Soko la waliosoma sheria (LLB)

F

Faymario

Member
Joined
Aug 11, 2011
Messages
23
Likes
0
Points
0
F

Faymario

Member
Joined Aug 11, 2011
23 0 0
jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
 
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Messages
4,892
Likes
1,475
Points
280
Age
28
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2011
4,892 1,475 280
hakuna course bora kuliko nyingine..cha msingi utoke na GPA nzuri. Thats it.
 
Perry

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Messages
10,033
Likes
914
Points
280
Perry

Perry

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2011
10,033 914 280
We kasome 2 uje 2sugue wote benchi huku kitaa...
 
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Messages
3,259
Likes
197
Points
160
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2009
3,259 197 160
We kasome 2 uje 2sugue wote benchi huku kitaa...
Kusugua benchi wakati una shahada ya sheria ni kiashiria cha kutokomaa kwako kisheria kwa vitendo. kuwa mwanasheria sio lazima uajiriwe mahakamani, kwenye ofisi za mashirika, kwa mwanasheria wa serikali etc. Elimu ya sheria uliyonayounaweza kuitumia kwa faida yako na mamalioni ya watanzania ambao huduma za sheria kwao ni kama mbingu na nchi.

Unaweza kuwa paralegal, unaweza kuanzisha NGO za kuelimisha mamia ya raia haki zao za ardhi, mikataba, uraia etc, kuna mashirika mengi tu yanaweza kutoa funds ukiingia kwenye njia hiyo.

Usifikirie sana kufanya kazi au kuajiriwa kwenye ofisi za wanaosheria zinavuma haitakuwa kwako kufanikiwa.
 
LordJustice1

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Messages
2,264
Likes
12
Points
0
LordJustice1

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2011
2,264 12 0
Kusugua benchi wakati una shahada ya sheria ni kiashiria cha kutokomaa kwako kisheria kwa vitendo. kuwa mwanasheria sio lazima uajiriwe mahakamani, kwenye ofisi za mashirika, kwa mwanasheria wa serikali etc. Elimu ya sheria uliyonayounaweza kuitumia kwa faida yako na mamalioni ya watanzania ambao huduma za sheria kwao ni kama mbingu na nchi.

Unaweza kuwa paralegal, unaweza kuanzisha NGO za kuelimisha mamia ya raia haki zao za ardhi, mikataba, uraia etc, kuna mashirika mengi tu yanaweza kutoa funds ukiingia kwenye njia hiyo.

Usifikirie sana kufanya kazi au kuajiriwa kwenye ofisi za wanaosheria zinavuma haitakuwa kwako kufanikiwa.
Kweli kabisa, mfundishe mtu kuvua samaki itamsaidia milele badala ya kumpatia samaki ambaye atamla kwa siku moja kisha akarudi tena kesho yake kuomba samaki!
 
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Messages
3,259
Likes
197
Points
160
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2009
3,259 197 160
Kweli kabisa, mfundishe mtu kuvua samaki itamsaidia milele badala ya kumpatia samaki ambaye atamla kwa siku moja kisha akarudi tena kesho yake kuomba samaki!
Na vyuo vinavyotoa shahada za sheria vianze kuweka mitaala ya kuwafanya wanafunzi wajione sio lazima waishie kwenye Law firms kubwakubwa
 
Bambanza jr.

Bambanza jr.

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2011
Messages
356
Likes
0
Points
0
Bambanza jr.

Bambanza jr.

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2011
356 0 0
Mie ndo nme2piwa LLB MZUMBE lakn mkopo NO LOAN!
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
80,852
Likes
46,335
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
80,852 46,335 280
Unaweza kuwa paralegal, unaweza kuanzisha NGO za kuelimisha mamia ya raia haki zao za ardhi, mikataba, uraia etc, kuna mashirika mengi tu yanaweza kutoa funds ukiingia kwenye njia hiyo.
Duh! Yaani uwe paralegal huku una LLB? Aisee.....no wonder why.......
 
mikatabafeki

mikatabafeki

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
12,827
Likes
2,112
Points
280
mikatabafeki

mikatabafeki

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
12,827 2,112 280
Mie ndo nme2piwa LLB MZUMBE lakn mkopo NO LOAN!
usiogope mdogo wangu waambie nyumbani wakulipie ada then chakula ntakuwekea bili kwa CHACHA au DADA GIFTI,stationery utaenda pale KYUNGU napo ntwaweka bili,bia utakunywa GREEN au kwa BAUNSA, watto wazuri pale MATOLA na NYERERE hall
 
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Messages
3,259
Likes
197
Points
160
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2009
3,259 197 160
Duh! Yaani uwe paralegal huku una LLB? Aisee.....no wonder why.......
Ungejua idadi ya wenye LLB walio barabarani usingeshangaa ndugu yangu. Idadi ya wanafunzi wanaomaliza LLB kwa mwaka hailingani kabisa na soko la ajira katika fani hiyo.

