Habari wana JF,
Mimi naona CHADEMA bado ina safu inayojitosheleza kuongoza nchi ikiongozwa na Dr Slaa, ofcoz japokuwa chama hakijachagua mgombea kwa mwaka 2015. Sioni kwa nini mtoa hoja umeona kuna pengo linalomwitaji Mzee Sita. Sijafikiria kama kuna mtu Tanzania mwenye uwezo wa kuongoza hii nchi zaidi ya Dr Slaa kwa sasa. Sita, Magufuli, sumaye, Ahmed salimu, Mwakyembe, Sinde, Mwandosya, na wengine kama wakitaka kuhamia CHADEMa wahamie lakini si kwa lengo la kugombea nafasi ya Uraisi 2015. Watahitaji kufanya kazi ya ziada kwa kuwa tayari CHADEMA kuna candidate wa nguvu na wala hatuchanganywi na propaganda za kuanza kuonyesha kwamba et CHADEMA hakina competent candidate wa kuongoza nchi hadi kianze kumezea mate makada wa CCM.
Nimeona hoja za udini zinatumiwa na watu waliokata tamaa ili kuwagawa wa Tz. Ni jambo la ajabu sana kuona mtu anapokosa hoja anakimbilia katika uchochoro wa udini. Acheni mambo hayo. Tanzania hakuna udini. Hatutachagua kiongozi kwa misingi ya kidini bali tutachagua viongozi kwa misingi ya uwezo wao kutuongoza. Dini ndiyo zichague viongozi wake kwa misingi ya dini huko huko katika mambo yahusuyo dini na wala msituletee habari hizo za dini zenu katika masuala ya uendeshaji wa Serikali.
Itakuwa ni jambo la kujidhalilisha ikiwa eti na sisi wengine tutahamishwa kwenye hoja za misingi na watu wasio na uelewa wa kina wanaoshindwa kuchanganua hoja na kuamua kuchochora kwenda usawa wa udini. NAOMBA WANA JF AMBAO WENGI WANAELEWA, TUWE TUNADHARAU NA KUTOKUYUMBISHWA TUNAACHA MAMBO YA MSINGI, TUNAANZA KWENDA UCHOCHORONI KUJADILI udini, hoja ambazo zinachomekewa kutoka kusikojulikana kwa lengo la kuhamisha mijadala.
HAKUNA UDINI TANZANIA. ANAYEKOSEA ATADHIBITIWA NA ANAYEFANYA VEMA ATAPEPELEWA BILAKUJALI DINI ZAO.