Pongezi kwa TAKUKURU Mlele halmashaur ya Mpimbwe kwa Kusimamia Uwajibikaji na Kuruhusu Sheria Kufuata Mkondo Wake

Pongezi kwa TAKUKURU Mlele halmashaur ya Mpimbwe kwa Kusimamia Uwajibikaji na Kuruhusu Sheria Kufuata Mkondo Wake

A

Anonymous

Guest
Nawapongeza TAKUKURU Wilaya ya Mlele halmashaur ya Mpimbwe kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika kuchunguza tuhuma mbalimbali za ubadhirifu na matumizi mabaya ya rasilimali za umma katika Idara ya Afya.

Hatua zilizochukuliwa dhidi ya aliyekuwa DMO wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe na sasa ni DMO Halmashauri ya mji Nanyamba, Dkt. Mahmoud, zinaonesha kuwa hakuna aliye juu ya sheria na kwamba taasisi zetu zinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Watumishi wengi wamefurahi kuona kuwa angalau kwa kiwango fulani haki inaanza kutendeka na kwamba malalamiko na tuhuma zinazowasilishwa na wananchi au watumishi zinapewa uzito unaostahili.

Hongereni TAKUKURU kwa kusimamia misingi ya uwajibikaji, uwazi na utawala bora. Tunaendelea kuamini kuwa uchunguzi utaendelea kwa haki na ukweli wote utawekwa wazi kwa manufaa ya umma.
 
Back
Top Bottom