...basi you are one in a million...kuna watu wakifika nyumbani tu, cha kwanza mke/mume anaikagua mobile phone kisha anaiweka kibindoni mwake mpaka kesho utapoenda kazini, kila sms au simu itayoingia ataisoma au kuipokea yeye kwanza.....kwenye social network ndio balaa...anataka kujua sababu, nia na madhumuni ya kupewa comment, like, au tagged!
...eeeh? ushaona mtu anakusimamia u log in skype, au msn messenger kwakuwa anajua kuna live video, kisha yeye anajibanza nyuma ya kiti? paropokwe neno tu hapo,
...akikukosa huko, ana-print chat history!
Uamuzi wa busara sana huo. Maana unaweza ukaalikwa kwenye kikao Hongera Bar...mwenyewe ukafika huna hata wazo au nia mbaya. Ile unaketi tu unaulizwa 'we ndo Mbu?'. Kabla hata hujajibu chupa ya Balimi ishakupasukia kichwani....hahahaaa.
Hakika inauma.
oyaaaa arifu Balimi haizuwi Hongera, hizi zinapatikana kanda ya Ziwa huko...au huko kuna hongera Bar pia....manake ukigusa biya unagusa maslahi muhimu sana kwangu lol
Ooh kumbe haiuzwi lol! Basi hapo ndo ujue ikija kwenye mambo ya kilaji mi mweupe kabisa! Hongera Bar yenyewe huwa naionaga kwa mbali tu. Na ndo hiyo hiyo niijuayo mimi...ya hapo Shekilango.
Tulikuwa wachumba shostii, ndoa ilikuwa bado, ila on process.
Kwanza akaanza kujifutua, maana nilianza na mengine kwa upole tu na unyenyekevu wa high degree. Akakanusha, na akazidisha jeuri akasafiri na kusafiri. Afu akasugest ananiacha eti nina malalamiko na namsingizia sana through sms. Upande wa pili anadeka kweli kweli, eti anataka anione, aonje utamu wangu. Yeye yupo alone, na yuko conviced mimi ndo mke anaemhitaji. UPOO. Tukapanga kuonana mkoa tofauti na tulipo but hajui anapanga na mm. Tatizo likaja kwa sbb za kiafya nilikuwa bedrest na sikuruhusiwa kusafiri. Ndo nikaamua kumwaga ugali, nikimuuliza yote unadeny na hili? Stori ni ndefu shosti na kuna mengi ndani yake, i wish ndo ningekuwa nakuelezea face to face ingenoga. Facebooook!
[*]Kupunguza 'real time' cheating, lol (hapo inategemea definition ya cheating...a 'new' topic altogether)
Huo ni mtizamo wangu. tuendeleee
Tusiende mbali. Tuanzie na hapa hapa JF!
Wangapi humu kwa ufahari na majivuno kabisa wameutangazia umma wa JF kuwa wako kwenye ndoa na kwamba wenza wao hawapo hapa JF (sijui hata wanajuaje kwa uhakika maana humu wengi tunatumia majina bandia! Jitu linaweza likawepo na hata usijue kama lipo lol), lakini humu wamepata wenza wengine ambao wanataniana (huenda kuna zaidi ya kutaniana) na kuitana kila majina ya kimahaba?
Wewe unajidai ni mke au mume wa mtu lakini humu kuna mtu au watu unaowaita 'hun', 'honey', 'laaziz', 'sweetheart', na kadhalika. Na pengine unafanya hivyo bila ya ufahamu wa mwenza wako. Kwa nini? Hivi mwenza wako akijua unafanya hivyo atafurahia na kukaa kimya kweli? Labda huenda wapo ambao hawatatatizwa lakini pia wapo wengi ambao watakwazika!
Mimi nishasema mara kibao humu kuwa mtandao umechangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibu mahusiano ya kimapenzi. Hapa silaumu mtandao bali natambua mchango wake. Mwenye na wenye kubeba lawama mwisho wa siku ni muhusika na wahusika. Hilo halina ubishi. Lakini pia mchango wa mtandao katika kurahisisha utovu wa uaminifu hatuwezi kuukataa.
Kwa watu wahalisia kama mimi inakatisha tamaa kabisa. Manake ukikaa na kuanza kufikiria nini ambacho mtu anaweza kufanya kwa kutumia mtandao pasipo wewe kujua unabaki unatikisa kichwa na kujishika tama.
