Slaa amgomea JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa amgomea JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 15, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Slaa amgomea JK
  • Amtaka aache Watanzania waunde Katiba yao

  na Mwandishi wetu, Shinyanga

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameeleza kushtushwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete inayolenga kuzuia wananchi kujadili kuhusu Muungano wakati wa mchakato wa marekebisho ya Katiba.
  Dk. Slaa aliye katika ziara ya kichama kukagua uhai wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kukijenga, alitoa dukuduku lake hilo jana wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shycom, mjini Shinyanga.
  Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu tangu Rais Kikwete alipowaapisha wajumbe 30 wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya inayoongozwa na mwanasheria na mwanasiasa anayeheshimika, Jaji Joseph Warioba.
  Wakati akizindua tume hiyo juzi, pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alisema tume hiyo katika kazi yake haitahusika katika kuhoji kuhusu kuwapo ama kutokuwapo kwa muungano.
  Kwa upande wake Dk. Slaa aliwataka Watanzania kuachana na maneno ya watawala na kutobweteka baada ya kuundwa kwa tume hiyo ya Jaji Warioba.
  “Jamani Watanzania wenzangu wa Shinyanga, naomba tuzungumze kidogo hili la Katiba mpya, kwanza nawaomba msibweteke eti kwa sababu tume imeundwa, kuundwa tume hakuleti katiba mpya na bora. Pia tunataka Kikwete ajue kuwa Watanzania hawatengenezi katiba ya Kikwete wala ya CCM. Wanataka Katiba mpya na bora ya kwao.
  “Nami namuomba ni bora akajitahidi kujiepusha na matamko ya ajabu, maana anaendelea kutupatia ajenda. Anasema suala la muungano lisijadiliwe wakati wa mchakato wa utoaji maoni. Hapa anataka kutuma ujumbe gani…” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa.
  Akiuchambua muungano, Dk. Slaa alisema ni haki ya Watanzania kwa maana ya wale wa Zanzibar na wa Bara kujadili muungano wanaoutaka kwani kufanya hivyo hakuna nia ya kuuvunja.
  “Sisi CHADEMA tunasimamia nini? Tunataka Watanzania wajadili wanataka muungano wa aina gani, tunataka Zanzibar ipate haki zake kama ilivyokuwa mwaka 1964.
  “Hapa hoja si muungano uwepo ama usiwepo, hoja ni aina gani ya muungano wa kisiasa Watanzania wanautaka. Tunaamini kuwa hakuna mwanasiasa mwenye akili timamu anaweza kuhubiri kuvunja muungano.
  “Mwanasiasa anayezungumzia kuvunja muungano huyo ni mwendawazimu, maana muungano wa kweli wa Watanzania uko kwenye damu zao. Lakini katika suala la kiutawala wananchi waachwe waamue wanataka aina gani, hii ndiyo hoja hapa,” alisema Dk. Slaa.
  Akifafanua, Dk. Slaa alisema wanazo taarifa kwamba tayari CCM kupitia katika Halmashauri Kuu yao ya Taifa wameshafikia hatua ya kuwatumia makada wao, wakiwamo viongozi wa kiserikali kama wakuu wa mikoa na wilaya katika kuhakikisha yale ambayo chama hicho tawala kinayataka, yanaingizwa katika Katiba mpya.
  “Napenda kumwambia haya huku akijua kuwa, mkononi kwangu au ofisini kwetu tayari tunao uamuzi wa Halmashauri Kuu ya chama chao, ambayo imewaagiza viongozi ambao ni makada wao, kuhakikisha masuala ambayo chama hicho kinataka yanaingia katika Katiba mpya, hii ni hatari,” alisema Dk. Slaa.
  Akifafanua, alisema chama hicho kitaendelea kuwa mstari wa mbele kuwaongoza Watanzania waandike Katiba mpya inayozingatia haki za msingi kama vile masuala ya ardhi, huku pia akisisitiza kuwa suala la mamlaka ya rais linapaswa kuangaliwa upya na kurekebisha.
  Aliongeza kuwa, moja ya mwarobaini wa kuachana na wateule wengi wa rais ni kuwa na serikali za majimbo ambako viongozi wake sharti wachaguliwe na watu badala ya sasa wananchi kutawaliwa na mkuu wa mkoa au wilaya wasiyemjua.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  serikali ya majimbo hatuitaki ni kutaka kuibagua mikoa isiyo na rasilimali,tumeshajua nia yenu ni kaskazin yenu muitenge ipate maendeleo kuliko kanda nyingine,hatutaki kubaguliwa hivyo,acha dhambi zako za kibaguzi TANZANIA HAtujafikia uwezo wa kuwa na majimbo au KASKAZIN Mnataka kujitenga kama BEGHAZI,?serikal ya majimbo iliyokuwa kwenye ideology ya JAMAHIRIA ya LIBYA Ilishndwa kuleta maendeleo sawa LIBYA?itawezekana TANZANIA yenye ideology ya kibebari?

  Sasa madhara ya majimbo ni kujengeana chuki kati jimbo moja na jingine na kuamini kuwa jimbo moja linafaidi matunda ya uhuru kuliko jimbo lingne
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ukweli unabaki kuwa serikali haikuwa na dhamira ya dhati ya kuleta Katiba mpya.

  Lengo lilikua ni kupreempt chadema kwani wao walikuwa na nia thabiti ya kubadili Katiba, serikali imedandia treni kwa mbele bila hata kujua hiyo treni inakwenda wapi, sasa hawajui cha kufanya.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Dr Slaa yupo right kabisa. Muungano ni LAZIMA ujadiliwe na umma.
   
 5. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wewe mbona unakurupuka? Hamutaki serikali ya majimbo wewe na nani? Wewe unamsemea nani hapa na nani amekupa huo wadhifa wa usemaji? Na hilo suala la majimbo umelitoa wapi kwenye hii topic? Hapa tunazungumzia katiba na elekezo la JK kwamba suala la Muungano lisijadiliwe. Usijaribu kututoa kwenye topic? Twambie je ni sahihi JK kusema muungano usijadiliwe wakati wa mjadala wa katiba mpya? Otherwise wahi Lumumba kwa Nepi ukachukue mshiko tayari umetimiza wajibu wako hapa JF. Tiba
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa mud ani huu sasa kama si sasa lini tena tutaujadili wakati katiba itakuwa tayari ipo bila kuusemea muungano??nashangaa sana!!!
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kaskazini kuna mali gani ya ajabu? Kwanza kama hujui maana ya majimbo si ukae kimya tu. Na tunataka Zanzibar iwe jimbo, nayo ina mafuta.
   
 8. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  slaa acha tume ifanye kazi tafuta hoja nyingine au ulitaka uwemo humo?
   
 9. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  naona hatuko pamoja mkuu, nikuache kwanza.
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani tunajadili katba ya Tanganyika au ya Jamhuri ya Muungano. Kama ya muunga, basi upende usipende muungana utajadiliwa ili uboreshwe. Bado kuna kero za muungano, unataka nani akatujadilie. Dr Slaa yuko right. Unajua upole wetu usiwafanye mkajiona ni wafalme. Msipojadili muungano sasa utavunjika. Wait and see.
   
 12. e

  elishilia Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hansen, fanya utafiti kwanza kuhusu miundo na uendashaji wa serikali za majimbo.nimekuelewa kuwa una kero kubwa kuhusu ukanda fulani kuwa tajiri zaidi kirasilimali na kwamba kipato kitokanacho na rasilimali hizo kitaishia kuendeleza ukanda huo.Lakini,kama moja ya provisions za katiba itatamka kwamba (kwa mfano) asilimia 50 ya pato la jimbo itakwenda federal govt,na iliyobaki state/provincial govt,shida iko wapi?pato litakalo kwenda federal govt litakuwa linaelekezwa kwenye majimbo yanayohitaji support kujiendeleza,kama jimbo lako kwa mfano!kwa karne zote za serikali ya jamhuri mbona kanda flani bado ziko nyuma?mbona serikali za majimbo katika Marekani zimeendelea sana kwa mfumo wa state govt kama tunaohitaji?Penda usipende,hakuna mtawala yeyote mtakaeletewa ambae sio mzaliwa wa ukanda wenu ambae atakuwa na uchungu wa rasilimali zenu,matumizi yake na maendeleo mnayoyataka kama mtawala mzawa wa jimbo lenu na aliyepewa dhamana na wanajimbo lenu na hivyo kuwajibika kwenu.Lakini la msingi sana ni kwamba mtakuwa na fursa ya pekee ya kumchagua governor wa jimbo lenu kwa sifa mnazozitaka wenyewe.kwa mfano uzawa wake,vision yake kwa jimbo LAKE, mikakati yake kwa jimbo LAKE, na mengineyo mengi kwa jimbo LAKE.Lakini pia,huyu kiongozi atakuwa accountable kwa wanajimbo waliomchagua!na siyo kwa mtu fulani mmoja.Faida za kuwa na serikali za majimbo ni nyingi sana!Kama taifa,tume-centralize sana power & authority.na ndiyo maana mfumo huu unachelewesha maamuzi muhimu na ya haraka katika kanda.rasilimali za taifa letu zinapotea kwa sababu ya wanaotakiwa kuzilinda kutokuwa na uchungu nazo kwa sababu ama siyo wazawa na au wanawajibika kwa mtu fulani na sio wanajimbo au kanda!msipotoshwe na kuchoshwa na propaganda za chama kilichotufikisha kwenye umaskini tulionao.abject poverty.FIKIRIA,CHUKUA HATUA!
   