Mfano wa haraka :

university of Dar es salaam 200
Mzumbe Morogoro Campus 400
Mzumbe Mbeya Campus 100
Tumaini DSM 300
Tumaini Iringa 200
Makumira 100
Ruaha University Mwanza 200
Ruaha University Iringa 200
Sebastian Kolowa Lushoto 50
Zanzibar University 50
University of Dodoma 300
Open University of Tanzania 200
Total 2,300

Wahitimu kutoka vyo vya nje India, marekani uganda kenya etc wanafika 2600, namba hiyo utawaweka wapi wote hawa
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
80,852
Likes
46,335
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
80,852 46,335 280
Ungejua idadi ya wenye LLB walio barabarani usingeshangaa ndugu yangu. Idadi ya wanafunzi wanaomaliza LLB kwa mwaka hailingani kabisa na soko la ajira katika fani hiyo.

Mfano wa haraka :

university of Dar es salaam 200
Mzumbe Morogoro Campus 400
Mzumbe Mbeya Campus 100
Tumaini DSM 300
Tumaini Iringa 200
Makumira 100
Ruaha University Mwanza 200
Ruaha University Iringa 200
Sebastian Kolowa Lushoto 50
Zanzibar University 50
University of Dodoma 300
Open University of Tanzania 200
Total 2,300

Wahitimu kutoka vyo vya nje India, marekani uganda kenya etc wanafika 2600, namba hiyo utawaweka wapi wote hawa
Hapo sasa nimekupata mkuu. Ni bora mara mia uwe na LLB halafu uwe paralegal kuliko kuwa nayo halafu usiwe na ajira kabisa.

Marekani nadhani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na ma lawyer wengi hapa duniani. Yaani huwezi amini idadi yao. Idadi hiyo kubwa ndiyo inayosabisha watu wai despise hii fani kwa sababu soko la ajira limekuwa over saturated kiasi kwamba wengi wao wanaishia kuwa matapeli tapeli.

Kwenye county courthouses kwa mfano, utawakuta wamejazana lundo wakisubiri dei waka. Wanavizia watu wenye kesi zao walioenda kusomewa mashitaka/ mashauri yao. Wakikuona tu uko peke yako bila counsel...hao wanaanza kukuzonga na kukupa vi business cards vyao na kukuomba contact particulars zako. Wanatia aibu kwa kweli.
 
Kijuche

Kijuche

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2010
Messages
419
Likes
2
Points
35
Kijuche

Kijuche

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2010
419 2 35
hakuna course bora kuliko nyingine..cha msingi utoke na GPA nzuri. Thats it.
Unaweza kuwa na GPA nzuri lakini je, unajua nini kuhusu kile ulichokisomea hasa linapokuja suala la ajira?
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,741
Likes
2,024
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,741 2,024 280
I supposed kila kitu kinakwenda sawasawa, hakuna jibu rahisi kwenye swali lako
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,216
Likes
30,059
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,216 30,059 280
jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
Faymario, kama unataka kusoma LL.B ili kupata ajira haraka, uko kwenye wrong professional. Nilidhani wewe ni mkureketwa wa haki, hivyo unasoma ili kuwasaidia Watanzania kupata haki zao!, kumbe wewe unaitafuta LL.B ili uajiriwe?.

Nakupa angalizo moja tuu, kusoma LL.B ni kitu kimoja, kupata ajira kwa haraka ni kitu kingine, na kufanikiwa kimaisha kama mwanasheria nacho ni kitu kingine.

Kwa vile wewe lengo lako ni ajira, piga GPA kubwa ili ubaki hapo hapo chuo, au law firms zikugombanie. Kufanikiwa kama mwanasheria ni juhudi zako binafsi na kichwa chako jinsi ya kutafsiri sheria.
 
