Sofia Simba naye ajitangaza kupambana na mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sofia Simba naye ajitangaza kupambana na mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 27, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni - Simba

  27 September 2009
  Majira
  Na Gladness Theonest


  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bibi Sophia Simba amesema hatamwonea haya fisadi yeyote hata aende na shilingi bilioni moja.

  Pia waziri huyo amewataka wanawake wa Tanzania na Taifa kwa ujumla kumwombea kwa kuwa ni mwanamke pekee aliye katika nafasi ngumu ya kupambana na mafisadi nchini.

  Bibi Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga Kongamano la Wanawake Waombolezao kitaifa, lililofanyika katika kanisa la Sinza Christiane Centre jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa fisadi yeyote asitarajie kwenda kwake kwa dhana potofu inayotafsiriwa na wengi kwamba wanawake ni dhaifu na kumpa rushwa ya bilioni moja akitegemea kuwa kesi dhidi yake itasitishwa isiende mahakamani, kwani atakuwa anajidanganya.

  "Wanawake wenzangu nikiwa kama mwanamke na kulingana na wadhifa wangu wa kusimamia utawala bora nchini, sitamwonea haya fisadi yeyote hata aje na bilioni moja ili tuyamalize. Hilo kwangu halitawezekana kwani natetea maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisema Bibi Simba.

  Aliwatoa hofu wanawake nchini kuwa serikali inafanya kazi kwa nguvu zake zote katika masuala mbalimbali hasa la kupambana na mafisadi baada ya sheria ya Takukuru kufanyiwa marekebisho.

  Amewataka wanawake wote nchini kuiga mfano wake, kwa kukataa kutoa rushwa sehemu ambazo wanatakiwa wapate haki zao kama hospitalini na mahakamani.

  Waziri huyo aliwaonya viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa kuachana na tabia hiyo ili kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu.

  "Nawaasa wanawake nchini na taifa kwa ujumla kuwapuuza viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa na dini, bali nawaasa wafanye kazi ya kuongoza watu kiroho na masuala ya siasa waachie wanasiasa," alisema Bibi Simba.

  Aidha amewataka wanawake nchini kutokubweteka kwa kutegemea maendeleo yatawafuata mahali walipo bali pale wanapoona kuwa serikali inatoa fursa ya mikopo kwa wanawake wawe mstari wa mbele kufuatilia nafasi hizo.

  Naye Mchungaji wa Kanisa hilo, Godfrey Emmanuel alisema akina mama na Taifa kwa ujumla hawana budi kusimama imara katika maombi ili kuwaokoa vijana ambao wamechakaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

  Kongamano hilo liliwakusanya wanawake wapatao 200 kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania bara na visiwani na wengine kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda na Congo.

  mwisho.

  My Take:
  Tumekwisha. Nasubiri Rostam na EL nao wajitokeze kulaani mafisadi na kujitaja kuwa wanapigana na ufisadi kwa namna yao. Very soon.
   
 2. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hii ni kali!! Yote yanaendana na dhana ya watawala kudhani kuwa watanzania ni wasahaulifu sana. Misimamo na kauli zake kuhusu Chenge, Richmond na kauli zake za kumshambulia Mengi na uwezo wake wa kufikiri unakinzana na hayo anayojigamba kwayo. Ipo siku tutaanza kutembea na mayai viza...
  Kwa mtaji huu ni kweli EL na RA wanaweza kujitokeza na kujigamba wanapambana na ufisadi.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkapa uko wapi? Tokeza na wewe kupinga Ufisadi....!
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Tatizo la wanasiasa wa Tanzania asilimia kubwa ni wanafiki na wanakigeugeu, hubadilika kulingana na uelekeo wa upepo. Hawatilii maanani wanachokiongea, mfano ni huyu Bibi na mwenzake Makamba, majuzi tu walikuwa wakali kama mbogo kwa wanaoupinga ufisadi, mara ghafla wamegeuka na wanayameza matapishi yao.

  Shame upon them.
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli tumekwisha ... kama hata watetezi wa mafisadi nao leo hii wanasimama majukwaani na kutuambia wanapambana na ufisadi, hii ni kali ya mwaka!

  Huyu mama alimrushia Bwana Mengi maneno ya kejeli tena kwa kutumia lugha za mtaani, kwamba "kwa kitendo cha kuwataja mapapa wa ufisadi, Mengi alikuwa amechemsha".

  Sasa anatuambia na yeye yuko kwenye mapambano na ufisadi, anategemea tumuamini ama anadhani tumesahau?

  Akiwa kama waziri wa utawala bora wakati wa saga la Mengi hakutakiwa kutoa comment yoyote ama kuonyesha kwamba yuko upande gani.

  Bado ninamsubiri Mkuchika ambaye alisema kwamba serikali ilikuwa inapitia maelezo ya Mengi aliyoyatoa kwa waandishi wa habari ili waone kama serikali inaweza kumshitaki. Soon nae tutamsikia kwamba yuko mstari wa mbele kwenye mapambano.

  Kuelekea 2010 tutasikia mengi na yote lengo lake ni kuiponya CCM na serikali yake.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Gimme a break!
   
 7. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  watamdai hela zao muda si mrefu na kuna uwezekano akapoteza hadi uwaziri
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  hivi makanisani ndo imekuwa sehemu ya kila mtu 'kujisafisha' na kujinadi kupambana na ufisadi?
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  It is sooooooooooooooo funny............
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Je akija na zaidi ya shilingi bilioni moja? Hapa haja onyesha kuwa hanunuliki bali anajionyesha kuwa anajiona yeye ni wa bei ya juu. Ukitaka akusikilize nenda na zaidi ya bilioni moja.  1.Muda wote tokea awe na wadhifa huo kafanyaje kupambana na ufisadi? Kwa nini ana tangaza vita sasa? where was she?

  2.Wala yeye siyo mwanamke pekee katika nafasi ngumu ya kupambana na mafisadi. Wanawake hao ni wale wasio na hela lakini hospitalini wanaombwa rushwa ili wagonjwa wao wasife. Wanawake ambao wapo kwenye nafasi ngumu ni wale ambao wana poteza maisha yao au ya watoto wao wakati wa kujifungua kwa sababu ya kuomba rushwa. Wanawake ambao wapo kwenye nafasi hiyo ni wale wanaoombwa rushwa ya ngono na kudhalilishwa ili mradi tu kupata haki yao. Yeye yupo kwenye nafasi ya kuacha maamuzi magumu yafanywe na raisi nayeye atekeleze tu.  Mkuu Mwanakijiji nadhani hapo ulimaanisha Christian siyo Chrisitiane mkuu. Kama nime kosea samahani.


  Bado anaendelea kusisitiza kikomo cha bilioni moja. Baadhi ya mafisadi wameiba zaidi ya bilioni moja na wana uwezo mkubwa sana wa kuamua kumlipa zaidi ya bilioni moja. Kwa nini asiseme tu mafisadi wasi tegemee chochote kwake hata waje na kiasi gani?

  Yale yale. Aionyeshe basi nia ya kweli ya kutetea maslahi ya mataifa na si kuhubiri tu majukwani. Aache lip service.

  Bado ni maneno tupu. Tuone vitendo.


  Mfano upi? Ni lini tumesikia Sophia Simba kakataa rushwa? Hapa anasema waige nini ambacho angefanya na si nini ambacho amesha fanya. Na je ana waambiaje wanawake ambao wanabidi wachague kati ya kutoa rushwa au kufa mahospitalini?


  Kwa nini wanasiasa wengi wanaogopa maneno ya viongozi wa kidini? Si siri kwamba viongozi wa kidini wana uwezo wa kufikia watu wengi sana na kuwa shawishi. Hapa wana jaribu kudivert attention. Hongera mama muda mfupi tu ndani ya kutangaza zita dhidi ya ufisadi umeonyesha wewe ni mpiganaji wa aina gani.