 13. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nasri, wewe huijui Tanzania vizuri! Hivi ni sehemu gani hamna raslimali kama unavyosema? Kanda ya kati kuna dhahabu, uranium, chuma e.t.c. Kusini kuna mafuta, gesi, dhahabu, n.k. Kaskazini hivyohivyo nchi yetu hamna kanda maskini kama unavyofikilia maskini ni mawazo yetu tuu
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tatizo lake huwa mnakurupuka tu kutoa comments bila kuwa na evidence za kutosha. mimi nimeshaishi kwenye nchi kadhaa zinazoendesha serikali zake kwa style hii, na imesaidia sana kuinua hali ya maisha ya maeneo ambayo bado yapo katika hali duni. Ni vema ukauliza ujue serikali ya majimbo inafanyeje kazi. Pengine itakusaidia kuelewa ni nini ambacho kinatokea kwa kila Jimbo.
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Zanzibar Daima (Source)

  Uhuru wa Kuujadili Muungano
  Katiba ni makubaliano ya wananchi juu ya namna wanavyotaka kujitawala. Kwa hivyo wana haki ya kuijadili juu ya mambo yote yanayowahusu wao. Bila shaka, tutaona kuwa Muungano ni jambo muhimu sana linalowahusu waZanzibari zaidi ya mambo yote mengine yaliyomo katika katiba. Rais Shein tayari ametuhakikishia kwamba tunao uhuru kamili kuijadili Katiba Mpya.
  Shirikisho au Muungano?
  Kabla ya kuujadili Muungano, inafaa tutazame chanzo cha dhana ya Umoja wa Afrika Mashariki. Tukumbuke kwamba kabla ya uhuru wa nchi zote za Afrika Mashariki, vyama vyote vya siasa hapa Zanzibar na Afrika Mashariki vilikubaliana na wazo la kuungana katika Shirikisho la Afrika Mashariki (EAF).
  Mw. Nyerere alikuwa tayari kuahirisha uhuru wa Tanganyika kama nchi zote za Afrika Mashariki zingeweza kupata uhuru kwa pamoja na wakaungana. Kwa bahati mbaya, hili halikuwezekana. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake kamili.
  Miezi 4 tu kabla ya uhuru wa Zanzibar, Agosti, 1963, Waziri Tom Mboya wa Kenya alipelekwa na Kenya, Uganda na Tanganyika, kuiuliza Serikali ya Zanzibar kama wako tayari kuanza mazugumzo juu ya EAF ya nchi 4. Zanzibar ilitafakari na ikajibu kwamba walikuwa tayari.
  Zanzibar ilipata uhuru wake kamili Disemba 10, 1963. Kama tunavyojua, Mapinduzi yakatokea Januari 12, 1964, lakini Zanzibar bado ilibakia na uhuru na madaraka yake kamili, pamoja na bendera, nembo, na haki zote za kitaifa, pamoja na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) na OAU.
  Kwa ghafla ilitangazwa Aprili 1964, siku 100 tu baada ya Mapinduzi, kwamba Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zinaungana katika Muungano wa nchi 2 tu. Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa. :
  Suali la kwanza: Kwa kiasi gani watu wa Zanzibar walishauriwa kabla ya kubadilisha muundo mzima wa serikali, na kupoteza uhuru wetu tuliopigania kwa miaka mingi?
  Tunajua kwamba watu wa kawaida hawakuulizwa;
  Inajulikana kwamba Marehemu Mzee Karume hakupewa fursa ya kuwa na mshauri wa kisheria wake mwenyewe – Hati ya Muungano iliandikwa na washauri wakizungu 2 wa Mw. Nyerere, na wao walitumia mfumo wa kikoloni wa Ireland ya Kaskazini kutuandikia Hati ya Muungano.
  Hati ya Muungano haikuridhiwa (ratified) na Baraza La Mapinduzi, na Mwanasheria Mkuu wa SMZ amesema katika Mahakama kwamba SMZ haina nakala ya Hati ya Muungano.
  Suali la pili: Kwa nini tukaiacha dhana ya Shirikisho ya Afrika Mashariki ya nchi 4, na tukavumbuwa Muungano mwengine mpya wa nchi 2 tu?
  Hata Afro-Shirazi Party (ASP), ilikuwa haijataja katika katiba na ilani yake kwamba dira yao ilikuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Hebu na tujiulize, kama kweli Mw. Nyerere alikuwa anaheshimu utaifa wa Zanzibar sawasawa na wa Tanganyika, pale alipoamua kuimeza sehemu kubwa ya Zanzibar ili isiweze kusimama tena kama nchi kamili?
  Ingekuwa kweli azma ilikuwa kuleta Muungano wa Afrika nzima, mbona hata marafiki wake, Obote wa Uganda na Kaunda wa Zambia, walishindwa kujiunga katika Muungano wetu?
  Mw. Nyerere alikua anapenda kuueleza Muungano kutumia mfano wa makapu, na leo hii tutautumia mfano huo huo. Kama nilivyosema mwanzoni, Tanganyika ilipata uhuru wake kamili 1961, na Zanzibar vilevile ilipata uhuru wake kamili 1963. Kwa hivyo, nchi mbili hizi zilikuwa na madaraka na haki za kimataifa sawasawa pale walipopata uhuru wao, na hata baada ya Mapinduzi.
  Imeelezwa na Balozi wa Marekani kwamba aliporudi kutoka Dar es Salaam, Mzee Karume alikuwa anaamini kwamba amesaini Mkataba wa Ushirikiano baina ya nchi mbili hizi, kama alivyokuwa anaifahamu. Alipoulizwa Mzee Karume kwa nini haipo serikali ya Tanganyika kama ya Zanzibar, alijibu kwamba hilo lilikuwa shauri lao wenyewe. . Jibu hilo halikuwa sawa, kwa sababu imeipa fursa Tanganyika kubadilisha gamba na kuvaa gamba la Tanzania, na kumeza madaraka mengi ya Zanzibar, kama tutavyoona.
  Hati ya Muungano
  Katika Hati ya Muungano, kitu kilichofanyika ni kwamba, jina la Serikali ya Tanganyika likabadilishwa na kupewa jina la Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae ikabidilishwa kuwa Tanzania, na kutaka kuufuta kabisa utaifa wa Zanzibar. Wako wanaosema kuwa hiyo haikuwa sawa. Hata Katiba ya Tanganyika ikatumika, baada ya kurekebisha mambo machache tu, kama kubadilisha jina na bendera.
  SMZ ikabakia, lakini madaraka 11 ya serikali hiyo yalihamishwa na kupelekwa kwenye Serikali ya Muungano. Sasa, tukiweka serikali 2 hizi katika mizani, zitakuwa hazina usawa tena, kwa sababu Serikali ya Muungano sasa imekusanya madaraka yote ya Tanganyika na mambo 11 ya Zanzibar.
  Mambo haya 11 ya Muungano si yote yana sura ya kimataifa, bali yanahusu mambo mengi ya uchumi wa ndani. Biashara ya Nje ni katika mambo hayo ya Muungano, lakini uchumi wetu wakati ule ulikuwa unategemea sana uuzaji wa karafuu nchi za nje. Hali kadhalika, Kodi ya Mapato na Ushuru wa Bidhaa yote haya yamehodhiwa na Serikali ya Muungano, na SMZ inapewa ruzuku ya aslimia nne nukta tano (4.5%) tu. Vilevile, SMZ inakosa madaraka juu ya biashara na kodi, hivyo inakosa uwezo wa kupanga uchumi wa nchi moja kwa moja. SMZ imeachiwa kazi ya kuendesha serikali bila kupewa nyenzo ya fedha. Kwa hivyo, hata mgawanyo wa madaraka haukuwa wa usawa.
  Hati ya Muungano ni mkataba wa kimataifa kama unavyojulikana katika sheria ya kimataifa, na haiwezi kubadilishwa kila mara. Iligawana madaraka kati ya SMZ iliobakia na mambo yote yasiokuwa ya Muungano, na Serikali ya Muungano iliokuwa na madaraka yote ya Tanganyika yasiyo ya Muungano, na Mambo 11 ya Muungano ya Tanganyika na ya Zanzibar.
  Mambo ya Muungano ya Ziada
  Lakini mambo hayakuishia hapo. Kila mwaka au miaka 2, madaraka mengine ya Zanzibar yalikuwa yananyakuliwa na kufanywa Mambo ya Muungano, haya ni pamoja na sarafu (1965), mafuta na gesi (1968), na hata Baraza la Mitihani (1973). Mpaka sasa, mambo mengine 11 yamehamishwa kutoka katika madaraka ya SMZ na kupelekwa Dodoma – wengine wanasema mambo haya ni 22. Maana yake ni kwamba ile mizani iliyoinama sana baada ya kuundwa Muungano, basi sasa imelala chini kabisa.
  Hapa tunapaswa tujiulize suali, jee hii ilikuwa ni halali? Hapa hatuna budi kumnukuu Prof. Shivji, mwanasheria aliyebobea katika sheria ya katiba. Huyu sio Mzanzibari lakini ni Mtanganyika; yeye si adui wa Mw. Nyerere bali ni mpenzi wa mawazo ya Mw Nyerere, na sasa hivi anakalia kiti cha Uprofesa wa Mw. Nyerere kule Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; yeye hachukii umoja, bali ni mkereketwa wa Umoja wa Afrika, na kiti chake cha Uprofesa kinaitwa Kiti cha Muungano wa Afrika.
  Mwaka wa 1990 alitoa hotuba yake muhimu sana kama tunataka kufahamu chanzo na sababu za ‘Kero za Muungano':
  Alieleza kwamba sehemu ya Hati ya Muungano inayotaja mambo 11 ya Muungano, ndiyo iliyogawana madaraka kati ya serikali mbili, na kwa hivyo haiwezi kubadilishwa bila kuvuruga muundo mzima wa Muungano.
  Na anaendelea kusema kwamba, si Bunge wala Baraza la Wawakilishi, kwa kila mmoja peke yake, hawana madaraka ya kubadilisha sehemu hii ya Hati ya Muungano. Kwa hivyo, Bunge kubadilisha sehemu hii, kama ilivyofanya mara 11, ni kuzidisha madaraka yake, na kuipokonya Zanzibar. Huu ni ‘unyang'anyaji na ubomoaji wa mfumo halisi wa Muungano.' Mwisho wake SMZ itabakia na kete tupu.
  Prof Shivji anamalizia kwa kusema kwamba, mabadiliko yote yaliyofanyiwa sehemu hii ya Hati ya Muungano ni ‘haramu na batili.'
  Kwa bahati mbaya, Serikali ya Tanzania hawakujali onyo la Profesa Shivji, baada ya miaka miwili tu, waliporejesha mfumo wa vyama vingi, wakaendelea na mtindo wao wa kawaida. Wakachukuwa fursa ya kumnyima Rais wa Zanzibar, anaechaguliwa na watu wa Zanzibar, nafasi yake kama Makamo wa Rais wa Tanzania, iliyotajwa katika Hati ya Muungano. Yeye alikuwa kiungo muhimu kati ya SMZ na Serikali ya Muungano. Sheria hii ilipitishwa na Bunge bila kuhitaji kura ya Thuluthi Mbili (2/3) kwa pande zote mbili. Wabunge wengi wa Zanzibar waliogopa kupinga msimamo wa chama tawala, na wakihiari kwenda kunywa chai au kwenda kujisaidia chooni badala ya kupinga chama chao.
  Baadaye tu wakazinduka na wakaamua kumuingiza Rais wa Zanzibar kama Waziri bila Kazi Maalum katika Baraza la Mawaziri la Tanzania, ambayo ni kumvunjiya heshima yake. Badala yake, wakaleta mfumo wa Makamo Mwenza anaechaguliwa na Watanzania wote, na anatakiwa awashughulikie Watanzania wote, lakini hana nafasi katika SMZ.
  Kwa ufupi, ongezeko la Mambo ya Muungano baada ya 1964, na kumuondosha Rais wa Zanzibar kutoka nafasi yake ya Makamo wa Rais wa Tanzania, yamevuruga kabisa muundo wa Muungano. Vilevile, yamevunja Hati ya Muungano, ambayo ilikuwa mkataba wa kimataifa kati ya Tanganyika na Zanzibar.
  Hati ya Muungano ndio Katiba Mama ya Tanzania. Kwa kiasi kikubwa, mambo yaliofanyika baada 1964 kwa makusudi hayakutaka kuheshimu makubaliano kati ya Marehemu Mzee Karume na Mw. Nyerere, na kuheshimu utaifa wa Zanzibar. Sasa, hata Jaji Mkuu na Waziri Mkuu wanathubutu kusema Zanzibar si nchi.
  Katiba ya Muungano, 1977
  Lakini mambo hayakuishia hapa. Tuangalie Katiba ya Tanzania ya 1977 inayoendesha nchi hii kwa sasa hivi. Nirudie maneno niliosema mwanzoni kwamba katiba ni makubaliano ya wananchi juu ya namna wanavyotaka kujitawala. Lakini, kabla ya katiba kupata uhalali, inahitaji kupata ridhaa ya wananchi walioshirikishwa katika uundaji wa katiba ile, kama sasa tunavyoshiriki katika kuandika Katiba Mpya – hi ndio maana ya uhalali (legitimacy) tunapofikiria katiba.
  Tukumbuke vipi Katiba ya 1977 iliandikwa. Mwaka ule vyama viwili vya ASP na TANU viliamuwa kuungana na kuunda chama kimoja, yaani CCM. Wenyeviti wawili waliteua kamati ya watu 20 chini ya Marehemu Thabit Kombo kuandika Katiba ya CCM – hiyo haitahusu sasa hivi.
  Walipomaliza kazi ile, palepale, tarehe 16 Machi, 1977, Mw Nyerere, kama Rais wa Tanzania, aliteua kamati ileile kuandika Katiba Mpya ya Tanzania. Baada ya wiki moja tu, Tume ya Katiba ikawasilisha Muswada wa Katiba kwenye NEC ya CCM kupata baraka zake. (Hapa tufahamu kwamba muswada ule ulikuwa umeshatengenezwa hata kabla ya kuundwa Tume). Baada ya wiki 4 tu, na bila wananchi kupata fursa kuisoma na kuujadili muswada ule, ikapelekwa katika Bunge la Katiba.
  Bungeni, watu watatu tu walijaribu kuijadili, lakini palepale Waziri Mkuu Sokoine akawambia kwamba muswada ule ushakubaliwa na Chama tawala chini ya mfumo wa chama uliokuwepo, kwamba Chama kimekamata hatamu, kwa hivyo haina haja kuujadili tena. Iliyobaki ni kupigiwa makofi.
  Sasa tujiulize kama katiba iliyopitishwa namna hii bila kuwapa fursa wananchi kuijadili katiba yao, kama sisi sasa tunavyoijadili, inastahiki kukubaliwa kama ni takatifu na halali– kwa maana tuliotaja hapo mwanzoni?
  Kuna matatizo mengi katika Katiba ya 1977, na ndio maana hata Serikali ya Muungano imekubali kuandika Katiba Mpya badala ya kutia viraka juu ya viraka. Lakini kuhusu Muungano, mimi nataka kuongea juu ya mambo 2 tu.
  Jambo la kwanza ni kwamba nchi 2 ziliungana 1964, na kitu kilichowaunganisha ni Hati ya Muungano, na ndio inahisabika kama Katiba Mama ya Tanzania. Hio Hati ndio iliyozaa Katiba ya Serikali ya Tanzania na ya Serikali ya Zanzibar kama watoto wawili pacha. Katiba ya Tanzania haikuzaa Katiba ya Zanzibar, kwa sababu Serikali ya Tanzania haina madaraka juu ya mambo yasio ya Muungano ya Zanzibar.
  Katiba ya Zanzibar inapata uhalali wake kutoka wananchi wa Zanzibar tu. Sasa, kwa nini Katiba ya Tanzania ya 1977 imeingiza sura nzima juu ya Serikali ya Zanzibar? Katiba ya Muungano haina madaraka yoyote juu ya rais wa Zanzibar, BLM au SMZ kwa ujumla, wala juu ya Baraza la Wawakilishi linalochaguliwa na watu wa Zanzibar tu chini ya Katiba ya Zanzibar.
  Sasa kwa nini katiba ya Tanzania imetaka kujiingiza katika madaraka ya Zanzibar? Hii ni kutaka kujidai tu kwamba Katiba ya Zanzibar inatokana na Katiba ya Muungano, ambayo si kweli. Katika Katiba Mpya tunayotaka kuandika sasa, tusikubali kabisa kuwa na sura kama hii.
  Mlango wa Nyuma wa Kuzidisha Mambo ya Muungano
  [Katiba ya Tanzania kulipa Bunge mamlaka hata katika mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar.] Baya zaidi ni Ibara 64 ya Katiba ya Muungano ya 1977. Tunavyofahamu, Katiba ya Muungano inatakiwa ishuhulikie Mambo ya Muuangano na Mambo ya Yasio ya Muungano ya Tanganyika tu, na Katiba ya Zanzibar inatakiwa ishuhulikie Mambo yasio ya Muungano kwa upande wa Zanzibar. Lakini Ibara 64 kwa makusudi imeweka mlango wa nyuma wa kuzidisha mambo ya Muungano kinyemela.
  Kifungu cha 4 kinasema kwamba:
  (4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lolote haitatumika Tanzania Zanzibar ila kwa mujibu wa masharti yafuatayo-
  (a) Sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Zanzibar
  29. Huu ni udanganyifu mtupu. Kama jambo ni la Muungano, haihitaji kusema kwamba itatumika Zanzibar vile vile; lakini kama si la Muungano, basi Bunge haina madaraka ya kusema itafanya kazi Zanzibar, full stop.
  Lakini ndugu zetu wa damu waliendelea kutumia njia hii kutunyonya damu, na kuipora madaraka Zanzibar kila mwaka kutoka 1977. Kati ya 1977 na 2011, wamepitisha sheria ***? juu ya mambo yasio ya Muungano, na wakabandika bango kusema itatumika Zanzibar. Kwa mfano:
  Siasa na vyama vya siasa sio mambo ya Muungano, lakini Sheria ya Vyama vya Siasa ya 1992 inasema kwamba sheria ile itatumika Bara na Zanzibar.
  Bahari na uvuvi sio mambo ya Muungano, lakini Mwaka 1989 Bunge lilipitisha sheria ya Mamlaka ya Bahari na Maeneo ya Uchumi wa Bahari (Territorial Sea & Exclusive Economic Zone), ambayo ilisema kwamba hata maili 12 ya bahari wanamovua wavuvi wetu iko chini ya Muungano; na mwaka 1998 ikapitisha sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu, na yote yalitamka kwamba yatatumika Zanzibar. Juzi juzi Waziri wa Bara alikwenda New York kutaka kuzidisha maeneo ya Tanzania katika Bahari Kuu bila kushauriana na kukubaliana na SMZ. Wiki mbili zilizopita, Wachina waliokamatwa wakivua kwa njia ya haramu Mashariki ya Zanzibar 2009, walitozwa faini ya Sh. 20 billion na Mahakama ya Dar es Salaam – pesa hizi zitaishia Bara kama wale samaki wa Magufuli.
  Kupora mamlaka ya Zanzibar ni suala la kikatiba, lakini Bunge halikuhitaji ata kura ya 2/3 kupitisha sheria hizi. Ni dhahiri kwamba hii ndio ilikuwa njia ya siri ya kuitekeleza sera iliomponyoka Mhe. Ali Hasan Mwinyi katika Bunge mwaka 1994[?]. G55 waliposema kwamba bora kulifikiria suala la Serikali Tatu kutatua kero za Muungano, Mzee Mwinyi aliteleza ulimi na akasema kwamba sera ya CCM ilikuwa kutoka Serikali Mbili na kuenda kwenye Serikali Moja, sera ambayo haikuwahi kutangazwa kabla ya hapo. Ajabu ni kwamba Mw. Nyerere alilaumu sana G55 na Waziri Mkuu Malecela kwamba Serikali Tatu haikuwa sera ya CCM, lakini hakukataa na hakumlaumu Mzee Mwinyi kwamba yeye vilevile aliokosea.
  Bila shaka tuhakikishe kwamba Ibara kama hii isiwepo katika Katiba Mpya, na sheria zote zilizopenyezwa chini ya ibara hii zifutwe mara moja.
  Hitimisho:
  Kabla ya Uhuru tulikubaliana vyama vyote Zanzibar na nchi zote za Afrika Mashariki kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini lilioundwa 1964 haikuwa shirikisho lakini ni Muungano wa Serikali moja na nusu (1 ½).
  Wananchi hawakuulizwa juu ya suala la Muungano. Hati ya Muungano haikupata ridhaa (ratification) ya BLM, na Mwanasheria Mkuu wa SMZ alisema Mahakamani kwamba haijulikani iko wapi. Kwa ufupi, inakosa ridhaa na uhalali kutoka kwa wananchi;
  Hati ya Muungano ilitaja mambo 11 ya Muungano, lakini mambo mengine, kama biashara za nje na kodi, yanaathiri uchumi wa Zanzibar moja kwa moja;
  Mambo mingine 11 yamezidishwa kinyemela, pamoja na mafuta na gesi, na Profesa Shivji anasema yanavuruga mfumo wa Muungano wa 1964, na ni haramu na batili;
  Ibara 64 ya Katiba ya Muungano wa 1977 imefunguwa mlango wa nyuma ya kuipora mambo mengine mengi ya Zanzibar, kama Bahari Kuu.
  Tukiendelea na mfumo huu wa Muungano, mwisho wake Serikali ya Zanzibar itakuwa kete au kapu tupu
  – tutabakiwa na bendera na wimbo ya Taifa,
  - BLW itakuwa halina kazi ya kupitisha sheria;
  - SMZ itakuwa haina kazi ya kutawala nchi yetu;
  - tutakuwa na mawaziri wanaopunga upepo tu;
  - tutakuwa na rais wa pambo tu.
  Basi na tujiulize kwamba, Huko ndiko tunakotaka kwenda?
  Suala ni tuende wapi kutoka hapa kutatua ‘kero za Muungano' zote.
  Ni dhahiri kutokana na uchambuzi wetu tutaona kwamba hizi sio kero za juu juu tu; lakini ni matatizo na hata migogoro iliyosababisha kulazimishwa Rais Jumbe ajiuzulu. Matatizo haya yanatokana na:

  • Muundo (structure) wenyewe wa Muungano,
  • Tafauti kubwa ya kiwatu na ya kieneo kati ya nchi yenye watu milioni moja na nchi yenye watu milioni 45,
  • Maslahi na uchumi tafauti kati ya pande mbili,
  • Makosa yanayotokana na dharau wanayoionyesha Serikali ya Muungano tunapolalamika,
  • Udanganyifu na kutoaminiana pande zote mbili, n.k., n.k.

  Hatuwezi kuendelea hivi. Lazima tukubali kwamba kuna matatizo mengi sana. Katika miaka 48 ya Muungano tumeunda tume na tumeandika ripoti zaidi ya 40, bila kutatua matatizo ya maana, na kila siku yanajitokeza matatizo mengine.
  Sasa na tuwe majasiri kuandika Katiba Mpya ambayo itaweza kufikiria muundo muafaka na itakayoweza kukidhi mahitaji ya Zanzibar: serikali moja, mbili, tatu, Muungano wa mkataba, au nchi mbili hizi ziungane katika Shirikisho la Afrika Mashariki.
  Pia jambo la msingi ni kuwashirikisha wananchi Wazanzibari juu ya suala la Muungano pekee. Wazanzibari hawajapata kushiriki kwa kuulizwa kuhusu Muungano, hivyo ni wakati muafaka kwa SMZ na Baraza la Wawakilishi kuwauliza Wazanzibari kuhusu Muungano. iIkiwa tunania njema na Zanzibar na Muungano wenyewe hili linawezekana na Katiba ya Zanzibar inaturuhusu kuwauliza jambo lolote la kitaifa wananchi kupitia Kura ya Maoni kabla ya kuingia kujadili na kupiga Kura ya Maoni kuipitisha hio Katiba Mpya ya Tanzania.
   
 16. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hebu tueleze 'Kaskazini' itafaidika vipi na sera ya majimbo?

  Ni vizuri tukaelewa maana ya kuwa na majimbo yenye mamlaka kamili katika kuamua matumizi ya rasilimali kwa kuweka vipaumbele kulingana na mahitaji. Serikali kuu ibaki kusimamia utekelezaji wa sera za kitaifa. Hii ni hoja inayopaswa kipingwa kwa hoja na si kuingiza ukablia au ukanda. Anayefanya hivyo amefilisika kimawazo.
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sadaka Zahor Mjawir, Zanzibar
  VIONGOZI wa Tanzania kama wangekuwa wasikivu kwa kutekeleza mapendekezo ya msingi ya Tume ya Jaji Mstaafu Francis Nyalali, basi msamiati wa kero za Muungano pengine ungekuwa umeshazikwa na Shirikisho la Tanzania lingekuwa linatimiza umri wa miaka 19.
  Si haba Aprili 26 mwaka huu, Watanzania wangeadhimisha miaka 19 ya kuzaliwa kwa Shirikisho hilo ambalo lingekuwa mwendelezo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964.
  Katika mapendekezo yake, Tume ya Nyalali kimsingi iliridhia muundo wa Shirikisho kwa kuwa na Serikali Tatu, ile ya Tanganyika kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika na SMZ kwa mambo yoye yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Zanzibar.
  Mambo mengi yalipendekezwa katika Tume hiyo, lakini la msingi hapa kwa leo ni hili la Muundo wa Muungano ambao umepata hata kuungwa mkono na wabunge 55 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Wakati huo aliyekuwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere akiwa nje ya madaraka alionekana kupingana na fikra hizo huku viongozi kadhaa wa juu wakashinikizwa waachie madaraka kwa kile kilichoitwa ni kwenda kiunyume na sera za chama kimoja.
  Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Harace Kolimba wakajiondoa bila ya wao kutaka ili kuinusuru nchi.
  Katika pendekezo la kugeuza mfumo wa Muungano wa Serikali mbili na kuundwa kwa mfumo wa Shirikisho la Serikali Tatu, CCM kwa wakati huo ilikataa mfumo huo kwa hoja dhaifu sana.
  Hata hivyo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio la kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Jamhuri ya Muungano baada ya kundi la wabunge 55 kutoka majimbo ya Tanzania Bara kuwasilisha hoja binafsi Bungeni na kukubaliwa.
  Kimsingi Bunge lilipitisha kwa kauli moja, Agosti 1993 Azimio la kutaka Serikali ya Tanzania kupelekwa muswada wa sheria kubadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuwa na Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano.

  Yafaa kuelewa kuwa kwa madai ya wabunge hayakuwa yao, ni ya wananchi waliowengi na kwa mantiki hiyo ni matakwa ya wananchi wa Tanzania, ingawa CCM iliyabeza wakiongozwa na Mwalimu Nyerere.
  Sintofahamu ikakikumba CCM na hata Serikali ambapo Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alilazimika kulivunja Baraza la Mawaziri kwa sababu ya Azimio la Bunge ambalo dhahiri lilikuwa kinyume cha sera ya CCM, lakini lilibeba maoni ya umma licha ya bezo la Nyerere na CCM yake.
  Pamoja na kubezwa huko, ukweli wa suala hili unabaki pale pale kwamba Watanzania bado wanadai mfumo wa Shirikisho kwa kuwa na muundo wa Muungano wenye Serikali Tatu.
  Haikuishia kulivunja Baraza la Mawaziri tu, Novemba 12-14 , 1993, ulifanyika Mkutano Maalum wa Pamoja kati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Wajumbe wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Wajumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM, na Mawaziri wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mjini Dodoma.
  Mkutano huo uliamua kwamba kwa kuwa suala la kutazama upya Muundo wa Muungano linahusu Sera ya CCM, wana-CCM waulizwe juu ya suala hili na watoe maoni yao.

