BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Slaa anyaka skendo lingine
2008-01-24 17:22:18
Na Job Ndomba, Jijini
Yule mbunge maarufu wa kulipua maskendo, Dokta Wilbroad Slaa (CHADEMA-Karatu) amenyaka skendo jingine bab`kubwa linalohusisha ulaji wa mabilioni kibao ya pesa za walalahoi.
Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Dk.Slaa amesema pesa hizo zilizoliwa na vigogo ni kutoka katika mfuko wa Import Support uliokuwa ukifadhiliwa na Serikali ya Japan.
Amesema mfuko huo uliokuwa na mabilioni kibao ulilenga kuwasaidia wafanyabiashara wadogo, lakini mapesa hayo yakaliwa hivi hivi na vigogo baada ya kukopeshana na kushindwa kulipa.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, mfuko huo sasa umefutwa baada ya kugundulika umetumiwa vibaya na vigogo hao anaodai, wengi wao walifungua makampuni hewa kwa ajili ya kukamilisha ulaji wao.
``Vita dhidi ya ufisadi haijaisha, kwani baada ya hili la BoT najiandaa kulipua hili la upotevu wa mabilioni, kutoka katika mfuko wa Import Support,`` akasema Dk. Slaa.
Amesema nchi hii ina maskendo mengi sana yanayofanywa na vigogo na hivyo lazima wachache wajitolee kuwashitaki kwa wananchi kwa ajili kuokoa uchumi wa taifa.
``Unajua tunapowataja mafisadi hawa, wananchi wanatakiwa watuunge mkono kwa kuwa kuna mapesa kibao yameibwa na vigogo,`` akaongeza.
Amesema mfuko wa Import Support ulianzishwa kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, lakini wakapigwa changa la macho na mapesa hayo kuwafaidisha vigogo wachache.
Hata hivyo Dk. Slaa hakutaka kutaja ni lini atalipua bomu hilo, lakini amesisitiza kuwa yuko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha uchunguzi wake.
``Kwa sasa siwezi kukuambia ni lini nitalipua ila wakati ukifika, nitawasilisha madai yangu mahali husika kama ilivyokuwa kwa lile skendo ya BoT, licha ya kwamba baadhi ya watu walianza kunibeza,`` akasema.
Dk. Slaa ndiye aliyeibua skendo la BoT Julai mwaka jana, katika kikao cha Bunge wakati Waziri wa Fedha Bi.Zakhia Meghji akiwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya wizara hiyo.
Hata hivyo baada ya kuibua hilo, Dk. Slaa alitakiwa kutoa hoja binafsi ambapo pia aliamua kushitaki kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara pale Mwembeyanga, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya matokeo ya skendo la Benki Kuu ni kubainika kwa ulaji wa zaidi ya shilingi bilioni 133 na kutimuliwa kazi kwa aliyekuwa gavana wa taasisi hiyo, Dk. Daud Balali.
SOURCE: Alasiri