Soko maarufu la Samunge jijini Arusha laungua kwa moto

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,749
2,437
Wakuu muda huu SOKO MAARUFU la SAMUNGE JIJINI hapa LINAUNGUA Moto. Serikali imeimarishwa ulinzi na fire wanajitahidi kuuzima Moto huu. Tuwaombee wafanyabiashara maana hasara inaweza kuwa kubwa sana.

-----
Soko Maarufu la Samunge lililopo katika jijini la Arusha Limeungua vibaya na kuteketeza bidhaa mbalimbali za mamilioni ya fedha huku mfanyabiashara mmoja akifariki dunia kwa mshtuko baada ya kushuhudia mali zake zikiwemo Friji zikiteketea .

Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao ,vibanda vilivyoteketea ni zaidi ya 1000 vya wafanyabiashara mbalimbali vilivyokuwa vimejengwa kwa mabati,Mbao na Maturubai huku mamia ya wafanyabiashara wengi wao wakiwa wanawake wakiangua kilio wasijue cha kufanya.

Akizungumzia tukio hilo kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa Mara baada ya kutembekea Soko hilo,Koka Moita alisema kuwa moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana ulizuka Jana majira ya SAA 5.30 usiku na kuteketeza vibanda vyote huku thamani ya Mali zilizoteketea ikiwa bado haijafahamika.

Alisema kuwa Jeshi la zima moto na uwokozi waliweza kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto huo Leo majira ya asubuhi uliokuwa umetekezeka takribani vibanda vyote.

Kaimu kamanda alisema kuwa katika tukio hilo hapakuwepo na madhara kwa binadamu kujeruhiwa na moto ila mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina la James Temba, (57) aliweza kufariki dunia kwa mshtuko Mara baada ya kukuta vibanda vyake viwili vikiteketea kwa moto.

Alisema kuwa marehemu Temba mkazi wa Moshono alifika katika Soko hilo baada ya kupata taarifa ya moto katika Soko hilo ndipo alipokuta vibanda vyake vimeteketea ambapo alianguka chini kwa mshtuko na kuzimia.

Marehemu alipelekwa katika hospital ya Mount Meru kwa ajili na matibabu lakini alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu ya kuokoa Maisha Yale na mwili wake umehifadhiwa katika hospital hiyo kusubiri uchunguzi wa daktari na ndugu wa marehemu.

"Natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona majanga kama haya ya moto kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kudhibiti matukio kwa haraka kabla ya kuleta madhara makubwa" Alisema Moita

Aidha aliwaomba wananchi pamoja na wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vikifanya
uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

Naye Mkuu wa wiallaya ya Arusha ,Gabriel Gaqaro ambaye alifika eneo hilo,aliwataka wananchi na wamiliki wa vibanda hivyo kuwa watulivu wakati mamlaka husika wakifanya tathimini ya bidhaa zilizoteketea.

Soko hilo limekuwa Maarufu kwa wafanyabiashara wakati na wadogo kufanyabiashara zao huku wengi wao wakijenga vibanda kwa kutumia mabati Turubai na Mabanzi jambo ambalo ni hatari pindi kunapotokea moto
 
Back
Top Bottom