Sofia Simba naye ajitangaza kupambana na mafisadi

Wana JF,
Pamoja na kulaani, nafikiri tumefanya kazi kubwa sana kuwabadilisha hawa watu hayo wanayoyasema. Miaka yote ya nyuma tangu tupate UHURU, tulicheza jinsi ma DJs wetu wa nchi walivyotupigia mziki. Kwa mara ya kwanza tumedisa na kusema, hapana. Hii miziki yenu mnayotupigia ya "SAFARI TRIPERS - Mkuki moyoni" hatuitaki tena. Sasa wamegundua kuwa mambo hayaendi na wamekuja kwa gia ya kuanza kuondoa AFRO zao kichwani ingawa bado wamevaa Raizon na Bugalou.

Inabidi sasa tuende hatua moja mbele yao. Kusema kupiga vita ufisadi siyo deal tena. Tuanze kuwabana viongozi wote kuwa JE UMEWAFANYA NINI MAFISADI? Mafisadi wanatakiwa kuadhibiwa na tena ilitakiwa mambo kama RUSSIA enzi za Mzee Joe Stallin. Wanachukuliwa MAFISADI wote viwanja vya jangwani na unawekwa UKUTA na jamaa wanafungwa pale na Watindiga na mishale yao ya SUMU wanakuja na kuwamaliza.
Hata BIBLIA inasema kuwa "damu husafisha makosa". Bila watu kadhaa kuja kumwaga damu zao pale, hakuna heshima hata siku moja kwa mali za Watanzania. Mafisadi siku zote wataiba na kusema "sana sana watanifukuza". Kama angelijua kuwa "ukiiba basi ni wanao watafaidi" sidhani kama watu wangelikuwa wanakula hata bila kunawa. Tukaze kamba kwani mwelekeo ni mzuri. Zamani hatukufahamu kabisa kuhusu hili (rejea ujumbe wa Mwanakijiji juu ya Watanzania Waasia kutujulisha ufisadi wa wenzao na viongozi wetu), baadaye tukaanza kuliongelea kwa shida na mwisho hadharani na sasa hata "vinyonga" wa bungeni na wao wanaanza kupigia kelele ufisadi. Nafikiri imebaki hatua moja tu sasa, kuwapandisha watu kizimbani na kuwatunza KEKO. Hata kama Mkapa akishinda, kitendo cha kupanda KIZIMBANI itakuwa mwanzo mzuri.
 
Huyu mama ni m-pambanaji na amedhamiria kupinga ufisadi kwa msio mjua mama Simba hanunuliki ni mtu wa msimamo na hateteleki.

Tatizo ili mtu awe mpinga ufisadi lazima awe na surname Mwakyembe, Selelii, Kilango, sendeka, kimaro et al. Mnaibinafsisha vita ya ufisadi kalabagho!
 
maneno ni tofauti vitendo. yeye mwenyewe alipataje Uenyekiti wa UWT (CCM). taifa bila kuhongwa na hao mafisadi angepata?. sasa lazima ajikombe.

Pole sana mama umechelewa
 
huyu mama ni m-pambanaji na amedhamiria kupinga ufisadi kwa msio mjua mama simba hanunuliki ni mtu wa msimamo na hateteleki.

Tatizo ili mtu awe mpinga ufisadi lazima awe na surname mwakyembe, selelii, kilango, sendeka, kimaro et al. Mnaibinafsisha vita ya ufisadi kalabagho!
anatembea kama bata, anakunya kama bata, anatafuna kama bata, anabweka kama bata = bata!!! .... Nini tofauti ya sophia na mafisadi wengine?
 
uchaguzi umekaria keshokutwa mzee wa richmodu naye utamsikia akipiga vita ufisadi so msishangae
 
Tunamkaribisha kundini but kwanza atutajie mafisadi anaowafahamu ambao atawapinga kwa nguvu zake zote..otherwise ni walewale ambao washaona tunaelekea kipindi gani...anyway lazima naye atakuwa mzugaji tu...
 
