Slaa amgomea JK

Slaa amgomea JK

hoja ya Dr W. Slaa ina maslahi kwa taifa. naunga mkono 100%
 
Huwezi kujadili au kutoa maoni ya muungano wa Tanzania bila kugusia muungano wenyewe. sasa kama Jk hataki tujadili muungano tutajadili nini sana??? aache watanzania wajadili kwa uhuru lipi wanalolitaka na lipi hawalitaki
 
serikali ya majimbo hatuitaki ni kutaka kuibagua mikoa isiyo na rasilimali,tumeshajua nia yenu ni kaskazin yenu muitenge ipate maendeleo kuliko kanda nyingine,hatutaki kubaguliwa hivyo,acha dhambi zako za kibaguzi TANZANIA HAtujafikia uwezo wa kuwa na majimbo au KASKAZIN Mnataka kujitenga kama BEGHAZI,?serikal ya majimbo iliyokuwa kwenye ideology ya JAMAHIRIA ya LIBYA Ilishndwa kuleta maendeleo sawa LIBYA?itawezekana TANZANIA yenye ideology ya kibebari?

Sasa madhara ya majimbo ni kujengeana chuki kati jimbo moja na jingine na kuamini kuwa jimbo moja linafaidi matunda ya uhuru kuliko jimbo lingne
Kwani kaskazini wana rasilimali gani kubwa kupita sehemu nyingine? Kama madini Kanda ya ziwa ya kibao, Viwanda mashariki ndio usisema, Mbuga za wanyama hata mikoa mingine zipo. Tukubali tu kwamba kaskazini wamekua wakitumia vizuri rasilimali walizonazo na hata kutawanyika kanda nyingine kuchuma rasilimali. Kubwa ni kujifunza kujitegea.
 
Juma Mohammed

Sasa la mgambo limelia kuna jambo kubwa Tanzania, Katiba mpya inakuja shime Watanzania kujitokeza kwa wingi kutoa maoni katika Tume hiyo huku tukitanguliza uzalendo mbele katika kuhakikisha tunapata katiba yenye tija kwa pande zote mbili za Muungano. Hoja ya Tanzania kuwa na Katiba mpya ni kilio cha muda mrefu,wengine waliokuwa wakipaza sauti kudai hivi sasa hatunao tena, wametangulia mbele ya haki na wengine wapo hivi leo watatembea kifua mbele kuona kuwa jambo walilokuwa wakilipigania sasa limekuwa,nalo ni Tanzania kupata katiba mpya.

