Elections 2010 Slaa: Matokeo yataishangaza dunia

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
Chadema kimesema kitaishangaza dunia kutokana na matokeo ya kura za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu kwa kushinda kwa kishindo katika nafasi zote.

Aidha, chama hicho kimesema kinatarajia kushinda katika nafasi nyingi kuanzia udiwani, ubunge na urais kwa kuwa dalili za ushindi huo zimeanza kuonekaka kutokana na watu kuikubali ilani yake.

Kauli hiyo ilitolewa jana katika viwanja vya Kimara Suca, jijini Dar es Salaam, na mgombea wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa, wakati akizindua kampeni za mgombea ubunge jimbo la Ubungo, John Mnyika, pamoja na madiwani wa jimbo hilo.

Alisema CCM kijiandae kwa kubwagwa na kumtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, kuacha kuudanganya umma kwamba wana nafasi ya kuendelea kuitawala nchi, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

"Mwaka huu tutaishangaza dunia kwa kukiondoa madarakani CCM... kwa kuwa Watanzania wamechoka kuburuzwa na wako tayari katika mapambano ya kuleta mageuzi," alisema Dk. Slaa.

Alisema Chadema ikishinda hakitavunja Muungano kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, bali kitaboresha kwa kuunda serikali tatu ambazo ni, Serikali ndogo ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika ambayo itashughulikia masuala ya Tanzania Bara na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, itakayoshughulikia masuala ya ulinzi, fedha na mahusiano ya kimataifa.

Mbali na hayo, alisema taifa liko kwenye msiba kwa muda wa miaka 50 sasa ambao ni maradhi na umaskini uliokithiri.

Kwa upande wake, Mnyika alisema wakimchagua kwenda kuwawakilisha kwa miaka mitano ijayo, amejiandaa kutatua matatizo sugu ikiwemo, ajira, elimu, miundombinu, maji, ardhi na afya.

Mnyika aliwataka wananchi waamke kwa kuchagua madiwani wa Chadema ambao wataweza kupambana na ufisadi wa fedha za halmashauri yao ya Kinondoni.

CHANZO: NIPASHE
 
Chadema kimesema kitaishangaza dunia kutokana na matokeo ya kura za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu kwa kushinda kwa kishindo katika nafasi zote.

Aidha, chama hicho kimesema kinatarajia kushinda katika nafasi nyingi kuanzia udiwani, ubunge na urais kwa kuwa dalili za ushindi huo zimeanza kuonekaka kutokana na watu kuikubali ilani yake.

kweli siasa ni kitu cha ajabu sana.... najaribu kutafakari basis ya hii comment nashindwa kupata jibu

Mfumo uliopo sasa ni wa kibabe, maguvu, wizi, unyonyaji nk. Sijui Slaa amepata wapi hizi data zake

nafananisha hii view yake kama kuchukua xardiovascular system ya mtu ukampa tembo aitumie
 
Kweli wataushangaza dunia kwa kupata 10% ya kura zote,Padri ajiandae kurudi mizabahuni!
 
Unapoenda vitani lazima ujipe moyo!
Ila usije shangaa wakashinda kweli alafu rafu zikachezwa na tonge kuondolewa mdomoni kama kenya iliwezekana why not Tz
 
kweli siasa ni kitu cha ajabu sana.... najaribu kutafakari basis ya hii comment nashindwa kupata jibu

Mfumo uliopo sasa ni wa kibabe, maguvu, wizi, unyonyaji nk. Sijui Slaa amepata wapi hizi data zake

nafananisha hii view yake kama kuchukua xardiovascular system ya mtu ukampa tembo aitumie

utaelewa tu ngoja ifike october 31
 
utaelewa tu ngoja ifike october 31
Watu kama hao wasiohitaji mabadiliko kuna wakati tutawalazimisha kunywa maji kwa nguvu hata Nyerere alitumia fimbo kuwaelimisha watu wabishi kama hao waliopinga kujitawala.
 
lazima chadema kiiishangaze dunia iwapo kitachaguliwa huku kikiwa na mgombea mwenza mwenye elimu ya msingi :confused2:
 
Watu kama hao wasiohitaji mabadiliko kuna wakati tutawalazimisha kunywa maji kwa nguvu hata Nyerere alitumia fimbo kuwaelimisha watu wabishi kama hao waliopinga kujitawala.
once again, you didnt understand my post and Kigogo understood what i was referring to....

BTW, do you really take time to read and understand posts au ni ushabiki maandazi tu??
 
Kushinda uchaguzi si kazi rahisi, hasa kwa nchi yenye utawala kama tulionao...yawezekana kabisa Chadema kushinda majimbo kadhaa na Urais lakini bado CCM kwa kuwa wamesimamisha wagombea ngazi zote kwa 100% itakuwa ngumu kwa wapinzani kuishangaza dunia kwani wao wamesimamisha wagombea katika maeneo kadhaa na si kwa 100% hivyo kuongoza nchi yaweza kuwa kitu kigumu zaidi kwao kuliko kushinda huo uchaguzi...all in all, ushindi unawezekana ila unaweza kuwa wa taabu sana kwani yanayotokea kwenye chaguzi tunayajua...tusubiri tuone change itatokea au chama tawala kitaendelea kutawala..
 
once again, you didnt understand my post and Kigogo understood what i was referring to....

BTW, do you really take time to read and understand posts au ni ushabiki maandazi tu??
mtaelewa tu hata kwa fimbo ikibidi
 
Vijana kwa wazee tuhakikishe tunapiga kura kwa CHADEMA hapo october 31 2010.
 
Kushinda uchaguzi si kazi rahisi, hasa kwa nchi yenye utawala kama tulionao...yawezekana kabisa Chadema kushinda majimbo kadhaa na Urais lakini bado CCM kwa kuwa wamesimamisha wagombea ngazi zote kwa 100% itakuwa ngumu kwa wapinzani kuishangaza dunia kwani wao wamesimamisha wagombea katika maeneo kadhaa na si kwa 100% hivyo kuongoza nchi yaweza kuwa kitu kigumu zaidi kwao kuliko kushinda huo uchaguzi...all in all, ushindi unawezekana ila unaweza kuwa wa taabu sana kwani yanayotokea kwenye chaguzi tunayajua...tusubiri tuone change itatokea au chama tawala kitaendelea kutawala..

Thanks mkuu, the challenge ni ile lack of joint and collective strategy among opposition network... to me it is impossible to oust a ruling party kama ccm if we continue with our fanaticism, what we need is a joint approach and effective intelligence ya mbinu watumiazo ccm, and one of them ni intimidation, especially to the poor people na hivyo kunyang'anya rights zao

Ningefurahi zaidi kama angesema chadema itaishangaza dunia kwa jinsi itakavyopambana na wizi wa kura na public intimidation ya voters kwa kusambaza elimu ya uchaguzi, haki na wajibu kwa wananchi...

safari bado ndefu sana
 
Waambie!! Hao ndiyo wale 70 % wa JK. Mwaka huu mpaka kieleweke.
inshallah october 31mungu akiniweka hai ntajifunza, na nitafufua hii mada tarehe 6 november kama watu wataikaukia.... read post #20
 
CHADEMA wataiishangaza dunia kwa vile sisi wananchi hatukubali kuwa mirija ya kunyonywa na CCM ni sisi tutakao fanya maamuzi magumu nakuipigia kura CHADEMA,habari ndio hiyo
 
Back
Top Bottom