SMZ haina ubavu wa kuyaondoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ haina ubavu wa kuyaondoa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jul 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Yaambiwa hiyo ni kazi ya Bunge
  [​IMG]
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.  Wakati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza kuondoa suala la mafuta ya petroli na gesi asilia kwenye orodha ya mambo ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano imesema hawana uwezo wa kuchukua hatua hizo.
  Kauli ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, bungeni jana akijibu swali dogo la Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
  Malima alisema SMZ haiwezi kufikia uamuzi huo kinyemela bila kujadiliwa na Bunge. Zitto alitaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu uamuzi wa SMZ wa kuondoa suala la mafuta yani petroli na gesi asilia kama ilivyotangazwa kwenye Baraza la Wawakilishi na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari jana.
  Malima akitoa kauli hiyo inayotafsiriwa kama mwanzo wa mvutano wa serikali hizo, jana wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF, walionyesha furaha yao kwa hatua iliyochukuliwa na SMZ, kuondoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano.
  Msimamo wa SMZ ulitolewa juzi na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2009/10 katika Baraza la Wawakilishi.
  Akieleza furaha yake kwa uamuzi wa SMZ, Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani, Ali Suleiman Ali, alisema Baraza la Mapinduzi Zanzibar, linastahili kupongezwa kwa uamuzi liliouchukua kwa vile suala hilo limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu na wananchi kupitia wawakilishi wao.
  Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Ali Denge Makame, alisema Waziri Mansour amefanyakazi kubwa kutetea maslahi ya Zanzibar katika suala la mafuta na gesi asilia na anastahili kuitwa ‘dume la mbegu’.
  Naye Mwakilishi wa Chonga, Abdallah Juma Abdallah, alisema kwa kuwa eneo la Tundaua Kisiwani Pemba ndio lenye dalili ya kuwepo mafuta serikali inapaswa kuanza kuchukua hatua za awali kutengeneza miundombinu ya barabara na maji kabla ya kuanza kukaribisha wawekezaji katika sekta hiyo kwa ajili ya utafiti na uchimbaji.
  Hata hivyo, Mwakilishi wa Kitope, Makame Mshimba Mbarouk, alisema hivi sasa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watapumua kwa vile wananchi walikuwa wakiwauliza kila mara kuhusu suala la mafuta.
  Mwakilishi wa Mkanyageni, Haji Faki Shaali, alisema hatua iliyofikiwa na Baraza la Mapinduzi, inastahili kuungwa mkono na wajumbe wote kwa vile suala la mafuta na gesi asilia litasaidia kutatua kero nyingi za umasikini zinazowakabili wananchi wake.
  Awali Malima alisema Wizara yake imesikia azma ya SMZ na kwa sasa inasubiri taarifa yake ya maandishi na kuiwasilisha katika Bunge hilo ili ijadiliwe kwa kina kwa kuwa chombo hicho ndicho chenye mamlaka ya kutoa uamuzi huo.
  Hata hivyo, baada ya swali la Zitto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, aliomba mwongozo wa Spika kwa madai kuwa kile alichoeleza kwamba ni upotoshaji mkubwa uliofanywa na Zitto alipokuwa akiuliza maswali yake.
  Katika maelezo yake, Marmo alisema: “Zitto ametoa matamshi mawili mazito ambayo yanaupotosha umma, sio kweli kwamba mwaka 1968 hakukuwa na Katiba ya Jamhuri, upotoshaji wa pili alioufanya mheshimiwa Zitto ni ule wa kusema kwamba kwenye Katiba kuna jambo limenyofolewa, naomba mwongozo wako mheshimiwa Spika kwa kumtaka Zitto afute kauli zake.”
  Hata hivyo, Spika Samuel Sitta, aliokoa jahazi kwa kueleza kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kunyofoa kitu kwenye Katiba isipokuwa Bunge na kumtaka Zitto awe makini katika matamshi yake.
  “Hakuna Mtanzania anayeweza kunyofoa kitu kwenye Katiba bila Bunge…mheshimiwa Zitto uwe makini na kauli zako, yote uliyosema leo ni sifuri na ninakusamehe kwa sababu mwaka 1968 hukuwa umezaliwa,” alisema.
  Katika swali la msingi, Mbunge wa Magogoni (CUF), Vuai Abdallah Khamis, alihoji faida ambayo imepatikana kutokana na uchimbaji wa gesi asilia na kuhoji pia kiasi cha faida ambacho kimepelekwa Zanzibar. Akimjibu, Malima alisema hadi Aprili mwaka huu, gesi asilia yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 149.7 imezalishwa kutoka Songo Songo na Mnazi Bay.
  Alifafanua kuwa tangu matumizi ya gesi asilia yalipoanza, serikali imeingiza kiasi cha Sh. bilioni 50.8.
  Aliongeza kwamba mapato hayo yamekuwa yakiingizwa kwenye mfuko mkuu wa Hazina ambao unagharimia kazi za Serikali ya Muungano.