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Messages
3,061
Likes
395
Points
180
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2008
3,061 395 180
jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
Mimi nadhani kulingana na idadi ya wati inavyozidi kuongezeka na changamoto zinavyozidi kuongezeka ndivyo mahitaji pia yanavyozidi kuongezeka. Ukisikia watu wenye matatizo ya kisheria yanazidi idadi ya wahitimu kila mwaka. Hapa Tanzania tuna mahitaji mengi yanayohitaji wanasheria kuliko idadi ya watu waliopo. Hivyo, kama ni changamoto ya ajira hiyo ni kwa kila fani siyo sheria tu. Na hata kama ajira hi haba, haina maana kuwa ukihitimu na kuwa mwanasheria basi utakosa ajira.

Chukulia katika eneo la biashara kuna wanaofirisika na kuna wanaokuwa matajiri. Katika maisha ya ndoa, kuna wale ambao ndoa zao zinavunjika na kuna wanaoa au kuolewa. Hivyo, kwa mtazamo wangu hakuna mtu ambaye yuko kwenye loss. Kinachotakiwa ni competency. Mwanasheria mzuri na mwadilifu hata kama kuna tatizo la ajira yeye anakuwa marketable.

Si ulishaona mtu anauza duka na bidhaa zote kwa vile anadhani hakuna wateja na kwenda kufungua sehemu nyingine na wakati huohuo mtu mwingine anayenunua duka na bidhaa hizo yeye anapata wateja? Hivi ndivyo life ilivyo. Kama una kipaji cha kuwa mwanasheria - unapenda kuwa mwanasheria na unaweza kuwa mwanasheria mzuri, piga moyo konde, the future will unfold for you!
 
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Messages
3,259
Likes
197
Points
160
Ngambo Ngali

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2009
3,259 197 160
Mimi nadhani kulingana na idadi ya wati inavyozidi kuongezeka na changamoto zinavyozidi kuongezeka ndivyo mahitaji pia yanavyozidi kuongezeka. Ukisikia watu wenye matatizo ya kisheria yanazidi idadi ya wahitimu kila mwaka. Hapa Tanzania tuna mahitaji mengi yanayohitaji wanasheria kuliko idadi ya watu waliopo. Hivyo, kama ni changamoto ya ajira hiyo ni kwa kila fani siyo sheria tu. Na hata kama ajira hi haba, haina maana kuwa ukihitimu na kuwa mwanasheria basi utakosa ajira.

Chukulia katika eneo la biashara kuna wanaofirisika na kuna wanaokuwa matajiri. Katika maisha ya ndoa, kuna wale ambao ndoa zao zinavunjika na kuna wanaoa au kuolewa. Hivyo, kwa mtazamo wangu hakuna mtu ambaye yuko kwenye loss. Kinachotakiwa ni competency. Mwanasheria mzuri na mwadilifu hata kama kuna tatizo la ajira yeye anakuwa marketable. Si ulishaona mtu anauza duka na bidhaa zote kwa vile anadhani hakuna wateja na kwenda kufungua sehemu nyingine na wakati huohuo mtu mwingine anayenunua duka na bidhaa hizo yeye anapata wateja? Hivi ndivyo life ilivyo. Kama una kipaji cha kuwa mwanasheria - unapenda kuwa mwanasheria na unaweza kuwa mwanasheria mzuri, piga moyo konde, the future will unfold for you!

Fanya utafiti kwanza, nenda Kisutu ona aina ya watu na aina ya kesi za jina na madai ni tofauti kabisa na kesi zilizopo Mahakama ya kinondoni na Temeke. Vilevile mahakama kuu kesi zilizopo kanda ya Sumbawanga haziwezi kuwa sawa hatakidogo na kesi zilizopo dar es salaam. Katika mifano hiyo miwili Kanda ya DSM na Mahakama ya Kisutu ziko tofauti sababu kubwa ni uwezo wa kiuchumi unafanya sheria zishamiri. Mtu hawezi kukubali kulala njaa kisa ametoa hela kwa wakili haitatokea. Wenye shibe na excess ndo wanaweza litigation. Maskini hawezi kulitigate.

Idadi ya watu sio Kigezo hata siku moja usidanganyike.
 
MKOBA2011

MKOBA2011

Senior Member
Joined
Jul 12, 2011
Messages
143
Likes
1
Points
0
MKOBA2011

MKOBA2011

Senior Member
Joined Jul 12, 2011
143 1 0
Jamani ebu watanzania tubadilike na tuwabadilishe watoto wetu hasa katika kuchagua kitu cha kusoma maana nimeona watu wengi wanaulizia soko la ajira wakati huo huo ndiyo anakwenda kuanza first year bila kujua employment opportunities it changes with time.Watu wanaweza kuhitajika katika field flani then after one year ile field inakuwa na watu wengi kwa hiyo akimaliza hana soko.

