Watanzania waiomba na kuipigia Magoti CCM iwaletee Rais Samia Uchaguzi Ujao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu watanzania,

Kutokana na uchapa kazi wa Rais Samia ,juhudi zake katika kuimarisha uchumi,demokrasia ,kuvutia wawekezaji,wafanyabiashara, kukuza na kujenga uchumi jumuishi, kujenga na kuimarisha umoja wa kitaifa,kujenga miradi mbalimbali ya kimkakati iliyochochea mzunguko wa fedha mitaani, kuimarisha huduma za kijamii na kusogeza karibu ya wananchi, kupambana na mfumuko wa Bei kishujaa, kurudisha mamlaka na kuiweka serikali mikononi mwa wananchi, kuwa mtetezi wa wananchi pamoja kuwasikiliza wananchi wanataka Nini.

Mambo hayo yamepelekea watanzania kuguswa na utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia na serikali yake,hivyo kuiomba CCM iwaletee mama Samia Uchaguzi Ujao ili walimpe kwa kumpigia kura za Ndio kwa kishindo kwa kuwa amekidhi matarajio Yao na kukata kiu yao, wameiomba CCM kwa kuwa wanafahamu na kutambua ya kuwa Rais Bora, shupavu, imara, mzalendo, Jasiri na madhubuti Ni lazima atoke CCM, wanatambua ya kuwa Ni CCM pekee yenye uwezo wa kutoa Rais wa kuongoza Taifa letu,Ni CCM pekee yenye uchungu na maisha yao na Taifa lao, wanatambua kuwa Ni CCM pekee yenye mfumo imara wa kiuongozi wenye kutoa kiongozi na viongozi wenye uadilifu na uzalendo na Taifa letu.

Ni jukumu la CCM na wanaccm kusikiliza sauti za watanzania zinataka Nini ,zinamtaka Nani na kwa sababu zipi, sauti za mamilioni ya watanzania zinasema Rais Samia anatosha Kuendelea Kuliongoza Taifa Letu kwa muhula wa pili kwa kuwa ameonyesha uwezo wa kiuongozi katika kuiongoza na kuisimamia serikali Yake katika kuwahudumia watanzania.

Ni Rais Samia na serikali Yake ametuvusha watanzania kipindi kigumu Cha mdororo wa uchumi uliotokana na ugonjwa wa corona pamoja na Vita vya ukrein vilivyopelekea mfumuko wa Bei,kushuka kwa uzalishaji viwandani,kupungua kwa mzunguko wa fedha mitaani, kufungwa kwa shughuli nyingi za kibiashara,kupungua kwa watalii n.k, lakini kwa ushupavu na umadhubuti wa kiuongozi wa Rais Samia na serikali Yake alikabiliana na Hali hiyo kwa kutoa mabillioni ya Ruzuku katika Nishati ya mafuta pamoja na kilimo, alivutia wawekezaji kuja Tanzania, watalii kuongezeka kutokana na wazo lake la kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake vya kiutalii kupitia Royal Tour,kuimarisha mazingira ya kiuwekezaji,kusaidia secta binafsi kukua na hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa vijana kwa wingi,kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na hivyo kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutokana na kuwa na Imani na serikali pamoja na Sera zake za kiuwekezaji.

Ni Rais Samia na serikali Yake waliotufikisha hapa tulipo ambapo Sasa Elimu Ni bure Mpaka kidato Cha sita,hakuna mwanafunzi anayeshindwa au kukaa nyumbani kwa ukosefu wa vyumba vya madarasa hii Ni baada ya kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20, Sasa Biashara zinafunguliwa kila Kona ya nchi na Hakuna habari za kufungwa kwa biashara au kupunguzwa kwa wafanyakazi, mapato au makusanyo ya Kodi yameongezeka mpaka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi pasipo kufukuzana Wala kuwafungia biashara wafanyabiashara mitaani. Sasa Tanzania inaandikwa kwa mema kimataifa na kutangazwa vyema katika TV za kimataifa,Sasa Tanzania Ni chaguo namba moja la watalii na wawekezaji huku wakipishana angani Kuja Tanzania,Sasa viongozi wa mataifa makubwa wanapanga ziara na kuitembelea Tanzania na kuja na kila aina ya mafursa ya kiuchumi kwa watanzania.

Ukweli Ni kuwa Rais Samia anapendwa Sana na watanzania bila kujali itikadi za kisiasa,anakubalika Sana na makundi yote hapa nchini, Ameziteka mioyo ya mamillioni ya watanzania kutokana na uchapa kazi wake.