  :: IPPMEDIA
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa nini SMZ imeona uzito kulipeleka suala hili Bungeni? Kama wanadai kama wameliondoa suala la gesi/mafuta kwenye mambo ya Muungano maana yake hayo yalikuwa ni mambo ya muungano. Sasa utaratibu wa kuyaondoa mambo hayo kutoka kuwa mambo ya muungano ni kupitia Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi? Wanachokiogopa ni nini?
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inaonekana hujalielewa hili jambo vizuri. SMZ hwajasema wameliondoa. Wanachosema baraza la mapinduzi (ndiyo SMZ ) hiyo inataka kuliondoa kwa maslahi ya Wazanzibari.. SMZ Imepeleka uamuzi wake Baraza la wawakilishi penye wawakilishi wa Zanzibar yote- Wa CUF na wa CCM- kwa maana hiyo Zanzibar nzima (siyo CCM tu)katika hali ile ili kupata ridhaa ya Wajumbe hao. Na wao kwa kauli moja wameridhia. Sasa SMZ itapeleka jambo hilo mbele kwa Sekali ya Muungano na Serikali ya muungano nayo italijadili katika Baraza lake la mawaziri. Ikikubaliana na uamuzi wa SMZ italipeleka Bungeni ambako (kimsingi kuna wawakilishi wote wa Jamhuri nzima ya muungano) sasa tatizo lipo wapi hapo. SMZ wamekikosea nini? Utaratibu gani haufuatwi. Au wewe umekuwa kichwa ngumu kuelewa utaratibu unaoutetea ambao mwenyewe huufahamu? Zaidi katika taratibu. Kama Bunge litakataa kuondoa suala hilo. Rais wa Jamhuri anaweza kuvunja Bunge. Ukaitishwa uchaguzi wakachaguliwa Wabunge wengine ambao kimsingi watapitisha hoja hiyo ya Serikali (SMZ na SMT). sasa huo ubabe wa wabunge na Spika Sitta uko wapi?
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SMZ haiogopi kulipeleka suala hilo katika bunge la Muungano. Lakini haini haja ya kufanya hivyo kwa kuwa hata mamlaka ya bunge kuliingiza suala hilo katika mambo ya muungano mwaka 1968 haikupata ridhaa ya wazanzibar. Ileweke kuwa kwa mujibu wa taratibu tulizojiwekea za sheria, sheria yoyote itakayotungwa na bunge kwa madhumuni ya kutumika kwa Jamhuri yote ya Muungano lazima badala ya kupitishwa bungeni iridhiwe na BLW(mtaona kama wanajifurahisha au vp) wakikubali ndo inatumika wakiktaa haitatumika hata kama rais ataisani (rejea sheria ya kuundwa Tume ya Haki za Binaadamu walivyoipigisha jaramba). Kama suala la mafuta liamuliwe na bunge si tatizo kama ule utaratibu wa awali wa kupitisha mambo ya Muungano bungeni utafuatwa. Hapa nakusudia kuwa ule utaratibu wa thuluthi mbili ya wabunge wa zanzibar pekee waridhie chini ya hapo, hakuna kitu hata kama bunge zima la wabunge wa bara wataridhi. Hivyo ndo utaratibu ulivyokuwa. Utaratibu huu umekiukwa katika mambo mengi mfano mabadiliko ya 11 ya katiba ya Muungano, ya kuyaondoa mamlaka ya Rais wa Zanzibar asiwe tena makamo wa Rais wa Muungano na kutumbukiza suala la Mgombea Mwenza katika kiti cha urais wa muungano. Ilichukuliwa thuluthi mbili ya mbili ya bunge zima badala ya utaratibu wa awali ya wabunge wa kila upande kufikia kiasi hicho katka maamuzi ya kupitisha mambo ya muungano. Mambo kama haya zanzibar ikilalamika wanaambiwa wanapiga kelele wakati wana hoja za wazi na za msingi kabisa. Lakini hataivyo kwa suala la mafuta na mengine tupo tayari kufika ICJ ambako tutajuwa mbivu na mbichi kwa kuwa muungano haukuundwa kwa sheria bali kwa mkataba wa kimataifa ambao ICJ wana mamlaka nayo. Hatuna hofu hatuna mashaka wala hatuogopi kitisho cha mdudu yoyote awe sitta saba nane hata tisa.......
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo penye kazi, zipi ni kazi za serikali ya muungano ambazo haziihusu zanzibar, na ni kwa vipi mapato yanayotokana na shughuli za muungano yanahakikiwa kuhakikisha kila upande wa muungano hauishii kuunyonya upande mwingine?

  Mie ndio sababu naamini hadi kesho kuwa, la msingi ni kuwa na serikali moja, hiyo zanzibar iwe kama ilivyo ukerewe, au vinginevyo Wazanzibar wapewe nafasi waende kama taifa. Ukweli ni kuwa majibu ya waziri yanaonyesha wazi kuwa hakuna mwenye kujua kuwa ni kiasi gani kimeisaidia upande wa zenji, japo wao wana-enjoy zaidi kwenye muungano kuliko tufanyavyo wabara!
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo hela (ya gesi) ukiitia katika mfuko mkuu inahudimia mambo ya Muungano. Polisi, Jeshi, Mambo ya Nje na yote yale yaliomo katika Muungano . Lakini kweli itakuwa imewahudumia Wazanzibari kama inavyowahudumia Wa-Bara katika mambo ya elimu, afya, kilimo, usafiri, na mengineyo? sasa hebu nieleze katika picha hiyo pana- kweli Wazanzibari wamefaidika na gesi kama wanavyofaidika wenzao wa Bara? Chambua kwa upana -Bwana.
   
Loading...