Soda ni Sumu; Je, TFDA wanafanya nini?

Soda ni Sumu; Je, TFDA wanafanya nini?

Cha ajabu zaidi na kushangaza kama sio kusikitisha ni pale ambapo Mkuu wa kitengo kinachohusika na maswala hayo (ya vyakula na madawa) yaani TFDA alipoulizwa kuhusu jambo hilo na akatoa majibu mepesi na hoja tepetepe kabisa.
>>>alijibu soda sio kinywaji hatari kwakuwa kinatumiwa na watu wengi duniani.

Kwahiyo kama kingenywewa na watu wachache basi kingekuwa sumu!!
 
Soda ni km sigara,hakuna faida hata moja
Acha dharau kijana au kwasababu ww hautumii nani kasema sigara haina faida hata moja moja ya faida ya sigara ni kuupa Mwili Joto hasa kipindi cha baridi na haka kamvua mvua kanakonyesha.....
 
Mkuu,
Hakuna akulazimishaye kunywa soda.

Ukitambua kuwa soda ni sumu acha kunywa.

Just take a decision which is simple and clear.
Issue sio kulazimishwa bali kuna wengine hawatambui kabisa sasa watatambuaje.
Mfano mdogo tu vile vinywaji vya kuongeza nguvu havitakiwi vitumiwe na baadhi ya watu na vimeandikwa kabisa (but in English) watoto, wajawazito, wanaonyonyesha n.k lakini kwa kukosa kuwekwa msisitizo leo hao waliotajwa wangapi wanaotumia vinywaji hivyo
 
soda ni sumu inayoua taratibu sawa
kwani nani anataka kufa haraka ?

wanaotaka kufa haraka watakunywa sumu ya panya ila sisi ambao hatutaki kufa haraka tutakunywa soda
Sawa
 
Acha dharau kijana au kwasababu ww hautumii nani kasema sigara haina faida hata moja moja ya faida ya sigara ni kuupa Mwili Joto hasa kipindi cha baridi na haka kamvua mvua kanakonyesha.....
Pole
 
Anayeweza akusaidie link ya nini, TFDA wakisema soda sio sumu au wataalam wanaoonyesha kwamba soda ni sumu?

Katika masuala ya uthibitisho na migongano ya hoja yule anaesema kitu chanya ndio anadaiwa proof. Ukisema soda ni sumu wewe ndio thibitisha. Mimi nikisema Mungu hayupo siwezi kudaiwa uthibitisho kwa sababu hayupo, nitam prove vipi?

Sasa wewe tueleze umesikia wapi kwamba soda ni sumu, na ni sumu gani, na inafanyaje kazi mwilini, biochemically.
Nimesoma kwenye Muungwana Blog na imeandikwa hivyohivyo kuwa "soda ni sumu"
Hayo yote uliyoyataka utayapata humo na ndio link niliyoshindwa kuweka hapa. Nadhani nimeeleweka
 
Sometimes tuache lalamika ovyo tufanye kazi!... sasa unaifungulia soda thread ipigwe marufuku je sigara na pombe hujaona madhara yake ya haraka zaidi!?..Kila kitu kina madhara hata maji ELIMU ELIMU!!..
Sidhani kama nimeonesha kutaka ipigwe marufuku.
 
Sidhani kama nimeonesha kutaka ipigwe marufuku.
Ulikua unamaanisha nini kwenye hizi sentensi zako?.
Cha ajabu zaidi na kushangaza kama sio kusikitisha ni pale ambapo Mkuu wa kitengo kinachohusika na maswala hayo (ya vyakula na madawa) yaani TFDA alipoulizwa kuhusu jambo hilo na akatoa majibu mepesi na hoja tepetepe kabisa.
Majibu gani mazito ulitaka ayatoe Mkuu wa TFDA kwamba soda ni hatari msiitumie!!.
>>>alijibu soda sio kinywaji hatari kwakuwa kinatumiwa na watu wengi duniani.
Hili jibu lilijitosheleza sio kinywaji hatari yeah hata WHO wanakiweka kwenye uhatari only when in high consumptions.
Wananchi huwa tunapokea maelekezo kwa wataalam kutoka mamlaka husika Sasa je kwa hali hii tutategemea tuna mamlaka imara ya kutulinda wananchi kweli dhidi ya afya zetu?, mana hiyo ni soda tu je na vingine (ambavyo huenda tunatumia na wao wapo kimya)
Ukaishia lalamika falacy zisizo na maana bila toa way forward!.
 
Habari zenu ndugu zangu

Niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu... ni kuhusu kinywaji cha (aina ya) soda ambacho wataalamu wengi wa afya (kama sio wote) wamekifafanua sana kwamba ni hatari kwa afya na ni sumu inayoua polepole.

Sasa cha ajabu ni kwamba hapa kwetu (nchini) kinywaji hiki kimekuwa kikitumiwa (kuuzwa na kunywewa) bila hata ya tahadhari wala miongozo yoyote.

Cha ajabu zaidi na kushangaza kama sio kusikitisha ni pale ambapo Mkuu wa kitengo kinachohusika na maswala hayo (ya vyakula na madawa) yaani TFDA alipoulizwa kuhusu jambo hilo na akatoa majibu mepesi na hoja tepetepe kabisa.
>>>alijibu soda sio kinywaji hatari kwakuwa kinatumiwa na watu wengi duniani.

Wananchi huwa tunapokea maelekezo kwa wataalam kutoka mamlaka husika Sasa je kwa hali hii tutategemea tuna mamlaka imara ya kutulinda wananchi kweli dhidi ya afya zetu?, mana hiyo ni soda tu je na vingine (ambavyo huenda tunatumia na wao wapo kimya)

Nimeshindwa kuweka link hapo lakini nimesoma kwenye Muungwana anayeweza anisaidie tafadhali
Heeeh huwajui wasomibwa TZ watakwambia hata mkeo au mmeo ni sumu!
 
Back
Top Bottom