Deni la TANESCO na TPDC kuhamishiwa Serikalini, huyu CHADEMA kaongea kitaalamu sana

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
DENI LA TPDC

Huu ni mkopo wa shirika kupitia hazina kutoka EXIM BANK CHINA kwaajili ya mradi wa gesi wa mtwara na songo songo kuja Dar lakini ilipofika DAR badala ya kumalizia usambazaji wa gesi kwa watumiaji ili wapate hela waanze kulipa deni wamebadili mradi sasa wanazungumzia LNG !! Laini pia mtaji uliosajiliwa wa TPDC ni 2.5billion na serikali imelipia hisa za 2.2 billion bado za milioni 300 tu huku shirika likidaiwa trillion 2.8 kama nilivyosema mwanzo ! Sasa sijui wanahamishaji deni lote kuwa mtaji usiosajiliwa ?

DENI LA TANESCO
Hawa mtaji wao uliosajiliwa ni 2.4 trilion na serikali imelipia 1.1 trilion hivyo hisa zisizo lipiwa ni 1.3 trillion wakati deni lao ni 2.4 trilion ( kwa mujibu wa waziri) hivyo hata wakinunua hisa zote bado hawalipi deni zima amablo limetokana na mikataba yao mbali mbali ya kununua umeme .

Sio sahihi kuwa hakuna tatizo kwa wananchi sababu jukumu la kulipa lilikuwa la mashirikia kutokea kwenye mkataba wa mkopo na mpangp mkakati wa kazi wa shirika lenyewe ! sasa nani kasabisha ufeli ? alichukuliwa hatua zipi? Je mashirika mengine Zaidi ya 200 yakifanya hivyo hivyo tutakuwa wapi? Japo haibadilishi muonekano wa vitabu lakini inadanganya uhalisia wa vitabu vyao ie. Disclosure kwenye vitabu vya serikali inahama kutoka guarantee kuwa actual loan ya kulipwa na wananchi kwa matozo na kodi !!

Sheria ya kodi inakataza kuhamisha deni kuwa hisa bila kuwepo hamisho la cash, je serikali /tanesco /TPDC wanavunja sharia za nchi ?.

Lakini pia ukipitia hotuba ya bajeti 2022/23 ya waziri wa nishati hakuna popote alipolieleza bunge nia hii ya kuwabebesha mzigo watanzania.

Kama bunge la wananchi tumeona wananchi wasibebeshwe mzigo wa kulipa adeni haya kwa matozo yaliyoletwa na uzembe mkubwa kwa kukosekana responsibility , accountability and transparency (uwazi) kwenye utendaji hasa kwenye maeneo yafuatayo;


1.MAKUSANYO
i) Ukusanyaji duni mapato ya ndani
Shirika la maendeleo ya Petrol lilikusanya asilimia 65% tu bajeti yake katika mwaka wa fedha ulioisha 2021 ambapo bajeti ilikua bilioni 860 lakini walikusanya bilioni 562 na kwa taasisi zote za serikali bajeti makusanyo yao ilikuwa trilioni 2.5 ila yakakusanya trillion 1.6 sawa na 63% tujue sababu ni zipi? yanajiendeshaje ?yakikopa tena yatalipaje ?

NB: Tukumbuke bajeti ya nchi ni trillion 41 na mwaka jana ilikuwa trillion 38 sasa piga hesabau 2.5 ni asilimia ngapi ya bajeti!

ii) Ukusanyaji Duni wa Madai ya Kibiashara Shilingi Trilioni 3.71
Namnukuu CAG Kati ya taasisi 200 nilizozikagua katika mwaka 2020/21, nilibaini mashirika ya umma 93 yana madai makubwa ambayo hayajalipwa hadi tarehe 30 Juni 2021 ya jumla shilingi trilioni 3.71. Mengi ya madeni haya yalihusiana na huduma zilizotolewa kwa wateja. Hali hii inaathiri mtiririko wa fedha wa mashirika haya na kusababisha kutotekelezwa kwa shughuli zilizopangwa

iii) Madai ya Shilingi Trilioni 1.1 kutoka kwa Mashirika Mengine ya Serikali
Mashirika 93 niliyoyakagua yakiwa na jumla ya madai ya shilingi trilioni 3.71 yalijumuisha mashirika 21 ambayo yalikuwa na kiasi kikubwa cha madai ya jumla ya shilingi trilioni 3.41 sawa na asilimia 92 ya madai niliyoyahakiki. Kati ya shilingi trilioni 3.41, shilingi trilioni 1,97 (asilimia 58) zinadaiwa kutoka taasisi za umma, na shilingi trilioni 1.45 (asilimia 42) zinadaiwa kutoka taasisi binafsi. Tathmini hii inaonesha kuwa mashirika ya umma yana madai makubwa kwa taasisi zingine za umma kuliko taasisi binafsi. Madai haya yanaathiri mtiririko wa fedha katika taasisi hizi, na hivyo kusababisha kutotekelezwa kwa shughuli zilizopangwa.

Mhe. Ahobokile Mwaitenda
Mjumbe Kamati ya Fedha na Uchumi wa Bunge la Wananchi
 
Back
Top Bottom