Wakati tukijiandaa kutoa maoni katika Tume ya Katiba ni vizuri pia kuzungumzia mustakabali wa mfumo wa muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao katika kipindi chote cha uhai wake umekumbana na misukosuko ya kila aina.
Bila shaka wengi tunakubali kuwa muundo wa sasa una kasoro,kasoro ambazo zinahitaji kurekebishwa kwa kuweka mfumo mwengine wa muundo wa Muungano na kwa jinsi upepo unavyovuma wengi wanapendekeza kuwepo na Muungano wa Mkataba kama ilivyo ule wa Umoja wa Ulaya.
Ni jambo lisilokuwa na ubishi kuwa muundo wa Serikali mbili haufai na ndio maana Tume zote mbili zilizoundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania takriban miongo miwili iliyopita zilikubali na kutoa mapendekezo ya kubadili mfumo wa muundo wake.
Rais wa awamu ya Pili Tanzania,Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliunda Tume mwaka 1991 iliyoongozwa na Jaji Francis Nyalali ambayo ilikuwa na wajumbe 22 kati ya hao kumi kutoka Zanzibar na wengine kumi kutoka Tanzania Bara.
Baada ya Tume kukamilisha kazi yake,Wajumbe nao walitoa maoni yao ambapo kati ya 22, wajumbe 12 walipiga kura ya ndio kukubali mfumo wa muundo wa Muungano uwe wa Serikali tatu sasa huku wengine 7 walikubali uendelee muundo wa Serikali mbili. Katika ripoti ya Tume ya Nyalali utaona wajumbe watatu wao hawakupiga kura kabisa.
Tume ya Jaji Nyalali ilijenga hoja kwamba chini ya muundo wa Serikali mbili kuna mambo ni magumu utekelezaji wake,wakitaja suala la Uraia,milki ya fedha za kigeni,ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kutokana na kodi na ushuru wa forodha,tatizo la fomula ya kuchangia gharama za uendeshaji Serikali ya Muungano.
Mwaka 1998,Rais wa awamu ya tatu,Benjamin William Mkapa aliunda Tume iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga,ikapeleka kwa wananchi waraka wa Serikali maarufu Whitepaper , kama ilivyo kwa Tume ya Nyalali, Tume hii nayo ikarudia yale yale kuwa muundo wa Serikali mbili haufai.
Ripoti ya Jaji Kisanga imesema kasoro za Muungano zilizobaki hazirekebishiki. Maana yake ni kwamba kuna hitajika mfumo wa muundo wenye kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye utakaokuwa tiba ya matatizo mbalimbali.
Chini ya muundo wa Serikali mbili matatizo yamezidi kuongezeka licha ya kuwepo kwa kamati za kushughulikia matatizo hayo,lakini bado mambo yameonekana kutokwenda sawia.
Katika kipindi cha miaka 48 ya Muungano wenye muundo wa Serikali mbili,wapo watu Zanzibar wanaeleza bayana kutokuona faida ya kiuchumi huku wakijenga hoja kwamba kwa muda zote malalamiko yamekuwa ni yale yale ambapo sasa wanaona njia pekee ya kumaliza hali hiyo ni kuwa na muundo usiosababisha manung’nuniko kwa kila upande,hawana nia ya kuvunja Muungano.
Muundo wa sasa una mambo ambayo utekelezaji wake unasababisha malalamiko,kwa mfano suala la Zanzibar kujiunga na Jumuiya za Kimataifa nalo linazungumzwa ni tatizo na wanataja kisa maarufu cha OIC.
Mara baada ya Zanzibar kujiunga na OIC, Kamati Kuu ya CCM Agosti 10 mwaka 1993 ilitoa uamuzi wa Zanzibar ijitoe kwenye Jumuiya hiyo,Rais wa Zanzibar,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hasiwe Makamu wa Rais Tanzania, kupinga Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Nyalali.
Wakati CCM ikitoa uamuzi huo, Wabunge 44 wa Majimbo ya Tanzania Bara walijiandikisha kuwasilisha hoja binafsi kutaka Serikali ya Tanganyika na hoja yao ilionekana kuungwa mkono na kundi kubwa la wananchi na hata baadhi ya Mawaziri.
“Nilipokwisha kuhakikishiwa kuwa sasa sera ya Serikali Tatu ndiyo sera rasmi ya Bunge la Muungano na Serikali ya Muungano, niijaribu kupata maelezo kutoka kwa viongozi wetu;lakini sikufanikiwa” anasema Nyerere katika kitabu chake uongozi na hatma ya nchi yetu.
Kikao cha Bunge cha Agosti 14 mwaka 1993 Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Rais Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu John Samwel Malecela walikwenda Bungeni kuzima hoja ya kuanzishwa Serikali ya Tanganyika, Zanzibar kujitoa OIC na kufuta Rais wa Zanzibar kutokuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mabadiliko ya 11 ya Katiba ya Muungano ya mwaka 1994 yaliongeza tatizo latika mfumo wa sasa kwa kuwepo kwa mgombea mwenza kwenye Uchaguzi wa Rais mabadiliko ambayo wanasheria wanayataja kuwa yalivunja makubaliano ya Muungano ya 1964 kwa kumuengua Rais wa Zanzibar ambaye ni mshirika sawa kutokuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Mfumo wa uchaguzi haufahamiki kama ni wa Westminster yaani wa Kiingereza au ule wa Presidential System wa Marekani wanaokuwa na mgombea mwenza,huku tukiwa na Waziri Mkuu.
Kasoro kubwa katika muundo wa Serikali mbili ni kuwa mfumo huo ulijengeka katika misingi ya Chama kimoja cha siasa, ‘State Party’ ambapo mwaka 1992 mfumo wa Chama Dola ukafa kwa hivyo nguzo za muundo wa Serikali mbili ukawa unakasoro lukuki.
Inaonekana wazi kuwa wakati ule CCM ilikuwa ikiogopo upande mmoja wa Muungano kikishinda Chama cha Upinzani itakuwaje uendeshaji wa Serikali hiyo kwa ushirikiano mzuri ndio maana kwa woga huo ndio yakafanyika marekebisho ya Katiba na kuweka mgombea Mwenza.