Sasa basi soma weka alternatives nasoma nikikosa ajira nitafanya kitu flani from beginning ukimaliza usumbuki maana tayari una malengo ni sawa na mtu aliyepo kwenye ajira sijui ni wangapi wameweka malengo iwapo leo ataambiwa kazi basi atafanya kitu gani, Thats why watu wanaposimamishwa au kufukuzwa kazi wengi wanafrustuate why because no future plan.

Na hata ukiwa kwenye ajira weka malengo you work for certain years not till retirement wengi hawafanyi vizuri soon after retirement why because they are not after risk and believe me always the winner is the risk taker kwa hiyo hata ukiangalia unapoishi always wanaofanya vitu vizuri si waajiriwa ni wajasiriamali kwa hiyo ebu tujikite sana huko mafanikio yanakuwa na muda mfupi kama utajituma kuliko kusubiria mishahara kila mwezi ambayo huwa aimalizi mwezi.

Ebu kijana nitafute nikupe ushauri utoke vipi na hiyo sheria yako siyo uende chuo ukatafute GPA mwisho wa masomo unaleta first class tukikuingiza sokoni hamana kitu that is the challenge.
 
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Messages
3,061
Likes
395
Points
180
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2008
3,061 395 180
Fanya utafiti kwanza, nenda Kisutu ona aina ya watu na aina ya kesi za jina na madai ni tofauti kabisa na kesi zilizopo Mahakama ya kinondoni na Temeke. Vilevile mahakama kuu kesi zilizopo kanda ya Sumbawanga haziwezi kuwa sawa hatakidogo na kesi zilizopo dar es salaam. Katika mifano hiyo miwili Kanda ya DSM na Mahakama ya Kisutu ziko tofauti sababu kubwa ni uwezo wa kiuchumi unafanya sheria zishamiri. Mtu hawezi kukubali kulala njaa kisa ametoa hela kwa wakili haitatokea. Wenye shibe na excess ndo wanaweza litigation. Maskini hawezi kulitigate.

Idadi ya watu sio Kigezo hata siku moja usidanganyike.
OK wewe uliyefanya utafiti kigezo cha soko la ajira ni nini kama siyo kuwepo watu wengi wanaohitaji huduma husika? Kwani ukifungua biashara unaangalia nini kama siyo kuwepo watu wanaohitaji aina ya huduma unayotaka kuitoa? Mleta mada hajasema ni huduma gani ina unafuu wa gharama. Ameuliza je ni weathwhile kusoma LLB? Lakini kwa kutumia reasoning yako ni huduma gani inatolewa bure na ni biashara? Hata hospitali watu wanashindwa kulipia gharama yet, kuna madaktari wengi wanasoma ili wafanye hiyo kazi kwa vile wanaona kuna soko. Upande wa elimu ni hivyo pia. Kuna watu wengi wanashindwa kumudu gharama za elimu lakini kuna watu wengi wanaanzisha shule kwa vile wanaona ni biashara inayolipa. Kwa vile wewe umefanya utafiti basi twambie ni kozi gani mleta mada asome kwa vile ina soko na wanaohitaji huduma yake hawatalipia.
 
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Messages
3,061
Likes
395
Points
180
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2008
3,061 395 180
Fanya utafiti kwanza, nenda Kisutu ona aina ya watu na aina ya kesi za jina na madai ni tofauti kabisa na kesi zilizopo Mahakama ya kinondoni na Temeke. Vilevile mahakama kuu kesi zilizopo kanda ya Sumbawanga haziwezi kuwa sawa hatakidogo na kesi zilizopo dar es salaam. Katika mifano hiyo miwili Kanda ya DSM na Mahakama ya Kisutu ziko tofauti sababu kubwa ni uwezo wa kiuchumi unafanya sheria zishamiri. Mtu hawezi kukubali kulala njaa kisa ametoa hela kwa wakili haitatokea. Wenye shibe na excess ndo wanaweza litigation. Maskini hawezi kulitigate.

Idadi ya watu sio Kigezo hata siku moja usidanganyike.
Kwa hiyo, mawakili wengi ni jobless kwa vile ni watu wachache tu wanaomudu gharama za kuwakilishwa mahakamani?
 
Forum statistics

Threads 1,237,184
Members 475,465
Posts 29,280,575