  Kura za maoni za siri za wana CCM zilipigwa nchi nzima Aprili, 1994 na matokeo yalikuwa kwamba wananchi wanataka mfumo wa Serikali mbili uendelezee, hiki kilikuwa ni kama kituko kilichoambatana na mchezo wa sinema ule wa kina Mr. Bean au Charlie Chaplin.
  Haingii akilini kwamba tayari CCM ilishatoa msimamo wake kuhusu Ripoti ya Nyalali kwamba haitaki Serikali Tatu, lakini baadaye iwaulize wanachama wake wana maoni gani huku ilikuwa kuendeleza maigizo katika ustawi wa demokrasia.
  Muundo wa Serikali mbili ulijengeka juu ya msingi wa chama kimoja ambapo kwenye mazingira ya ushindani wa vyama vingi muundo huo umepoteza msingi wake na hauna budi kuondoka.
  Aidha, katika mfumo wa Serikali mbili huenda Zanzibar isimezwe, lakini ikabaki mdomoni mwa Tanganyika ikitafunwa huku malalamiko yakishika kasi kila uchao.
  Katiba ya Tanzania imeweka vifungu vya haki za binadamu ambapo haki za binadamu msingi wake mkuu ni usawa wa watu binafsi (equality of individuals).
  Izingatiwe kuwa watu binafsi ni sehemu ya vikundi vya jamii katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo kwa sababu za kihistoria na nyinginezo haviko sawa.

  Kwa muktadha huo, haitoshi kutoa kipaumbele kwa dhana ya usawa bila ya dola kuwa na wajibu wa kutoa upendeleo wa makusudi kwa vikundi vya wanyonge (Underprivileged).
  Hoja ya kuwa na mfumo wa Shirikisho inaungwa mkono pia na Tume ya Jaji Robert Kisanga ambaye ni mtalaamu wa mambo ya Katiba na sheria. Benjamin Mkapa kama ilivyo kwa mtangulizi wake, Ali Hassan Mwinyi hakumteua kada wa chama chake kuongoza Tume hiyo.
  Bila shaka Mkapa na Mwinyi walitambua ukweli na uzito wa kuimarisha Muungano kwani kama wangetaka usanii kwa kulinda fikra za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa sera ya CCM ndiyo iwe kioo cha kuimarisha Muungano, hoja ya Shirikisho ingekuwa inapata matokeo hasi.
  Ripoti ya Jaji Kisanga imesema kasoro za Muungano zilizobaki hazirekebishiki pengine kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa Muungano utaendelea kuwa na matatizo mpaka tutakapoamua kuwa na muundo unaotakiwa na umma.
  Kwa mshangao wa wale wasiomfahamu Mkapa, walishangazwa pale alipobeza ushauri wa Tume ya Jaji Kisanga na kufuata mafundisho ya Mwalimu wake katika Shule ya Sekondari Pugu, Julius Nyerere.

  Mkapa alikuwa mtetezi sahihi wa mafundisho ya Baba wa Taifa kwa vitendo ingawa mtihani wa utandawazi ulimfanya kupuuza wosia wa Mwalimu wake kwa kubinafisisha mali za wanyonge kwa wazungu chini ya mwamvuli wa sera ya ubinafsishaji na ujio wa utandawazi.
  Kwa hakika, kaka Ben alisimama katika nadharia ya msimamo wa chama chake wakati Jaji Kisanga alikuwa amezingatia mahitaji ya wakati ule na ya baadaye ya Muungano hali halisi na hatima ya Muungano wenyewe kikatiba. Bila shaka mzee wa zama za uwazi na ukweli aliendeleza siasa za kihafidhina huku Jaji Kisanga alisimamia katika medani ya sheria.
  Wakati wa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ni lazima Zanzibar ikaendesha mchakato wake wa kura ya maoni kuwauliza Wazanzibari aina ya mfumo wa muundo wa Muungano wanaoutaka maana haiwezekani nchi yenye watu wasiozidi milioni moja na nusu kuchanganywa kwa mfano na Wilaya ya Kindondoni yenye watu zaidi ya milioni tatu!
  Uamuzi wa Wazanzibari ndio utakayokuwa dira ya muundo wa Muungano ambao nina uhakika zaidi ya asilimia 70 watakubali mfumo wa Serikali Tatu kwa kuimarisha Muungano.

  Dhana ya Muungano ni pana mno kihistoria ikiambatana na matakwa ya sera na isimamo ya vyama vya TANU kwa upande mmoja na ASP kwa uapande mwinge hasa katika kuitazama Zanzibar.
  Tazama hisia na mitazamo ya wananchi ikiambatana na viongozi wa juu Zanzibar kufuatia mjadala wa muswada wa uundwaji wa Katiba mpya na hoja za msingi.
  Waziri wa zamani wa SMZ, Hamza Hassan Juma hakukubaliana na kutokea kwa mwelekeo wowote utakaoifanya Zanzibar kuwa msindikizaji na mshereheshaji wa kivuli cha Muungano na kuwa kama yatima.
  Hatua hiyo pia ikamuinua Waziri Mansoor Yussuf Himid aliyetoa maoni na kuitaka SMT kukubali kufumbua macho na kubaini kasoro zilizofichwa kwa miaka mingi ambazo sasa haziwezi tena kujificha au kuendelea kufichwa fichwa.
  Waziri wa zamani wa Sheria katika Serikali ya kwanza ya SMZ, Mzee Hassn Nassor Moyo kama shahidi thabit wa Muungano anakataa unafiki na kuzitaka SMZ na SMT kusikiliza matakwa ya kizazi kipya.

  Bila ya kubeza Muungano Mzee Moyo anaelezea kwa undani waliyoyasimamia wao na wakati wao na kuifikisha nchi baada ya miaka 50 kupita na tija ya kusiliza au kuheshimu matakwa ya umma kwa wakati uliopo na wala hakuwa akibezel na kuudhihaki Muungano kama inavyotaka kukuzwa na baadhi ya wasioitakia mema Zanzibar.
  Kama kuna watu wana ndoto za kuwa na Serikali moja wanapaswa kutambua kuwa muundo huo ni mapendekezo ambayo yanaweza kusababisha kumezwa kwa Zanzibar na kufutika katika ramani ya dunia.
  Itakumbukwa kuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliungana zikiwa mataifa huru, hakukua na mkubwa wala mdogo katika suala hilo. Jambo hili lieleweke.
  Ndiyo maana kuna visiwa vidogo vidogo sana, lakini ni wanachama kamili wa Umoja wa Mataifa na wana nguvu na haki sawa kama walivyo wanachama wengine wenye idadi kubwa ya watu na ukubwa wa eneo.
  Kisiwa cha Nauru kina jumla ya watu 12,809 kikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 21 na kimepata uanachama wa kudmu wa UN Septemba 14, 1999 wakati Kisiwa cha Palau kina watu 20,016 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 459 ambayo ilipewa uanachama na UN Desemba 15, 1994 na Kisiwa cha Marshall chenye watu 57,738 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 181 mwanachama wa UN tangu Septemba 17, 1991.
  Visiwa vingine na idadi ya watu wake kwenye mabano ni Saint Kitts na Nevis (38,836) mwanachama wa UN Septemba 23, 1983, Grenada (89,357) mwanachama wa UN tangu Septemba 17, 1974, Antigua na Barbuda (68,320) mwanachama wa UN tangu mwaka 1981 na Shirikisho la Micronesia (108,155).
  Visiwa vingine ambavyo ni mataifa kamili ni Saint Vincent na Grenadines (117,193) mwanachama wa UN tangu Septemba 16, 1980, Sao Tome and Principe (181,565) mwanachama wa UN tangu Septemba 16,1975, Saint Lucia (164,213) mwanachama wa UN tangu Septemba 18,1979, Barbados (278,289) mwanachama wa UN tangu Desemba 9, 1966, Bahamas (299,697) mwanachama wa UN tangu Septemba 18,1973.
  Nimeyataja mataifa hayo kuthibitisha kwamba Zanzibar ni mshiriki sawa katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar licha ya udogo wake wa eneo na idadi ya watu, lakini ina watu wengi ikilinganishwa na visiwa nilivyovitaja awali.
  Lakini la kushangaza, kwa muda mrefu sasa viongozi wa Tanganyika wamekuwa wakiidharau Zanzibar huku wengine wakifikia kuifananisha na Kisiwa cha Ukerewe au Mafia wakati wakijua kuwa bila Zanzibar hakuna Tanzania.

  Mpaka leo wapo baadhi ya watendaji wa idara za Tanganyika wanamtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hii si sahihi hata kidogo na tabia hii haina budi kukoma.
  Ndiyo maana katika kitabu chake The Partner-ship, Aboud Jumbe anaweka wazi usawa wa viongozi hao akisema “Hii ilikuwa ni moja katika mara chache ambapo Nyerere alimtaja Karume kama mtu waliyekuwa na mamlaka sawa.”
  Viongozi waliojaribu kuitetea Zanzibar kama vile Alhaji Aboud Jumbe aliishia kuvuliwa nyadhifa zake kibabe kwa kisingizio cha ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’
  Kitendo cha NEC ya CCM kumvua madaraka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ilikuwa kukiuka na kuchezea kwa ‘makusudi’ mkataba wa Muungano na sheria za Muungano kwa kisingizio cha eti chama kushika hatamu.
  Mkataba wa Muungano ulitaka kuwapo kwa Serikali Tatu au mamlaka ambazo zingeundwa kiuunganishi ambazo katika waraka huo zilitajwa kuwa ni mmoja ya Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano, sasa kosa la Jumbe lilikuwa wapi?
  Mbali ya Mzee Jumbe, Seif Shariff Hamad na wenzake wengine waliokuwa makada wa CCM walitimuliwa na chama hicho mwaka 1988 kwa kisingizio cha kuchafua hali ya hewa ya kisiasa. Lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni mwendelezo wa kuwafunga midomo viongozi wa Zanzibar waliopaza sauti kuitetea.
  Dk. Salmin Amour naye nusura yamkute ya Aboud Jumbe kuhusu suala la Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).
  CCM haikutajwa kuwa ni mshiriki katika Muungano huo na wala si Chama cha TANU au ASP vilivyotajwa zaidi ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.
  Kwa sababu hiyo, CCM haina uwezo wa kisheria wa kujiingiza kisheria na kulazimisha haki na wajibu wa Muungano kwa upande wa Tanganyika, Zanzibar au Jamhuri ya Muungano.
  Tatu zilizoungana kuwa nchi moja yenye muundo wa Shirikisho. Shirikisho halisi la nchi mbili litakuwa ni nchi moja yenye Serikali Tatu, Serikali ya Shirikisho, na Serikali mbili za nchi mbili za awali zilizoungana kuzaa nchi mpya moja.
  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umejengeka kutokana na mahusiano ya dahari na karne baina ya watu wa visiwa vya Zanzibar na mwambao wa upwa wa Afrika ya Mashariki hasa Mrima ambayo ni sehemu kubwa ya Tanzania Bara ya sasa.
  Udogo wa Visiwa vya Zanzibar haulingani na umuhimu wake katika historia ya Afrika Mashariki, Bahari ya Hindi, Arabuni hadi Mashariki ya Mbali, ustaarabu wa Visiwa hivi unatajwa na wasafiri wengi waliotembelea Zanzibar kwa nyakati tofauti.
  Umaarufu wa Zanzibar mbali ya maendeleo ya kibiashara na kiuchumi, ni ustaarabu uliojengeka karne nyingi zilizopita imekifanya kutambulika zaidi katika mataifa mbalimbali.
  Wataalamu wa akiolojia wanathibitisha kuwa dola ya Zanzibar ni miongoni mwa dola kongwe Kusini mwa Jangwa la Sahara.
  Wakati fulani, pwani ya Tanganyika ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar na uthibitisho wa hilo ni kuanzishwa kwa Mji wa Dar es Salaam ulioazishwa na Sultan Majid wa Zanzibar au ukipenda Bandari Salama wenyewe wenyeji wa Mji huo wanauita Mzizima.
  Ardhi ya Bagamoyo ni sehemu ya Zanzibar na hata Padri Mfaransa, Anthony Hooner alipata kibali cha kumilikishwa ardhi kutoka kwa Sultan wa Zanzibar ili kuhamia Bagamoyo na kuanza kazi zake za imani ya Kanisa Katoliki.

  Himaya ya Waajemi (Washirazi) katika eneo hili ambayo baadhi ya wanahistoria wanaiita Himaya ya Zenj (Zenj Empire) ilipojengeka kutokana na ujio wa wale ndugu saba wa El-Hasa karne ya 13 ambao walianzisha tawala katika vituo mbali mbali vya mwambao wa Afrika Mashariki (mfano Kilwa, Barawa, Lamu, Unguja, Pemba, n.k.), maingiliano ya watu wa maeneo haya yaliendelea bila ya vikwazo.
  Zanzibar inaelezwa kutajwa kwa majina tofauti tangu miaka 500 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (a..s.). Uvumbuzi wa akiolojia katika viunga vya Unguja Ukuu unathibitisha kuwapo kwa makazi ya watu tangu zama za mawe.
  Katika kitabu maarufu chenye kumbukumbu za wasafiri wa kale wa Ugiriki waliotembelea mwambao wa Afrika Mashariki kiitwacho Periplus of the Erythrean Sea kilichoandikwa mwaka 100 A.D. (kabla ya Nabii Issa), Zanzibar imetajwa kwa jina la ‘Menouthias’ ikiwa tayari ni nchi yenye watu mchanganyiko tena walio na ustaarabu wakiwa wanavaa nguo za hariri.

  Nchini Uingereza, kuna ramani ya wasafiri wa Kiarabu iliyotayarishwa karne ya 11 ambayo inaonesha visiwa vya Zanzibar na Mji Mkuu wake ukiwa Unguja Ukuu.
  Tunu yote hii ilioanza kuimulika Zanzibar karne kwa karne kamwe haitazimika na watu wake kukubali kuburuzwa kwa kisingizio cha Muungano unaotaka kuvitia shimoni visiwa vyao na kusahaulika ili kuipamba Tanzania iliozuka na kutaka kuzifudikiza historia za Tanganyika na Zanzibar.
  Suluhisho la msingi ili kujenga umoja na mshikamano uliojengeka kwa maiaka 47 ni lazima zipatikane Serikali Tatu, Zanzibar isimame mambo yasiyokuwa ya Muungano, kuwapo na Tanganyika na shirikilsho kama ilivyopendekezwa na Rais Jumbe zikiwamo na Tume za Nyalali na Kisanga.  My take: Sasa hii tume ya katiba isiende kwa mashinikizo ya Mtanzania wote, Bali iheshimu mjadala wa Katiba ya Janhuri ya Muungano bila kuweka mipaka na mikwara. La sivyo tutapoteza muda na rasilimali.
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Zanzibar Daima (Source)
  Uhuru wa Kuujadili Muungano
  Katiba ni makubaliano ya wananchi juu ya namna wanavyotaka kujitawala. Kwa hivyo wana haki ya kuijadili juu ya mambo yote yanayowahusu wao. Bila shaka, tutaona kuwa Muungano ni jambo muhimu sana linalowahusu waZanzibari zaidi ya mambo yote mengine yaliyomo katika katiba. Rais Shein tayari ametuhakikishia kwamba tunao uhuru kamili kuijadili Katiba Mpya.
  Shirikisho au Muungano?
  Kabla ya kuujadili Muungano, inafaa tutazame chanzo cha dhana ya Umoja wa Afrika Mashariki. Tukumbuke kwamba kabla ya uhuru wa nchi zote za Afrika Mashariki, vyama vyote vya siasa hapa Zanzibar na Afrika Mashariki vilikubaliana na wazo la kuungana katika Shirikisho la Afrika Mashariki (EAF).
  Mw. Nyerere alikuwa tayari kuahirisha uhuru wa Tanganyika kama nchi zote za Afrika Mashariki zingeweza kupata uhuru kwa pamoja na wakaungana. Kwa bahati mbaya, hili halikuwezekana. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake kamili.
  Miezi 4 tu kabla ya uhuru wa Zanzibar, Agosti, 1963, Waziri Tom Mboya wa Kenya alipelekwa na Kenya, Uganda na Tanganyika, kuiuliza Serikali ya Zanzibar kama wako tayari kuanza mazugumzo juu ya EAF ya nchi 4. Zanzibar ilitafakari na ikajibu kwamba walikuwa tayari.
  Zanzibar ilipata uhuru wake kamili Disemba 10, 1963. Kama tunavyojua, Mapinduzi yakatokea Januari 12, 1964, lakini Zanzibar bado ilibakia na uhuru na madaraka yake kamili, pamoja na bendera, nembo, na haki zote za kitaifa, pamoja na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) na OAU.
  Kwa ghafla ilitangazwa Aprili 1964, siku 100 tu baada ya Mapinduzi, kwamba Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zinaungana katika Muungano wa nchi 2 tu. Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa. :
  Suali la kwanza: Kwa kiasi gani watu wa Zanzibar walishauriwa kabla ya kubadilisha muundo mzima wa serikali, na kupoteza uhuru wetu tuliopigania kwa miaka mingi?
  Tunajua kwamba watu wa kawaida hawakuulizwa;
  Inajulikana kwamba Marehemu Mzee Karume hakupewa fursa ya kuwa na mshauri wa kisheria wake mwenyewe – Hati ya Muungano iliandikwa na washauri wakizungu 2 wa Mw. Nyerere, na wao walitumia mfumo wa kikoloni wa Ireland ya Kaskazini kutuandikia Hati ya Muungano.
  Hati ya Muungano haikuridhiwa (ratified) na Baraza La Mapinduzi, na Mwanasheria Mkuu wa SMZ amesema katika Mahakama kwamba SMZ haina nakala ya Hati ya Muungano.
  Suali la pili: Kwa nini tukaiacha dhana ya Shirikisho ya Afrika Mashariki ya nchi 4, na tukavumbuwa Muungano mwengine mpya wa nchi 2 tu?
  Hata Afro-Shirazi Party (ASP), ilikuwa haijataja katika katiba na ilani yake kwamba dira yao ilikuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Hebu na tujiulize, kama kweli Mw. Nyerere alikuwa anaheshimu utaifa wa Zanzibar sawasawa na wa Tanganyika, pale alipoamua kuimeza sehemu kubwa ya Zanzibar ili isiweze kusimama tena kama nchi kamili?
  Ingekuwa kweli azma ilikuwa kuleta Muungano wa Afrika nzima, mbona hata marafiki wake, Obote wa Uganda na Kaunda wa Zambia, walishindwa kujiunga katika Muungano wetu?
  Mw. Nyerere alikua anapenda kuueleza Muungano kutumia mfano wa makapu, na leo hii tutautumia mfano huo huo. Kama nilivyosema mwanzoni, Tanganyika ilipata uhuru wake kamili 1961, na Zanzibar vilevile ilipata uhuru wake kamili 1963. Kwa hivyo, nchi mbili hizi zilikuwa na madaraka na haki za kimataifa sawasawa pale walipopata uhuru wao, na hata baada ya Mapinduzi.
  Imeelezwa na Balozi wa Marekani kwamba aliporudi kutoka Dar es Salaam, Mzee Karume alikuwa anaamini kwamba amesaini Mkataba wa Ushirikiano baina ya nchi mbili hizi, kama alivyokuwa anaifahamu. Alipoulizwa Mzee Karume kwa nini haipo serikali ya Tanganyika kama ya Zanzibar, alijibu kwamba hilo lilikuwa shauri lao wenyewe. . Jibu hilo halikuwa sawa, kwa sababu imeipa fursa Tanganyika kubadilisha gamba na kuvaa gamba la Tanzania, na kumeza madaraka mengi ya Zanzibar, kama tutavyoona.
  Hati ya Muungano
  Katika Hati ya Muungano, kitu kilichofanyika ni kwamba, jina la Serikali ya Tanganyika likabadilishwa na kupewa jina la Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae ikabidilishwa kuwa Tanzania, na kutaka kuufuta kabisa utaifa wa Zanzibar. Wako wanaosema kuwa hiyo haikuwa sawa. Hata Katiba ya Tanganyika ikatumika, baada ya kurekebisha mambo machache tu, kama kubadilisha jina na bendera.
  SMZ ikabakia, lakini madaraka 11 ya serikali hiyo yalihamishwa na kupelekwa kwenye Serikali ya Muungano. Sasa, tukiweka serikali 2 hizi katika mizani, zitakuwa hazina usawa tena, kwa sababu Serikali ya Muungano sasa imekusanya madaraka yote ya Tanganyika na mambo 11 ya Zanzibar.
  Mambo haya 11 ya Muungano si yote yana sura ya kimataifa, bali yanahusu mambo mengi ya uchumi wa ndani. Biashara ya Nje ni katika mambo hayo ya Muungano, lakini uchumi wetu wakati ule ulikuwa unategemea sana uuzaji wa karafuu nchi za nje. Hali kadhalika, Kodi ya Mapato na Ushuru wa Bidhaa yote haya yamehodhiwa na Serikali ya Muungano, na SMZ inapewa ruzuku ya aslimia nne nukta tano (4.5%) tu. Vilevile, SMZ inakosa madaraka juu ya biashara na kodi, hivyo inakosa uwezo wa kupanga uchumi wa nchi moja kwa moja. SMZ imeachiwa kazi ya kuendesha serikali bila kupewa nyenzo ya fedha. Kwa hivyo, hata mgawanyo wa madaraka haukuwa wa usawa.
  Hati ya Muungano ni mkataba wa kimataifa kama unavyojulikana katika sheria ya kimataifa, na haiwezi kubadilishwa kila mara. Iligawana madaraka kati ya SMZ iliobakia na mambo yote yasiokuwa ya Muungano, na Serikali ya Muungano iliokuwa na madaraka yote ya Tanganyika yasiyo ya Muungano, na Mambo 11 ya Muungano ya Tanganyika na ya Zanzibar.
  Mambo ya Muungano ya Ziada
  Lakini mambo hayakuishia hapo. Kila mwaka au miaka 2, madaraka mengine ya Zanzibar yalikuwa yananyakuliwa na kufanywa Mambo ya Muungano, haya ni pamoja na sarafu (1965), mafuta na gesi (1968), na hata Baraza la Mitihani (1973). Mpaka sasa, mambo mengine 11 yamehamishwa kutoka katika madaraka ya SMZ na kupelekwa Dodoma – wengine wanasema mambo haya ni 22. Maana yake ni kwamba ile mizani iliyoinama sana baada ya kuundwa Muungano, basi sasa imelala chini kabisa.
  Hapa tunapaswa tujiulize suali, jee hii ilikuwa ni halali? Hapa hatuna budi kumnukuu Prof. Shivji, mwanasheria aliyebobea katika sheria ya katiba. Huyu sio Mzanzibari lakini ni Mtanganyika; yeye si adui wa Mw. Nyerere bali ni mpenzi wa mawazo ya Mw Nyerere, na sasa hivi anakalia kiti cha Uprofesa wa Mw. Nyerere kule Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; yeye hachukii umoja, bali ni mkereketwa wa Umoja wa Afrika, na kiti chake cha Uprofesa kinaitwa Kiti cha Muungano wa Afrika.
  Mwaka wa 1990 alitoa hotuba yake muhimu sana kama tunataka kufahamu chanzo na sababu za ‘Kero za Muungano':
  Alieleza kwamba sehemu ya Hati ya Muungano inayotaja mambo 11 ya Muungano, ndiyo iliyogawana madaraka kati ya serikali mbili, na kwa hivyo haiwezi kubadilishwa bila kuvuruga muundo mzima wa Muungano.
  Na anaendelea kusema kwamba, si Bunge wala Baraza la Wawakilishi, kwa kila mmoja peke yake, hawana madaraka ya kubadilisha sehemu hii ya Hati ya Muungano. Kwa hivyo, Bunge kubadilisha sehemu hii, kama ilivyofanya mara 11, ni kuzidisha madaraka yake, na kuipokonya Zanzibar. Huu ni ‘unyang'anyaji na ubomoaji wa mfumo halisi wa Muungano.' Mwisho wake SMZ itabakia na kete tupu.
  Prof Shivji anamalizia kwa kusema kwamba, mabadiliko yote yaliyofanyiwa sehemu hii ya Hati ya Muungano ni ‘haramu na batili.'
  Kwa bahati mbaya, Serikali ya Tanzania hawakujali onyo la Profesa Shivji, baada ya miaka miwili tu, waliporejesha mfumo wa vyama vingi, wakaendelea na mtindo wao wa kawaida. Wakachukuwa fursa ya kumnyima Rais wa Zanzibar, anaechaguliwa na watu wa Zanzibar, nafasi yake kama Makamo wa Rais wa Tanzania, iliyotajwa katika Hati ya Muungano. Yeye alikuwa kiungo muhimu kati ya SMZ na Serikali ya Muungano. Sheria hii ilipitishwa na Bunge bila kuhitaji kura ya Thuluthi Mbili (2/3) kwa pande zote mbili. Wabunge wengi wa Zanzibar waliogopa kupinga msimamo wa chama tawala, na wakihiari kwenda kunywa chai au kwenda kujisaidia chooni badala ya kupinga chama chao.
  Baadaye tu wakazinduka na wakaamua kumuingiza Rais wa Zanzibar kama Waziri bila Kazi Maalum katika Baraza la Mawaziri la Tanzania, ambayo ni kumvunjiya heshima yake. Badala yake, wakaleta mfumo wa Makamo Mwenza anaechaguliwa na Watanzania wote, na anatakiwa awashughulikie Watanzania wote, lakini hana nafasi katika SMZ.
  Kwa ufupi, ongezeko la Mambo ya Muungano baada ya 1964, na kumuondosha Rais wa Zanzibar kutoka nafasi yake ya Makamo wa Rais wa Tanzania, yamevuruga kabisa muundo wa Muungano. Vilevile, yamevunja Hati ya Muungano, ambayo ilikuwa mkataba wa kimataifa kati ya Tanganyika na Zanzibar.
  Hati ya Muungano ndio Katiba Mama ya Tanzania. Kwa kiasi kikubwa, mambo yaliofanyika baada 1964 kwa makusudi hayakutaka kuheshimu makubaliano kati ya Marehemu Mzee Karume na Mw. Nyerere, na kuheshimu utaifa wa Zanzibar. Sasa, hata Jaji Mkuu na Waziri Mkuu wanathubutu kusema Zanzibar si nchi.
  Katiba ya Muungano, 1977
  Lakini mambo hayakuishia hapa. Tuangalie Katiba ya Tanzania ya 1977 inayoendesha nchi hii kwa sasa hivi. Nirudie maneno niliosema mwanzoni kwamba katiba ni makubaliano ya wananchi juu ya namna wanavyotaka kujitawala. Lakini, kabla ya katiba kupata uhalali, inahitaji kupata ridhaa ya wananchi walioshirikishwa katika uundaji wa katiba ile, kama sasa tunavyoshiriki katika kuandika Katiba Mpya – hi ndio maana ya uhalali (legitimacy) tunapofikiria katiba.
  Tukumbuke vipi Katiba ya 1977 iliandikwa. Mwaka ule vyama viwili vya ASP na TANU viliamuwa kuungana na kuunda chama kimoja, yaani CCM. Wenyeviti wawili waliteua kamati ya watu 20 chini ya Marehemu Thabit Kombo kuandika Katiba ya CCM – hiyo haitahusu sasa hivi.
  Walipomaliza kazi ile, palepale, tarehe 16 Machi, 1977, Mw Nyerere, kama Rais wa Tanzania, aliteua kamati ileile kuandika Katiba Mpya ya Tanzania. Baada ya wiki moja tu, Tume ya Katiba ikawasilisha Muswada wa Katiba kwenye NEC ya CCM kupata baraka zake. (Hapa tufahamu kwamba muswada ule ulikuwa umeshatengenezwa hata kabla ya kuundwa Tume). Baada ya wiki 4 tu, na bila wananchi kupata fursa kuisoma na kuujadili muswada ule, ikapelekwa katika Bunge la Katiba.
  Bungeni, watu watatu tu walijaribu kuijadili, lakini palepale Waziri Mkuu Sokoine akawambia kwamba muswada ule ushakubaliwa na Chama tawala chini ya mfumo wa chama uliokuwepo, kwamba Chama kimekamata hatamu, kwa hivyo haina haja kuujadili tena. Iliyobaki ni kupigiwa makofi.
  Sasa tujiulize kama katiba iliyopitishwa namna hii bila kuwapa fursa wananchi kuijadili katiba yao, kama sisi sasa tunavyoijadili, inastahiki kukubaliwa kama ni takatifu na halali– kwa maana tuliotaja hapo mwanzoni?
  Kuna matatizo mengi katika Katiba ya 1977, na ndio maana hata Serikali ya Muungano imekubali kuandika Katiba Mpya badala ya kutia viraka juu ya viraka. Lakini kuhusu Muungano, mimi nataka kuongea juu ya mambo 2 tu.
  Jambo la kwanza ni kwamba nchi 2 ziliungana 1964, na kitu kilichowaunganisha ni Hati ya Muungano, na ndio inahisabika kama Katiba Mama ya Tanzania. Hio Hati ndio iliyozaa Katiba ya Serikali ya Tanzania na ya Serikali ya Zanzibar kama watoto wawili pacha. Katiba ya Tanzania haikuzaa Katiba ya Zanzibar, kwa sababu Serikali ya Tanzania haina madaraka juu ya mambo yasio ya Muungano ya Zanzibar.
  Katiba ya Zanzibar inapata uhalali wake kutoka wananchi wa Zanzibar tu. Sasa, kwa nini Katiba ya Tanzania ya 1977 imeingiza sura nzima juu ya Serikali ya Zanzibar? Katiba ya Muungano haina madaraka yoyote juu ya rais wa Zanzibar, BLM au SMZ kwa ujumla, wala juu ya Baraza la Wawakilishi linalochaguliwa na watu wa Zanzibar tu chini ya Katiba ya Zanzibar.
  Sasa kwa nini katiba ya Tanzania imetaka kujiingiza katika madaraka ya Zanzibar? Hii ni kutaka kujidai tu kwamba Katiba ya Zanzibar inatokana na Katiba ya Muungano, ambayo si kweli. Katika Katiba Mpya tunayotaka kuandika sasa, tusikubali kabisa kuwa na sura kama hii.
  Mlango wa Nyuma wa Kuzidisha Mambo ya Muungano
  [Katiba ya Tanzania kulipa Bunge mamlaka hata katika mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar.] Baya zaidi ni Ibara 64 ya Katiba ya Muungano ya 1977. Tunavyofahamu, Katiba ya Muungano inatakiwa ishuhulikie Mambo ya Muuangano na Mambo ya Yasio ya Muungano ya Tanganyika tu, na Katiba ya Zanzibar inatakiwa ishuhulikie Mambo yasio ya Muungano kwa upande wa Zanzibar. Lakini Ibara 64 kwa makusudi imeweka mlango wa nyuma wa kuzidisha mambo ya Muungano kinyemela.
  Kifungu cha 4 kinasema kwamba:
  (4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lolote haitatumika Tanzania Zanzibar ila kwa mujibu wa masharti yafuatayo-
  (a) Sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Zanzibar
  29. Huu ni udanganyifu mtupu. Kama jambo ni la Muungano, haihitaji kusema kwamba itatumika Zanzibar vile vile; lakini kama si la Muungano, basi Bunge haina madaraka ya kusema itafanya kazi Zanzibar, full stop.
  Lakini ndugu zetu wa damu waliendelea kutumia njia hii kutunyonya damu, na kuipora madaraka Zanzibar kila mwaka kutoka 1977. Kati ya 1977 na 2011, wamepitisha sheria ***? juu ya mambo yasio ya Muungano, na wakabandika bango kusema itatumika Zanzibar. Kwa mfano:
  Siasa na vyama vya siasa sio mambo ya Muungano, lakini Sheria ya Vyama vya Siasa ya 1992 inasema kwamba sheria ile itatumika Bara na Zanzibar.
  Bahari na uvuvi sio mambo ya Muungano, lakini Mwaka 1989 Bunge lilipitisha sheria ya Mamlaka ya Bahari na Maeneo ya Uchumi wa Bahari (Territorial Sea & Exclusive Economic Zone), ambayo ilisema kwamba hata maili 12 ya bahari wanamovua wavuvi wetu iko chini ya Muungano; na mwaka 1998 ikapitisha sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu, na yote yalitamka kwamba yatatumika Zanzibar. Juzi juzi Waziri wa Bara alikwenda New York kutaka kuzidisha maeneo ya Tanzania katika Bahari Kuu bila kushauriana na kukubaliana na SMZ. Wiki mbili zilizopita, Wachina waliokamatwa wakivua kwa njia ya haramu Mashariki ya Zanzibar 2009, walitozwa faini ya Sh. 20 billion na Mahakama ya Dar es Salaam – pesa hizi zitaishia Bara kama wale samaki wa Magufuli.
  Kupora mamlaka ya Zanzibar ni suala la kikatiba, lakini Bunge halikuhitaji ata kura ya 2/3 kupitisha sheria hizi. Ni dhahiri kwamba hii ndio ilikuwa njia ya siri ya kuitekeleza sera iliomponyoka Mhe. Ali Hasan Mwinyi katika Bunge mwaka 1994[?]. G55 waliposema kwamba bora kulifikiria suala la Serikali Tatu kutatua kero za Muungano, Mzee Mwinyi aliteleza ulimi na akasema kwamba sera ya CCM ilikuwa kutoka Serikali Mbili na kuenda kwenye Serikali Moja, sera ambayo haikuwahi kutangazwa kabla ya hapo. Ajabu ni kwamba Mw. Nyerere alilaumu sana G55 na Waziri Mkuu Malecela kwamba Serikali Tatu haikuwa sera ya CCM, lakini hakukataa na hakumlaumu Mzee Mwinyi kwamba yeye vilevile aliokosea.
  Bila shaka tuhakikishe kwamba Ibara kama hii isiwepo katika Katiba Mpya, na sheria zote zilizopenyezwa chini ya ibara hii zifutwe mara moja.
  Hitimisho:
  Kabla ya Uhuru tulikubaliana vyama vyote Zanzibar na nchi zote za Afrika Mashariki kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini lilioundwa 1964 haikuwa shirikisho lakini ni Muungano wa Serikali moja na nusu (1 ½).
  Wananchi hawakuulizwa juu ya suala la Muungano. Hati ya Muungano haikupata ridhaa (ratification) ya BLM, na Mwanasheria Mkuu wa SMZ alisema Mahakamani kwamba haijulikani iko wapi. Kwa ufupi, inakosa ridhaa na uhalali kutoka kwa wananchi;
  Hati ya Muungano ilitaja mambo 11 ya Muungano, lakini mambo mengine, kama biashara za nje na kodi, yanaathiri uchumi wa Zanzibar moja kwa moja;
  Mambo mingine 11 yamezidishwa kinyemela, pamoja na mafuta na gesi, na Profesa Shivji anasema yanavuruga mfumo wa Muungano wa 1964, na ni haramu na batili;
  Ibara 64 ya Katiba ya Muungano wa 1977 imefunguwa mlango wa nyuma ya kuipora mambo mengine mengi ya Zanzibar, kama Bahari Kuu.
  Tukiendelea na mfumo huu wa Muungano, mwisho wake Serikali ya Zanzibar itakuwa kete au kapu tupu
  – tutabakiwa na bendera na wimbo ya Taifa,
  - BLW itakuwa halina kazi ya kupitisha sheria;
  - SMZ itakuwa haina kazi ya kutawala nchi yetu;
  - tutakuwa na mawaziri wanaopunga upepo tu;
  - tutakuwa na rais wa pambo tu.
  Basi na tujiulize kwamba, Huko ndiko tunakotaka kwenda?
  Suala ni tuende wapi kutoka hapa kutatua ‘kero za Muungano' zote.
  Ni dhahiri kutokana na uchambuzi wetu tutaona kwamba hizi sio kero za juu juu tu; lakini ni matatizo na hata migogoro iliyosababisha kulazimishwa Rais Jumbe ajiuzulu. Matatizo haya yanatokana na:

  • Muundo (structure) wenyewe wa Muungano,
  • Tafauti kubwa ya kiwatu na ya kieneo kati ya nchi yenye watu milioni moja na nchi yenye watu milioni 45,
  • Maslahi na uchumi tafauti kati ya pande mbili,
  • Makosa yanayotokana na dharau wanayoionyesha Serikali ya Muungano tunapolalamika,
  • Udanganyifu na kutoaminiana pande zote mbili, n.k., n.k.
  Hatuwezi kuendelea hivi. Lazima tukubali kwamba kuna matatizo mengi sana. Katika miaka 48 ya Muungano tumeunda tume na tumeandika ripoti zaidi ya 40, bila kutatua matatizo ya maana, na kila siku yanajitokeza matatizo mengine.
  Sasa na tuwe majasiri kuandika Katiba Mpya ambayo itaweza kufikiria muundo muafaka na itakayoweza kukidhi mahitaji ya Zanzibar: serikali moja, mbili, tatu, Muungano wa mkataba, au nchi mbili hizi ziungane katika Shirikisho la Afrika Mashariki.
  Pia jambo la msingi ni kuwashirikisha wananchi Wazanzibari juu ya suala la Muungano pekee. Wazanzibari hawajapata kushiriki kwa kuulizwa kuhusu Muungano, hivyo ni wakati muafaka kwa SMZ na Baraza la Wawakilishi kuwauliza Wazanzibari kuhusu Muungano. iIkiwa tunania njema na Zanzibar na Muungano wenyewe hili linawezekana na Katiba ya Zanzibar inaturuhusu kuwauliza jambo lolote la kitaifa wananchi kupitia Kura ya Maoni kabla ya kuingia kujadili na kupiga Kura ya Maoni kuipitisha hio Katiba Mpya ya Tanzania.
   
 19. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ishu ya kuwachagua viongozi wa maeneo mbalimbali kama mkoa/jimbo ni jambo la msingi sana tuliunge mkono.
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani jk kama hataki ujadiliwe sasa anataka aje kuandaa tume nyingine ya kuhoji hilo ndo katiba iandaliwe ama anataka je maana simwelewielewi!
   
Loading...