Slaa: Watanzania ipuzeeni CCM- Asema imeonyesha dalili za kufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa: Watanzania ipuzeeni CCM- Asema imeonyesha dalili za kufa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by sijui nini, Oct 11, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka Watanzania kupuuza ujumbe mfupi wa maneno (sms) unaosambazwa kupitia simu mikononi kuwa ni ujanja wa Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuona kimekabwa koo kila kona. Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Kalinzi, Dk. Slaa alisema CCM imekabwa koo kila idara hivyo imelazimika kutuma ujumbe kuwahadaa Watanzania ili waamini uongo unaosambazwa.

  “Nimesikia wanasambaza ujumbe kwenye simu za mikononi wanasema mimi ni mropokaji… nawaambia Watanzania wenzagu, wapuuzeni CCM hii ni dalili tosha kwamba tumewakamata kila kona wanahaha kujinasua…hizi ni porojo za CCM; zinaonyesha wazi sasa wameanza kutapatapa kama mtu anayetaka kufa, imeonyesha sasa ni kama inapumulia mashine,” alisema Dk. Slaa.
  Alisema kutokana na hali hiyo, CCM imekuwa bingwa wa kumzushia mambo mbalimbali ambayo hayana ukweli wowote mbele ya jamii.

  Akizungumzia suala la yeye kuambiwa anataka kwenda Ikulu kwa njia ya kumwaga damu, Dk. Slaa alisema amekuwa mbunge wa jimbo la Karatu kwa kipindi cha miaka 15 bila kumwaga damu ni kitu ambacho hakiwezekani hata siku moja.

  “Nimekuwa mbunge wa Karatu kwa kipindi cha miaka 15, sikumwaga damu… sasa hiyo damu itatoka wapi? Kwa vile tumefanikiwa kuwabana wanahangaika kujinasua,” alisema Dk. Slaa.
  Alisema pamoja na yeye kuitwa mropokaji, anakubali kwa vile uropokaji huo umezaa matunda kipindi chote alichokuwa bungeni.

  “Wananiita mropokaji, mimi nasema sawa nimeropoka na matunda yangu yameonekana, niliwataja watu kama Basil Mramba, Gray Mgonja na Daniel Yona mbona wamefikishwa mahakamani? “Kama nisingefanya hivi wangeendelea kutafuna fedha za walipa kodi wa nchi hii….nawaambieni jamani hata wakati ule nilimtaja Rais Jakaya Kikwete mbona hawajanikamata kama ulikuwa uongo?” alihoji Dk. Slaa na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.
   
 2. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hapaa patamu hapa..
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Watanzania wa leo sio wa mwaka 47 wanajua kuwa CCM ni chuya na CHADEMA ni Mchele
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata Wakitumia Style za Mafia...Character Assassination, hawana jinsi, ni watanzania wanamwona Dr Slaa kama shujaa wao na sio CCM wawaelekeze watanzania maana wao CCM wamekuwa Madarakani kwa karibia Miaka 50 na waanzilishi wao, hawakuweza kuwapa wananchi somo na Ufahamu ambalo Dr Slaa anawapa Watanzania wote kwa muda wa Miezi miwili na nusu tu ya Kampeni hadi CCM inakaribia kupasuka kwa migongano na fadhaa! Je kama Dr Slaa akiwa Rais na kukaa madarakani kwa Mwaka, au Miaka mitano wananchi watafumbuka na kupata mafanikio kiasi gani?? Na sembuse hiyo miaka 10 ya awamu mbili kama akiipata??
   
 5. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  kwanini kama..!!
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  go dr. Slaa........................go to the state house................................................
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sisi tunatakiwa kuitafakari hali hii...Tuungane na tupaaze SAUTI YA PAMOJA KUWA, NCHI YETU INAKOMBOLEWA, Imepata MKOMBOZI. Hakuna wa kuziba midomo ya wanyoge na wenye haki. Hata nguvu za Mafia zilishindwa, Ukomunisti ulifikia kikomo, Marekani - Republican walitumia style hii hii ya CCM kumdhoofisha Obama kwa kusema ataiweka Marekani kwa Magaidi, yeye mwenyewe gaidi-msomali na sio Raia, ila kwa kuwa mabadiliko yalikuwa ni mkondo usiopindwa kwa njia za kifidhuli na kutisha watu...Obama aliikomboa Marekani, alikomboa kizazi chote na bila mwaka kupita, Obama ametunikiwa Nishani, na heshima ya Marekani imezidi kungara...! Ndiyo maana tunasema, hata wakitumia mbinu chafu, Umafia na kudhoofisha fikra za watanzania kwa woga, mabadiliko lazima...CHANGES ARE COMING...YES WE CAN CHANGE TANZANIA...!
   
Loading...