Sitta: Wabunge wamedhalilishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Wabunge wamedhalilishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  * Asema wamehojiwa bila kufuata taratibu, kanuni
  * Shellukindo akiri kuhojiwa, ahusisha na Richmond
  * TAKUKURU: Tuko sahihi, hakuna aliye juu ya sheria


  Na Edmund Mihale
  Majira
  26 October 2009


  SAKATA la uchunguzi unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya wabunge kupokea posho mara mbili limechukuwa hatua mpya baada ya Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta kusema kitendo hicho kimewadhalilisha wabunge kwani taasisi hiyo haikufuata utaratibu.

  Kauli hiyo ya Bw. Sitta imekuja siku moja baada ya TAKUKURU kutoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi tuhuma za kuchukua posho katika taasisi mbalimbali wanazotembelea huku wakiwa wameshalipwa na Ofisi ya Bunge.

  Katika taarifa yake iliyokaririwa na vyombo vya habari jana, TAKUKURU ilisema Ofisi ya Bunge ndiyo iliomba ufanyike uchunguzi dhidi ya wabunge wanaoomba na kulipwa takrima serikalini na katika mashirika wanayotembelea katika ziara zao za kazi.


  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Bw. Sitta alisema hatua iliyofikiwa na TAKUKURU ni udhalilishaji na imekiuka utaratibu na kanuni na sheria za nchi dhidi ya bunge kama taasisi inayojitegemea.

  "Mimi sijui kama kuna jambo hilo kwani sijataarifiwa na kama limefanyika bila kunitaarifu, huu utakuwa ni udhalilishaji mkubwa katika ofisi yangu na wabunge pia," alisema Bw. Sitta.

  Alisema hata hivyo yeye kama spika hadi sasa hajui ni nini kinachohojiwa na taasisi hiyo kutokana na kutokuwa na taarifa yeyote katika ofisi yake bali anashangaa kuliona jambo hilo katika vyombo vya habari.

  Bw. Sitta alisema kimsingi ofisi ya TAKUKURU ilitakiwa kuandika barua katika ofisi yake juu ya tuhuma hizo za wabunge kuwa inahitaji kufanya uchunguzi huo na ilipaswa kuwataarifu wabunge juu ya suala hilo kuliko ilivyolichukuliwa na taasisi hiyo.


  "Natoa tahadhari kwa taasisi nyingine za uchunguzi kama TAKUKURU kuwa linapotokea jambo kama hilo ni lazima watoe taarifa kwa maandishi katika ofisi za bunge ili bunge liwe na taarifa ya bunge litoe utaratibu.

  "Wabunge wana kinga kama walivyo viongozi wengine wa serikali, ona kitendo kilichofanywa na Polisi Morogoro kwa kumdhalilisha mbunge kwa kumburuza katika pick-up kisa sh 7,000 za bili ya maji tena kilifanywa askari wa ngazi ya chini wasioelewa nini maana ya kinga ya mbunge kuwa ni moja ya udhalilishaji," alisema Bw. Sitta.

  Alisema kisheria mbunge anapaswa kukamatwa au kuhojiwa na mtu wa ngazi ya juu wa chombo chochote cha usalma kwa kufuata utaratibu, kanuni na sheria za nchi kwani mbunge hawazi kukimbia, na siyo askari wa ngazi za chini kama ilivyofanya TAKUKURU na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro.

  Lakini Msemaji wa TAKUKURU, Doreen Kapwani alipozungumza na Majira jana alisisitiza kauli ile ile ya juzi kuwa wabunge hawako juu ya sheria, na Katiba ya Nchi inasema hivyo, kwa hiyo walistahili kuhojiwa.

  "TAKUKURU inapenda kuujulisha umma kwamba wabunge kama ilivyo kwa mwananchi mwingine yeyote wanawajibika kisheria kuitikia wito katika ofisi za TAKUKURU iwe ni kwa kuhojiwa au kwa kutoa ushahidi kwani hakuna raia yeyote aliye juu ya sheria na Katiba ya Nchi iko wao wazi kwa hili," alisema.

  Wakati taarifa ya juzi ya TAKUKURU iliweka bayana kuwa Ofisi ya Bunge iliiomba rasmi taasisi hiyo ifuatilie nyendo za wabunge hao, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah alikana kufanya hivyo, badala yake akasema ofisi yake iliandikiwa barua na uongozi wa juu wa serikali ikimtaka kutoa ushirikiano.

  Bw. Kashililah alisema barua hiyo iliitaka ofisi yake itoe ushirikiano kwa taasisi hiyo pale inapobidi na hivyo aliandika kukubali ombi hilo lakini alitegemea kupata majibu ya utekelezaji wa uchunguzi huo lakini hadi leo hajui nini walichofanyiwa wabunge hao.

  Wakati taasisi hizo zikiumana, Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, Bw. William Shelukindo ambaye vyanzo vyetu ndani ya TAKUKURU vilidai kuwa amegoma kutoa ushirikiano katika uchunguzi huo, alizungumza na gazeti hili na kukiri kuhojiwa na taasisi hiyo kuhusu tuhuma hizo na kuwa alitoa ushirikiano wa kutosha.

  "Hawa watu wananitaka nini mie au kwa kuwa Mkurugenzi wao tunamkaanga wiki ijao ndiyo wanatufanyia visa hivi, nilipigiwa simu na mtu mmoja anaitwa Kigoni mwezi mmoja uliopita nikachoma mafuta yangu kutoka jimboni kwangu hadi Dar es Slaam nikahojiwa na nikatoa ushirikano wa kutosha sasa wanataka ushirikano upi.

  "Niliwaambia kuwa kweli nimechukuwa posho hiyo kama takrima na wala si kosa kwani ni taasisi tofauti kama ingekuwa ni ofisi moja hili lingekuwa ni kosa.

  "Hapa ninaona kuna kuna jambo linatafutwa hapa, kwanini hoja hii ije wakati huu tunapojadili jambo la Richmond ambapo bosi wao anahusika, naomba niwambie kuwa sitarudi nyuma katika hili, tunaingia bungeni na tutalijadili kwa kina jambo hilo hadi hapo tutakapopata ukweli wasitubabaishe," alisema Bw. Shelukindo.

  Alisema kitendo kilichofanywa na TAKUKURU kumhoji bila kutoa taarifa katika ofisi yake ni udhalilishaji mkubwa kwa Bunge.

  Alisema kuwa kama inafanya fitina hizo ili kumnusuru bosi wao wamechelewa kwani walitakiwa kufanya hivyo kabla hajatoa uamuzi kuutangazia umma kuwa hakukuwa na rushwa katika kuingia mkataba wa kampuni tata wa Richmond.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughukia Sera, Utaratibu na Bunge. Bw Philip Marmo alisema iwapo wabunge hao wanaona kuwa wamedhalilishwa wanapaswa kwenda katika vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake na sio kukimbilia katika vyombo vya habari.

  Kwa miezi mwili TAKUKURU imekuwa ikifanya uchunguzi na kuwahoji wabunge wa wanaotuhumiwa kuchukuwa posho mara mbili katika masharika ya umma wanapoyatembelea katika ziara mablimbalia za kikazi.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Hadi hii leo TAKUKURU haijathubutu hata mara moja kumhoji papa fisadi Rostam Aziz katika ufisadi wake chungu nzima alioufanyia nchi yetu pamoja mafisadi wengine akina Idrissa Rashid, Chenge, Mzindakaya na Mkono kwa kuhusika kwao na kuchota mabilioni ya shilingi pale BoT, lakini wamekuwa na speed ya ajabu kuwahoji Wabunge waliodaiwa kuchukua masurufu mara mbili. Hii inaonyesha wazi jinsi TAKUKURU walivyo na priorities zao kinyumenyume.
   
 3. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Hizi habari ndo huwa zinanichosha kabisaaaaa! Hi nchi bwana....
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hosea alishawambia wabunge siku mmoja kwenye kikao live, kuwa "wanamfuata fuata sana" nayeye atawachunguza wanavyochukua posho mbili mbili za serikali ofisi ya bunge na kwenye mashirika ya umma.

  Lakini hii kama alifikiri litamsaidia waogope kumsulubu bungeni , basi amechemcha, Hosea ameingia choo ya kike!!! Ajaribu kupima ufisadi unaoongelewa hapa ni wa Bilions of money, nayeye anaongelea viposho vya vikao havizidi laki 2!!! wapi na wapi!!!!!!!!!!!!
   
 5. GP

  GP JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kwani wabunge wana kinga yoyote kisheria??, au wao wako juu ya sheria??, huyu 6 vipi!.
   
 6. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Binafsi hili nilishawahi kuliongelea kipindi cha nyuma, kamati za bunge kila zinapotembelea taasisi kadhaa za serikali wabunge wanalipwa posho na ofisi za bunge na taasisi hizo pia. Mfano nimeshuhudia kamati ya bunge (jina kapuni) ikitembelea taasis kama nne kwa siku moja huku kila mbunge katika kila taasisi akilipwa kati ya sh. 250,000 mpaka sh. 400,000 bila kujarisha kwamba tayari wamesharipwa na ofisi ya Bunge.

