SLO Iramba na walimu wakuu kadhaa watiwa mbaroni kwa matumizi mabaya ya Tsh milion 170

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Habari wadau wa JF.

Habari kutoka wilayani Iramba ni kuwa Afisa takwimu wa idara ya elimu msingi, na walimu wakuu kadhaa wanashikiliwa kwa maelekezo ya TAKUKURU wilaya.

Chanzo cha kushikiliwa kwa SLO huyo Bwana Mgimba ni matumimizi mabaya ya hela za ujenzi wa vyoo saba ktk shule saba wilayani hapo. Inadaiwa serikali imetoa Tsh million 170 kwa ujenzi huo lakini watuhumiwa hawa, walizitoa pesa haraka na kuruhusu wakandarasi kuanza kazi bila kufuata utaratibu wa Zabuni.

Awali mkuu wa wilaya Emmanuel Luhahula, alibaini tatizo hili na kuagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi. Baada ya TAKUKURU kuanza kazi SLO Mgimba alitaka kuwahonga jambo hili liishe salama na ndipo TAKUKURU wakamwekea mtego ulioweza kumtia ktk ushahidi shahidi uliowezesha kutiwa kwake mbaroni.

Utaratibu wa kuwasaka walimu wengine umekamilika na muda wote watapelekwa mahakamani kujibu makosa ya uhujumu uchumi, ukiukwaji wa sheria ya zabuni na manunuzi ya Umma. Pia makosa mengine ni matumizi mabaya ya madaraka na kumkosea adabu mwajiri.

Pia TAKUKURU kwa tetesi inadaiwa itawahoji na kuelekeza mamlaka za teuzi kuwaajibisha Maafisa Elimu wa kata husika kwa kuruhusu walimu kuchota fedha za Umma pasipokuzingatia utaratibu.
 
Kwa serikali hii ya kukusanya mapato, hapo watapewa option ya kulipa hizo pesa tu wakishindwa inakula kwao.
 
Habari wadau wa JF.

Habari kutoka wilayani Iramba ni kuwa Afisa takwimu wa idara ya elimu msingi, na walimu wakuu kadhaa wanashikiliwa kwa maelekezo ya TAKUKURU wilaya.

Chanzo cha kushikiliwa kwa SLO huyo Bwana Mgimba ni matumimizi mabaya ya hela za ujenzi wa vyoo saba ktk shule saba wilayani hapo. Inadaiwa serikali imetoa Tsh million 170 kwa ujenzi huo lakini watuhumiwa hawa, walizitoa pesa haraka na kuruhusu wakandarasi kuanza kazi bila kufuata utaratibu wa Zabuni.

Awali mkuu wa wilaya Emmanuel Luhahula, alibaini tatizo hili na kuagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi. Baada ya TAKUKURU kuanza kazi SLO Mgimba alitaka kuwahonga jambo hili liishe salama na ndipo TAKUKURU wakamwekea mtego ulioweza kumtia ktk ushahidi shahidi uliowezesha kutiwa kwake mbaroni.

Utaratibu wa kuwasaka walimu wengine umekamilika na muda wote watapelekwa mahakamani kujibu makosa ya uhujumu uchumi, ukiukwaji wa sheria ya zabuni na manunuzi ya Umma. Pia makosa mengine ni matumizi mabaya ya madaraka na kumkosea adabu mwajiri.
Tutadesa hapa pindi tunamfikisha magufuli mahakamani
maana makosa yanafanana.
 
mbona hatari hii,watu bado wanatupiga tuu.
Tatizo watumishi wengi wa Umma hasa wakuu wa idara huwa wana tamaa sana. Hata waongezwe mishahara hawawezi kuacha wizi. Wanaamini ukiwa mkuu wa idara ndiyo wakati muafaka wa kujitajirisha kwa fedha za walalahoi/Umma.
 
Back
Top Bottom