"Nawaasa wanawake nchini na taifa kwa ujumla kuwapuuza viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa na dini, bali nawaasa wafanye kazi ya kuongoza watu kiroho na masuala ya siasa waachie wanasiasa," alisema Bibi Simba.kuwa wanapigana na ufisadi kwa namna yao. Very soon.[/QUOTE]

KICHEFUCHEFU huyu mama nashindwa kumuelewa anapokwenda kanisani na kuwaambia waumini KUWAPUUZA VIONGOZI WA DINI!Haya ni matusi ya nguoni huyo mama alikua anapaswa kufukuzwa mara moja katika mkutano huo.Anamaana gani kua viongozi wa dini wafanye kazi za kiroho?Anaelewa kazi za kiroho ni ni zipi na roho za kina nani?Kama inavyofahamika misingi ya dini nyingi zinakemea USIUE,USIIBE,USINYANG'ANYE MALI ZA WATU,USIZINI N.K.Huyo mama anataka kutuambia vilivyotajwa hapo juu havipo ktk chama tawala na serikali.Hawa watu naona wanahitaji kutumia pesa kuagizi washauri kutoka nje ya nchi.Kwani kwa kauli zao hasa wakati huu kila mtu anafyatuka kivyaki na wengi hawajui hata walisemalo.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni - Simba

27 September 2009
Majira
Na Gladness Theonest

Waziri huyo aliwaonya viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa kuachana na tabia hiyo ili kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu.

.

Viongozi wa Dini nao wamezidi kukicha kuwaalika Viongozi wa Serikali makanisani, hivi hawakujua huyu mama ni Fisadi?? Wacha akawaaibishe!
 
Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni - Simba

27 September 2009
Majira
Na Gladness Theonest

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bibi Sophia Simba amesema hatamwonea haya fisadi yeyote hata aende na shilingi bilioni moja.

Pia waziri huyo amewataka wanawake wa Tanzania na Taifa kwa ujumla kumwombea kwa kuwa ni mwanamke pekee aliye katika nafasi ngumu ya kupambana na mafisadi nchini.

Bibi Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga Kongamano la Wanawake Waombolezao kitaifa, lililofanyika katika kanisa la Sinza Christiane Centre jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa fisadi yeyote asitarajie kwenda kwake kwa dhana potofu inayotafsiriwa na wengi kwamba wanawake ni dhaifu na kumpa rushwa ya bilioni moja akitegemea kuwa kesi dhidi yake itasitishwa isiende mahakamani, kwani atakuwa anajidanganya.

"Wanawake wenzangu nikiwa kama mwanamke na kulingana na wadhifa wangu wa kusimamia utawala bora nchini, sitamwonea haya fisadi yeyote hata aje na bilioni moja ili tuyamalize. Hilo kwangu halitawezekana kwani natetea maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisema Bibi Simba.

Aliwatoa hofu wanawake nchini kuwa serikali inafanya kazi kwa nguvu zake zote katika masuala mbalimbali hasa la kupambana na mafisadi baada ya sheria ya Takukuru kufanyiwa marekebisho.

Amewataka wanawake wote nchini kuiga mfano wake, kwa kukataa kutoa rushwa sehemu ambazo wanatakiwa wapate haki zao kama hospitalini na mahakamani.

Waziri huyo aliwaonya viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa kuachana na tabia hiyo ili kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu.

"Nawaasa wanawake nchini na taifa kwa ujumla kuwapuuza viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa na dini, bali nawaasa wafanye kazi ya kuongoza watu kiroho na masuala ya siasa waachie wanasiasa," alisema Bibi Simba.

Aidha amewataka wanawake nchini kutokubweteka kwa kutegemea maendeleo yatawafuata mahali walipo bali pale wanapoona kuwa serikali inatoa fursa ya mikopo kwa wanawake wawe mstari wa mbele kufuatilia nafasi hizo.

Naye Mchungaji wa Kanisa hilo, Godfrey Emmanuel alisema akina mama na Taifa kwa ujumla hawana budi kusimama imara katika maombi ili kuwaokoa vijana ambao wamechakaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

Kongamano hilo liliwakusanya wanawake wapatao 200 kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania bara na visiwani na wengine kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda na Congo.

mwisho.

