Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Pamoja na uhaba wa ajira unaoikabili nchi yetu. Hakuna daktari aliyewahi kuomba kazi serikalini akanyimwa. Watanzania wengine ambao nao wana haki ya kupata ajira kama madaktari wamekuwa wakihaha mitaani kutafuta kazi na vibahasha vya khaki. Wengine wamekaa mtaani zaidi ya miaka miwili kabla ya kupata kazi ingawa wana degree. Badala ya serikali kuongeza nguvu kwenye kuongeza maposho ya wabunge na makundi mengine ya watumishi wa umma, ili kuwa fair ni LAZIMA serikali itoe kipaumbele kwenye kutengeneza ajira mpya ili kila aliyefanya jitihada za kupata ujuzi aweze kupata ajira au kuwezeshwa kujiajiri. Sasa hivi nchi imekutwa na KANSA ya watu wachache waliopata fursa kutaka kufyonza rojorojo yote na wale ambao hata kidogo hawajapata kusahaulika. Kila anayeitaia mema Tanzania hivi sasa anatakiwa atoe kipaumbele kwenye kuhakikisha vijana wetu waliosoma uhasibu, sheria, uhandisi, maendeleo ya jamii na fani nyingine wanapatiwa ajira. Hili ndio jambo ambalo linatakiwa kufanywa MARA MOJA sio kusema wale walioshapata kafursa fulani waongeze fursa hiyo kwa asilimia 500. Watanzania tunaumizana wenyewe kwa wenyewe...
hii asilimia 500 unaipataje? una uhakika kama serikali imeajiri madaktari wote waliomaliza masomo?unajua mwaka huu wameajiri M.Ds wangapi kwa mwaka huu ?serikali ina fedha bana si umeona sherehe za miaka 50 ya uhuru zilivyofana!!si uliona maonyesho ya nane nane wale watu wa wizara ya afya walivyopendeza na mabazee!!!!ha ha ha ha acheni upuuzi yani mkidaiwa maslahi zaidi mnasema hamna fedha lakini kwenye sherehe mifwedha bwerere.
 
Kuna madaktari waliona mshahara wa serikali hautoshi ninatoa live examples.

Dr. Bake: Huyu alikuwa anafanya kazi Tumbi hospital akilipwa sh laki 4 kama specialist wa mifupa. Alikuwa smart enough kuona kuwa hawezi kuishi maisha anayotaka kwa mshahara huo. Aliacha kazi kwa notice ya masaa 24 mwaka 1996. Hivi sasa anamiliki kituo cha afya ya mifupa huko Kibaha. Watu wanasafiri long distance kwenda kumuona. Halalamikii tena mshahara.

Daktari anayelilia serikali imuwezeshe kuishi kama mfalme ni yule ambaye hana uhakika na skills zake. kama una skills watu watakufuata popote. Kama watanzania walitumia mamilioni kwenda Loliondo, hawatashindwa kukufuata wewe utakapokuwa.

Kama madaktari wanaweza kuchangiana mamilioni kwa ajili ya harusi, wanashindwa nini kuchanga kufungua vituo vyao binafsi vya tiba? Madaktari wa kihindi wameonyesha kwamba it is possible: Aga Khan, Regency, TMJ, Hindu Mandal etc. Wake up doctors, kutumia muda mwingi kufikiria jinsi ya kuongezewa mshahara is a wrong approach, tumia muda huo kufikiria jinsi utakavyodevelop private practice. Mkifungua vituo vyenu, serikali itatambua thamani yenu, sasa hivi serikalli inajua mna options chache, prove it wrong...
 
Hakuna daktari aliyeomba kazi serikalini akakosa, labda kama amekataa kwenda alikopewa kazi. Watu waliosomea fani nyingine hata huko mawilayani hawapewi kazi. Kipaumbele kwa sasa lazima kiwe kuhakikisha vijana wote wenye degree wanapata kazi.
 
1. Huwaambii rudini mlipotoka, hilo siyo kazi yako. Unachofanya ni kuwaambia kuwa vitanda vimejaa. wataenda wapi? thats none of your business. Kimsingi madaktari wanaonyesha udhaifu wa weledi pale ambapo mgoonjwa anapewa referral toka Kigoma to Muhimbili na madaktari hawajadevelop utaratibu wowote wa kuicontact Muhimbili kama ina nafasi ya kumpokea huyo mgonjwa! Jukumu la kubuni utaratibu ambao ni functional ni la wataalam ambao ni madaktari. Usipokee waginjwa wengi kuliko uwezo wako kwa sababu in the end hutampa hata mmoja kati yao huduma anayostahili.

2. Unaposema haiingii akilini kukataa kupokea mgonjwa toka kigoma kwa sababu ya kutokuwepo kwa vitanda inabidi ujiulize je, inaingia akilini kukataa kuwahudumia watu waliotoka nchi zima kwa mgomo? Kwa kifupi hapa umeshasema huungi mkono mgomo.

Unawaambia vitanda vimejaa, halafu?! Hoteli na Guest Houses ndo sehemu pekee wanazoweza kufanya hivyo kwa uhuru na bado watu wakajiondokea kwenda kutafuta pengine bila madhara makubwa!
Mbona hujajiuliza kwa nini mtu atoke umbali wote huo,kigoma hadi Dar, kuja kwa ajili ya kutibiwa?!
Tena labda kwa ajili ya kipimo tu!?
Sidhani kama unajua unachokiongea!
 
Kama daktari anaweza kuamua kugoma kabisa na asitoe huduma kwa mtu yeyote yule, sioni kwa nini kwa daktari huyo iwe vigumu kukataa kupokea wagonjwa ambao hana pa kuwalaza.
 
Hakuna daktari aliyeomba kazi serikalini akakosa, labda kama amekataa kwenda alikopewa kazi. Watu waliosomea fani nyingine hata huko mawilayani hawapewi kazi. Kipaumbele kwa sasa lazima kiwe kuhakikisha vijana wote wenye degree wanapata kazi.
nimekuuliza unajua serikali ilipanga kuajiri M.Ds wangapi mwaka huu??na je unajua ni M.Ds wangapi wanamaliza mafunzo ya udaktari kwa mwaka?acha porojo bana pale wizarani kuna longolongo sana ndio maana matatizo kama haya yametokea.
 
Senior expert????
Huwezi elewa umuhimu wa daktari kama hujawahi ona uhangaikaji wao tangia masomoni mpaka mafunzoni na kisha wanapoajiriwa, ni mateso kuanzia mwanzo mpaka futi sita kaburini
Yes,nakubaliana na wewe ni watumishi wa umma kama walimu, na wengineo
VIpi unaonaje siku mkeo akiwa anapata uchungu wa kujifungua na hakuna daktari wa zamu?
wanachotaka madktari ni mambo ya msingi, nakushauri uyasome kwa hatua then uyatafakari kuliko kukimbilia kujaza inbox hapa kama viongozi wako
 
Kuna madaktari waliona mshahara wa serikali hautoshi ninatoa live examples.

Dr. Bake: Huyu alikuwa anafanya kazi Tumbi hospital akilipwa sh laki 4 kama specialist wa mifupa. Alikuwa smart enough kuona kuwa hawezi kuishi maisha anayotaka kwa mshahara huo. Aliacha kazi kwa notice ya masaa 24 mwaka 1996. Hivi sasa anamiliki kituo cha afya ya mifupa huko Kibaha. Watu wanasafiri long distance kwenda kumuona. Halalamikii tena mshahara.

Daktari anayelilia serikali imuwezeshe kuishi kama mfalme ni yule ambaye hana uhakika na skills zake. kama una skills watu watakufuata popote. Kama watanzania walitumia mamilioni kwenda Loliondo, hawatashindwa kukufuata wewe utakapokuwa.

Kama madaktari wanaweza kuchangiana mamilioni kwa ajili ya harusi, wanashindwa nini kuchanga kufungua vituo vyao binafsi vya tiba? Madaktari wa kihindi wameonyesha kwamba it is possible: Aga Khan, Regency, TMJ, Hindu Mandal etc. Wake up doctors, kutumia muda mwingi kufikiria jinsi ya kuongezewa mshahara is a wrong approach, tumia muda huo kufikiria jinsi utakavyodevelop private practice. Mkifungua vituo vyenu, serikali itatambua thamani yenu, sasa hivi serikalli inajua mna options chache, prove it wrong...

mkuu mi sielewi argument yako ni nini.. sasa madactari wote wakikimbilia private sector mwananchi wa kawaida atakimbilia wapi..?

wanachodai madactari ni kuboreshwa kwa maslahi na mazingira ya kazi .ni mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa serikali .. ni kirudi kwemye ili point uliyonijibu kwamba mgonjwa aliyetoka kigoma na kuwa reffered hospitali muhimbili akafika pale vitanda vimejaa ukanijibu kwamba wamkatae kwa sababu hospitali haina vitanda tutakataa wagonjwa wangapi..?? ... hivi mkuu mwenzetu weye ni mmoja wa wale wanaotibiwa INDIA ..?? au either haupo TZN .. sasa huyu mama wa kigoma akikataliwa aende wapi..?! mambo mengine sio ya kubishana kabisa
 
nimekuuliza unajua serikali ilipanga kuajiri M.Ds wangapi mwaka huu??na je unajua ni M.Ds wangapi wanamaliza mafunzo ya udaktari kwa mwaka?acha porojo bana pale wizarani kuna longolongo sana ndio maana matatizo kama haya yametokea.

Huna haja ya kuniuliza maswali. Kama kuna daktari ameomba kazi wizarani akakosa nipe jina lake kwenye PM.
 
Kuna madaktari waliona mshahara wa serikali hautoshi ninatoa live examples.

Dr. Bake: Huyu alikuwa anafanya kazi Tumbi hospital akilipwa sh laki 4 kama specialist wa mifupa. Alikuwa smart enough kuona kuwa hawezi kuishi maisha anayotaka kwa mshahara huo. Aliacha kazi kwa notice ya masaa 24 mwaka 1996. Hivi sasa anamiliki kituo cha afya ya mifupa huko Kibaha. Watu wanasafiri long distance kwenda kumuona. Halalamikii tena mshahara.

Daktari anayelilia serikali imuwezeshe kuishi kama mfalme ni yule ambaye hana uhakika na skills zake. kama una skills watu watakufuata popote. Kama watanzania walitumia mamilioni kwenda Loliondo, hawatashindwa kukufuata wewe utakapokuwa.

Kama madaktari wanaweza kuchangiana mamilioni kwa ajili ya harusi, wanashindwa nini kuchanga kufungua vituo vyao binafsi vya tiba? Madaktari wa kihindi wameonyesha kwamba it is possible: Aga Khan, Regency, TMJ, Hindu Mandal etc. Wake up doctors, kutumia muda mwingi kufikiria jinsi ya kuongezewa mshahara is a wrong approach, tumia muda huo kufikiria jinsi utakavyodevelop private practice. Mkifungua vituo vyenu, serikali itatambua thamani yenu, sasa hivi serikalli inajua mna options chache, prove it wrong...
nenda pale MOI uone cases zilizotoka kwa Dr Bake na kupata complications.halafu unataka kila daktari ajiendeshe kibiashara unadhani yule bibi yako wa kasulu aliyeambiwa huduma ni bure ataweza kuafford??mbona una mawazo mgando namna hii?
 
mkuu mi sielewi argument yako ni nini.. sasa madactari wote wakikimbilia private sector mwananchi wa kawaida atakimbilia wapi..?

wanachodai madactari ni kuboreshwa kwa maslahi na mazingira ya kazi ... ni kirudi kwemye ili point uliyonijibu kwamba mgonjwa aliyetoka kigoma na kuwa reffered hospitali muhimbili akafika pale vitanda vimejaa ukanijibu kwamba wamkatae kwa sababu hospitali haina vitanda tutakataa wagonjwa wangapi..?? ... hivi mkuu mwenzetu weye ni mmoja wa wale wanaotibiwa INDIA ..?? au either haupo TZN .. sasa huyu mama wa kigoma akikataliwa aende wapi..?! mambo mengine sio ya kubishana kabisa

Swala la watakakotibiwa wananchi sio la daktari. Hilo ni swala la viongozi wa nchi, wao ndio wanatakiwa kujua kuna wananchi wangapi na wanapata vipi huduma za kijamii.

Kama madaktari wanajali sana kuwa wananchi hawakosi huduma basi kwanza waache kugoma kuwahudumia hao wanaowajali. Huwezi kusema unajali sana kumpa mtu huduma halafu unagoma kumhudumia. Kuna njia nyingi za kuprotest, kwa nini madaktari wameamua kuchagua njia ya mgomo? Kwa nini mshahara wa siku walizogoma wanauchukua?
 