Saa ingine unabaki kuwaza sijui urudi tu Ikungu ukatafute ambaye hajui hata kutumia mtandao. Lakini hata Ikungu vi Nokia vyenye intaneti vipo. Facebook na yenyewe ishafika, hata Tagged nayo ipo. Gademu! Huna ujanja. Huna pa kukimbilia.
Mwisho wa siku inabidi tu ukubaliane na hali halisi kuwa ukiwa kwenye mahusiano na mtu uwezekano wa wewe kutendwa ni mkubwa kuliko hata unavyodhania. Kama bado hujatendwa basi ujue kutendwa kunakuja na usije shangaa kiungo cha kutendwa kikawa ni intaneti.
Duh, umeongea kwa hisia.
Hadi umenitisha hata kuwa hapa jf
ukiachia mbali fb ambapo napaogopa siku zote
sijui nilog off for good?!!
Kaka dearest,
Kwanza I mrs u (yaani missing u nyingi)
Pili, vile wewe ni mwanaume na if u don't do it u won't know how far it goes; lakini internet cheating sasa imefikia post doctoral whatever. Watu wanafanya cyber sex ile mbaya. Kuwa kwenye mtandao ni kama kupambana na vibaka wa buguruni, manake unakuwa na kazi ya kufokea na kugombeza invitations za hizo mambo hadi unachoka. Ukiskia mtu anasema king' anaringa, mjeuri, ana dharau wewe jua aisifiaye mvua imemnyea. Nitapita kwenu baadae,siku njema
Kumbe mbona hujaniambia hao wanaokugas gasi 'niwashughulikie' au inaingia kwen 'privacy' lol!
Hapo underlined, nadhani mi ni mnovisi, na hivi leo ni jumapili, ngoja ni do ze nidiful.....ntacheki PM yako baadaye..karibuni sana home tunawasubiri!.:A S-coffee:
No...dont bana tutakumiss Kongosho lol
Duh, umeongea kwa hisia.
Hadi umenitisha hata kuwa hapa jf
ukiachia mbali fb ambapo napaogopa siku zote
sijui nilog off for good?!!
hiki ndicho kipimo cha "akili" za mwanadam.wewe ambae unajitambua kama tunavyoambia kuwa mwanadam anajitambua kuliko viumbe vingine halafu unalalamikiwa kufanya mambo kama wasiojitambua inamaana gani?unawasiliana na mtu usiemjua au umemwona kwenye picha at the same time umeoa au umeolewa,mnaambiana mambo ya kijinga,mnapeana namba za simu,mnakutana kisha mnavuana nguo!kwa yule ambae yuko singo sina usemi,ila wewe ambae ni "mali" ya mtu unakua ni mzima au akili yako ina walakini?
Najaribu kujiuliza hivi hawa siku wakija kugundua walikua wanaflirt na waume/wake zao wenyewe nani atakua wa kwanza kumlaumu mwenzake? Nani atakua na ujasiri wa kumwambia mwenzie hajatulia? Au ndio kila mmoja atajikausha kama vile hamna kilichotokea?
Hahahaaha. . . yale yale ya "privacy muhimu". Yani mtu anakua na mambo ambayo watu wengine lukuki wanaweza kuona isipokua mpenzi wake!! Hapo ukute simu nayo haruhusu iguswe, JF yupo ila hajawahi.hata kumdokeza mwenzie. Nadhani watu wengine hawana haja ya kua kwenye mahusiano (wasio waaminifu, wasiotaka wenzi wao hata wafahamu kuna JF wakati ye anadai anafaidika nayo, wanaotaka kila kitu kibaki kuwa chake chake ) maana mwisho wa siku wanaishia kusumbuliwa na kukoseshwa raha tu na uwepo wa wenzi wao.
sasa kama tunakulana changa za mwili famili nzima itakuwaje?
Na sie wenye watoto wakubwa, ukute binti yako yuko huku, kijana wako na baba yao wote wako humu.
Tunajibiana pumba na kuambiana swit, han si laana hiyo.
Anyway, ngoja niendelee kuperuzi kwanza.
Jaribu kuwa mwelewa na upunguze wivu usiokuwa na tija, though akiamua kukusaliti anakusaliti tu!!!