Kweli nimeamini Siasa ni Upepo kama wenyewe wanavosemaga "UPEPO wa KISIASA" hasa za CCM Chama Tawala!
Mwanzoni mapacha 3 wa kujivua Gamba Mahiri na kuonekena nguzo ya chama,sasa hivi ni Mzigo kwa Chama tena ni chanzo cha Chama Kupoteza Mvuto!
Sasa Upepo Uhamia kwa Mapacha watatu CCJ(Laukama wanaikataa CCJ,Mh.Mpendazoe Amewataja na kusema alikuwa Nao).
Watu kuamua Kujenga Chama Chao ndio Siasa,Angalizo kwa Chama Husika ni Kuangalia na Historia ya watu wanao watumia kwa Ujenzi na Umahiri wao wa Kujenga Hoja na Uvumilivu wao katika mapito mbalimbali!Hasa katika Kipindi ambacho chama kimepoteza Mvuto na Kutikisika!
Mathalan,Kule Mbeya Pacha 1 alisema tatizo la Umeme si Uhaba wa Maji ni Mikataba Mibovu ya Umeme!Hapa najiuliza mikataba mibovu ya Umeme mingapi ni ipi zaidi ya Ule wa Dowani na IPTL!Na hata Ukiangalia mikataba yenyewe ilikuwa ya umeme wa Dharura tu na si wa Kudumu,kimsingi mikataba haikuwa ya kutatua tatizo la Umeme bali kukabiliana na Dharura kwani umeme wake haukuwa si kutosheleza hitaji la Taifa!Nilichotegemea Kusikia nini kilifanyaka toka mikataba mibovu imeingiwa katika kumaliza tatizo la Umeme.Kadhalika kuwaeleza wananchi chanzo mbadala zaidi ya kutegemea Maji kuwa Chanzo namba moja cha Umeme wa Taifa,waweke wazi ni vyanzo vingapi vipya vya Umeme wa Kudumu vimeshapatikana na vitaanza kumwaga Umeme lini!
Pili,Historia ya Kujivua gamba iliyotolewa itasaidia nini wananchi,wananchi tunataka majawabu ya matatizo yetu ya sasa na yaliyotuzingira kama Kupanda kwa Gharama ya maisha ya kila siku na Mustakabali wa Elimu Bora kwa Wanetu,Afya zetu sisi wote hasa sie wavijijini,Hatiima ya Kilimo Kwanza,Namna ya Kuwekeza na sehemu za kupata mitaji na Masoko kuuzia mazao yetu na kupata senti walau za Kujikimu wa Familia Zetu!
Tatu,Serikali imejipanga vipi Kuwahudumia wazee wote nchi hii na Makundi ya wasiojiweza ili wakati Serikali inahudumia wazee na makundi ya wasio Jiweza Sie wananchi wengine tunachapa kazi ili kukuza Uchumi wa Taifa utaoliwezesha kujimudu na kuhudumia watu wake sambamba na namna ya Kulinda Rasilimali zetu zilizobaki na kuonesha mchango wa Rasilimali zetu zinazotumika sasa kwa maendeleo ya Taifa
Nne,wengine wanaanza kuwaambia haditi ya Maamuzi Magumu,mara yanatakiwa Maamuzi Makini,Malumbano ya Nini,kwani hamjui katika chama chenu malumbano ndio yaliyo wagharimu!Siku hizi siasa za Malumbano haziuzi Chama!(Waungwana Hulumbana ndani ya Nyumba na Si Hadharani)
Kwahiyo Mambo ya Histori tuwekewe kwenye TV na vombo vya Habari na tuelezewe zaidi Siku ya Sherehe ya Jubilee ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika(Siyo Tz)!
Jamani Ndg Mapacha 3 wa CCJ nawapongeza kwa kuaminiwa!
Lakini wenzenu tunataka "MAISHA BORA YAYOONEKANE KATIKA MAZINGIRA YETU"
Leo Mkweche kawa "politiko konsaltanti"