Kama ingelikuwa ni nyumba basi imebakia nguzo moja ambayo ni muundo wa Serikali mbili uliokuwa na ufa na kila siku tunaona jinsi nguvu ya nguzo hiyo zinazidi kupungua na kufanya haja ya kuwa na muundo mujarab kwa mazingira ya leo na kesho ya Muungano katika dhana ya kuwa na Muungano wa treaty.
Muundo wa Serikali mbili kimsingi ulibuniwa kwa haraka haraka wakati ule kama inavyofahamika Zanzibar ndio kwanza Mapinduzi yamefuzu na Jamhuri ya Tanganyika ikiwa na miaka mitatu tangu kupata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1961, hivyo kwa kuwa imepatikana fursa ya Katiba mpya ni muda muafaka kubadili mfumo wa muundo wa Muungano kuwa wa kiuchumi zaidi.
Hilo likitendeka litaufanya Muungano kuwa wenye madhubuti na wenye kuvutia nchi nyengine kujiunga na hatimaye kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi , Kwa mfano dai mojawapo la wapenda mabadiliko ni kuwa Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano anaposhughulikia jambo linalozihusu pande zote mbili, kuna uwezekano mkubwa wa Waziri huyo kuipendelea Nchi yake ya asili(Tanganyika)
Lakini pia Wazanzibari wapenda mabadiliko wanahoji hivi inakuwaje kasma za bajeti zinalundikwa pamoja kwa serikali ya Muungano na Tanzania Bara bila ya kutafautishwa?
Ukiacha suala hilo,lakini kuna jambo jengine la kuongezeka na kupungua kwa madaraka ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukitolewa mfano wa kuunganishwa kwa Afro Shiraz Paty na Tanganyika African Union mwaka 1977.
Kabla ya kuunganishwa vyama,jambo hilo lilikuwa ndani ya uwezo wa Zanzibar,lakini kama tunavyoelewa hilo lilikuwa ni miongoni mwa mambo yaliokuja kuelezwa ni katika kuimarisha Muungano,lakini jambo la kukumbuka ni kwamba vyama vya ASP na TANU havikuwa sehemu ya mambo ya Muungano mwaka 1964.(tazama mapatano ya Muungano).
Wengi wanakumbuka mkasa uliompata Rais wa Pili wa Zanzibar,Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi alipotakiwa kujiuzulu na Chama Dola Chama cha Mapinduzi kule Dodoma mwaka 1984.
Katika hati ya Muungano,CCM haikutajwa kuwa ni mshiriki katika Muungano huo na wala sio Chama cha TANU au ASP vilivyotajwa zaidi ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.
Wataalam wa mambo ya katiba wanasema kwamba kwa sababu hiyo, CCM haina ubavu wa Kikatiba kujiingiza kisheria na kulazimisha haki na wajibu wa Muungano kwa upande wa Tanganyika, Zanzibar au Jamhuri ya Muungano.
Wengi wanahoji vipi CCM ilimuondoa Rais wa nchi aliyechaguliwa kwa mujibu wa sheria ambaye ni mshirika sawa katika Serikali ya Muungano?CCM haikuwa sehemu ya mambo ya Muungano.
Wadadisi wa mambo wanatafsiri hatua ya kumshinikiza Mzee Jumbe ilikuwa sawa kudhalilisha Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 yalioondoa uonevu,dhulma na manyanyaso, kwa kweli kushinikizwa kuachia ngazi kwa Mzee Jumbe ilikuwa ukiukwaji mkubwa wa mkataba wa Muungano na pia kuwadhalilisha Wazanzibari na Kiongozi wao.
CCM kwa kuelewa walikosea walipomwondoa Jumbe madarakani,CCM hiyo hiyo iligeuka na kuunga mkono hoja za Mzee Jumbe kuhusu Serikali tatu na uthibitisho ni kalipio la Mwalimu Nyerere kwa Halmashauri Kuu ya CCM mwaka 1993
Katika Kikao cha NEC kilichofanyika Mjini Dodoma Oktoba 14 mwaka 1993, Mwalimu Nyerere alikemea vikali hoja ya kutaka Serikali tatu ambayo wakati ule ilionekana wazi ikiungwa mkono na kundi kubwa la Wabunge na wanasiasa wengine.
“Nilipouliza kwanini hawakupinga hoja ya Serikali tatu kama tulivyokubaliana,majibu ya viongozi wetu wakuu yalikuwa ni ajabu kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa wakali kama mbogo” anasema Nyerere katika kitabu chake.
Miongoni mwa mashujaa katika uamuzi wa Serikali tatu wakati ule ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye alikubali kusoma alama za nyakati licha ya CCM kupinga,lakini kwa kuwa Muungano sio jambo la CCM Serikali ya Mwinyi ilikubaliana na hoja ya Wabunge wa kundi la 55(G55).
Hatimaye Julai 30 mwaka 1993 Wabunge 55 walitoa taarifa Bungeni kusudio lao la kutaka Serikali tatu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na walijenga hoja ya msingi juu ya kushindwa kwa Serikali mbili. Hoja ya G 55 ni sawa na hii ya sasa ya Wazanzibari wanaotaka Muungano wenye maslahi kwa pande zote ukitilia maanani mabadiliko ya mfumo.
Katika hoje yao walisema “kwa kuendelea mfumo huu wa Muungano usiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja(Tanganyika) ni kuhatarisha kuendelea na kudumu kwa Muungano na pia kuathiri uelewano kati ya watu wa pande zote mbili”.
Tunawaheshimu waasisi wetu ambao wameunganisha Mataifa huri mawili na kuunda Taifa moja lenye nchi mbili,lakini pia kizazi cha leo kina haki ya kufanya marekebisho katika muundo wa Muungano huo.
Kamwe chini ya muundo wa Serikali mbili kila siku kutazuka malalamiko kwa kuongezeka matatizo,lakini kama ilivyokuwa mazowea kila likizuka jambo litazimwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete atamaliza muda wake huku akiandika historia ya kuwapatia Watanzania katiba mpya
 
Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}
29112011

Dr Harith Ghassany
"Hapana shaka yoyote kuwa Mkataba [wa Muungano] uliandaliwa kwa siri sana. Maofisa wawili [wa Kiingereza] Brown na Fifoot walihusika kwa karibu sana. Hakukuwa na mshauri wa kisheria kwa upande wa Zanzibar. Karume hakuliarifu Baraza la Mapinduzi. Jumbe alikuwa hajui.
Inawezekana Babu alikuwa anafahamu kuwa kulikuwa kuna kitu kinaendela, na inawezekana alishiriki katika mazungumzo ya kijumla, lakini hakutarajia kuwa Muungano utafanyika kwa haraka namna ile. Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi] aliuona Mkataba [wa Muungano] kwa mara ya kwanza pale ‘bahasha yenye Mkataba ulipowasili Ikulu kwa ajili ya kutiwa saini na Karume'.
Karume alimuelekeza Salim asimuonyeshe Dourado ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo. Salim alimuambia Karume kuwa Mkataba wa Muungano ulihitajia ushauri wa kisheria. Salim akapanga kumleta Nabudere, wakati huo alikuwa ni mwanasheria kijana kutoka Uganda ambaye Salim alionana naye London lakini Nabudere alipofika Zanzibar Mkataba wa Muungano ulikuwa tayari umo katika mchakato wa kusainiwa.
Katika mahojiano na muandishi [Issa Shivji], Nabudere alithibitisha kuwa wafuasi wa chama cha Umma, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walimuita ende Zanzibar. Alipofika Zanzibar, aliwekwa peke yake afanye kazi ndani ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Wakati huo, Mwanasheria Mkuu Dourado, alikuwa hayupo.


Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume
Nabudere alipewa kopi ya Mkataba wa Muungano ambayo ilikuwa bado haijatiwa saini. Alitumia baadhi ya siku kuzipitia nyaraka husika za sheria za Zanzibar na makabrasha mengineyo. Baadae akenda Ikulu kuonana na Karume. Alimuarifu Karume kuwa kimsingi [Muungano] ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa. Utaifa wa Zanzibar utakabwa sana lakini uamuzi wa mwisho wa kisiasa anao yeye Karume.
Karume akasema yeye hana matatizo na Muungano kwa hiyo Nabudere akasema basi atakuwa hana mchango [wa kisheria]. Baadae Karume akashuka chini na Nabudere na kumuambia kuwa Nyerere amekuja kuonana nae. Nyerere alikuwa na Roland Brown. Jumla walikuwepo watu wane. Nabudere akajuulishwa na Nyerere.
Hakukuwa na mazungumzo khasa juu ya Mkataba wa Muungano. Baada ya kidogo, Nabudere akaondoka. Alipotoka nje ya Ikulu aliwaona baadhi ya wafuasi wa Umma waliokuwa wakiupinga Muungano. Nabudere alionana na Babu jioni ya siku ile. Inavyoonsha Babu aliwasili Zanzibar siku hiyo hiyo.
Nabudere alimueleza Babu kuhusu mkutano wake na Karume. Babu akasema kuwa yeye hana matatizo na Muungano. Nabudere akasafiri asubuhi ya siku ya pili au baada ya siku moja.
Nabudere hakuweza kuzikumbuka tarehe za kuwasili na kuondoka kwake Zanzibar. Na hakushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muungano, na wala hakushiriki katika mazungumzo yoyote yale ya Mkataba wa Muungano.

Inawezekana Nabudere alifika Zanzibar siku chache kabla ya Mkataba kutiwa saini. Inawezekana alikutana na Karume tarehe 22 au 23 [Januari], lakini kwa vyovyote hakushiriki katika mazungumzo juu ya Mkataba wa Muungano na wala hakutoa ushauri wowote ule wa kisheria.
Kwa hiyo kauli alioyoitowa Dourado miaka 20 baadae kuwa Zanzibar haikupata ‘ushauri wa kisheria au wa kikatiba kutoka kwa Mwanasheria wake Mkuu' ni ya kweli.
Pia ni kweli kuwa Karume hakupewa ushauri wowote ule wa kisheria, na inawezekana sana kama ilivoonekana mara nyingi, kuwa alikuwa hajali kuhusu sheria au mambo ya kisheria katika uendeshaji nchi au mambo mengineyo.
Jumbe aliuona Mkataba wa Muungano kwa mara ya kwanza baada ya mawaziri wa Zanzibar kurudi kutoka Dar es Salaam ambako walikwenda kushuhudia kuidhinishwa kwa Mkataba wa Muungano ndani ya bunge la Tanganyika.
Jumbe anasema alimuambia Karume kuwa kulikuwa kuna kitu hakipo barabara. ‘Vipi sisi tunayo serikali lakini Tanganyika haina!' Jumbe alifanya kama kusema tu. Kama ilivyo kawaida yake, Karume akapuuza: Tutarekebisha baadae.

Prof. Issa Shivji
Kama hawana serikali [ya Tanganyika] si shauri yao wenyewe!
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini Zanzibar tarehe 22 Aprili 1964…Tamko rasmi la safari ya Nyerere kwenda Zanzibar ambayo ilikuwa ni ya mara ya kwanza kutokea kufanyika mapinduzi, ilielezewa kuwa ilikuwa ni "safari ya heshima." Safari hiyo ilidumu kwa masaa mawili tu.

Nyerere alikwenda na Ronald Brown na Fiffot. Picha ya utiaji saini [Mkataba wa Muungano] ipo mpaka leo, na inamuonyesha Abdulaziz Twala, Kasim Hanga na Ali Mwinyigogo kutoka upande wa Zanzibar na Oscar Kambona, Job Lusinde na Bhoke Munanka kutoka upande wa Tanganyika."
Kuuidhinisha Mkataba wa Muungano
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.

Mkataba wa Muungano ni mkataba wa kimataifa ambao ulitiwa saini na viongozi wawili wa nchi mbili. Katika mfumo wa kisheria wa kawaida ambao unafuatwa na Zanzibar na Tanganyika, mikataba ya kitaifa inahitajia kuidhinishwa na mabaraza ya kisheria ili kuipa nguvu za kisheria.
Kifungu viii cha Mkataba [wa Muungano] kinasema wazi kuwa Mkataba wa Muungano ‘lazima uidhinishwe kisheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na pamoja na Baraza la Mawaziri liidhinishe na liipe nguvu za kisheria Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar'.
Ni muhimu kuwa kifungu hichi hakizungumzi tu juu ya uidhinishaji wa Mkataba wa Muungano bali kinalazimisha sharti juu ya mabaraza mawili kutoka Tanganyika na Zanzibar kuudhinisha na kuupa nguvu kwa ajili ya serikali za nchi zote mbili.
Hilo ndilo khasa lililofanywa na Bunge la Tanganyika. Tarehe 25 Aprili 1964 (ambayo ilikuwa ni siku ya Jumamosi), Rais wa Tanganyika, Julius Nyerere, aliliita bunge kwa ajili ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Wajumbe wengi wa Baraza la Mapinduzi walikuwepo wakati Bunge la Tanganyika lilipokuwa likijadili muswada wa sheria mpya wa kuuidhinisha kisheria Mkataba wa Muungano.
Aliusisitiza uhusiano mrefu wa kihistoria baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, ambao umeufanya muungano baina yao uwe kama ni kitu cha kawaida.
Pia alitilia nguvu hamu ya watu wa Afrika kuujenga Umoja wa Afrika. Alilitilia mkazo suala la kuundwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki na kuwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar hautoziathiri [kwa vibaya] juhudi zao katika kuelekea kwenye Umoja wa Waafrika. Kurasa 82-83.
Wakati mchakato wa kuuidhinisha [Mkataba wa Muungano] kwa upande wa Tanganyika ulifuatwa hatua kwa hatua na ulifuata taratibu kama zinavatakiwa na sheria ya Mkataba wa Muungano, hayo hayawezi kusemwa kuwa yalifuatwa kwa upande wa Zanzibar. Ukurasa 85.
Jumbe na Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi] wote wawili hawakubali kuwa kuliwahi kufanywa mkutano wa Baraza la Mapinduzi kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Kwa mujibu wa kiapo aliochoapa Salim Rashid Mahakama Kuu ya Zanzibar, katika kesi ya Rashid Salum Adiy na watu 9 wengine dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu 4 wengine (Nambari 20 ya 2005), ameshuhudia [Salim] kuwa hajawahi kuulizwa na wala hakuwahi kuitisha kikao cha Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano. Hajawahi kuulizwa na hakuwahi kumpa taarifa mwandishi yoyote kuiandika sheria ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Ukurasa 89.
"Katika kipindi chote cha utawala wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere, uhakika wa kisheria wa Muungano ulinyimwa jukwaa. Ikionekana ni usaliti kujadili au hata kuutaja Mkataba wa Muungano wa 1964.


Hayati Mwalim julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa vile Mwalimu Nyerere alivimiliki vyombo rasmi vya habari na kwa sababu kulikuwa hakuna vyombo huru, maovu yake makubwa ya uvunjaji wa Katiba hayakuweza kuripotiwa." Profesa Hamza M. Njozi kwenye dibaji ya kitabu cha Rais Mstaafu Mzee Aboud Jumbe, The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union 30 Turbulent years ambacho kilichapishwa mwaka 1994 na Al Khayria Press Ltd na kuenezwa na Amana Publishers.
Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Jumuiya ya Mataifa (United Nations)
Kutoka Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, Ukurasa 334.
"Ukweli unabakiya kuwa Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar haukuwahi kusajiliwa katika Seketeriet ya Umoja wa Mataifa [UN].

Kwa mujibu wa Andrei Kolomoets wa Ofisii ya Mambo ya Kisheria ya Umoja wa Mataifa "Kama ulisajiliwa basi kungelikuwepo rekodi katika Data Base na shahada ya usajili ingelikuwepo. Nimecheki, haipo."
Kamisheni ya Katiba na Bunge la Katiba
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.

Itakumbukwa kuwa Mkataba wa Muungano uliagiza kuchaguliwa kwa kamisheni ya katiba na kufuatiliwa na bunge la katika ndani ya mwaka mmoja kutokea siku ya kutiwa saini Mkataba wa Muungano ili katiba ya Muungano ipatikane.
Haikufanyika na wakati wa kuyatekeleza hayo ukaakhirishwa moja kwa moja. Kisheria ilifanywa hivyo pale bunge la Muungano lilipopitisha Sheria ya Bunge inayoitwa Sheria ya
Bunge la Muungano, 1965 (Nambari 18)…Kwa hiyo kimyakimya, kisirisiri, bunge la Muungano limeubadilisha Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.

Inaweza kuhojiwa kama (a) upande mmoja wa bunge la Muungano una mamlaka ya kuubalilisha Mkataba wa Muungano ambao ni mkataba wa kimataifa na (b) kuibadilisha sheria ya Zanzibar ambayo inasemekana kuwa ilipitishwa na Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano.
Inaweza ikahojiwa, na kwa njia safi na ilio wazi zaidi, kuwa njia nzuri ingelikuwa kwa viongozi watendaji wawili, Karume na Nyerere, na Nyerere kwa uwezo wake kama ni mkuu wa ‘Tanganyika', angelipatana upya kuhusu Mkataba wa Muungano.
Lakini kisiasa njia hiyo ingelikuwa ni msiba kwa sababu ingeliuunja muungano hapo hapo. Ukurasa 163-164.
Kama unamjuwa adui yako na unajijuwa wewe mwenyewe, utakuwa huna wasiwasi wa matokeo ya vita hata viwe mia. Lakini kama unajijuwa wewe mwenyewe lakini humjui adui yako, basi kwa kila vita utakavyoshinda basi pia utashindwa. Na kama humjui adui yako na hujijui wewe mwenyewe basi utashindwa katika kila vita – Sun Tzu.



My take: This is a golden chance to put things in order, so people should not hate the union. Hapa hakuna suala la uhaini bali kufungua macho na kukabili matatizo yote ya Jamhuri ya Muungano.
 
Tatizo lake huwa mnakurupuka tu kutoa comments bila kuwa na evidence za kutosha. mimi nimeshaishi kwenye nchi kadhaa zinazoendesha serikali zake kwa style hii, na imesaidia sana kuinua hali ya maisha ya maeneo ambayo bado yapo katika hali duni. Ni vema ukauliza ujue serikali ya majimbo inafanyeje kazi. Pengine itakusaidia kuelewa ni nini ambacho kinatokea kwa kila Jimbo.
Wapi? Mbona unaishia njiani?
Kwani NIGERIA HAWANA SERIKALI ZA MAJIMBO? Mbona hayo majimbo yanataka kujitenga? Mbona Jos ambako kuna mafuta wanataka uhuru?
Au unamaanisha CONGO? Au Kenya? Au Angola? Ambako Cabinda hainufaiki na mfuta yake?
Mkuu ukizungumzia majimbo, usifananishe United States na hizi nchi zetu za Africa, wenzetu wameanzisha hayo majimbo from scratch, na majimbo yalipotaka kujitenga ilibidi wauane sana!
Ni rahisi sana kusema HAYA MAMBO HAYAWEZI KUTOKDEA TANZANIA
 
Wapi? Mbona unaishia njiani?
Kwani NIGERIA HAWANA SERIKALI ZA MAJIMBO? Mbona hayo majimbo yanataka kujitenga? Mbona Jos ambako kuna mafuta wanataka uhuru?
Au unamaanisha CONGO? Au Kenya? Au Angola? Ambako Cabinda hainufaiki na mfuta yake?
Mkuu ukizungumzia majimbo, usifananishe United States na hizi nchi zetu za Africa,

Mbona mikoa yetu hajajitenga, au wilaya. Hii ni ile report ya intelligensia ya wakati wa mikusanyiko ya CDM. (Alkhaida, Alkhaida, Alkhaida, Alkhaida, Alkhaida)
 
Nasri, wewe huijui Tanzania vizuri! Hivi ni sehemu gani hamna raslimali kama unavyosema? Kanda ya kati kuna dhahabu, uranium, chuma e.t.c. Kusini kuna mafuta, gesi, dhahabu, n.k. Kaskazini hivyohivyo nchi yetu hamna kanda maskini kama unavyofikilia maskini ni mawazo yetu tuu
Nakubaliana na wewe kabisa. Hakuna mkoa au kanda itakayoundwa ambayo haitakuwa na rasilimali zake kwa ajili ya maendeleo. Nchi hii Mungu aliishushia neema za rasilimali kila kona.
 
“Hapa hoja si muungano uwepo ama usiwepo, hoja ni aina gani ya muungano wa kisiasa Watanzania wanautaka. Tunaamini kuwa hakuna mwanasiasa mwenye akili timamu anaweza kuhubiri kuvunja muungano.

“Mwanasiasa anayezungumzia kuvunja muungano huyo ni mwendawazimu, maana muungano wa kweli wa Watanzania uko kwenye damu zao. Lakini katika suala la kiutawala wananchi waachwe waamue wanataka aina gani, hii ndiyo hoja hapa,” alisema Dk. Slaa.
Sioni tofauti ya alichokisema Dr. Slaa na alichokisema Kikwete.
 
JK kapinga watu kujadili uwepo au kutokuwepo kwa muungano hakupinga watu kujadili aina ya muundo wa muungano nae slaa anasema hakuna mwanasiasa imara anaweza kupinga uwepo wa muungano bali watu wajadili aina ya muungano wautakao,sasa wapi wanapingana? Tukiwa makini hatuwezi kubwebwa na heading za kichonganishi za vipeperushi vilivyosajiliwa kama gazeti!
 
serikali ya majimbo hatuitaki ni kutaka kuibagua mikoa isiyo na rasilimali,tumeshajua nia yenu ni kaskazin yenu muitenge ipate maendeleo kuliko kanda nyingine,hatutaki kubaguliwa hivyo,acha dhambi zako za kibaguzi TANZANIA HAtujafikia uwezo wa kuwa na majimbo au KASKAZIN Mnataka kujitenga kama BEGHAZI,?serikal ya majimbo iliyokuwa kwenye ideology ya JAMAHIRIA ya LIBYA Ilishndwa kuleta maendeleo sawa LIBYA?itawezekana TANZANIA yenye ideology ya kibebari?

Sasa madhara ya majimbo ni kujengeana chuki kati jimbo moja na jingine na kuamini kuwa jimbo moja linafaidi matunda ya uhuru kuliko jimbo lingne

Hapana,

umejenga hoja zako kwenye negativity ya hii sera ya chadema n....a si kwenye realistic

Ukija kuangalia how our govt operates na inavyokusanya fedha kwenda central office na baadae kuzigawanya utaja gundua kuwa we need this kind of policy

Sera ya majimbo ya chadema italeta maendelea haraka, itafanya kila mji, kijiji, kitongoji, etc kupata fedha na kuendelea, zitawafanya wawe creative na kutumia fedha kwa kufuata priority za mahali husika

Itakuwa rahisi viongozi kuwa tracked wanatumiaje fedha, zinazalishwaje n.k

Let me tell you...HAKUNA SEHEMU YEYOTE HAPA TANZANIA AMBAPO kwa namna moja au nyingine kuna sehemu maskini au hawana uwezo wa kuzalisha kipato cha jamii husika

kikiwapo nieleze

Mfano mkoa wa mtwara ambao wewe unauona ni maskini pengine, ndio mkoa wa saba kwa kuongoza pato serikalini!

Wilaya ya Mbinga-ruvuma songea...ndio wilaya tajiri zaidi kuliko zingine zote hapa Tanzania!!

u need just a minute to think about this
 
Kwani tunajadili katba ya Tanganyika au ya Jamhuri ya Muungano. Kama ya muunga, basi upende usipende muungana utajadiliwa ili uboreshwe. Bado kuna kero za muungano, unataka nani akatujadilie. Dr Slaa yuko right. Unajua upole wetu usiwafanye mkajiona ni wafalme. Msipojadili muungano sasa utavunjika. Wait and see.
Mkuu Fredrick, ccm kuendelea kutulazimisha mfumo wa muungano wa serikali mbili, mimi ndani ya moyo wangu nilisha uvunja muungano siku nyingi sana. Simo kabisaa ndani ya muungano wenu niache kama nilivyo kivyanguvyangu!!!!!!
 
Hapa ndipo utafahamu kwamba Uwezo wa kufikiri wa mkuu wetu wakiitikadi na kwa manufaa binafsi.

