Slaa yupo safi, lakini....

Tolowski

Senior Member
Apr 28, 2011
122
20
Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kumsikiliza slaa kwa utulivu last saturday pale tegeta road kwenye kongamano la chuo kikuu cha ardhi! Nasema kwa utulive bcoz tulikuwa watu wachache and wengi tuliokuwepo pale ni wasomi.

Slaa yupo kwenye level nyingine kabisa ya utafiti wa mambo na uelewa. Nimekuwa najiuliza kama wanacdm wa kawaida hata wengine waliopo humu jamvini wanamwelewa yule mzee. Kuna vitu nilivipenda sana kuhusu slaa siku ile:

1. Yupo tayari kuomba msamaha akikosea na anakubali makosa,hilo alilionesha baada ya kuchelewa kufika kwa kama masaa3 hivi, alitoa sababu ya kuchelewa and akasema kwa mtu ambaye anataka kuongoza nchi halafu anachelewa basi hapo kuna walakini! Hivi kama Dr anaomba msamaha akikosea kwa nini humu jamvini watu ni wagumu sana kuapologize even if wanatoa kauli ambazo hazielezeki?

2. Slaa ni mkali sana, nakumbuka wakati anahutubia kuna sharobaro flan (makamu m/kiti BAVICHA Dsm) alikuwa anapiga stori na yule jamaa anaitwa benson, Slaa alimkaripia live bila chenga na kumwambia kama ni stori asubiri yeye akimaliza!

3. Ni mwelewa sana,kuna siku niliposti thread kuelezea ukosefu wa wanawake katika mikutano ya cdm,watu walinikashifu sana humu ndani! Lakini siku ile slaa alivyoiadress hiyo issue ni kama alisoma thread yangu! Pale pale aliwaagiza mdee and suzan lymo walishughulikie hilo swala. Alisema ukomboz unaowaacha wanawake nyuma una walakini! Since that day nimemsikiliza slaa nimetafakari sana na kujihisi wa tofauti sana,as if nimezaliwa mara ya pili au nimepigwa preaching kali na Benny Hinn!

Jamaa nimemkubali tena sana tu, kama ni makosa anayo and so is every human being, hakuna malaika hapa!

But pamoja na yote hayo inabidi tuhoji maamuzi yake, inabidi naye awe subject to scrutiny, asiwe Mungu mtu hapo ndipo tutaweza kujenga Tz bora zaidi! Slaa alisema msomi inabidi awe na hv vitu vitatu! SEE, JUDGE and ACT!

Tayari nimesee, judge and nataka kuact! Sijui niact vipi? Nipo kwenye ambiguity
 
Unaniangusha mkuu. Kama wewe ni msomi huhitaji mafunzo ya ziada kuelezwa u act vipi? Hiyo See, jugde na act usiipe narrow interpretations iko pana sana mkuu. ACT.
 
Ni kweli Dr.slaa Yupo safi.Ni kongamano ambalo lilikuwa zuri kwa malengo na mikakati iliyowekwa,..lakini watu walikuwa wachache sana,....Unajua tatizo nini,,....CHADEMA chuo cha ARDHI walipewa serikali ya Wanafunzi wakaiba pesa,...watu wakaona hii inakuwaje Kumbe mwizi ni tabia Sio CCM.Wakawatosa,...Shtuka weka maslahi ya taifa mbele sio chama.
 
Mkuu hata kusubiria muda wa ku ACT ni action. Life is all about ACTING.
 
Huyu dr silaa a.k.a dr mabunduki hana lolote si chochote anajidai anapigania wa tz lakin wapi! Hospilali ya CCBRT yeye ndie mdhamini mkuu na ndie aliefanikisha kuileta hapa Tz lakini ukifika pale gharama kubwa bei za madawa kubwa yaani wizi w2pu.Alafu anadanganya eti akipata Urais huduma za afya zitakuwa bure! Ni msanii.
 
Sijakuwahi kujua kama mtu anayeishi kwa kupingana na amri ya Mungu inayokataza ZINAA akawa msafi, mtampamba sana lakini ukweli upo palepale, uraisi utausoma kwenye magazeti. Msichoke na jitihada zenu

Chama
Gongo la Mboto
 
Huyu dr silaa a.k.a dr mabunduki hana lolote si chochote anajidai anapigania wa tz lakin wapi! Hospilali ya CCBRT yeye ndie mdhamini mkuu na ndie aliefanikisha kuileta hapa Tz lakini ukifika pale gharama kubwa bei za madawa kubwa yaani wizi w2pu.Alafu anadanganya eti akipata Urais huduma za afya zitakuwa bure! Ni msanii.
kwani serikali inampa pesa ya kuiendesha ike ccbrt'? Mpak atoe huduma bure? Kinana alilizungumzia hilo na majibu aliyopewa akurudia tena
 
wewe sio msomi hata kidogo, yani unamshangaa mwanasiasa ambaye hajapata anachokitaka kuongea maneno kama hayo!!!! mkumbuke jk na akina yakhe wengine, hata hivyo sio kwamba slaa sio mzuri ila point ulizotumia kumsifia ni dhaifu mno
 
Nina wasi wasi na umri, malengo na akili ya mtoa mada, sisi wengine tupo humu kila siku na tunatunza rekodi vizuri sana, huwezi kumkubali mtu kwa kumsikiliza mkutano mmoja wa tegeta wakati mwaka jana kulikuwa na uchaguzi mkuu na ndio ulikuwa muda wa kuwajuwa wagombea wote, na ulitakiwa ujiulize ni kwa nini Kikwete alimkimbia Slaa kwenye Mdahalo.
wewe una agenda yako ya siri na ukitaka nikuthibitishie nikuwekee post zako zote unazoiponda CHADEMA na Slaa. NIJUAVYO MIMI LABDA AJILA YAKO IMEKWISHA CCM, maana wengi siwaoni siku hizi humu.
 
Baba yako ndiyo anafaa nini au malimbukeni wenu CCM,Usiwe na akili mgando wewe na kuwaza kwa kutumia makamasi kama NAPE
 
kama yuko tayari kuomba msamaha basi awaombe watanzania msamaha kwa kulazimisha chama chake kimlipe mamilioni ya pesa ambayo yangesaidia kuboresha chama chake mikoani kwa kujenga ofisi na kuboresha zilizopo.
 
Huyu kijana/mzee aliyetoa hii mada anajiita msomi!!! Mbona maelezo yake hayathibitishi kama kweli yeye ni msomi? Huyu jamaa huenda ame2mwa na nina mashaka huenda ana kadi feki ya uanachama wa chadema ebu jaribuni kumchunguza.
 
Sioni ajabu mtu kusifia kitu apendacho,nikiwa muhitaji wa swala fulani hata kama ni mkorofi kiac gani lazima nitanyenyekea mpaka nifanikiwe!TUSIWE WAVIVU WA FIKRA iweni na akili tambuzi kabla ya kuwasilisha/kukosoa hata kupongeza,ushabiki ni ugonjwa
 
Back
Top Bottom