Sitta amwaga radhi TBC1

sitta mali yote aliyo nayo kaitoa wapi.

nyumba ya spika milioni 10 kwa mwezi huyo anajua umaskini wa watanzania. tunadanganyana bure.

tueleze mali aliyo nayo; siyo porojo. Orodhesha. nyumba ya spika siyo ya sitta; ni ya spika.
 
Amesema ataendelea kupambana na ufisadi pamoja na nchi kuwa na rasilimali za kutosha wananchi bado ni masikini- inakuaje watu 43mil wanatikiswa na watu hawazidi 10 HAPA TANZANIA ANASEMA MWAKA 2011 ndiyo mwisho wao!Wananchi tusikubali


Asiishie kusema tu................. Tunataka na vitendo!!! Vilevile, kwa nini asiwataje kwa majina????

Hivi ile list of shame ya Dr. Slaa iko wapi ili tuyapitie tena yale majina!! Nafikiri yalikuwa kama 10 hivi!!
 
wana jf fuatilieni taarifa ya habari.

---------

amesema ataendelea kupambana na ufisadi pamoja na nchi kuwa na rasilimali za kutosha wananchi bado ni masikini- inakuaje watu 43mil wanatikiswa na watu hawazidi 10 hapa tanzania anasema mwaka 2011 ndiyo mwisho wao! Amewataka wananchi wasikubali
wana jf orodhesheni majina hao watu kumi ni nani ????
 
Anapambana nao vipi? Anapambana na mafisadi kwa kutoa mafumbo? Get serious man. Wataje au sema unachokijua maana tunajua wewe ni mojawapo ya viongozi ambao wana CLASSIFIED INFO za serikali pamoja na chama chako. Kama kweli wewe ni mzalendo uliye na uchungu kwa nchi na wananchi wenzako, then toboa unachojua.....hatutaki mafumbo.

Nakubaliana nawe 100 %. Hakuna mwenye uchungu wa nchi CCM........................ Zogo lote hili ni danganya toto. Hakuna cha Mwakyembe, Sitta, Kilango wala nani. Wanatuzuga tu hapa. Mbona Slaa aliwataja, sasa yeye anaogopa nini?? anatwambia anapigana vita bila kututajia adui yake?? Can't buy this!!
 
tatizo ni pale ambapo hawezi kuwataja hao watu kumi......siku akiwataja ndo ntasema yuko siriaz
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,"Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM yenyewe." Na aliwahi vile vile kutabiri kwamba chama cha demokrasia na maendeleo angalao kilikuwa na muelekeo mzuri wa kushika dora siku za usoni.Hayo ndiyo yanatokea hivi sasa so wale wanaoelewa hawashangai it is a dream now becoming a reality.Sitta I salute you and God shall always protect you, na kwa kweili hauna sababu ya kuondoka kwenye chama hicho.Tell them the truth na watanzania wengi hivi sasa wanakuelewa na tuko nyuma yako.Keep it up sir
 
Wanajamvi lazima mjue prominent figure haiwezi kuhama chama kama wewe na mimi, hao wana siri nyingi ambazo zitawapa kiwewe wenzie katika chama.
 
Wanajamvi lazima mjue prominent figure haiwezi kuhama chama kama wewe na mimi, hao wana siri nyingi ambazo zitawapa kiwewe wenzie katika chama.


Sema tatizo la viongozi wa bongo ni uoga na wapenda madaraka mno. Hawana hakika kwa jinsi CCM walivyo wababe kama watakubali kuachia madaraka kwa wapinzani. Kwa jinsi hali ilivyo CCM ilitakiwa iwe imeshagawanyika. Mbona nchi nyingine vigogo huwa wanahama. Mfano Kenya, akina Kibaki na Odinga walikuwa KANU. Zambia Kiongozi wa upinzani Bwana Satta alikuwa MMD etc.
 
Huyu jamaa ni kama vile mpinzani, nadhani JK alikosea kumpa uwaziri maana saizi amejenga ufa mkubwa sana ndani ya chama kutokana na tabia yake na tabia imeambukiza wengine hivyo kuongeza hali tete kwa CCM, wakati huo CDM wakikenua meno.

Mtasema sana na wewe umejua CDM tu ni chama upinzani nalidhani ni NCCR na Cuf
 
Yuko kwenye mishe mishe zake za kitalii. Hapo anawa enjoy tu. Yeye malengo yake yoote yametimia. He dreamt of being a president that's all. Not a performing president. Kwa hiyo anawashangaa tu. Anawasoma humu humu akiwa anapiga raha somewhere. haumizi kichwa mzee wa watu. Anasubili muda wake uishe salama ale pensheni.

hivi mwenyekiti wao yupo ziara anabembea? mbona wanakwarurana hawa?
 
Wana JF fuatilieni taarifa ya habari.

---------

Amesema ataendelea kupambana na ufisadi pamoja na nchi kuwa na rasilimali za kutosha wananchi bado ni masikini- inakuaje watu 43mil wanatikiswa na watu hawazidi 10 HAPA TANZANIA ANASEMA MWAKA 2011 ndiyo mwisho wao! Amewataka wananchi wasikubali

I love ninaposikia wananchi wanaopenda nchi yao wakiongea. I just think huu ndio ushujaa na hakuna tena machoni pangu Tanzania. Lets protect this man and his family. Tunajua wazi enemies of Tanzania wanapanga vitu vibaya dhidi yake.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom