Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Ukiunganisha hizo semi za Sitta hapo kwenye red utagundua,Makonda hayupo peke yake,
Nyuma yake ipo nguvu kubwa kama iliyokuwa nyuma ya Nape wakati wa kampeni ya kuvua gamba,
Kinacholeta matumaini ni kuwa Kampeni ya nape iligonga mwamba na hii itagonga mwamba pia, maana msimamizi au mchochezi ni mmoja.Na hapa Warioba atashinda Damu ya Sengondo imetosha hatuhitaji kuona damu nyingine ya mjumbe wa tume ya katiba ikimwagwa juu ya ardhi ya Tz maana ni laana kwa nchi.
 
Mimi nilishasema huyu mzee warioba ataendelea kuadhirika Sana. Ile tume ilikuwa Na watu wengi Tu wenye akili Na busara zao wamekaa kimya huyu yeye anajifanya anajua Sana midahalo.ningekuwa Mimi ningekaa kimya ya nini kubishana kila siku kwenye vyombo vya habari hizi kazi angewaachia wanasiasa.
 
Kwa kauli hii, Samwel Sitta haoni tatizo na vurugu hizo; amezibariki kuwa ni halali. Nilitarajia kama mzee, wachilia mbali wadhifa wa uongozi alionao, kwanza alaani uvunjifu huo wa amani ambao pia unalenga kuwanyima Watanzania uhuru wa kukusanyika na kujadiliana kwa amani na uhuru mambo yanayowahusu. Huu ni upungufu mkubwa sana. Au tuseme laana ya kuwakejeli viongozi wa kiroho ndiyo imeanza kumtafuna. Sitta na wenzake wakae wakijua kuwa kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakitaraji Taasisi ya Mwalimu Nyerere iwafanyie kazi inayofanana na Mwalimu mwenyewe. Mchakato wa Katiba mpya umeonyesha kuwa Taasisi hii ikinyamaza, basi nayo itakuwa imeshiriki kuwadhulumu wananchi kama yule Mchungaji Niemoller wa Kijerumani wa Vita Kuu ya II.
 
Laiza hayo yote ni kuogopa nguve ya hoja. Mbona Prof wa Kichina amekuwa akizunguka na kuipigia debe katiba na hakuna aliyelalamika kwamba tuwaachie wananchi wachague. CCM mnaweza kufanya uhuni kama mlivyofanya jana lakini nakuhakikishia katiba yenu tutaichinjilia baharini na mtaaibika milele!
 
Huyo Sitta TOBA yake kwa kanisa katoliki inajadiliwa kesho kwa mujibu Askofu Ngalalekumtwa so aendelee tu kufunga na kuomba, ya mtoto makonda amwachie mwenyewe labda kama alihusika kumtuma!
 
Mzee 6 ameharibu sana sifa yake binafsi nilikuwa namshabikia hadi kuwa raisi kumbe ilikuwa tuje tuwe na raisi BOMU kabisa ktk historia ya Nchi hii! Hawezi kujilinganisha na Mzee Warioba hata chembe!
 
Huyu makonda sikuwahi kuwa na imani naye hata siku moja kwa sababu maisha yake binafsi, uwezo wake wa kusimamia familia yake na utendaji wake wa kazi niliufahamu miaka mingi tangu akiwa jeshini kusini.

Hana lolote ni msanii mpenda sifa na anasa tu!.

 
Kati ya hao ni wangapi walishawahi kuwa mawaziri wakuu? Kati ya hao wenye uwezo kuliko Mzee Warioba, ni wangapi walikuwa wenyeviti wa tume ile?

Wewe ni mpumbavu tena juha la kwanza.

Ungekuwa wewe ungekaa kimya kwa kuwa huna akli na ni marehemu badokuzikwa tu.

Kwa nini usinyamaze usubiri sanda na kupelekwa kaburini? Mbona unapiga kelele za kijinga hapa?

Pumbavu kweli kweli.

 
Tunamsubiri nae ajitokeze hadharani, ndio tutajua kati yake na Warioba nani anajitakia mwenyewe.

Tunashkru kama karuhusu na kushabikia vurugu.

Hapa ni kujibu mapigo tu hatuna namna.

...mia kwa mia,naye athubutu kukanyaga hizo anga ndo atajua kama kachumbari ni mboga. Wameanza tunamaliza,mpaka kieleweke...
 
Waziri wa Utangamano Afrika Mashariki anaruhusu fujo.......................

Kwa hali ya kawaida Waziri Sitta sio mtu wa kupanga vitu kama hivi.signature ya tukio sio yake.
 

...punguza kutumia masaburi unapotoa hoja mbele ya wanaume we bwanamdogo,nani mwanye sifa kama za warioba kwenye ile tume,ukianzia uzoefu wake na nyerere...
 
:A S 109:
Nadhani watanzania tunahaki ya kumsikiliza mtu tumatakaye.Haijafika zamu ya huyo Sitta,ni zamu ya Warioba ndiye tunayetaka kumsikiliza tupewe nafasi ya kumsikiliza,si Makonda wala Sitta atakaye weza kutunyima haki hiyo.Wamemaliza muda wao wakae benchi zamu ya WANANCHI wa TANZANIA kujua mbivu na mbichi.Haki yetu ya msingi ya kumsikiliza mtu tumtakaye.

Mbona hatufanyi fujo kwenye midahalo yenu ya kipumbavu?Kwa nini mtufanyie fujo tunaotaka kuelimika?Ni mpumbavu peke yake atakaye weza kumtetea huyu Makonda.
 
Kilichomkuta jana Warioba ni msiba wa kujitakia

........Wekeni ushabiki wenu wa kitoto katika matukio ya aina hiyo kisha mwisho wa siku mtakuja kujutia meneno yenu. Watu wanarekodi na huyo Makonda wenu mjue kuwa watu wapo nae mitaani, siku yakimkuta ya kumkuta ndipo mtaelewa kuwa si kila mtu ana entertain ujinga wenu.

Tuendelee kusubiria episode ijayo maana movie ndo mmeianzisha kwa style hiyo
 
sita anachotegemea ni ujinga wa watz na amewekeza kwenye hilo hivyo elimu inayotolewa na warioba inaweza mharibia mipango yake hivyo vurugu hizo ni njia ya kujihami, wananchi wasije elewa uhuni wa sita alioufanya kwenye katiba aliyopendekeza,kama ana uhakika na kazi aliyofanya aje aeleze zakia meghji alingia bmk kutokea bara alipigaje kura akiwa mjumbe wa znz? vipi kuhusu yule kiongozi wa nccr alipigaje kura wakati hakuwapo? sita kushabikia uhuni huu ni sawa, kwani ni mhuni pia.nirudi kwako mzee Warioba kazi unayofanya ni mhimu sana kwa taifa hili kwa sasa hivyo usipoifanya taifa hili lita pata hasara kubwa,usivunjwe moyo na kitendo cha jana,Tumtegemee MUNGU kutuvusha ktk kipindi hiki. sita aelewe amani ni zao la haki.
 
Kutakuwa na elimu ya ujraia kwa umma na kila kundi litashiriki kuitoa elimu hiyo na fedha zim eshatolewa na UNDP..sasa kinachofanyika ni kwa kina Warioba kukimbilia kuwadanganya wananchi kuwa rasimu imetupwa badala ya kutoa elimu ya uraia kupitia makundi husika...Taasisi ya mwalimu Nyerere sio kundi husika hivyo wao wangetulia au wangefanya midahalo yao bila kuwaalika akina Warioba.
 
Njaa zitakufanya wewe uingiliwe kwani unashabikia uvunjifu wa sheria...ungewashauri hao unaowateteta wapeleke hoja zao kwenye vikao vya bunge zijadiliwe na kumbukumbu ziwekwe na sio kumnunua warioba awasemee
Angalieni njaa zitafanya Sitta awaingilie.
 

Binafsi mimi sioni shida yeyote ile hasa ukizingatia kuwa ni ccm hao hao ambao wanadai kuwa wanasimamia misingi aliyoiacha Mwalimu Nyerere, kwa mfano suala la mfumo wa Muungano!
 
Hao viongozi wa dini nao wana laana ya kutoka kwa mungu, wanauza unga, wanatumika vibaya kwa wanasiasa wanaotajwa kutaka urais mwakani, wengine wanatumia vibaya misamaha ya kodi wanayopata, unatakuta hospital ya taaslsl ya dini ni ghali kuliko za watu binafsi hivyohivyo kwa shule haliyakuwa wanapata misamaha. Mwisho wanatafuna sadaka za waumini wao na kuishi maisha ya utajili na anasa wakati waumlnl wapo ktk lindi la umasikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…