Huwezi kuwalazisha watanzania (Bara na Visiwani) Kutengeneza mambo ya mstakabalia wa nchi yao nusunusu.

Hataki suala la Muungano lijadiliwe, kero zake zitatatuliwa vipi?

Yeye nimwajiriwa wa watanzania asiwapangie watanzania kuubeba muungano wenye kasoro na kero chungu mbovu, bali atuache tuujadili na tutafute njia bora na muafaka tena thabiti kwa huu muungano.

Kikwete atambue kwamba muungano si wa viongozi au wa wanasiasa bali wa watanzania wote na kuzuia watanzani wasiujadili nadhani ni kuingilia uhuru wa kujadili mambo ya msingi kabisa kuelekea undwaji wa katiba mpya iliyo bora.

Amri za kijeshi sio mahara pake katika jambo hili, huwezi kupata katiba nzuri endapo mambo makubwa na muhimu kama katiba unayaweka kando. Utaishia kuanza safari ya kuunda tume, mapendekezo na kuziba viraka mapema mno. na hizi tume ni wizi na ufisadi pia.
 
serikali ya majimbo hatuitaki ni kutaka kuibagua mikoa isiyo na rasilimali,tumeshajua nia yenu ni kaskazin yenu muitenge ipate maendeleo kuliko kanda nyingine,hatutaki kubaguliwa hivyo,acha dhambi zako za kibaguzi tanzania hatujafikia uwezo wa kuwa na majimbo au kaskazin mnataka kujitenga kama beghazi,?serikal ya majimbo iliyokuwa kwenye ideology ya jamahiria ya libya ilishndwa kuleta maendeleo sawa libya?itawezekana tanzania yenye ideology ya kibebari?

Sasa madhara ya majimbo ni kujengeana chuki kati jimbo moja na jingine na kuamini kuwa jimbo moja linafaidi matunda ya uhuru kuliko jimbo lingne


we hansen una chuki binafsi, katika yote alojadili doctor wa ukweli umeambua moja tu la majimbo?? na iyo sera ikisimamiwa vizuri ni nzuri kwa maendeleo ya haraka yanayozingatia committment kwa wanajimbo, Da wewe utakuwa upande wa magamba walopoteza uelekeo wa kuiongoza nchi, pole yako....
 
Kwa kweli hili suala sio rahisi kama tunavyofikiri. One mistake one goal, tena wakati wa kukusanya maoni wawe makini sana.
 
"Now or Never".
Kutokana na mapitio ya maoni yafauti taliyotangulia, ninachokiona hapa ni kuwa bado CCM wameganda katika sera za Chama kushika Hatamu bila ya kujali kuwa kuanzia 1992 CCM haina mamlaka ya Tanzania yote.

Kama watu kadhaa humu wanavyokuwa wanadhihaki lakini ndio ukweli, CCM ni janga la Taifa.

Ndugu zangu, hii ni fursa ya mwisho kwetu kama Watanzania na wala sio kama wanasisiemu, kuhakikisha tunaandika yetu inayotokana na maoni ya wengi. Vyenginevyo, hiyo kejeli inayosemwa kuwa CCM ni janga kwa taifa itakuja kuwa kweli pale tutakapowaachia kufanya watakavyo. Tusipotahadhari patakuja kuchimbika hapa. Miaka 50 ya kuburuzwa inatosha.

MTU HAWEZI KUKUPANDIA MGONGONI IKIWA HUKUINAMA - Tusiwaruhusu zaidi CCM kutupandia migongoni.
 
serikali ya majimbo hatuitaki ni kutaka kuibagua mikoa isiyo na rasilimali,tumeshajua nia yenu ni kaskazin yenu muitenge ipate maendeleo kuliko kanda nyingine,hatutaki kubaguliwa hivyo,acha dhambi zako za kibaguzi TANZANIA HAtujafikia uwezo wa kuwa na majimbo au KASKAZIN Mnataka kujitenga kama BEGHAZI,?serikal ya majimbo iliyokuwa kwenye ideology ya JAMAHIRIA ya LIBYA Ilishndwa kuleta maendeleo sawa LIBYA?itawezekana TANZANIA yenye ideology ya kibebari?

Sasa madhara ya majimbo ni kujengeana chuki kati jimbo moja na jingine na kuamini kuwa jimbo moja linafaidi matunda ya uhuru kuliko jimbo lingne

Wewe ni mpumbavu maana tayari mikoa imetubagua si kwa raslimali tu bali hata kikabila. Imeendeleza ukoloni na kuongeza gharama kubwa ya kuiongoza.
Leo serikali inalia haina fehda pamoja na mabilioni mengi wanayokusanya, sababu ni ujiga wenu huu.
kabala hujaandika utumbo fikiri kwa kichwa sio masa.......
 
Back
Top Bottom