Soko la mafuta ya kujipaka mwilini Vaselline limeingiliwa, Mtaani nimeuziwa sana mafuta feki, Hatimae nimejua pa kuyapata Original

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
images (4).jpeg

Nasikitika sana kuona hakuna udhibiti wa bidhaa feki hasa kwenye bidhaa za mwilini, bidhaa halisi na bora zinapotezea sokoni badala yake bidhaa feki zimetawala soko la nchi.

Miaka nenda rudi haya ndio mafuta nayoyapenda kujipakaa mwilini sambamba na sabuni ya kuogea ya Imperial.

Kuingiliwa kwa soko la mafuta haya kulianza kwa kubahatisha kuyakuta original maduka ya mtaani lakini hali ya sasa imekuwa mbaya sana, ni ngumu sana kuyakuta original mtaani.

Mwezi uliopita nilinunua maduka manne tofauti lakini yote nilitupa, yani kuanzia touch yake hadi harufu unaona kabisa ni tofauti.

Nikafikiria wapi naweza pata original nikakumbuka kwamba pharmacy nyingi huwa ni wasambazaji wa haya mafuta, nikaenda kwenye pharmacy kubwa za mjini nikanunua yale madogo kwa elf 3 kasoro, nilipofika nyumbani nikajiridhisha ni yenyewe original kwa kuyanusa sehem yenye hewa safi na kuyapima touch, nikarudi kununua yale makubwa.

Kwa hali ya sasa mitaani napata mashaka sana huenda hata sabuni za kuogea zikawa za mchongo
 
Kazi ya serikali ni kuidhibiti Chadema kwenye mikutano yake. Mengine wamesahau.
 
Mkuu wewe upo kama mimi hakuna kitu kinaboa kama bidhaa feki sokoni zinatutia hasara sana
Na inahuzunisha kwamba kuna watu wanalipwa mishahara kwaajili ya kudhibiti hilo
 
Mkuu wewe upo kama mimi hakuna kitu kinaboa kama bidhaa feki sokoni zinatutia hasara sana
Na inahuzunisha kwamba kuna watu wanalipwa mishahara kwaajili ya kudhibiti hilo
Kuna siku nilienda ktk duka la madawa kununua madawa kadhaa, Muuza duka akaniambia kwamba kuna dawa original na dawa zingine ambazo ni "Made in Mbagala," Kisha akaniuliza Je, ninataka zipi kwa sababu bei zinatofautiana. Nilishangaa sana, nilighairi sikununua.
 
Back
Top Bottom