Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
nilishawahi kuongea na wanaoandaa hivyo vitabu, wanasema wanafunika mashimo tu, hakuna mpangilio wala uhakika wa wanachoandika, wanapewa karibu nusu mwaka mzima kule mipango lakini kwa kuwa warsha ni nyingi na mashindano ya michezo, acha safari mbalimbali, basi inakuwa tabu tupu kwa wale wanaobaki, kazi haijawahi kuisha kila mwaka muda wa bajeti unafika wakati haijakamilika, basi ni kukata tu vipande na kupachika,
Katika bajeti nzima cha maana ni ile brief case na suti tu, hakuna kingine.
Muda mfupi uliopita mbunge wa Karatu amechangia hotuba ya bajeti.
-Ameonyesha jinsi vitabu vya serikali vya matumizi na vile vya mapato vinavyotofautiana kwa zaidi ya bilioni 130 wakati vinapaswa kuwa na urari. Akosoa makosa mengi kwenye vitabu vya bajeti. Awakosoa watanzania kwa kusifia bajeti kwa kusikiliza hotuba ya waziri inayosema vitu vichache wakati vitabu vimejaa uozo. Atangaza kutokuunga mkono bajeti kwa kuwa wakipitisha inakuwa sheria. Asema hawezi kupitisha sheria mbovu kama mbunge. Ataka serikali iviondoe hivyo vitabu vichafu vya bajeti na kuleta vingine.
-Aonyesha jinsi bajeti inatavyopandisha gharama za maisha ya wananchi. Aonyesha kwa takwimu na maoneo ya kodi ambayo waziri aliyaficha katika hotuba yake lakini yamo kwenye vitabu vya mapato.
-Aibua suala la Meremeta na Tangold, ampelekea maswali waziri ya kina akitaka majibu kuhusu akaunti za makampuni hayo na ukaguzi wa mahesabu.
-Aeleza jinsi wazawa wanavyonyanyashwa na TRA na wageni kuachwa, apeleka ushahidi kwa mkulo
Asha
Sasa hivi siyo uwezo finyu wa sirikali, bali hii sirikali imeoza. Ipo madarakani kwa maslahi ya kundi la watu wachache na siyo yale ya Watanzania. Sijui Mkullo na JK watasema nini kuhusu hili au kama kawaida yao wataamua kudhrau na kukaa kimya.
Mswalie mtume bwana, mwenzio hali yake unaijua!CCM lazima watoke kamasi,wale akina mchinga sound watachangia nini unadhani?
nilishawahi kuongea na wanaoandaa hivyo vitabu, wanasema wanafunika mashimo tu, hakuna mpangilio wala uhakika wa wanachoandika, wanapewa karibu nusu mwaka mzima kule mipango lakini kwa kuwa warsha ni nyingi na mashindano ya michezo, acha safari mbalimbali, basi inakuwa tabu tupu kwa wale wanaobaki, kazi haijawahi kuisha kila mwaka muda wa bajeti unafika wakati haijakamilika, basi ni kukata tu vipande na kupachika,
Katika bajeti nzima cha maana ni ile brief case na suti tu, hakuna kingine.
Hoja za Kabwe,Slaa na Cheyo zilikuwa na mshiko mkubwa sana na inaonyesha ni jinsi gani wao hufanya homework kuliko wenzao wa CCM.
Slaa ametoa somo kwa wabunge kwamba Bajeti siyo hotuba ya waziri bali ni Takwimu zinazotolewa na serikali na kwamba kama takwimu zinapishana basi hakuna bajeti bali ni uchafu unaopaswa kutupwa
Amemuomba mheshimiwa waziri kabla ya Ijumaa aje na vitabu vingine vya bajeti ya serikali au akubali kujibu hoja zake kiufasaha,jambo ninaloamini kwamba Mkulo haliwezi, lakini CCM wako wengi kwenye bunge na watapiga kura kwa kufungamana na chama chao,hakuna kitu! Hayo madudu watayapitisha kama yalivyo tena kwa "kura za kishindo".
Sasa sijui tutafanyeje maana watanzania tumefunga ndoa ya kikuria na CCM!