Sitta amwaga radhi TBC1

Sitta ana haki ya kutoa tamko kama hilo,kwanza hawa makada wa kweli ndugu sitta,ndg sumaye na wengineo wenye nia nzuri na watanzania.wana historia ndefu ndani ya chama kuliko makuwadi wa maslahi ndani ya chama wanaochipukia kama uyoga.
MUNGU AKUTANGULIE MZEE SITTA WALA USISITE KAMWE KUTETEA HAKI YA WALIO WENGI.
 
sitta mali yote aliyo nayo kaitoa wapi.

nyumba ya spika milioni 10 kwa mwezi huyo anajua umaskini wa watanzania. tunadanganyana bure.
 
Huyu jamaa ni kama vile mpinzani, nadhani JK alikosea kumpa uwaziri maana saizi amejenga ufa mkubwa sana ndani ya chama kutokana na tabia yake na tabia imeambukiza wengine hivyo kuongeza hali tete kwa CCM, wakati huo CDM wakikenua meno.
 
kama CCM watampuuza SITTA, navyoona chama kitazidi kumeguka tu!!
Kimeshameguka na hakuna wa kuweka mambo sawa pale ila kwa afrika ndio chama cha tokea uhuru kilichosalia hivyo wakati wake umefikia ukomo.sina hakika ila kuna chama chenye uhai madarakani miaka 50 afrika nzima kweli? They are in decline stage only renewal strategies culd help them but its too late!
 
avatar yako inatia kichefuchefu

avatar9537_7.gif
 
sitta mali yote aliyo nayo kaitoa wapi.

nyumba ya spika milioni 10 kwa mwezi huyo anajua umaskini wa watanzania. tunadanganyana bure.
Kwasasa tunachotaka ni ccm kuwatoa madarakani kwa namna yeyote hivyo lengo litimie hata kama wachezaji wengine hatuwapendi,system kuwa mpya tu na watz kuzoea mabadiliko itakuwa hatua kubwa,acha wachapane tu!
 
nadhani sitta ni mzalendo ila yupo in a wrong party. ccm hawawapendi watu wakweli. anafaa aje chadema tupambane na ccm

Mwache abaki huko achonge mpaka waparaganyike,kwakweli CCM safari yao iko ukingoni!!!
 
Kwa heshima zote namuomba Ndg. Sitta atoke ktk chama cha Mapinduzu.
Ajipange upya na kujiunga na wapiganaji wengine.
Asisubiri saana, tuunganishe nguvu. Achague chama kingine ajiunge nacho, ni wazi ccm sio riziki kwake! Sikio la kufa halisikii dawa!!
 
,ndg sumaye na wengineo wenye nia nzuri na watanzania.wana historia ndefu ndani ya chama kuliko makuwadi wa maslahi ndani ya chama wanaochipukia kama uyoga.
.

Commonmwananchi are serious?
Historia ndefu na CCM sawa lakini "nia nzuri na watanzania?
Sumaye?
Think again?
 
Huyu jamaa ni kama vile mpinzani, nadhani JK alikosea kumpa uwaziri maana saizi amejenga ufa mkubwa sana ndani ya chama kutokana na tabia yake na tabia imeambukiza wengine hivyo kuongeza hali tete kwa CCM, wakati huo CDM wakikenua meno.

kila mtu ana uhuru wa kuongea, kuwa ccm haimanishi USIONGEE kwani NYERERE alikua haongei? au anayoongea sitta yanauma zaidi? kubali tu kaka kwamba ccm ya sasa imebadili sura, acha kuitesa nafsi yako kwa kujilazimisha kukataa ukweli.
 
Mwambieni Sitta, hakiwezi kibaya kutokana na kibovu jamani. Kama Sitta anataka kweli kupambana na mafisadi aondoke kwenye jiko linalowapika hao mafisadi-ccm. Yeye ni sehemu ya huo mfumo unaowazalisha hao mafisadi, atawezaje kukwepa kuwa sehemu yake? Je, aweza mtu kusukuma gari akiwa ndani ya gari husika? Mwambieni Sitta aache mchezo huo, kama anataka kuwaambia wenye akili kitu kinachoingia kichwani atangaze kujitoa ccm, aingie cdm, aombe kugombea kiti cha urambo akiwa ndani ya jezi ya cdm arudi bungeni akiwa mpinzani wa kweli. Vinginezo kelele zote ni ama danganya toto ya kutafuta kiti 2015 kwa ticketi ya kijani au hajafumbuka macho kujua kuwa chama chake ni organization ilikwisha kufa, na isiyoweza kufufuka hata siku ya kiyama.
Wana JF fuatilieni taarifa ya habari.

---------

Amesema ataendelea kupambana na ufisadi pamoja na nchi kuwa na rasilimali za kutosha wananchi bado ni masikini- inakuaje watu 43mil wanatikiswa na watu hawazidi 10 HAPA TANZANIA ANASEMA MWAKA 2011 ndiyo mwisho wao! Amewataka wananchi wasikubali
 
kila mtu ana uhuru wa kuongea, kuwa ccm haimanishi USIONGEE kwani NYERERE alikua haongei? au anayoongea sitta yanauma zaidi? kubali tu kaka kwamba ccm ya sasa imebadili sura, acha kuitesa nafsi yako kwa kujilazimisha kukataa ukweli.
Mbona nyerere aliwasema wazi tu mpaka akatamka ccm si mama yangu lakini si uvccm wala yeyote aliyejibu! Kulikoni leo hawa makinda kuongea ovyo tena kujibu makada wa levo za sumaye kwa matamko ya kijinga?
 
Kwa heshima zote namuomba Ndg. Sitta atoke ktk chama cha Mapinduzu.
Ajipange upya na kujiunga ...
Kwani hamuwezi ku raise formidable leaders from without CCM?

Opposition wanatakiwa waombee wakina Sitta wengi waibuke humo humo CCM waparaganyishe chama. Sio kuwaomba na kuwalamba miguu wana CCM wenye itikadi huria waje upinzani.

Mbona CHADEMA huwa wanahangaishwa na Zitto anapokuwa na mawazo yake tofauti na amri na kauli mbiu za chama chake? Mbona CHADEMA wamemshindwa Shibuda ambae walimbembeleza kwa machozi aje upinzani? Sitta ni mwana CCM mwenye mawazo huria, CHADEMA wanaweza kushindwa kudili na dizaini zile.

Upinzani, zaeni viongozi kutoka upinzani, muwalee kutoka upinzani, wakapambane na CCM wakitokea upinzani. Watakuwa wanajeshi wa kweli wa upinzani.
 
picha ndioo! linaanza manake kasema 2011-2012 ndio mwisho wa mafisadi wasio zidi 10.Je,mafisadi watakubali kung'olewa?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom