Slaa awasha moto mwingine

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Muda mfupi uliopita mbunge wa Karatu amechangia hotuba ya bajeti.

-Ameonyesha jinsi vitabu vya serikali vya matumizi na vile vya mapato vinavyotofautiana kwa zaidi ya bilioni 130 wakati vinapaswa kuwa na urari. Akosoa makosa mengi kwenye vitabu vya bajeti. Awakosoa watanzania kwa kusifia bajeti kwa kusikiliza hotuba ya waziri inayosema vitu vichache wakati vitabu vimejaa uozo. Atangaza kutokuunga mkono bajeti kwa kuwa wakipitisha inakuwa sheria. Asema hawezi kupitisha sheria mbovu kama mbunge. Ataka serikali iviondoe hivyo vitabu vichafu vya bajeti na kuleta vingine.
-Aonyesha jinsi bajeti inatavyopandisha gharama za maisha ya wananchi. Aonyesha kwa takwimu na maoneo ya kodi ambayo waziri aliyaficha katika hotuba yake lakini yamo kwenye vitabu vya mapato.
-Aibua suala la Meremeta na Tangold, ampelekea maswali waziri ya kina akitaka majibu kuhusu akaunti za makampuni hayo na ukaguzi wa mahesabu.
-Aeleza jinsi wazawa wanavyonyanyashwa na TRA na wageni kuachwa, apeleka ushahidi kwa mkulo

Asha
 
Hoja zake zilikuwa nzuri sana; ameonyesha jinsi wataandaaji wa bajet wasivyo makini katika kazi yao. Kuna watu wamezoea ku-copy vitabu vya zamani bila hata kusoma wao wenyewe; na wabunge wetu wengi huwa hawavisomi sawasawa kab;a ya kuchangia.

Kama angepunguza 'jazba' kidogo, alikuwa amewashika pabaya serikali. Badala yake tutaanza kuona wabunge wakichangia kwa ushabiki wa ki-chama badala ya kufanyia kazi hoja ya Mh. slaa.
 
Inamaana kuna hatari Bajeti ya Upinzani ikachukua nafasi au sijafahamu maana ya kuwepo na bajeti kutoka upande wa pili wa Bunge embu nifaamisheni ,kila mwaka nasikia hawa wanataja yao na hawa wanataja yao wakati hakuna hata moja inayofuatwa zaidi ya kila mwenye uwezo kujikatia pande lake la feza akiwaacha wachunguzi wachunguze akijua hakuna lolote wala hatua atakayochukuliwa ,hebu nielezeni faida ya hizo bajeti mbili zinazopingana. ?
 
nilishawahi kuongea na wanaoandaa hivyo vitabu, wanasema wanafunika mashimo tu, hakuna mpangilio wala uhakika wa wanachoandika, wanapewa karibu nusu mwaka mzima kule mipango lakini kwa kuwa warsha ni nyingi na mashindano ya michezo, acha safari mbalimbali, basi inakuwa tabu tupu kwa wale wanaobaki, kazi haijawahi kuisha kila mwaka muda wa bajeti unafika wakati haijakamilika, basi ni kukata tu vipande na kupachika,
Katika bajeti nzima cha maana ni ile brief case na suti tu, hakuna kingine.
 
Slaa simama imara .Hata kama hawatafuata ila Watanzania wataujua ukweli , hili nalo ni muhimu sana .
 
Lengo la Bajeti mbadala ni kuonyesha mapungufu yaliyo kwenye bajeti ya serikali na kupendekeza namna ya kuiboresha.

Lakini serikali yetu ina kiburi kwa kuwa inajua wazi kuwa wapinzani wako wachache hata wakikosoa namna gani mwisho wa siku theluthi mbili itapatikana na bajeti itapita. Kitu pekee wapinzani wanaweza kufanya ni ku-walk out ambayo haiwasaidii. Hapa ndipo hoja ya Mch. Kishoka inapokuwa na maana zaidi kwamba mageuzi ya kweli yatakuja kwa kuwa na numbers ndani ya Bunge.

Michango ya wabunge wa CCM utawasikia wakikosoa bajeti na anapomaliza mchango wake anaunga mkono hoja 100 kwa 100! Utaungaje mkono hoja 100 kwa 100 wakati umetoa kasoro kibao? Ina maana unakubaliana na kitu ambacho kina kasoro au makosa? Kama siyo ujuha ni nini? Mwalimu hawezi kumpa mwanafunzi 100% kama kuna makosa kibao kwenye paper yake, hapo hamjengi bali anammaliza kwa kumpa alama ambazo hastahili.

Utasikia siku ya Ijumaa jinsi Mkulo atakavyokuwa anajibu maswali/hoja kisanii na baada ya hapo Bajeti itapitishwa bila kujali mapungufu ya msingi yaliyoainishwa.
 
Pongezi kwako Slaa tunakwaminia baba simama imara komaa nao mpaka kieleweke wamezoea sana kufanya usanii huku wakituingiza kwenye gharama za ***** komaa nao mkuu.
 
nilishawahi kuongea na wanaoandaa hivyo vitabu, wanasema wanafunika mashimo tu, hakuna mpangilio wala uhakika wa wanachoandika, wanapewa karibu nusu mwaka mzima kule mipango lakini kwa kuwa warsha ni nyingi na mashindano ya michezo, acha safari mbalimbali, basi inakuwa tabu tupu kwa wale wanaobaki, kazi haijawahi kuisha kila mwaka muda wa bajeti unafika wakati haijakamilika, basi ni kukata tu vipande na kupachika,
Katika bajeti nzima cha maana ni ile brief case na suti tu, hakuna kingine.

Aisee kama mambo ni hayo tumeliwa kabisa.
Ubabaishaji hata kwa kitu nyeti kama hiki
 
Hoja za Kabwe,Slaa na Cheyo zilikuwa na mshiko mkubwa sana na inaonyesha ni jinsi gani wao hufanya homework kuliko wenzao wa CCM.

Slaa ametoa somo kwa wabunge kwamba Bajeti siyo hotuba ya waziri bali ni Takwimu zinazotolewa na serikali na kwamba kama takwimu zinapishana basi hakuna bajeti bali ni uchafu unaopaswa kutupwa

Amemuomba mheshimiwa waziri kabla ya Ijumaa aje na vitabu vingine vya bajeti ya serikali au akubali kujibu hoja zake kiufasaha,jambo ninaloamini kwamba Mkulo haliwezi, lakini CCM wako wengi kwenye bunge na watapiga kura kwa kufungamana na chama chao,hakuna kitu! Hayo madudu watayapitisha kama yalivyo tena kwa "kura za kishindo".
 
Hii ni serikali ya watu wasiojua lakini wanajifanya wanajua. Hakuna ujinga wa kutokujua ujinga wako mwenyewe! Watanzania tumeliwa!
 
Muda mfupi uliopita mbunge wa Karatu amechangia hotuba ya bajeti.

-Ameonyesha jinsi vitabu vya serikali vya matumizi na vile vya mapato vinavyotofautiana kwa zaidi ya bilioni 130 wakati vinapaswa kuwa na urari. Akosoa makosa mengi kwenye vitabu vya bajeti. Awakosoa watanzania kwa kusifia bajeti kwa kusikiliza hotuba ya waziri inayosema vitu vichache wakati vitabu vimejaa uozo. Atangaza kutokuunga mkono bajeti kwa kuwa wakipitisha inakuwa sheria. Asema hawezi kupitisha sheria mbovu kama mbunge. Ataka serikali iviondoe hivyo vitabu vichafu vya bajeti na kuleta vingine.
-Aonyesha jinsi bajeti inatavyopandisha gharama za maisha ya wananchi. Aonyesha kwa takwimu na maoneo ya kodi ambayo waziri aliyaficha katika hotuba yake lakini yamo kwenye vitabu vya mapato.
-Aibua suala la Meremeta na Tangold, ampelekea maswali waziri ya kina akitaka majibu kuhusu akaunti za makampuni hayo na ukaguzi wa mahesabu.
-Aeleza jinsi wazawa wanavyonyanyashwa na TRA na wageni kuachwa, apeleka ushahidi kwa mkulo

Asha

Sasa hivi siyo uwezo finyu wa sirikali, bali hii sirikali imeoza. Ipo madarakani kwa maslahi ya kundi la watu wachache na siyo yale ya Watanzania. Sijui Mkullo na JK watasema nini kuhusu hili au kama kawaida yao wataamua kudharau na kukaa kimya.
 
Sasa hivi siyo uwezo finyu wa sirikali, bali hii sirikali imeoza. Ipo madarakani kwa maslahi ya kundi la watu wachache na siyo yale ya Watanzania. Sijui Mkullo na JK watasema nini kuhusu hili au kama kawaida yao wataamua kudhrau na kukaa kimya.

Sasa sijui tutafanyeje maana watanzania tumefunga ndoa ya kikuria na CCM!

Halafu naona huyu Dr Slaa sasa hivi ndio angekabidhiwa jahazi la upinzani. Wengine wampishe, wawe wasaidizi kama wapo serious na kuitoa CCM madarakani.
 
nilishawahi kuongea na wanaoandaa hivyo vitabu, wanasema wanafunika mashimo tu, hakuna mpangilio wala uhakika wa wanachoandika, wanapewa karibu nusu mwaka mzima kule mipango lakini kwa kuwa warsha ni nyingi na mashindano ya michezo, acha safari mbalimbali, basi inakuwa tabu tupu kwa wale wanaobaki, kazi haijawahi kuisha kila mwaka muda wa bajeti unafika wakati haijakamilika, basi ni kukata tu vipande na kupachika,
Katika bajeti nzima cha maana ni ile brief case na suti tu, hakuna kingine.

