Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa amemshangaa Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana kwa kuanza kulalamika kuhusu bei za Korosho, Ufisadi wakati Chama chake ndicho chenye serikali. Dr Slaa anasema ni bora CCM ikawa upinzani na yenyewe badala ya kuwahadaa wananchi.
Aidha amewashangaa watu wanaodai majina ya mafisadi wakati yeye alishawasilisha kwa DPP majina na akaunti za Mafisadi na watia sahihi wa akaunti hizo lakini serikali imekaa kimya hadi leo.
Slaa pia amewashangaa watu wanaodai CHADEMA ina makundi kwani huo ni uzushi usio na maana na CHADEMA haina muda huo wa kupoteza. Kazi ni moja tu ya kujenga Chama na wakati uchaguzi wa ndani ya Chama ukiwa unaendelea rushwa haitavumilika ndani ya CHADEMA hata kidogo.
Slaa ameyasema hayo katika Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Kagera ambalo pia lilihudhuriwa na Wenyeviti na Makatibu wote wa Mikoa wa CHADEMA.