Yanaweza kuwa yale yale haya makampuni hayatabili jana nime chat na hao jamaa wa Smile maana nilivutiwa na bundle zao wakanambia hizo bundle ni Unlimited kwa speed ulolipia i.e haupimiwi GB/TB za kutumia!
Kuna mtu nchi ya jirani ambako pia kuna Smile alinambia kuwa hizo bundle wanazi misuse nchi kwao unakuta mtu anapewa mpaka 200GB zikiisha imekula kwake!
Router za Smart ni za 4G hivo sina wasi wasi na uwezo wake katika perfomance ila pia Smart ni mtandao pekee ulokua ukitoa Unlimited ya 3G kwa watu waishio nje ya DSM kwa 20,000/= kwa mwezi bila kubaniana speed wala hizo GB kadiri ya mchangiaji mmoja wapo wa jukwaa hili!
Kuna rafiki anaishi Upanga hapo amewai kunitumia speedtest ya smart ilikua inacheza 21Mbps na aki download kwa IDM inapanda hata kufikia 4MB/sec
Mimi mwenyewe nilitumia kipindi cha nyuma kidogo hiyo smart ila speed haikuwa pleasing kwangu kabisa
Pitia Thread hii hapa nilianzisha mimi :
Angalie Smart 4G LTE ilivo Slow utafikiri 3G
Kuna mdau alitoa speed test yake kwa kutumia Simu japokuwa which I believe itakua hiyo hiyo kwa router
Kuhusu hizo Bundle za Unlimited labda usubiri kama kuna mtumiaji akupe experience ila vinginevyo waweza kupata picha ya perfomance incase watakua hawabani kitu chochote ila pia ungewapigia wakuhakikishie ili kitu kikienda mlama unawapandia hewani kuwauliza vipi inakuwa kinyume na walivokueleza