  Waandishi wa tz tafuteni habari, msisubiri kuitwa kwenye vipress conference uchwara, au mnafuata hizo senti za nauli mnazopewa????
   
 7. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa wabunge wasitake kujiona wapo juu ya sheria, wamekuwa wakichukuwa posho hovyo hovyo kwenye mashirika ya umma. Hii ni kinyume cha sheria na lazima wahojiwe. Mbona 6 amekuwa mstari wa mbele sana kutetea kila jambo la kamati ya Nishati na madini? kuna agenda gani?
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  kuweni waangalifu na mwana ccm yeyote yule, hasa wanaojiita wapiganaji,

  6 kama kweli mpiganaji, hatakiwi kusema hivi.

  Kesho na mimi ni kifanya kosa bosi wangu atasema jambo, wanajeshi wakikosea, basi mkuu wao lazima haruhusu wachunguzwe,

  what if kama yeye naye ana tabia hiyo??
   
 9. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mawazo kama haya ya hiii rushwa kubwa hii ndogo ndo inatufikisha hapa tulipo! rushwa ni rushwa tuu!
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,091
  Trophy Points: 280
  Dr. Hosea lazima awajibike kwa udhaifu wa ofisi yake juu ya Richmond. Alichokifanya Hosea ktk Richmond ni uhujumu uchumi na uhaini kwa Taifa na kazi yake. Hesea sasa ameamua kutumia madaraka vibaya ili kujilinda dhidi ya uhalifu wake juu ya richmond!

  Ni kweli kwamba wabunge wanafanya vibaya kuendekeza double payment, lakini Hosea anakosea zaidi kufanya kazi kwa visasi. Kwanini ameshindwa kuwahoji mafisadi papa na manyangumi? PCCB imekuwa silaya ya kuwalinda mafisadi na kukamata wananchi wanaopigia kelele ufisadi. ovyo kabisa hosea.
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je hao TAKUKURU wanachunguza pia mashirika yanayotoa hizo posho ama wanafuatilia wabunge wanaopokea peke yao. Nina uhakika kama ni kosa kwa Mbunge kupewa hizo pesa, ni jambo rahisi tu kwa serikali kutaarifu mashirika yake yaache kuwapa posho hizo kwa kuwa ni kinyume cha sheria (kama kweli hivyo ndivyo).

  Visasi vya kisiasa hasa vinavyofanywa na watendaji waliokula kiapo kifanya kazi zao kwa usawa ni vitu vinavyoweza kuyumbisha amani ya nchi. Inabidi TAKUKURU kutumia uwezo wake kufanya mambo yake kwa kuzingatia kanuni na sheria za nchi. Wasiwe na subira pia kuwahoji watuhumiwa wengine wa rushwa, kwa kuwa tu ni wenzao.
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Son:

  Ukiondoa Idrisa Rashid, waliobaki ni wabunge pia nao wana immune. [​IMG]
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi nimeipenda hii vita maana ukweli sasa utapatikana kwa haraka maana kila mmoja ataonyesha msuli . CCM itawekwa pabaya na wananchi watakuwa LIVE Dodoma wanasikiliza wenyewe then mwakani hakuna longo longo .
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kila mtu ana kinga kisheria ya kutoshitakiwa na mtu yeyote ili mradi tu hajavunja hiyo sheria. Ukivunja sheria kinga hiyo inaondoka mara moja hata uwe rais wa nchi, Ndiyo maana tunataka Mkapa ashitakiwe.

  Kitendo cha kutumia sheria kwa visasi pia nayo ni kuvunja sheria, kwani hutakiwi kuwa prejudiced katika kutekeleza wajibu wako. Kitendo cha Hosea kutuma vijana kuwahoji wabunge kisha tu wanamwandama bungeni ni uvunjaji wa sheria "Power abuse", hivyo naye ni lazima ashughulikiwe kwa kuacha kutimiza wajibu wake mpaka pale anakapoona una manufaa kwake, yaani kulinyamazisha bunge, kufurahisha waliomteua (kwa kuwaacha mafisadi papa bila kuwagusa mradi tu walimuweka madarakani anayeshikilia dhamana ya uteuzi wake)
   
 15. l

  lukule2009 Senior Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini hoja ya msingi hapa ni je walichukua hizo posho mara mbili au? Na kamam walichukua je ni sahihi au walivunja sheria?na kama walivunja sheria inakuwaje wanashtakiwa au wanarudisha hizo posho?

  Kujadili jinsi walivyokamatwa na kuhojiwa kama ni kuvunjiwa heshima au la sio la msingi.Sita unapendisha attention kutoka kwenye hoja ya msingi.

  Spika sita binafsi sina imani sana na wewe.. na nahisi ulijiunga kwenye vuta hii kama njia ya kulipa kisasi kutokana na mambo mengine ya huko nyuma. nahisi mambo yako yakiwekwa sawa utageuka. Napata tabu nikikumbuka ulipomshushua Dr Slaa kuwa analeta mambo ya ovyo ovyo ya kwenye internet pale kashfa ya EPA ilipotajwa kwa mara ya kwanza.. hadi Dr akachomoa hoja yake kwani ulitishia kumpeleka polisi.. ulipogombanan na RA na EL ndio ukaanza kutumia nafasi yako kuwanyonga .. kabla ya hapo ..mmh.

  Pia Sitta napata taabu kukuamini nikisikia kwamba uliomba na umekubaliwa kununuliwa gari jipya la spika lenye thamani ya milioni mia mbili na zaidi .. ili hali watoto wetu wanakaa chini darasani kwa kweli napata tabu kujua dhamira yako...napata tabu pia kukuamini nikikumbuka siku ile wabunge wa kenya walipotutembelea.. nakumbuka uliwaambia wabunge .. jamani na sisi tuboreshe maswali yetu si manaona wenzetu wa huko... na pia umekuwa mstari wa mbele kudai mafao zaidi kwa wabunge mishahahara minono .. bila kujali wananchi wa kawaida..

  Ni kama vile unasema ... wao serikali wanakula na sie tule jamani .. lakini wananchi je ...... Unajisikiaje kutembelea gari la milioni mia mbila na hamsini katika nchi ya pili kwa umaskini duniani na wewe ndio spika wa bunge la nchi hiyo?

  Unajisikiaje mheshimiwa Sitta? Raha? Tena nasikia uliomba na wewe upewe gari jipya... Sitta napata tabu kukuamini .. naona maswali kwako ni muhimu na siku yakiwekwa sawa utageuka ... ushahidi wa internet unakumbuka hayo maneno....?
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wabunge wanapodhalilishwa kikwelikweli, kama juzi Ngeleja alivyowaita "rubber stamp parliament" basically, Sitta huwezi kumsikia.

  Wanapoona mkono wa sheria unataka kuwafikia, wanataka kupindisha kila rule in the book kuji protect, including hii ya kudai wanadhalilishwa.

  Hii protection imewekwa kwa wabunge wanaosema kweli wasiwe harassed na dola. Lakini kama wabunge wana abuse positions zao kwa kujiingiza katika rushwa ni poa tu, sio wabunge tu, hata rais naye aweze kuwa impeached na kuhojiwa na TAKUKURU yenye credibility ya kweli.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wachukua posho wana kesi ya kujibu na takukuru wana keshi ya kujibu kwa kuisafisha richmond kwa maji taka .
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wabanwe tu maana hawako juu ya sheria; wao wana makosa yao na hao TAKUKURU na kiongozi wao nao wana makosa yao.

  Hii tabia ya wabunge wakiandamwa kukimbilia kutafuta Wachawi haitawasaidia.

  Kama wanapambana na madudu ya TAKUKURU, ni sawa kwa vyombo vingine vya dola kupambana na madudu ya bunge.

  Watu wanaochukua posho mbili bila hata aibu, wana haki gani ya kusema wamefadhaishwa kwasababu tu wamehojiwa na vyombo vya sheria vya umma?
   
 19. Zalendohalisi

  Zalendohalisi Senior Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hivi kwenye ripoti ya kamati ya Mheshimiwa Shelukindo ambayo wao wenyewe waliiwakilisha bungeni August mwaka huu, mbona wao wenyewe wanmsafisha Dr Hoseah! Hebu soma hizi nukuu kutoka kwenye ripoei yenyewe iliyopo kwenye Hansard:

  Kama kamati yake huyu Mheshimiwa Shelukindo inaafiki kuwa kulikuwa hakuna rushwa halafu anasema atamkaanga Hosea Dodoma, lipi la ukweli?

  ZalendoHalisi
   
 20. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona 6 hazungumzii ubadhililifu wa milioni 70 uliofanywa na mfanyakazi mmoja ndani ya ofisi yake anazungumzia posho za wabunge kulipwa mara mbili?

  Aisafishe ofisi yake kwanza kwa tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa huko.
   
Loading...