Siungi Mkono hoja ya Zitto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siungi Mkono hoja ya Zitto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SINA JINA1, Apr 19, 2012.

 1. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fikra za mwanadamu zinapotawaliwa na hulka ya ushabiki zaidi ya ukweli ,maamuzi hutolewa pasipo kuzingatia ukweli.Pia maamuzi hayo huambatana na hoja nyepesi zisizo na manufaa katika utatuzi wa tatizo kuu.

  Serikali ya Jk tokea imeingia madarakani awamu ya kwanza imegubikwa na vitendo vya rushwa na Ufisadi uliokithiri kupita kiasi.Hii ni kutokana na ukweli kwamba Jk kama Raisi hakuwa na uwezo wa kuongoza nchi. Kongozi yeyote asiye na uwezo wa uongozi ni dhahiri hata team/wasaidizi wake watakuwa ni wabovu.Jk amejaza washkaji zake kwenye nafasi mbalimbali kama wasaidizi wake.Hili limejirudia hata pale bunge lilipomuazibu kwa kumwondoa waziri mkuu EL ili achague team bora bado yamejirudia yale yale.

  Kwa nini siungi mkono hoja ya Mh. Zitto?
  Sababu nilizotoa hapo kwenye maelezo ni kuwa tatizo kwenye uongozi wa nchi yetu sio mawaziri ama waziri mkuu bali ni mfumo mzima wa uongozi wa Jk.Hapa kilichotakiwa ni kutibu ugonjwa kama sio chanjo/kinga kwa kumwadabisha JK .Kwanini Zitto amekimbilia hoja ya kumwondoa Pinda ili hali kulikuwa na nafasi ya kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na Raisi?.

  Hapo ndio pale wachambuzi wanapochimba zaidi na kuangalia kwa undani juu ya tuhuma za uswahiba wa Zitto na JK.Hii hoja kwa mtazamo wangu ni kupoteza mantiki ya hoja ya msingi iliyotaka kupelekwa bungeni ya kutaka kumng'oa JK.

  Mungu Ibariki Tanzania dhidi ya huu uwizi wa dhahiri dhidi ya mali za walalahoi.
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Haya mkuu kwa hiyo kama mfumo ni mbovu tusubiri mfumo mpya uletwe na nani? Anyway katiba mpya na je tuwaache waendelee kula hadi mfumo mpya? THINK BIG MKUU!
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hujaeleweka Zitto ameomba Mawaziri wabadhirifu wajiuzulu wenyewe wakishindwa waziri Mkuu awawajibishe naye akishindwa awajibishwe yy ili liundwe jipya
   
 4. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kinachotakiwa ni mawaziri wahusika kujitoa. Wakigoma ndo watatolewa kwa njia ya kumtoa PM sababu PM akitoka, cabinet inavunjwa.
   
 5. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ameomba uungwaji mkono wa wabunge 70+ ili aweze wasilisha hoja yake ya kumchomoa Pinda
   
 6. d

  dundula JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 541
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapo hakuna cha uswahiba huyo janki anajua analolifanya kwani katiba ya sasa inampa rais madaraka makubwa mno,wabunge wa ccm hawako tayari wanahofia madaraka yao,hv rais akivunja bunge na akajiuzulu na uchaguzi ukaitishwa upya sasa hv wabunge wangapi wa ccm watarudi mjengoni?
   
 7. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe umesikiliza bunge au umesimuliwa? ok sikiliza marudio umwelewe mh Zito
   
 8. Kitoga

  Kitoga Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  yawezekana kutokea hayo kweli?bongo hii?
   
 9. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Zitto ameamua kuanza na jambo ambalo linawezekana kutekelezwa na ndo maana ameamua kudeal na waziri.ni vigumu sana kumwajibisha rais moja kwa moja kwani yeye pia anaweza kulivunja bunge kabla halijamng'oa yeye.mkuu hata unapofanya mtihani unashauriwa kuanza na maswali mepesi kwanza!
   
 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  tuna waziri mkuu dhaifu... yeye ndiye mwenye dhamana nambari wani serikalini.... kumbuka pia yeye ndiye mwakilishi wa serikali bungeni, na mshauri mkuu wa rais when it comes to baraza la mawaziri kuanzia uteuzi hadi utendaji na tathmini

  naunga mkono hoja ya ZITTO

  PS: nahisi unatumika vibaya mkuu
   
 11. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tusubiri tuone mazingaumbwe.
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Lakini mfumo huo huo mbovu unaweza kuwarudisha mawaziri hao hao wabovu!
   
 13. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na mimi hapo ndipo napopata wasiwasi kuwa Jk atatafuta maswahiba wakke wengine ambao ataweza kushirikianna nao katika kufanya ufisadi.Hapa ni kwamba watu wanataka kumsafisha JK ili hali imedhihirika hata mwanae anafanya uchafu kama wa hao mawaziri.Kwa minajili hiyo wote watakuwa wanashirikiana naye kama sio yeye anawatuma
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  pinda ndo msimamizi wa shuhuli za serikali bungenii watendaji wa chini yake wameshindwa kuwajibika ivyo basi ni halali yeye kuwajibishwa, thats all, unaishi nchi gani??
   
 15. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimechoka na resolutions zisizozaa matunda, ooh jairo, oooh mkulo, ooooh pinda. no action. ngoja niende jamii jokes nikajiliwaze mie.
   
 16. t

  thengoshahimself Member

  #16
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa mbna hzo sabni zpo chadema wabunge 48..cuf 35,nccr 4 plus kna filpkunjombe.,serukamba n zambi.mbna inawezekana.
   
 17. B

  Baba Jotham Member

  #17
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Zito kawatega ccm,wanajifanya wanapiga makelele so tuone kama watasain.kawaweza sana coz icje ikawa wanachonga ngenga tu
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Anaishi nchi ya Wagagagigikoko kwenye pepo ya Mabwege.
   
 19. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tuko bungeni wewe unatupeleka ikulu hazimo wewe.
   
 20. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,098
  Likes Received: 1,483
  Trophy Points: 280
  na mimi nakuunga mkono Rais wetu hana uwezo wa kuongoza,watendaji anaoteua ni dhaifu itakuwa ni kumwonea tu Pinda kwani kila ishu nzito ikitokea rais yupo nje ya nchi kumbukeni mgomo wa madaktari halafu baada ya hapo anakusanya mafisadi kina iddi simba eti anaongea na wazee wa Dar es salaam Tatizo ni mfumo mzima kwani rais hasomi magazeti ,hapewi taarifa na watu wa usalama tusizunguke tukimwachia rais mpaka muda wake uishe tutapata hasara kubwa ni heri aambiwe waziwazi aondoe hizo takataka alizotuwekea
   
Loading...