Sitta: Uganda, Kenya, Rwanda waizidi kete Tanzania!

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
na Shehe Semtawa

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema mkutano wa siri wa nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EA), uliofanyika nchini Uganda hauna uhusiano na Jumuiya hiyo.

Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni ulihudhuriwa na Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, Paul Kagame (Rwanda), pamoja na Uhuru Kenyetta (Kenya).

Mkutano huo ulifanyika bila Tanzania kushiriki ambapo ulijadili masuala ya Jumuia hiyo, kitendo kilichotafsiriwa na wachunguzi wa siasa kuwa huenda nchi hizo zinajiandaa kuanzisha shirikisho lao.

Katika kikao hicho kulifikiwa makubaliano ya mikataba ya usafirishaji wa mafuta kati ya Uganda na Kenya kuendeleza ujenzi wa bomba la mafuta la Bandari ya Lamu, na Uganda kuacha kutumia Dar es Salaam au Mombasa kwa madai kuwa ni njia ndefu na yenye gharama kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa viongozi hao, pia walikubaliana kuhamasishana jinsi ya upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kujenga reli kutoka Kenya kupitia Uganda na Rwanda, lengo ni kusafirisha bidhaa za nchi hizo.

Rais Museveni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwake akisema: “Hata kama wangekuwa wawili au watatu, bado wangezungumzia kuhusu masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo, Sitta alisema Watanzania hawana haja ya kujiuliza maswali kuhusu mkutano huo, kwa sababu haukuwa wa shirikisho, bali uliandaliwa kama kikao cha ujirani mwema kupitia nchi zao, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya nchi hizo.

“Tanzania hatutishiki, cha muhimu ni kupata taarifa kamili na sahihi, tutazichambua na kusonga mbele,” alisema Sitta.

Sitta alisema Tanzania ilikosekana kwenye mkutano huo kwa kuwa haikualikwa.

Aliongeza kwamba kutokana na viongozi hao kutowashirikisha viongozi wa nchi nyingine husika, kuna haja ya masuala hayo kujadiliwa upya kupitia sekretarieti wakati itakapokutana tena mjini Arusha.
Nchi ambazo zinaunda Jumuiya hiyo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, ambayo nayo haikuwepo kwenye mkutano huo uliofanyika hivi karibuni nchini Uganda.

source: Tanzania daima
 
So, kwanini mkutano huo ulikuwa siri?
Nafikiri kuna agenda ya siri kutokana na kikao cha mkutano huo!
 
Museveni na Kagame wamenuna baada ya Mr. Dhaifu kuwashauri wakae meza moja na wapinzani wao wa kisiasa ambao wako msituni.
Kenyatta alichofanya ni kutumia mwanya huo ili kufanya biashara na nchi hizo mbili ambazo zimeamua kuikimbia bandari ya Dsm ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha kutokubaliana na ushauri wa Mr. Dhaifu.
Na kwakuwa hao maraisi waliokutana hawana masihara kwwenye mambo serious hasa ya kuinua uchumi wa nchi zao haitakuwa ajabu kama kikao hicho kikawa mwanzo wa kuparaganyika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati maraisi wengine wanafikiria na kutekeleza mipango ya kuinua uchumi na kuboresha vipato vya wananchi sisi huku Mr. Dhaifu yuko busy kupanga mipango ya kuihujumu Chadema.
 
Huo ndio ukweli,Kagame na Mseveni lao ni Moja kwanza nasikia wote ni watusi,ugomvi wa JK na Kagame na Mseveni kesha ambukizwa, acha tuone kwa mwendo huu kama kweli jumuia ya Africa mashariki itasimama.
 
Hivi siku hizi kisiwa cha Migingo ni mali ya nchi gani? Maana kuna watu walitaka kuzichapa siku chache huko nyuma na leo wanamsengenya jirani yao.
 
Mbona kichwa cha habari ni tofauti na habari yenyewe, du? Tz daima bwana,
mimi si mwandishi lkn hata km mtoto wa class one atagundua, angeanza hata kuelezea huo mkutano na maudhui yake, then aje na majibu ya sita kuhusu huo mkutano, angalau heading ingeendeana kidogo.
Any way lkn kusudi la kagame na mseven ni km kumtenga jk kwani anawanyima riziki congo, madine hayana wenyewe yale kwani vita ikiendelea ni chance nzuri ya kuyachota, pia nadhan hata jk ndio anayanyemelea kwa kutumia mgongo wa aman kumbe ni zahabu iliyoko kule,
 
na Shehe Semtawa

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema mkutano wa siri wa nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EA), uliofanyika nchini Uganda hauna uhusiano na Jumuiya hiyo.

Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni ulihudhuriwa na Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, Paul Kagame (Rwanda), pamoja na Uhuru Kenyetta (Kenya).

Mkutano huo ulifanyika bila Tanzania kushiriki ambapo ulijadili masuala ya Jumuia hiyo, kitendo kilichotafsiriwa na wachunguzi wa siasa kuwa huenda nchi hizo zinajiandaa kuanzisha shirikisho lao.

Katika kikao hicho kulifikiwa makubaliano ya mikataba ya usafirishaji wa mafuta kati ya Uganda na Kenya kuendeleza ujenzi wa bomba la mafuta la Bandari ya Lamu, na Uganda kuacha kutumia Dar es Salaam au Mombasa kwa madai kuwa ni njia ndefu na yenye gharama kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa viongozi hao, pia walikubaliana kuhamasishana jinsi ya upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kujenga reli kutoka Kenya kupitia Uganda na Rwanda, lengo ni kusafirisha bidhaa za nchi hizo.

Rais Museveni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwake akisema: “Hata kama wangekuwa wawili au watatu, bado wangezungumzia kuhusu masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo, Sitta alisema Watanzania hawana haja ya kujiuliza maswali kuhusu mkutano huo, kwa sababu haukuwa wa shirikisho, bali uliandaliwa kama kikao cha ujirani mwema kupitia nchi zao, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya nchi hizo.

“Tanzania hatutishiki, cha muhimu ni kupata taarifa kamili na sahihi, tutazichambua na kusonga mbele,” alisema Sitta.

Sitta alisema Tanzania ilikosekana kwenye mkutano huo kwa kuwa haikualikwa.

Aliongeza kwamba kutokana na viongozi hao kutowashirikisha viongozi wa nchi nyingine husika, kuna haja ya masuala hayo kujadiliwa upya kupitia sekretarieti wakati itakapokutana tena mjini Arusha.
Nchi ambazo zinaunda Jumuiya hiyo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, ambayo nayo haikuwepo kwenye mkutano huo uliofanyika hivi karibuni nchini Uganda.

source: Tanzania daima
Serikali ya Ccm wanabaki kupambana na Chadema wakati wenzao wanafanya kazi za maendeleo
 
Tusipoteze muda kujadili watu na mipango yao ya maendeleo. Tujadili sisi na mipango yetu ya maendeleo. Tujadili mkikataba tuliyoingia na CHINA hivi karibuni tuone kwamba itatupeleka mbele ki maendeleo. Pia tuhakikishe ziara ya OBAMA/USA iwe ya kuleta maendeleo hapa kwetu. Narudia-tusipoteze muda na nguvu zetu kujadili jirani kala nini,tujadili fursa na maendeleo tutayopata kwa ushirikiano wetu na hawa worlds super power utatuendeleza vipi individualy na Taifa ki u jumla.
 
Rais Museveni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwake akisema: "Hata kama wangekuwa wawili au watatu, bado wangezungumzia kuhusu masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki".

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo, Sitta alisema Watanzania hawana haja ya kujiuliza maswali kuhusu mkutano huo, kwa sababu haukuwa wa shirikisho, bali uliandaliwa kama kikao cha ujirani mwema kupitia nchi zao, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya nchi hizo.

"Tanzania hatutishiki, cha muhimu ni kupata taarifa kamili na sahihi, tutazichambua na kusonga mbele," alisema Sitta.

Sitta alisema Tanzania ilikosekana kwenye mkutano huo kwa kuwa haikualikwa.

Aliongeza kwamba kutokana na viongozi hao kutowashirikisha viongozi wa nchi nyingine husika, kuna haja ya masuala hayo kujadiliwa upya kupitia sekretarieti wakati itakapokutana tena mjini Arusha.
Nchi ambazo zinaunda Jumuiya hiyo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, ambayo nayo haikuwepo kwenye mkutano huo uliofanyika hivi karibuni nchini Uganda.

source: Tanzania daima

kwenye red hapo juu kuna umuhimu mkubwa sana.
 
Museveni na Kagame wamenuna baada ya Mr. Dhaifu kuwashauri wakae meza moja na wapinzani wao wa kisiasa ambao wako msituni.
Kenyatta alichofanya ni kutumia mwanya huo ili kufanya biashara na nchi hizo mbili ambazo zimeamua kuikimbia bandari ya Dsm ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha kutokubaliana na ushauri wa Mr. Dhaifu.
Na kwakuwa hao maraisi waliokutana hawana masihara kwwenye mambo serious hasa ya kuinua uchumi wa nchi zao haitakuwa ajabu kama kikao hicho kikawa mwanzo wa kuparaganyika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati maraisi wengine wanafikiria na kutekeleza mipango ya kuinua uchumi na kuboresha vipato vya wananchi sisi huku Mr. Dhaifu yuko busy kupanga mipango ya kuihujumu Chadema.
Kama Tanzania ingekuwa na kiongozi imara na mwenye ubunifu wa kutosha wa namna nzuri ya kulinda na kuitumia rasilimali ya ndani kujenga uchumi imara, wala nisingebabaika kabisa na hiyo jumuia ya Africa mashariki. Maana tungeweza kufanya biashara na mataifa ya ulaya na si kuitegemea Kenya, Rwanda na Uganda, lakini with Mr. Dhaifu, napata shaka sana kama tunaweza kufanya lolote. Huyu dhaifu ni kama kawatia udhaifu na mawaziri wake wote. Maana hakuna aliye strong wa kuweza kusimama imara na kufanya kazi zake kwa weledi. Kila mmoja anawaza kuiba tu.
 
na Shehe Semtawa

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema mkutano wa siri wa nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Maishariki (EA), uliofanyika nchini Uganda hauna uhusiano na Jumuiya hiyo.i

Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni ulihudhuriwa na Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, Paul Kagame (Rwanda), pamoja na Uhuru Kenyetta (Kenya).

Mkutano huo ulifanyika bila Tanzania kushiriki ambapo ulijadili masuala ya Jumuia hiyo, kitendo kilichotafsiriwa na wachunguzi wa siasa kuwa huenda nchi hizo zinajiandaa kuanzisha shirikisho lao.

Katika kikao hicho kulifikiwa makubaliano ya mikataba ya usafirishaji wa mafuta kati ya Uganda na Kenya kuendeleza ujenzi wa bomba la mafuta la Bandari ya Lamu, na Uganda kuacha kutumia Dar es Salaam au Mombasa kwa madai kuwa ni njia ndefu na yenye gharama kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa viongozi hao, pia walikubaliana kuhamasishana jinsi ya upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kujenga reli kutoka Kenya kupitia Uganda na Rwanda, lengo ni kusafirisha bidhaa za nchi hizo.

Rais Museveni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwake akisema: “Hata kama wangekuwa wawili au watatu, bado wangezungumzia kuhusu masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo, Sitta alisema Watanzania hawana haja ya kujiuliza maswali kuhusu mkutano huo, kwa sababu haukuwa wa shirikisho, bali uliandaliwa kama kikao cha ujirani mwema kupitia nchi zao, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya nchi hizo.

“Tanzania hatutishiki, cha muhimu ni kupata taarifa kamili na sahihi, tutazichambua na kusonga mbele,” alisema Sitta.

Sitta alisema Tanzania ilikosekana kwenye mkutano huo kwa kuwa haikualikwa.

Aliongeza kwamba kutokana na viongozi hao kutowashirikisha viongozi wa nchi nyingine husika, kuna haja ya masuala hayo kujadiliwa upya kupitia sekretarieti wakati itakapokutana tena mjini Arusha.
Nchi ambazo zinaunda Jumuiya hiyo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, ambayo nayo haikuwepo kwenye mkutano huo uliofanyika hivi karibuni nchini Uganda.

source: Tanzania daima

Jamani watanzania tusiwe na hofu na hawa jamaa kwanza mkutano haukuwa wa siri na ndiyo maana kilichojalidiwa sote tumekifahamu. Huu ulikuwa mkutano wa ujirani mwema sio jumuia ya EA hata sisi huwa tunafanya na nchi kama Msumbiji na majirani wengine.

Tanzania tuna rasilimali za kutosha kama mafuta, gas, uranium,bahari nk tujipange vizuri hawa Rwanda na waganda watarudi tu wenyewe na isitoshe jiografia yetu inaturuhusu kushirikiana na nchi za SADCC kama hawa jamaa wakituzingua
 
Sasa Rais wenu kila kukicha kiguu na njia watampata wapi, hata mume kama ana kawaida ya kuchelewa kurudi mama huwa akiivisha anapakua hakuna kusubiri mtembezi.
 