  Mh so far kuachia siasa kwa wanasiasa ime tufikisha wapi?

  Na hizo fursa nazo zitakuwa ufisadi proof? Au wanawake wata tegemewa watoe rushwa za aina mbali mbali kupata hiyo mikopo?


  Swali: Kwa nini viongozi wetu wa kisiasa wanasema viongozi wa kidini wasiingilie maswala ya kisiasa lakini wao wanaenda kuzungumzia siasa kwenye nyumba za ibada? Mimi naona hapa wanakua wanafiki wakubwa sana hawa viongozi wetu wa kisiasa.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wakina nani watamdai haki zao na ni haki zipi hizo?
   
 12. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35

  Nina makengeza? au sioni vizuri?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Tutaona vioja na viroja vingi kuelekea 2010. Alianza Mkuu wao kwa kudai, "Najivunia rekodi yangu ya kupambana na mafisadi." Wakati huo huo majina ya mafisadi waliorudisha shilingi bilioni 70 na kiasi kilichorudishwa na kila mmoja wao hadi hii leo ni siri kali. Mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe kuhusiana na ufisadi wa Richmond/Dowans hadi hii leo hajayafanyia kazi. Rostam Aziz pamoja na ushahidi wa kutosha dhidi yake kwa ufisadi wa Richmond/Dowans na Kagoda hata kumhoji tu wanaogopa! Chenge Vijisenti, Lowassa, Msabaha, Makamba, Idrissa Rashid, Mkapa na mapapa wa ufisadi bado wanapeta mtaani lakini pamoja na hayo yote VDG wetu bado anajivunia rekodi yake! Sijui naye RA atatangaza lini kwamba atapambana na mafisadi kwa hali na mali.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  tuendelee kuwahesabu wale walioonekana kutetea mafisadi na sasa wanajionesha wamepata "ufunuo"

  - Chiligati
  - Makamba
  - Sofia Simba
  -
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani huyu mi ndo ananichekesha kweli kweli.Huyu si ndo mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa CCM huyu...nadhani kasahau kuwa alifanya ufisadi wa kutisha wakati wa kampeni zake za kuutaka huo uenyekiti wa UWT CCM
   
 16. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  watu wameona kusema wanapinga ufisadi ndio gia ya kuingilia
   
 17. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mwl Nyerere alisema , unamsikiliza mtu kama huyu na kumkazia macho usoni, ili kupima ukweli wa maneno yake.
  Most probably Mama Sophia asivyo na uwezo wa upembuzi ndo sasa anan'gamua kuwa uchaguzi mkuu ni mwakani.
  Vitendo vyake na kauli zake havionyeshi kuupendeza umma wa watanzania.Kibaya zaidi watu hatuja sahau kuwa alikuwa 100% upande wa mafisadi.Hatuja sahau kuwa aliwapiga vita tena hadharani wabunge wenzie wanao pinga vita ufisadi.
   
 18. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nini kilitokea katika kikao cha kamati kuu ya mwisho ya CCM jamani, mbona sasa kila mtu anajifanya anapinga ufisadi..kuna ajenda gani ya siri..
  1. mmeona makamba alipoenda kujikosha kwa sita kule Tabora
  2. Mzee Msekwa na kuwasupport wapiganaji wa CCM....
  3. Mzee ruksa nae kurusha dongo kwa mafisadi kule jimboni kwa kilango........
  4. hata Sofia nae..??

  nikweli tusubir EL, RA, Mkapa nao waje wakemee ufisadi.....

  "Tanzania itajengwa na mafisadi.." TUSIDANGANYIKE...
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Anawakana wakati ndio hao hao walio mweka katika kitengo hicho ana ubavu wa kuwageuka walio mpa mkate wa kila siku au anajibalaguza alafu pembeni anaendelea kugongeana bilauli za mvinyo?
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  mkuu huoni kama hizi ni mbio kuelekea katika uchaguzi ...???
   
Loading...