My Take:
Tumekwisha. Nasubiri Rostam na EL nao wajitokeze kulaani mafisadi na kujitaja kuwa wanapigana na ufisadi kwa namna yao. Very soon.

Safi sana.
Sasa akina Mwakyembe watasema nini iwepo kila mtu anapinga ufisadi?
 
Naomba mwenye taarifa kamili atusaidie kuiweka hapa ili tufaham ni nani hasa anang'ang'aniza kumuhonga huyu mama ''mwana maombi''.
 
1. Kwanza heshima kwa wote kwenye safu ya mijadala. Ninatambua na kuthamini sana kazi kubwa mnayoifanya ya kulijenga Tanzania tofauti na hii tunamoishi.

2.Najua kwanini Mwanakijiji amevutika stori hii ya Sofia Simba naye kupambana na ufisadi Tanzania. Amekwisha eleza ktk makala zake kadhaa!

3. Mimi nimuunge mkono tu Mwanakijiji kwamba hii vita ya ufisadi kwa sehemu kubwa imepoteza mwelekeo baada ya kuvamiwa na magenge ya siasa za ndani ya CCM. Ndani ya CCM wote wanajitambulisha kupambana na ufisadi hawana uhalali huo. Leo watu wanauliza Sofia Simba alikuwa wapi siku zote hata atokee leo, wanasahau kuwauliza wabunge wote wa CCM wanaojitambulisha kupambana na ufisadi walikuwa wapi hata watokee mwaka 2007? 2008? 2009?.... kama kuna kipindi nchi imeuzwa ni kipindi cha Mkapa.

Walikuwa wapi? ...Kwa mujibu wa taarifa za bunge, hoja binafasi ya mwisho iliwasilishwa mwaka 1997 .....tangu hapo hoja iliyofuata ilikuja baada ya miaka10, yaani 2007, ambapo kijana zitto aliwasilisha hoja ya Buzwagi iliyosababisha asimamishwe kazi....tangu hapo hoja binafsi zimebaki kufurika bungeni utadhani serikali ya CCM imenza wizi leo.

Ufisadi ndani ya serikali ya CCM haujaanza leo, na nchi hii wengi ndani na nje (kwenye vyama vya upinzani) kumejaa mafisadi lukuki. We hujasikia ruzuku inavoleta migogoro huko? ...nchi hii inanuka!

Ni vigumu kumpata mtu mwenye uhalali wa kukemea ufisadi ...Labda kama sikosei watu aina ya Dk Salim aliyeshindwa urais na Kikwete 2005 ...tunao wangapi? Wanasema?...
 
Aiiiii Bhaghosha
Natubhagha nene,

Kama hali ndio Hii jamani kila kukicha mtu anajidamkia na lake hawa viongozi huwa hawana tape recorder wawe wana reply back kila walichokiongea vipindi vya nyuma na wakajionea wanavyo visema sasa,
Makamba,
Chliligate,
Tambwe Liza,
sophia,
JK
na wengineo me ningeliomba Mhariri wa gazeti lolote atutolee machache ya kauli za utata za viongozi wetu hawa ili wajikumbushie kuwa watanzania wapo na wanakumbuka yote waliokuwa wakituambia, jamani Hapa naoona hawa viongozi wanashindwa kujua na kuzifahamu fika alama za nyakati na wakati huu twaelekea kwa uchaguzi 2010 viongozi watajikanganya kwa maneno mengi sana jana "mmoja wao huko UN ati kasema mgogoro wa Zanzibar utakuwa umeisha kabla ya uchaguzi ujao tena mbele ya UN Sec.Gen " Kwa halaka halaka huyo si anadhamilaa kujiandaaa kwa uchaguzi ujao??
Kweli si watu watakuuliza kumbe wewe wangojea uchaguzi ukalibie ndio uanze tatua matatizo yako??

Je ufumbuzi usipo patikana utaliambiaje Taifa na Umoja wa Mataifa UN??

Ndugu zangu wa Mwanza tuliambiwa soon Rock City itakuja badirishwa kuwa kama Carifonia - Los Angles na tutangoja sana.

Swala lingine bunge lijalo ndugu zangu hapo sasa ndipo patashika nguo kuchanika this time kila mtu atakuwa kivyake au makundi mapya yataibuka upya wote wanataka wajitakase mle mjengoni. subirini mtajionea mambo.
 
anatembea kama bata, anakunya kama bata, anatafuna kama bata, anabweka kama bata = bata!!! .... Nini tofauti ya sophia na mafisadi wengine?

no no noo!! sio bata huyo, hiyo yote ni coincidence tu ... huyo ni kunguru mwenye mdomo mpana...!
 
Wana JF,
Pamoja na kulaani, nafikiri tumefanya kazi kubwa sana kuwabadilisha hawa watu hayo wanayoyasema. Miaka yote ya nyuma tangu tupate UHURU, tulicheza jinsi ma DJs wetu wa nchi walivyotupigia mziki. Kwa mara ya kwanza tumedisa na kusema, hapana. Hii miziki yenu mnayotupigia ya "SAFARI TRIPERS - Mkuki moyoni" hatuitaki tena. Sasa wamegundua kuwa mambo hayaendi na wamekuja kwa gia ya kuanza kuondoa AFRO zao kichwani ingawa bado wamevaa Raizon na Bugalou.

Inabidi sasa tuende hatua moja mbele yao. Kusema kupiga vita ufisadi siyo deal tena. Tuanze kuwabana viongozi wote kuwa JE UMEWAFANYA NINI MAFISADI? Mafisadi wanatakiwa kuadhibiwa na tena ilitakiwa mambo kama RUSSIA enzi za Mzee Joe Stallin. Wanachukuliwa MAFISADI wote viwanja vya jangwani na unawekwa UKUTA na jamaa wanafungwa pale na Watindiga na mishale yao ya SUMU wanakuja na kuwamaliza.
Hata BIBLIA inasema kuwa "damu husafisha makosa". Bila watu kadhaa kuja kumwaga damu zao pale, hakuna heshima hata siku moja kwa mali za Watanzania. Mafisadi siku zote wataiba na kusema "sana sana watanifukuza". Kama angelijua kuwa "ukiiba basi ni wanao watafaidi" sidhani kama watu wangelikuwa wanakula hata bila kunawa. Tukaze kamba kwani mwelekeo ni mzuri. Zamani hatukufahamu kabisa kuhusu hili (rejea ujumbe wa Mwanakijiji juu ya Watanzania Waasia kutujulisha ufisadi wa wenzao na viongozi wetu), baadaye tukaanza kuliongelea kwa shida na mwisho hadharani na sasa hata "vinyonga" wa bungeni na wao wanaanza kupigia kelele ufisadi. Nafikiri imebaki hatua moja tu sasa, kuwapandisha watu kizimbani na kuwatunza KEKO. Hata kama Mkapa akishinda, kitendo cha kupanda KIZIMBANI itakuwa mwanzo mzuri.
Sikonge, hiyo option ya kwanza nadhani ndiyo sahihi kuliko hiyo ya pili. Maana tumeshuhudia wakipelekwa Keko kwanza wanaandaliwa vyumba VIP kabla ya kupelekwa na ikibidi Waziri wa Mambo ya Ndani anawatembelea jioni hiyo hiyo kuhakikisha jamaa wako "comfortable"
 
Mimi nawashangaa mnaopinga sofia simba kusema anapambana na mafisadi. kwani hao waliojibatiza mgambo wa kupambana na ufisadi wamepata wapi uhalali wa kusema wanachukia ufisadi?....unahoji kwanini sofia simba aseme leo, alikuwa wapi? kwani akina Mwakyembe, Annae Killango, Olesendeka, Mengi na wenzao walikuwa wapi nchi yetu ikiuzwa na mkapa waone leo?
 
Back
Top Bottom