Sitta amwaga radhi TBC1

he!

huyu mchungaji wasapila mbona amevaa shati la ccm?

source: ITV


Anatekeleza sera ya CCM ya kasi zaidi kwenye matibabu. Matokeo yake mpaka sasa suala la Dowans limekwisha habari yake. Haliandikwi tena kwenye magazeti.
 
Sitta ana haki ya kutoa tamko kama hilo,kwanza hawa makada wa kweli ndugu sitta,ndg sumaye na wengineo wenye nia nzuri na watanzania.wana historia ndefu ndani ya chama kuliko makuwadi wa maslahi ndani ya chama wanaochipukia kama uyoga.
MUNGU AKUTANGULIE MZEE SITTA WALA USISITE KAMWE KUTETEA HAKI YA WALIO WENGI.

Wana nia nzuri ya kuinusuru CCM wala hawajaLi chochote kuhusu WATANZANIA. Sumaye na Sitta wamefanya ufisadi na kuchuma kupitia CCM.
 
Huyu jamaa ni kama vile mpinzani, nadhani JK alikosea kumpa uwaziri maana saizi amejenga ufa mkubwa sana ndani ya chama kutokana na tabia yake na tabia imeambukiza wengine hivyo kuongeza hali tete kwa CCM, wakati huo CDM wakikenua meno.

Mkuu vp umekunywa maji ya bendera ya kijani nini?
 
Kwa nilivyomuona kwenye sura yake jamaa yuko ready to get it on! aliwauliza huu mwaka gani..wakajibu 2011..akawaambia basi sasa ni 2011, 2012 ndo watakuwa mwisho wao. let watch this out!
 
Mimi navyoona mheshimiwa six kwa mujibu, kama chama makini kwa hayo aliyoongea ingekuwa ccm hapatoshi,
 
CCM ilizaliwa, ikakua ikafikia 'optimal point' sasa inashuka tena kwa kasi mpaka ife, hakuna wa kuizuia isiporomoke.Chochote chenye uhai huzaliwa hukuwa hatimaye hufa. Sasa hivi ipo kwenye hatua za kufa. Last destinastion ni kifo chake.
 
Hii masinema huwa hamayachoki waungwana!!
Uungwana ni vitendo.

Nilipita tu mara moja...
 
Sitta ana haki ya kutoa tamko kama hilo,kwanza hawa makada wa kweli ndugu sitta,ndg sumaye na wengineo wenye nia nzuri na watanzania.wana historia ndefu ndani ya chama kuliko makuwadi wa maslahi ndani ya chama wanaochipukia kama uyoga.
MUNGU AKUTANGULIE MZEE SITTA WALA USISITE KAMWE KUTETEA HAKI YA WALIO WENGI.
Ndg commonmwananchi huyo SUMAYE uliyemtaja hapo mtoe tu hayupo kwenye list ya kupinga ufisadi.
Kwa taarifa yako UVWCCM wametekwa na mafisadi, unategemea nini ikiwa mkutano wao unakuwa funded na RA pamoja na yule jamaa wa rada Somaiya.
Kwa watu wenye uchungu na nchi hii hawa wote wanatakiwa kuwa jela ili wajibu mashitaka ya kutufilisi. Mwambie Bashe apeleke taarifa za JF. SALAAM.
 
Jamani kama sitta anawajua hao waujumu uchumi, kwanini tusimuunge mkono na kumuomba ushaidi wa jinsi hao watu wanavyoujumu uchumi ili kwa pamoja(wazalendo) takawashitaki hawa watu, lakini kama tunasubiri eti hadi uchaguzi huku tunaendelea kuibiwa me nazani ni uvivu wa kuchukua hatua wakati muafaka, jamani uchaguzi ni kwaajili ya kawaondoa viongozi wasiowajibika lakini kwa hawa wanaovunja sheria wanaitaji kushitakiwa.
Ndg yangu katiba yetu haina nguvu za kushitaki mafisadi, kwani EPA mafisadi si walijulikana mkuu wa nchi Raisi akawasamehe, nchi gani duniani inasamehe wezi eti warudishe walicho iba tena si chote wenyewe wakadilie!!!.
Ripoti ya DOWANS NA RICHIMOND tume ya Dr Mwakyembe si ilikuwa inatosha kupeleka watu jela hata kwa uzembe kusababishia serikali hasara ya mabilion.Lakini haikuwa hivyo, watu wanapeta tena wanapanga eti kugombea urais.
Tunapo jadili tusisahau kuwa katiba mpya ndiye mkombozi wa Tanzania, toka mikono ya wezi mfisadi!!!!!!!!!!!
 
Kwa kweli sita nakupomgeza pambana na mafisani mpka mwisho ukifaka 2015 unahamia chadema
 
Safi msana Mzee Sita tuko nyuma yako kuwatokomeza mazandiki hawa mwaka huu 2011, hata dawa ya babu wa loliondo haiwatibu mafisadi hivyo ni wa kuangamia tuu mwaka huu.
 
Mbona mzee MENGI aliwataja na maovu yao lakini wananchi hawakuchukua hatua yoyote?nadhani hata maandamano ya kuunga mkono kauli yake walau ingetosha!matokeo yake mengi kapelekwa mahakamani hakuna wa kumsaidia

ivi ulitegemea mtu anayechangia kampeni za ccm awaponde mafisadi? Kesi imeishia wapi? Mbona yeye kawa kimya. Acha kujidanganya. Kama unakumbuka vizuri ilifuata ishu ya uanachama wa Mengi. Mara ishu yote ikazimishwa ghafla, kama vile mtu kapuliza mshumaa. Wewe unadhani hawa ni wajinga wang'ate mikono inayowalisha?
 
CCM ilikufa na Nyerere; iliuwawa na Mkapa. Matatizo yanayoikumba sasa hivi wakati wa Kikwete ni matokeo hayo ya kufa zamani sasa inaanza kunuke. Watu wanoamlaumu Kikwete kwa kuiua CCM wanamuoenea tu kwani alibebeshwa marehemu CCM tangu awali. Kama CCM ingekuwa iko hai wakati wa Mkapa, basi Kikwete asingekuwa rais mwaka 2005.

Mkapa aliiuaje ccm? kwa nini usiseme kuwa nyerere ndio aliua ccm kwa kuwachagulia mwenyekiti out of nowhere mwaka 1995? ccm sasa ivi imebaki na watu wanaojiona kuwa level moja. Wewe unadhani kikwete anaweza kumwambia sitta kitu? and vice versa? hawaheshimiani na kila mmoja anataka kuiba. Hilo ndilo tatizo la wezi kukaa pamoja.
 
CCM ilikufa na Nyerere; iliuwawa na Mkapa. Matatizo yanayoikumba sasa hivi wakati wa Kikwete ni matokeo hayo ya kufa zamani sasa inaanza kunuke. Watu wanoamlaumu Kikwete kwa kuiua CCM wanamuoenea tu kwani alibebeshwa marehemu CCM tangu awali. Kama CCM ingekuwa iko hai wakati wa Mkapa, basi Kikwete asingekuwa rais mwaka 2005.

Mkuu uko sawa kabisa.
 
Well well well,............patakuwa hapakaliki hapa.......Mh Sitta Watch out!.................tik tak tik tak tik tak

...Saa yako ni mbovu?? It should be...tik tok tik tok tik tok...!

 
Hivi ili jeshi letu la polisi liko vipi?

Mengi alitoa ushahidi mpaka majina ya mapolisi, lakini cha ajabu mpaka sasa mimi binafsi sijasikia hata mtu mmoja kupelekwa mahakamani.

Kama kuna mtu anajua chochote atujuze maana inatia shaka uwajibikaji wa jeshi la polisi.

Au jeshi nalo linamilikiwa na wachache?? maana hii nchi kama inawenyewe vile.

Tujuzane wakuu..
 
Kwa kuwa hatua ya awali ya kuoteshwa juu ya dawa ya kutibu magonjwa sugu...
Sasa kinachofuata ni hatua ya pili.... hii itausisha na ndoto ya babu ya rais ajeye, ambaye atatokea maeneo ya umasaini... nywele yeupe kama theruji... huvaa miwani ( kwa hatua hiyo yeye atakuwa anajifanya hamjui mtu mwenyewe ... ila atawaachia wapiga kura wenyewe wamjue na wengi wao watakaompigia muhusika ni wale ambao wameamini na kunywa dawa )

Nawasilisha

Subirini
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom