Dr Slaa siwezi kupinga unachokiongea maana wewe ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa hapa Tanzania, je? vipi wananchi tunaweza kuthibitisha kauli zako unazosema tunaomba utuletee na ushahidi na sio maneno maana tunawaelewa wana siasa mulivyo na maneno mengi vinywani mwenu, kama unazo hizo documents za ushahidi wa mapato ya Muheshimiwa RA na RIZ kwa nini musiwatumie wanasheria wenu wa CHADEMA kuwapeleka mahakamani kama muna wasiwasi na source za mapato yao.
Mengi unayoyaongea ni kwa ajili ya maslahi ya nchi lakini je Rizwan Kumiliki mabilioni ni kitu cha hatari? Naelewa kwa ufahamu wangu Rizwan ni mtoto wa RAIS na baba yake alikuwa waziri katika wizara nyingi sana hapa Tanzania kabla ya kuwa Rais; ninavoelewa mimi Rizwan kumiliki Bilioni moja si kitu cha ajabu, eti kamaliza shule juzi ndio asiweze kumiliki hiyo ela haiingii akilini hata kidogo kwa mtoto wa kimasikini sawa ila Riz sio mtoto wa kimasikini akashindwa kujiingiza kwenye masuala ya kutafuta pesa.
Kama mna ushahidi wa wizi wa fedha muende mahakamani au kama ni siasa tu basi endeleeni (sikupingi Dr Slaa huwa napenda ila ushahidi wako uko wapi?) tuwekee ushahidi ila tunapomwita mtu fisadi kama Riz kweli tujue ili tusipate dhambi kumjadili mtu bila ya ushahidi.
huyo silah,hebu mwambieni aende unyantuzu(bariad)akawaone vijana wadogo under25 wakimiliki mali za mabilion ,hawajaenda hata zaidi ya std seven.
Sio watoto wa katibu tarafa wala rais.
Ajue kua ukiwa na mtaji kumake ni suala la mwaka.aende kahama aone vijana wa kinyantuz wanavyoporomoa maghorofa,haakusoma wamefanya biashara maduka,mifugo leo wanapesa.
Ache kulalama afanye kazi
matajiri wangapi vijana wamemaliza chuo juzi mbona hamuwafatilii ? Husda ndio zinawasumbuaswala si utajiri ameupateje?wakati amemaliza chuo juzi juzi tu!
Ndugu wewe huelewi kinachoendelea huko usukumani waulize wanaotoka huko watakupa uhalali wa utajiri wa hao vijana. Kwa taarifa yako mali ile si ya hao unaowaona wewe wwale ni washika pembe tu wenyewe ni walewale unaowajua. Fatilia vizuri huwezi kuamini mtu anapata utajiri wa kumiliki maroli na viwanda ndani ya mwaka au miwili na huku alikuwa anafanya biashara ya kondoo na hata hawakuwahi kufika kumi miaka michache iliyopita. Nakumbuka mtu huyu hajui hata kusoma wala kuandika.
Mafisadi huwatumia hawa mbumbu kuficha utajiri wao maana hawajui chochote hawataweza kuwadhulumu maana hawana hata elimu ya mikataba ya biashara.
Karagabaho endelea kuamini kuwa kutajirika ni rahisi kiasi hicho! Bila kuwa mwizi hakuna utajiri wa mwaka mmoja a miwili it take you time and proper management to get you up there!
Kama utajiri ungekuwa rahisi hivyo hakuna ambaye angebaki masikini wa kutupwa ilihali kumbe hata ukiwa na mtaji wa elufu hamsini unaweza kuboresha maisha. pia kila mtu angeachana na kazi zingine akafanya biashara.
Unaowaona wana kwea juu ni wizi wa mali ya umma kwa kufanya madili na serikali. hakuna biashara inayolipa zaidi ya tenda hewa za serikali kama tulivyoona mikataba ya umeme na madini
Hivi kwako utajiri wa namna hii ni halali kwako au ni ufisadi tu.
Tulishuhudia biashara za mabasi ya scandinavia, wakubwa walipochomoa hisa zao leo hii wakowapi?
Fikiri mara mbili kama na wewe sio mshika pembe wa kwa mafisadi ndo maana unatetea hoja kama hii bila kujali maumivu wanayofanyiwa watz na hizi biashara hewa za wizi wa jasho la walalahoi.
don't blame the messenger, blame jk who decided to sit on his hands and let his crooks friends destroying the country.
Dr Slaa siwezi kupinga unachokiongea maana wewe ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa hapa Tanzania, je ? vipi wananchi tunaweza kuthibitisha kauli zako unazosema tunaomba utuletee na ushahidi na sio maneno maana tunawaelewa wana siasa mulivyo na maneno mengi vinywani mwenu, kama unazo hizo documents za ushahidi wa mapato ya Muheshimiwa RA na RIZ kwa nini musiwatumie wanasheria wenu wa CHADEMA kuwapeleka mahakamani kama muna wasiwasi na source za mapato yao. Mengi unayoyaongea ni kwa ajili ya maslahi ya nchi lakini je Rizwan Kumiliki mabilioni ni kitu cha hatari, naelewa Kwa ufahamu wangu Rizwan ni mtoto wa RAIS na baba yake alikuwa wazizri katika wizara nyingi sana hapa tanzania kabla ya kuwa Rais ninavoelewa mimi Rizwan Kumiliki Bilioni moja si kitu cha ajabu eti kamaliza shule juzi ndio asiweze kumiliki hio ela haiingii akilini hata kidogo kwa mtoto wa kimasikini sawa ila Riz sio mtoto wa kimasikini akashindwa kujiingiza kwenye masuala ya kutafuta pesa ( kama muna ushahidi wa wizi wa fedha muende mahakamani au kama ni siasa tu basi endeleeni (sikupingi Dr Slaa huwa napenda ila ushahidi wako uko wapi) tuwekee ushahidi ila tunapomwita mtu fisadi kama Riz kweli tujuwe ili tusipate dhambi kumjadili mtu bila ya ushahidi.
Dk. Slaa afichua mabilioni ya Rostam
Asema anapokea bil. 280/- kwa mwaka, ataka akamatwe
na Joseph Senga
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.
Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.
Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kungangania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona.
Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.
Alisema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na nia ya kweli angemshirikisha kuwakamata mafisadi badala ya kuwapa siku 90 kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa Kikwete amewapa mafisadi hao siku hizo kuondoka ndani ya chama pamoja na kuachia ubunge, naye hana budi kujipa siku hizo, kwani naye ni fisadi.
Alisema kujitokeza kwa mmiliki wa Dowans Brigedia Jenerali (mstaafu), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ulikuwa ni usanii wa picha ya Rostam kwani baadaye ndiye atakayelipwa fedha hizo za Dowans.
Alisema CHADEMA haitakubali fedha hizo zilipwe na kwamba itaitisha maandamano nchi nzima kupinga.
Dk. Slaa alisema ufisadi mwingine wa serikali katika sakata hilo la Dowans ni serikali kuweka mawakili watatu kinyemela na kupanga kuwalipa sh bilioni tano.
Nilimtaja Rostam kuwa ni mmoja wa mafisadi kule Mwembeyanga, naye alinitumia vitisho kwa ujumbe mfupi kuwa nina sekunde chache za kuishi hivyo nipige magoti, nisali. Nilimjibu na nasema nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja, sitaogopa kusema ukweli, alisema Dk. Slaa.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema moto uliowashwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) umeifanya serikali ya CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kulala.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki jana aliposimama kuwasalimia wakati akitokea Singida kuelekea Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema Lissu ni mbunge jasiri katika Bunge ambaye amediriki kumnyooshea kidole hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema.
Katika hotuba yake hiyo alisema wananchi hawana imani tena na serikali ya Jakaya Kikwete na kama atafanya mchezo hataweza kurudisha imani hiyo wala kumaliza kipindi chake cha utawala.
Alisema mambo mengi yamejitokeza ambayo yamesababisha wananchi kukosa imani naye, yakiwamo ya ufisadi unaofanywa na yeye mwenyewe pamoja na watu walio karibu naye.
Wananchi wanaona yanayofanyika, mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete, amemaliza shule hivi karibuni lakini leo ni bilionea. Haya yote hayawezi kuvumilika hata kidogo.
Akiwashukuru wananchi wa kijiji hicho, Dk. Slaa alisema si tu kwamba wamemchagua mbunge wa Jimbo la Singida, bali ni mbunge wa nchi nzima na kwamba ni nyundo itakayotumika kuwaponda CCM.
Akizungumzia suala la CCM kujivua gamba, alisema neno fisadi alilianzisha yeye na chama chake na kwamba anayepaswa kujivua gamba hilo ni Kikwete halafu awavue wengine.
source: Dk. Slaa afichua mabilioni ya Rostam
Kama alivyosema Dr, ushahidi huwa hautolewi kwenye mikutano ya hadhara. Ushahidi wa mambo nyeti kama hayo hutolewa mahakamani pindi yule aliyetuhumiwa au kuhusishwa na kashfa ile atakapoenda kusema nimedhalilishwa.
Sasa kwenye hili anayetakiwa kushtaki ni Riz, na Dr ataitwa kuthibitisha, na hapo ndipo atatakiwa kutoa vielelezo.
matajiri wangapi vijana wamemaliza chuo juzi mbona hamuwafatilii ? Husda ndio zinawasumbua
Stop speaking nonsense here! wewe ni nani uanyewasemea hao mafisadi waache wao waombe ushahidi yeye anao ndiyo maana kasemaDr Slaa siwezi kupinga unachokiongea maana wewe ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa hapa Tanzania, je? vipi wananchi tunaweza kuthibitisha kauli zako unazosema tunaomba utuletee na ushahidi na sio maneno maana tunawaelewa wana siasa mulivyo na maneno mengi vinywani mwenu, kama unazo hizo documents za ushahidi wa mapato ya Muheshimiwa RA na RIZ kwa nini musiwatumie wanasheria wenu wa CHADEMA kuwapeleka mahakamani kama muna wasiwasi na source za mapato yao.
Mengi unayoyaongea ni kwa ajili ya maslahi ya nchi lakini je Rizwan Kumiliki mabilioni ni kitu cha hatari? Naelewa kwa ufahamu wangu Rizwan ni mtoto wa RAIS na baba yake alikuwa waziri katika wizara nyingi sana hapa Tanzania kabla ya kuwa Rais; ninavoelewa mimi Rizwan kumiliki Bilioni moja si kitu cha ajabu, eti kamaliza shule juzi ndio asiweze kumiliki hiyo ela haiingii akilini hata kidogo kwa mtoto wa kimasikini sawa ila Riz sio mtoto wa kimasikini akashindwa kujiingiza kwenye masuala ya kutafuta pesa.
Kama mna ushahidi wa wizi wa fedha muende mahakamani au kama ni siasa tu basi endeleeni (sikupingi Dr Slaa huwa napenda ila ushahidi wako uko wapi?) tuwekee ushahidi ila tunapomwita mtu fisadi kama Riz kweli tujue ili tusipate dhambi kumjadili mtu bila ya ushahidi.