Suala hapa si kuunga au kutounga mkono huo mgomo. Jambo la msingi ni Serikali kuwa serious katika kuwajali wananchi wake kihuduma. Serikali hapo serious hata kidogo kwamfano;

Kwangu mimi ni serikali ndiyo inayochochea madhara ya mgomo huu, masuala hayo ya madaktari si ya leo ni ya muda mrefu, serikali si sikivu hata kidogo na imejaa viongozi wasio sikia na wasiojali,ni usanii mtupu.

Lakini juu ya yote, naomba tusiwabeze madaktari,jamani kazi yao si sawa na ualimu n.k, jamani wapewe haki zao.

Serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima na pesa ipelekwe kwenye maeneo nyeti kama afya. Mbona JK haishi kusafiri tena na kundi la watu? Mbona Mawaziri haweshi kuishi mahotelini wakati nyumba za serikali zimeuzwa? Mbona Posho za Wabunge zaachwa zipite pasi longolongo? Mbona matamasha na semina elekezi zenda pasi wasi wala neno juu ya ukata?

Jamani,tuache siasa, kushindwa kwa serikali kutatua suala la madaktari, ni alama tosha kuwa serikali sasa imeelemewa, imeshindwa kuwahudumia wananchi wake.

Mwisho kabisa, ikumbukwe kuwa, kwa mujibu wa sheria za kazi, mgomo ni halali na ni sehemu mojawapo ya hatua za kufuata katika kutatua migogoro baina ya waajiri na waajiriwa. Tusiwabeze madaktari. Tuibeze serikali yetu,isiyosikia vilio vya wananchi.

Mwasema madaktari walogoma wafukuzwe, sawa, hao watakaoajiriwa ndo waje sema NDIYO kwa kila neno? Huo si Ujeshi na Ubabe? Je tukifika huko, si udikteta?

Jamani tuache siasa, tudai haki zetu kwa kila nyanja.

Nawasilisha
 
nenda pale MOI uone cases zilizotoka kwa Dr Bake na kupata complications.halafu unataka kila daktari ajiendeshe kibiashara unadhani yule bibi yako wa kasulu aliyeambiwa huduma ni bure ataweza kuafford??mbona una mawazo mgando namna hii?
Hakuna surgical clinic ambayo haina complications. Hata ukienda kwa Bake utakuta cases za MOI zilizopata complications pia.
 
Swala la watakakotibiwa wananchi sio la daktari. Hilo ni swala la viongozi wa nchi, wao ndio wanatakiwa kujua kuna wananchi wangapi na wanapata vipi huduma za kijamii.

unaposema hilo ni swala la kiongozi wa nchi ... huyu mama kutoka kigoma atatibiwa na nani bado jibu lako ni dhaifu.. kwa hiyo unataka kunambia huyu mama akishafika pale muhimbili akaambiwa vitanda vimejaa... aende moja kwa moja kwa Mh. PINDA akamtafutie hospitali ambayo kuna vitanda vya kutosha , kuna dawa za kutosha, kuna ct scans na pia wauguzi wa afya si MADACTARI .. sidhani kama ipo hospitali ya aina hiyo tanzania
 
Hakuna surgical clinic ambayo haina complications. Hata ukienda kwa Bake utakuta cases za MOI zilizopata complications pia.
usikae kusifia sifia ukadhani kila mtu hajui.maskini wangapi wanaweza kwenda kwa bake,TMJ,Aga khan,regency? yaani wewe mawazo yako yanaishia posta tu,unadhani tanzania nzima ni kama posta.tembea uone wananchi wanavyoishi maisha duni halafu uwapelekee mawazo yako ya kisharobaro.
 
huyu jamaa ametumwa au ni mmoja ya wale wenye uwezo wa kwenda kutibiwa INDIA.... acha niende zangu msikitini .. nitarudi
 
Tamko la serikali limetolewa na PM. Jumatatu madaktari waende kazini kama hawaendi wamejifukuza kazi. Kumbe kiongozi wao siyo mtumishi.wa serikali!

Uwezekano wa kutumia wanajeshi kama mwaka 2004 ni mkubwa!
 
huwezi kuunga mkono kwa kuwa nawe waweza kuwa ni moja ya tatizo, viongozi ni vyanzo vya haya yote kwani their are so selfish
 
Back
Top Bottom