Siungi mkono Rais kutukanwa!

wameanza kushika ADABU, walishazoea kumtukana JK naZZK.
 
Asante Lema,

Lakini mbona kama alichangiwa 4.5m za faini na viongozi wa chama chako mkoa, au mlimchangia baadae mkamwambia lakini kijana umekosea au ulinyamaza kimya.
Iko namna sio bure....
 
Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Tunapaswa kuiiga Marekani kwa kila jambo.Kama wanaruhusiwa kumtukana rais wao kwanini kwetu iwe nongwa.Pia wamarekani wanaruhusu ushoga..........
 
Lema! Kuna kitu si bure, tutakijua awamu hii hii.
 
Ni Mara ngapi JK alitukanwa mpaka kwa njia ya picha? Mbona hukutia neno?
Au akina Lowassa,mgombea wa chama chako ametukanwa Mara ngapi? Au yeye anastahili matusi ya kuji.NY.ea KWA kuwa sio rais? Sasa bwana mkubwa,kila enzi na kitabu chake.
Acha akina Pepsin tuendelee kutukanwa KWA kuwa sisi sio marais!
 
Bwege!!! kila nikilazimisha kamusi yangu ione kuwa hilo neno ni tusi nakuta haiwezekani....nahofia hata kusema mheshimiwa ni mzembe.
 
Hapana uhuru wa mtu uheshimiwe. Mimi sioni shida kama mtu anataka kuwa shoga inakuhusu nini. Haki yako ipi imevunjwa nambie. Usiniambie mambo ya dini. Wengine hatuna Mungu. Hiyo ni personal
 
Hapana uhuru as mtu uheshimiwe. Mimi sioni shida kama mtu anataka kuwa shoga inakuhusu nini. Halo yako ipi imevunjwa nambie. Usiniambie mambo ya dini. Wengine hatuna Mungu. Hiyo ni personal
Umeenda mbali sana, sidhani kama ushoga tunaupinga kwa sababu ya Dini tu, ila tamaduni zetu hasiruhusu pia. Alafu mkuu mtu akisha kuwa shoga tayari hasara kwa Taifa, nguvu kazi ya kiume imepotea tayari, shoga hamudu kunyanyua vitu vizito vilivyowekwa chini mfano ndoo ya maji, tofari, nyunia Nk. Unaponyanyua vitu vizito kuna misuri lazima ikaze, shoga wengi hulegea kama wanawake tu, hawamudu kazi ngumu tena tena afadhari ya mwanamke. Fikiria mwanao wa kiume umentuza vizuri umemsomesha, sasa anataka kujitegemea, alafu siku ya siku akuletee habari amepata bwana mwenye pesa zake anataka kuolewa nae, wewe kama mzazi utaipokea kwa furaha tu, eti ushoga wake haukuhusu. Mimi naamini madhara ya ushoga, madawa ya kulevya, jambazi na mabaya mengine yanatuhusu sote kama Taifa. Mbona tunapiga kelele kuhusu Chid Benz na Ray C.
 
Well, kwa upande mmoja kutukana ni kosa. Kwa upande wa pili neno kuwa tusi lazima liwe na maana isiyo sahihi na ya kulazimisha. Km yanataja aspect ya mlalamikaji kwa uhasilia sio tusi. Si ajabu kuwa na rais mzinzi au mwizi au mdini..au hata bwege. Ukimwita mdini , mzinzi au bwege km Uhalisia wake ikawa nongwa.


Pengine tungejiuliza aliyetukanwa ni rais au nafasi ya rais ambayo hata mwizi alifika anakuwa na nguvu zote? Nadhani katiba itakuwa na shida km itafunga midomo rais kuitwa kwa sifa zake na ikibidi hayo matendo yamfikishe mahakamani.
 
Ni vichwa vyenu tuu vina shida? Ndio maana hamjijui kwanini rais ana nguvu nyingi. Rais ni raia km wewe na kinacho mpa heshima ni tabia yake na uadilifu na si nguvu za ikulu. Km anazini km Clinton anachekwa tuu km wengine. Na anaadhibiwa. Ila kwa hizi tabia yenu rais akibaka mbakaji ndie atahukumiwa kwa ku tuka na rais.
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.
Kumchangia ni sawa kabisa kuliko serikali ikatumie mamilioni kumlisha akiwa jela kwa kosa hilo kweli angalia pande zote
 
Ni vichwa vyenu tuu vina shida? Ndio maana hamjijui kwanini rais ana nguvu nyingi. Rais ni Raia km wewe na kanacho mpa heshima ni tabia yake na si nguvu za ikulu.
Wewe ndiyo unajiona unaakili sana, mkuu nakushauri usipende tabia kuona wewe unaelewa, eti wenye mtizamo tofauti wote hawana akili, kuto jua Lugha ya staha ndicho kinachotupelekea kuwepo mjadala huu. Kwa nikubariane na wewe awe Rais au kiongozi mwingine au mtu yeyote yule, asipokuwa na Lugha ya staha asitegemee kuheshimiwa na jamii. Sioni kama mada unauhusiano na Rais kutokua na staha na naamini hayuko hivyo, inahusu kutukwanwa Rais, nikwambie tu Rais ni raia kama wewe na mimi sawa, ila ana hadhi tofauti na wewe na mimi. Ndiyo maana anapewa ulinzi wewe hulindwi, lakini hata hadhi ya wazazi wako hailingani na yako, ndiyo maana unaona mtu akitukanwa yeye shuguri yake yaweza kuwa ndogo tu, ila mzazi wako hee, moto wake hauzimwi kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…