauri wa Regia haukupata upinzani katika majadiliano kwenye kikao cha Kamati Kuu ambapo hoja nzito zilijengwa kuuimarisha baada ya wajumbe kuona kuwa ni ushauri muhimu unaofaa kufanyiwa kazi.

Wakati Zitto akinukuliwa hivyo, waraka ambao gazeti hili limenasa unaonyesha wazo la viongozi wa CHADEMA kupanga kukutana na serikali lilianzia kwenye sekretarieti ambako Regia hakuwa mjumbe.

Waraka huo wenye kurasa 10 uliandaliwa na ofisa mmoja katika idara ya utafiti na sera, ambaye aliingiza hoja ya viongozi wakuu wa CHADEMA kuomba kuwasiliana na serikali.

Nyaraka zinaonyesha ofisa huyo aliteuliwa na kikao cha sekretarieti cha 15 Novemba 2011 jijini Dar es Salaam kilichoitishwa kuandaa kile kilichoitwa, “Mapendekezo ya mkakati endelevu wa kutafuta haki nje ya Bunge.”

Aidha, ofisa huyo aliwasilisha waraka wenye mapendekezo ya kuundwa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu kwenye mkutano wa CC uliofanyika 29 Novemba 2011.

Kikao cha sekretarieti kilichompa jukumu ofisa huyo kuandaa mapendekezo ya “mkakati endelevu,” kilifanyika saa chache baada ya wabunge wa chama hicho kutoka nje ya ukumbi wa bunge Dodoma, kupinga utaratibu uliotumika kuwasilisha muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Kwa mujibu wa waraka wa CHADEMA, kwenye ukurasa wa nane, “Sekretarieti inapendekeza njia ya kwanza ya kupata suluhisho ni majadiliano.”

Waraka unasema, “Baada ya pande mbili hizi – CCM/serikali na CHADEMA kutofautiana kwa hoja, sekretarieti inaona ni busara Kamati Kuu iunde timu ya watu wachache wataalamu ambayo itakuwa na wajibu wa kuandaa hoja zote ambazo CHADEMA inapingana nazo na kuzipeleka serikalini.”

Shabaha ya kazi hiyo ilikuwa “…kuangalia mambo ambayo angalau tunaweza kukubaliana nayo na yale ambayo chama kinaweza kukubaliana kutokubaliana nayo.”

Waraka unasema mapambano ya aina ya mjadala yana faida kubwa tatu. Kwanza, yataondoa dhana kwamba CHADEMA wanalalamika bila kuleta maandishi rasmi.

Unasema Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwahi kupotosha taifa kwamba hadi wabunge wa chama hicho wanatoka bungeni, alikuwa hajajua hoja zao.

Unasema Makinda alinukuliwa akisema hata pale ambapo kiongozi wa upinzani, Freeman Mbowe alipokutana naye, hakumweleza hoja za msingi ambazo chama hicho kinazisimamia, jambo ambalo umeliita “…uzushi uliopitiliza.”

Pili, waraka unasema kwa kutumia njia ya mjadala, jamii ya kimataifa, wanaharakati na wananchi wengine wataona kwamba CHADEMA haikufunga milango ya majadiliano na kwamba, kama serikali itaziba masikio, basi malalamiko yote yataelekezwa kwake.

Tatu, waraka unaeleza, “Lengo la mpango huu ni kuweka kumbukumbu sahihi, kwamba CHADEMA ni chama makini na kipo tayari kushika dola.”

Inaelezwa katika ukurasa wa saba wa waraka kwamba mjadala juu ya muswada wa sheria uliendeshwa kwa ushabiki na upotoshaji mkubwa.

Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema, waziri wa sheria, Celina Kombani na Rais Kikwete mwenyewe, wanatajwa kuendesha mjadala “kwa ushabiki.”

Waraka unapendekeza “…sekretarieti ya chama itoe elimu ya uelewa wa muswada kupitia mfumo wa chama kikatiba wa makongamano, mikutano ya hadhara na vyombo vya habari.”

“Majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA zinaweza kupata dondoo za ukweli, lakini majimbo na halmashauri zinazoongozwa na CCM na vyama vingine, wataendelea kupotoshwa na hivyo kupunguza uungwaji mkono wa hoja zetu,” umeeleza waraka.

“Serikali na chama chake wametumia muda mwingi bungeni na kwenye vyombo vya habari, kuijadili na kuisema CHADEMA, wabunge na viongozi wake,” unalalamika waraka.

“Hali hiyo itaendelea sasa na hivyo ni muhimu kutafuta njia nzuri ya kueleza ukweli wa jambo hili kwa Watanzania,” unaeleza waraka.

Kama serikali itashindwa kuwasikiliza, unasema waraka, “…kukaa na hata kukabiliana na timu ya wataalamu ya CHADEMA… tutakuwa tumepata fursa adhimu ya kuandaa mchakato wa katiba na hatimaye kupata katiba mpya itakayoshindanishwa na ile inayoandaliwa na serikali.”

Wakati sekretarieti inapendekeza yote hayo, Zitto alikuwa kwenye matibabu India na kikao cha CC ambamo ulisomwa waraka huu, kilifanyika siku mbili baada ya Zitto kuwasili.

You aree OFF TRUCK. Taarifa zako hazina ukweli wowote.
 
Kwanza nampa pole nyingi ndugu yetu huyu na kumtakia maendeleo mema kiafya.mungu amsaide ili aweze kurudi katika siha njema kama awali.

*Mkuu unapaswa kuheshimu mahakama,huna uthibitisho wa tuhuma hizi, na mpaka sasa bado jambo hili liko mlkononi mwa vyombo husika vya dola kwa uchunguzi kamili.hivyo hizi ni tuhuma tu,
Kama ubabe uko kwenu ccm ambao mnapanda kwenye majukwaa na bastola vibindoni mfano halisi ni mh,Rage.
Mnawafokea waheshimiwa bungeni bila heshima nas kuwaambia "wametumwa" mfano halisi
Ni Mh omar nundu, waziri wa uchukuzi.

suala mbona liko wazi hata mhusika mwenyewe alitamka wazi kwamba wafuasi watiifu wa chadema ndio waliommwagia tindikali usoni na kumtia ulemavu unadhani kwa nini hakuwataja nccr mageuzi?ina maana wewe unajua kuliko yeye alieumia wakati hukuwepo hata eneo la tukio..msirudie tena mambo haya ya kipuuzi huko arumeru,muwaonye wafusi wenu nasikia wamepania kufanya vurugu huko
 
Kazi unayofanya ni ngumu sana.Kupika majungu na fitna sio mchezo
 
Back
Top Bottom