That is dangerous.
 
Hoja za Kabwe,Slaa na Cheyo zilikuwa na mshiko mkubwa sana na inaonyesha ni jinsi gani wao hufanya homework kuliko wenzao wa CCM.

Slaa ametoa somo kwa wabunge kwamba Bajeti siyo hotuba ya waziri bali ni Takwimu zinazotolewa na serikali na kwamba kama takwimu zinapishana basi hakuna bajeti bali ni uchafu unaopaswa kutupwa

Amemuomba mheshimiwa waziri kabla ya Ijumaa aje na vitabu vingine vya bajeti ya serikali au akubali kujibu hoja zake kiufasaha,jambo ninaloamini kwamba Mkulo haliwezi, lakini CCM wako wengi kwenye bunge na watapiga kura kwa kufungamana na chama chao,hakuna kitu! Hayo madudu watayapitisha kama yalivyo tena kwa "kura za kishindo".

kila kitu tunakijua na hali halisi tunaifahamu cha muhimu tuwaandalie hukumu 2010 tu tupeleke wabunge wengi wa upinzania kule bungeni na ambao wanatanguliza maslahi ya taifa na wananchi mbele kuliko kuendelea kubaki na hivi vichwa vya wenda wazimu.
 
Hata mimi huwa nashangaa sana kwa hii wanatusomea eti ni bajeti. Utashangaa baada ya siku kidogo tu unaona kodi fulani zimepanda na ukiuliza imepanda lini utaambiwa kuwa ni baada ya bajeti. Shida zaidi hakuna wa kumuuliza maana hata taxing system yetu haitupi nafasi ya ku question bali hawa TRA wakishasema wao ndio mwisho. Na mwisho wa siku hawa wakina Mkullo watasimama na kuwasifu kwa makusanyo makubwa wakati ulikuwa ni uonevu kwa walio na pesa ndogo na ulaji kwa mafisadi. Kwani BWM; RA: EL; AC wanalipa shillingi ngapi kama kodi?
 
Jamani leo nilikuwa nikizungumza na wananji fulani wa kule kijijini nikijaribu kuwaelewesha kuhusu nini kinaendelea katika nji hii na nilishangaa kuona kama hawana habari vile, na mambo yanavyokwenda katika nji hii. Nilijaribu kuwa brief na walishangaa sana kuona nji inaliwa hivi na hakuna aliyefurahia hata hao wanaojifanyaga nambari wani.
Ni ushauri wangu zifanyike juhudi za makusudi kuwafanya wananji wa nji hii kule vijijini kujua hali ya nji ilivyo. Vyama vya upinzani tusikae mijini na kudhani mambo yanakwenda. Tufanye juhudi za makusudi kama wakati ule wa Zitto. Nakwambia tutaikomboa nji yetu.
Na ikiwezekana zitengenezwe newsletters toka JF na sisi tutazidurufu na kuzisambaza huko vijijini.
Lazima message iwe sent vijijini jamani.
 
Bajeti zote zinashangaza sana kwani hakuna BF na kisha income sawa na expenditure sijui why one has to have the budget kama mapato sawa na matumizi na hivyo hamna salio! Yeah it means we are poor that all what we get does not cater for all of our needs...That is simple definition of poverty and missery we all facing; ufisadi nk.

Slaa tutetee kwani bado inaonekana kinadharia na vitendo kuwa bado tunatawaliwa na wewe tu ndiwe utakuwa Mwl wetu kutuondolea wakoloni hawa na kutuachia Tanzania yetu yenye amani na utulivu kiuchumi kwani tuko katika vita kuu kabisa ya kiuchumi.

Slaa we pray also that you live longer to help identify and chase them out of the authority by themselves as you initially did.
Cheers Slaa, Zitto, Mwakyembe et al and all who in one way or the other hate FISADOS
 
Sasa sijui tutafanyeje maana watanzania tumefunga ndoa ya kikuria na CCM!

Hivi kuna mtu alishafanya survey akahitimisha kwamba ni ndoa za wa-Mura peke yake ndio ziko abusive?

Manake kila siku tunasikia Wanawake wanakatwa mapanga na Wame zao kutoka pembe zote za nchi.

Wivu wa kike...Uroho wa Kichaga...Ufuska wa Kihaya...Ukabila wa Kinyakyusa... Hasira za Kizenji...Uchawi wa Kisukuma...Uomba Omba wa Kigogo...Kutokusoma kwa Wamachinga...U-house girl wa Kihehe...Ndoa za Kikurya, na kuendelea na kuendelea.

Hivi kama wewe ni Mhaya, tuseme, na sio Malaya, unajisikiaje ukisoma stereotype kama hizo zinarushwa rushwa hewani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom