Software ya kujumlisha kura za Urais

tanken

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
224
53
Wana JF,

Naomba tujadili hili kwasababu KURA zote za urais zitajumulishwa kwa kutumia aina ya software spesheli. Sielewi kuwa software hufanya kazi vipi, je,

Software yenyewe ni ya kwetu au kutoka NJE?
Wawakilishi wa vyama wameshirikishwa katika uamuzi wa kutumia aina ya software?
Usalama wa software unalindwa vipi?
 
Waje software au nn, tunatumia matokeo ya vituoni ambako wagombea nafasi zote yatajulikana na kubandikwa nje.
 
Mkuu,matokeo yakitangazwa hayawezi kubatilishwa. Mtahesabu vya vituoni,WENZETU wakitangaza mshindi ndo imetoka. Kingine,matokeo yanatumwa na yanajijumulisha yenyewe KUTUMIA software. Sielewi kama vyama vimeridhia formula inayotumika? Software,hutengenezwa.sasa NCHI zingine wapinzani wajifanya vipi kudhibitisha udanganyifu wa ki software. Hili nalo ni kete.
 
HAKUNAAA CHA SOFTWARE WALA HARDWARE HAPAAAAA....!!! Kitu MANUAL...!!!

Kila kituo Tanzania nzima, kisha kata, kisha Wilaya, kisha MKOA...!!

Kura za Jumla za Kila mkoa zikijulikana...

Then, ni KUJUMLISHA KWA MKONO TU...

Very easy... HAKUNA CHA SOFT WARE HAPA. .!! hata 1 + 1 software ya NINI..?

Mwaka huu, CCM out..!!
 
Kamanda, nakupata vizuri, ila nilisoma kwenye gazeti MOJA nchini kuwa nec wanajaribisha software itakayotumiwa kujumulisha KURA ZA URAIS. Naomba tutafakari hili bila jazba na kwa umakini. TAFAKARI! waliokaribu na Viongozi wa UKAWA wawailize,kuwa wamechukua Tahadhari kweli au kawaida tu. Waulize NCHI zilizotumia software, wakapige bao la kidole.
 
Hii software inadhaminiwa na kutengenezwa na ma Eng wa compyuter IT china ila made kutoka Japan! hii hatuitaki
 
Mkuu,matokeo yakitangazwa hayawezi kubatilishwa. Mtahesabu vya vituoni,WENZETU wakitangaza mshindi ndo imetoka. Kingine,matokeo yanatumwa na yanajijumulisha yenyewe KUTUMIA software. Sielewi kama vyama vimeridhia formula inayotumika? Software,hutengenezwa.sasa NCHI zingine wapinzani wajifanya vipi kudhibitisha udanganyifu wa ki software. Hili nalo ni kete.

1. Huku kitaa kura zimeshajumlishwa na calculator ikaonekana fulani kashinda. majimbo 265 sio mengi kama unavyofikiri. sasa itakuwaje waseme mwingine kashinda wakati wananchi wameshapiga hesabu wakaona fulani ndio kashinda ata kabla nec kutangaza. ni sawa na kusema wananchi wafanye 1+1=2 alafu nec wafanye 1+1=3, hii itakuwa ni uhasama na mwisho wake ni vita.

2. katika uchaguzi wowote ule, ni lazima mwisho wa uchaguzi, aliyeshindwa atokee mbele akiri kushindwa taifa litambue kuwa fulani ndio kidedea. sasa mgogoro huwa unatokea pale ambapo kumefanyika hujuma na anayekataa kushindwa anakuwa na ushahidi unaopingana na matokeo ambao ata kama kitanuka ndio ushahidi atakaoutumia icc.

matokeo yakishatangazwa hayawezi kupingwa sawa sikatai, lakini yanaweza yakatokea machafuko. na ikiwa yatatokea tayari muamuzi atakuwa si mahakama ya ndani tena. wananchi huwa wanamsikiliza kiongozi wao. ikiwa mtu atashindwa, na yeye akajitokeza hazarani kukubali kushindwa, huwa wananchi wanamuelewa na hali inakuwa shwari. ikiwa atajitokeza harazarani kupinga matokeo alafu dola ikatumia nguvu kuforce matokeo ndio mwanza wa nchi kuingia katika vita. hili linakuwa ni kosa kikatiba lakini wananchi wanaweza kutumia nguvu kulazimisha ikiwa haki haijatendeka.

Ndio maana katiba mpya inahitajika ili demokrasia iwe huru zaidi.

uchaguzi mwaka huu ni mgumu sana hata kuutabiri, watu wengi wanatumia kigezo cha nyomi kwenye mikutano kuwa ndio kuungwa mkono na wananchi wengi, lakini tukitumia kigezo cha nyomi, upinzani utashinda, sababu lowassa ana nyomi la kweli, magufuli ana nyomi la fiesta/watu wamevalia ngozi za kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu.

tafiti zinazoendelea hazileti maana wala hazina effect yoyote kwa wananchi sababu hazina misingi yaki tafiti ndio maana watu wanalalama kuwa hizo tafiti zinaratibiwa na viongozi wa ccm. na pili ni ngumu sana watu 1800 kuwakilisha wapiga kura 24m, huenda hata waliohojiwa walikuwa sio wapiga kura.

pia watu wanasema kuwa kama kukinuka jeshi litachukua nchi, ni sawa, lakini kwa uchaguzi huu ulivyo mgumu sidhani kama itakuwa hivyo sababu hata dola yenyewe ina itikadi tofauti zinazokinzana, kuna wenye imani na fulani na wenyewe imani na mwingine. Ikumbukwe kuwa Lowassa na magufuli, si kama kikwete na mbowe au kikwete na slaa au limbumba.

Kuna kazi kweli kweli. badi siku 28. tuombee amani tu taifa letu mama tanzania.
 
Tume imekuwa ya wana usalama wa taifa na wanajeshi...!!
Hizi mbinu si kwa bahati mbaya lakini nafurahi kusema kuwa zilishashindwa..!!
 
Sawa kiongozi, taarifa hizi za uwezekano ya udanganyifu lazima watu wafahamu MAPEMA. Tukubaliane, wakati wa kutangazi,hali ya nchi huwa tete.Ulinzi mkali,vitisho vingi. Waulize majirani ZETU.utaelewa.
 
UKAWA lazima wafanyie kazi this infos...

UKAWA intelligence unit, must work DAY & NIGHT for the next 40 days...!!!
 
Niliota kuna wachina na wanaijeria wameingizwa nchini kama wawekezaji ila kazi kubwa waliyoletewa ni kuja ku-hack system ya kuhesabia kura ili chama tawala kidumu kutawala. Nilipomaliza kuota ndoto hii nikastuka.
 
UKAWA lazima wafanyie kazi this infos...

UKAWA intelligence unit, must work DAY & NIGHT for the next 40 days...!!!

Mkuu,UKAWA wanafanya kazi nzuri sana ukizingatia kuwa ni Mara ya kwanza kuwa na muungano wa vyama. Ila kwa hizi SIKU chache zilizobaki UKAWA wanahitaji volunteers wengi na wawe coordinated katika KILA jimbo, angalau volunteers 20 kwa KILA jimbo,hawa ni wakutoka tarifaa sahiii kwa wakati maalum, kukusanya upepo wa kisiasa,hawa volunteers, ni kando na mfumo waki ofisi.hawa hasa wametoa taarifa kwa mtu MOJA alie na access kwa mgombea urais.japo mambo mengi ya kichama yana usiri,UKAWA ujipange haswa,kuwakilisha wanahusishwa na IT ya nec
 
Waje software au nn, tunatumia matokeo ya vituoni ambako wagombea nafasi zote yatajulikana na kubandikwa nje.

Isitoshe mawakala katika vituo vyote wana simu za mkononi,kinachotakiwa ni wao kuwa waaminifu tu.
 
Hilo halipingiki mkuu. Ila unazuiaje Dola iliyoingizwa kwenye taasisi nyeti kama NEC?

Haya mambo yoote, yalitakiwa kuwepo ktk katiba, kuwa matokeo ya mgombea kituoni ndo msingi wa matokeo yote, yenye ushahidi wa wananchi yakihesabiwa kwa mkono. Huu uficho wa sijui yajumlishwe na tume ndo itangazwe ndo madhaifu yakuja kuyaondoa ktk mchakato wa katiba mpya. Tukiwa na katiba safi yenye maridhiano kamwe migogoro ya kitoto hivi haitakuwepo.
 
Back
Top Bottom