Soko huria hili? Wakulima wakizalisha mahindi mengi hakuna soko. Kukiwa na uhaba wa mahindi wanakumbukwa

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,391
Kwa wale mliowahi kulima mahindi mnalijua hili utapata faida nzuri,pale tu ambapo wewe umepata wenzio hawajapata. Kwa lugha rahisi kabisa, mahindi hupanda bei kukiwa na uhaba na kwa muktadha waTanzania, ni lazima kuwe na uhaba wa mvua.

Kama hali ya hewa ni nzuri nchi nzima,kutakuwa na mavuno mazuri, hivyo bei ya mahindi kuporomoka. Kinachoendelea sasa kwa wakulima kuambiwa wajipongeze kwa bei nzuri ni kichekesho cha mwaka!

Kimsingi hakuna bei nzuri ya mahindi bali kuna njaa. Njaa haishangiliwi, ni muhimu wadau, serikali ikaweka sera nzuri kuliokoa zao hili.

Kama wote tukiamua kulima mahindi na Mungu akaleta neema ya mvua, tutauziana gunia Sh 20,000/= kama ilivyotokea mwaka juzi kule Rukwa na Katavi.

Tuache siasa za korosho.
 
Back
Top Bottom