Museveni na Kagame wamenuna baada ya Mr. Dhaifu kuwashauri wakae meza moja na wapinzani wao wa kisiasa ambao wako msituni.
Kenyatta alichofanya ni kutumia mwanya huo ili kufanya biashara na nchi hizo mbili ambazo zimeamua kuikimbia bandari ya Dsm ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha kutokubaliana na ushauri wa Mr. Dhaifu.
Na kwakuwa hao maraisi waliokutana hawana masihara kwwenye mambo serious hasa ya kuinua uchumi wa nchi zao haitakuwa ajabu kama kikao hicho kikawa mwanzo wa kuparaganyika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati maraisi wengine wanafikiria na kutekeleza mipango ya kuinua uchumi na kuboresha vipato vya wananchi sisi huku Mr. Dhaifu yuko busy kupanga mipango ya kuihujumu Chadema.
...kama ni hivyo basi tuna hasara ya muda tu..akitoka madarakani, mr dhaifu, biashara mwendo mdundo, au akiingia mwengine madarakani ktk rwanda na uganda...lkn ni iwapo ni iwapo tu, matumizi yao ya bandari yetu ya dar yalikuwa na manufaa zaidi kiuchumi na si " kumfurahisha so called, mr dhaifu"
 
Kama waganga na wanyaruanda wamekimbia kutumia bandari ya Dsm ni kwa maufaa yao,ukiritimba umezidi bandari ya Dsm,sio zamani sana wakongo nao walilamika kuhusu urasimu wa bandari ya Dsm,wazambia wanahiari watumie bandari ya Angola kuepuka uarasimu wa bandari ya Dsm,hivi lini Tanzania itasoma kuheshimu wateja wake,hivi lini tanzania itaachana na kejeli za sisi hatubabaiki!!!

Walichoyfanya wanyaruanda na waganda ni kwa maslahi ya nchi yao hilo sio kosa,na sisi watanzania tusome kuwaheshimu wateja wetu wanaotumia bandari ya dsm kwa kuwapa "services" nzuri
 
Tusipoteze muda kujadili watu na mipango yao ya maendeleo. Tujadili sisi na mipango yetu ya maendeleo. Tujadili mkikataba tuliyoingia na CHINA hivi karibuni tuone kwamba itatupeleka mbele ki maendeleo. Pia tuhakikishe ziara ya OBAMA/USA iwe ya kuleta maendeleo hapa kwetu. Narudia-tusipoteze muda na nguvu zetu kujadili jirani kala nini,tujadili fursa na maendeleo tutayopata kwa ushirikiano wetu na hawa worlds super power utatuendeleza vipi individualy na Taifa ki u jumla.

ushirikiano na super power yes, lakini siamini kuwa ni mbadala wa ushirikiano na majirani(nchi za EAC). Pia siamini kuwa waliyojadili hayatuhusu kwani yanaathiri nafasi yetu kwa mfano ya kufanya biashara kupitia na nchi landlocked kama Rwanda na Uganda kupitia bandari ya Dar kama wataimarisha mahusiano kutumia bandari ya Mombasa. Nimesikia pia wameongelea kuhusu kuondoa vizuizi barabarani- jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana kwa upande weut kuwa inafanya biashara zetu na za wale wanaotegemea barabara zetu kuwa less competitive.
 
Serikali ya Ccm wanabaki kupambana na Chadema wakati wenzao wanafanya kazi za maendeleo

Wanalilia ardhi ya watanzania, kwamba wananchi wao wawehuru kuja tz kujenga na kumiliki ardhi
 
tusipoteze muda kujadili watu na mipango yao ya maendeleo. Tujadili sisi na mipango yetu ya maendeleo. Tujadili mkikataba tuliyoingia na china hivi karibuni tuone kwamba itatupeleka mbele ki maendeleo. Pia tuhakikishe ziara ya obama/usa iwe ya kuleta maendeleo hapa kwetu. Narudia-tusipoteze muda na nguvu zetu kujadili jirani kala nini,tujadili fursa na maendeleo tutayopata kwa ushirikiano wetu na hawa worlds super power utatuendeleza vipi individualy na taifa ki u jumla.

well said mkuu take 5
 
Back
Top Bottom