Rais Samia Ni kiongozi mwenye maono, dira na muelekeo unaoeleweka, Ni kiongozi mwenye ndoto ya kuona Taifa hili linakuwa Nembo ya Afrika na kila mtanzania Anaishi maisha Bora, Ana ndoto za kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi mkubwa na ulio katika mikono ya watanzania, Ana ndoto ya kutaka kuona maadui zetu wa umaskini, ujinga na maradhi wanabaki kuwa historia, ndio maana ya kujenga shule , vituo vya Afya na kutoa mabillioni ya Ruzuku katika kilimo kwa kutambua ukweli kuwa ndio secta iliyobeba na kuajiri kundi kubwa la watanzania,hivyo ukigusa kilimo umegusa maisha ya mamillioni ya watanzania,ukiinua kilimo unakuwa umewainua watanzania.

CCM haina budi kusikiliza sauti za watanzania,Haina budi kupokea maoni ya watanzania juu ya hitaji lao la kuwapatia mama Samia Kama mgombea wa kiti Cha Urais, watu ndio wanajuwa Nani anapaswa kuwa kiongozi wao kutokana na uchapa kazi wake,usikivu wake,uzalendo wake,historia yake kiutendaji,uadilifu wake,utu wake katika kuwaongoza watu, busara na hekima katika kufanya maamuzi, misimamo yake kiuongozi kwa maslahi mapana ya Taifa na utayari wake katika kuwatumikia watu.

Katika kutathimini hayo watanzania wameona Rais Samia anawafaa na amekidhi vigezo hivyo ndio sababu ya kumhitaji na kuiomba CCM iwaletee uchaguzi ujao,wasingepeda CCM iwaletee mtu mbinafsi, katili, asiyeambilika Wala kusikiliza la mtu, atakaye wagawa watu kwa misingi ya ukabila,Dini na ukanda, atakayeleta ubaguzi, wasingepeda CCM iwaletee mtu atakaye pasua Taifa letu kwa ulimi wake,atakayewaliza na kuwabubujisha machozi watanzania, atakayewatia umasikini badala ya kuwainua kiuchumi,atakayewafanya wajione wanabahati mbaya kuzaliwa Tanzania, hawataki CCm iwaletee kiongozi wa namna hiyo, wanamtaka mama Samia atakaye kuwa Kama mfariji wao na Mtumishi wao, atakaye wategea masikio na siyo kuwararua masikio yao kwa kauli zake mbaya na za vitisho, hawataki waletewe mtu wa kuwadharau ,ndio maana wamemchagua na kupendekeza mama Samia maana wameona anakidhi vigezo vyao.

Mjumbe hauwawi ,Mimi Ni mjumbe tu niliyeleta ujumbe wa watanzania, nisichukiwe kwa kuleta ujumbe wa watanzania, Naendelea kumuunga mkono Rais Samia na serikali Yake katika kulitumikia Taifa letu, Naendelea kubaki mtetezi wa CCM na serikali yake hapa jukwaani na popote katika ardhi ya Tanzania na nitaendelea kulipigania Taifa langu wakati wote, sitaogopa kutukanwa na sitamtukana yeyote atakayenitukana kwa kuwa kifua changu ni kikubwa Sana na kilicho imara madhubuti na shupavu katika kuhimili vishindo vya matusi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Daah mkuu katika machawa we ni bonge la Chawa ... Unafaa kusimamia UVCCM, possibly unalipwa vzuri..
Daah mkuu katika machawa we ni bonge la Chawa ... Unafaa kusimamia UVCCM, possibly unalipwa vzuri..
Hapana Mimi silipwi kuja kuandika hapa,Ni uzalendo kwa Taifa langu unaonipa nguvu ya kuandika na siku zote wazalendo hufanya vitu kwa hiyari na kwa kujitolea na siyo kutaka malipo au kulipwa Fadhira na mtu
 
Eeehh Mwenyezi Mungu, twakuomba umpe afya na hekima mama yetu SSH, bado tunamuhitaji asafishe nchi. Ameen
Kwa hakika Mwenyezi MUNGU Aendelee Kumjalia Rais wetu mama Samia Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania,tunampenda na tunahitaji Sana Kuendelea kutupatia watanzania Tabasamu na matumaini ya kusonga mbele kiuchumi
 
Hapana Mimi silipwi kuja kuandika hapa,Ni uzalendo kwa Taifa langu unaonipa nguvu ya kuandika na siku zote wazalendo hufanya vitu kwa hiyari na kwa kujitolea na siyo kutaka malipo au kulipwa Fadhira na mtu
Hahaha Lucas mwashambwa ni ngumu sana Rais Samia kumtenga kinachoendelea. Sisi kama chawa tunapaswa tutafute taarifa za mitaani tumueleze mama ukweli na mategemeo ya wapiga kura. Kwa huu mtindo wako haumsaidii kabisa rais Dkt Samia na CCM. Hii ni kwa sababu huna ushahidi ila ufisadi, kukatika umeme na mfumuko wa bei una ushahidi tena uliojaa tele.
 
Back
Top Bottom