Sitta amjibu Sumaye kuhusu mabehewa mabovu

Sitta amjibu Sumaye kuhusu mabehewa mabovu

Hivi kwann madudu yote ya nchi hii mawaziri hawahusiki??
 
Wazir na naibu wazr inawezekan kabsa wanahusika katk ilo apa kuna ujanja ujanja safari ii mchawi mpe mtot akulelee twende na lowasa october 25 ,,,watasema tuu
 
Hebu Sitta aache kutufanya Watanzania wote majuha. Hivi Mkurugenzi Mtendaji pekee na management team yake (kwenye shirika ambalo ni la umma lenye Waziri mwenye dhamana? pamoja na bodi yake ya Wakurugenzi?) ati ana ubavu wa kuidhinisha ununuzi wa mabehema yenye thamani ya TZ shs. 220 billion bila idhini ya Waziri wake? bodi yake?... Halafu bila ya kupitia na kushindanishwa bodi ya manunuzi?

Common Sitta!..talk to us with your sense!

Wewe ndio hujui kuheshimu professionalism. Nenda ikalale ni wazi hujakomaa kuhoji masuala kwa kijenga hoja katika misingi ya kitaalam na kisheria. UNAKURUPUKA

Unae kurupuka ni wewe , sijui ni ugeni bado unakusumbua?

Hebu jipe muda wa kujifunza kusoma na kuelewa mijadala ya JF na kuweza kujenga hoja. Kama inakuuma kwa sababu nime m-criticize Sitta na Sitta ni nanii wako basi pole yako hiyooo! Na akirudi leo jioni mwambie (mpenzi) kule JF wanakuponda sana. Na usisahau kumkumbusha kuwa leo ni siku kuanza cyber crime kwa hiyo anaweza kuwashitaki wote wanaomsema...umesikia eeh!

Anyway, karibu JF.
 
Wazir wa wizara aliwajibika lini kujiuzulu?kashfa hiyo kama richmond tu mwakyembe awajibike
 
Hebu wenye kujua utendaji wa wizara unavyofanya kazi aniweke wazi hapa. Yawezekanaje ununuzi wa gharama kubwa hivyo ufanyike bila bodi wala mawaziri na katibu mkuu wa wizara kuhusishwa? Au Sitta anamfichia siri Mwakyembe na aliyemteua? Ni kweli baraza la mawaziri hawakutoa baraka zao hapa? Mbona ni wachache wanaotarajiwa kushtakiwa? Sitta funguka tukusome otherwise acha kutuona wageni.
 
Mwaka huu kwenye kampeni tutajua mengi,tunataka vitendo sio maneno tena wakati huu nchi inakwenda kwenye mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiutendaji
 
Sheria ya Mtandao naona imeanza kupunguza speed ya matusi humu JF! Vinginevyo, huyu mzee Sitta angeandamwa sana na matusi leo!
 
Hebu Sitta aache kutufanya Watanzania wote majuha. Hivi Mkurugenzi Mtendaji pekee na management team yake (kwenye shirika ambalo ni la umma lenye Waziri mwenye dhamana? pamoja na bodi yake ya Wakurugenzi?) ati ana ubavu wa kuidhinisha ununuzi wa mabehema yenye thamani ya TZ shs. 220 billion bila idhini ya Waziri wake? bodi yake?... Halafu bila ya kupitia na kushindanishwa bodi ya manunuzi?

Common Sitta!..talk to us with your sense!

wahurumieni wamepoteana sasa wameanza butua butua hawaonani
 
Mwakyembe awajibishwe,mbona kwenye sakata la Tokomeza mawaziri waliwajibika?kwanini yeye abaki?
 
Mwaka huu watajibu yote. Na hili la waliosafirisha magunia 18 ya madawa ya kulevya kwenda South Africa hawajamaliza uchunguzi ili wawafungulie mashtaka hao wahusika?

Vipi kuhusu mdahalo au amekwishaomba poo?
 
Wachagga wanataka matatizo ya watanzania yaendelee kuwepo ili wayatumie kama mtaji wa kisiasa hata kikifanyika kitu ilimradi hajafanya mangi wanabeza...
 
Edward Lowasa awajibishwe, huyu ndo aliyehusika kwa kutoa maelekezo ya hayo mabehewa kukuu kununuliwa! Fisadi sana! Wala msimpe kura mpuuzeni!

Tehteh teeeeh.Nimefurahi kuona "like" ya Mdanganywa kwenye huu uongo.Kweli jina lina impact
 
Hebu Sitta aache kutufanya Watanzania wote majuha. Hivi Mkurugenzi Mtendaji pekee na management team yake (kwenye shirika ambalo ni la umma lenye Waziri mwenye dhamana? pamoja na bodi yake ya Wakurugenzi?) ati ana ubavu wa kuidhinisha ununuzi wa mabehema yenye thamani ya TZ shs. 220 billion bila idhini ya Waziri wake? bodi yake?... Halafu bila ya kupitia na kushindanishwa bodi ya manunuzi?

Common Sitta!..talk to us with your sense!

Ni vema ukaweka wazi utaratibu mzima wa manunuzi katika wizara za serikali, hii itatusaidia kujua hasa mzigo huu ni wa nani na kwa namna gani anastahili kujibu tuhuma hizi, ila kwa kutoa maelezo ya ujumla tu bado kila mtu atanyoosha kidole moja kwa moja kwa waziri ilihali inafahamika kuwa waziri sio mtaalamu wa kutambua uzima au ubovu wa mabehewa.
 
Sitta anastahili kuwa waziri mkuu...karibuni Tanzania Mpya!
Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.

Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.

Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.

Kwahiyo amekubali bila shaka yoyote kwamba wamenunua mabehewa fake.
Haijalishi nani anabebeshwa mzigo sasa hivi, swala ni upotevu wa fedha za umma kwa uzembe wa serikali. Kwani walitegemea nani akawasaidie kusimamia ununuzi? UKAWA au Lipumba?
 
fiksi tu hzo

Muhuni na mnafiki huyu Mzee hana lolote miaka 54 ndio waje watuambie uongo. CCM wote ni waongo na wanafiki walikuwa wapi maka yote. Ahadi zao za uongo zinakuwa uchaguzi hadi uchaguzi. Wakiwa bungeni wanapitisha maslai wala sio wazalendo.
 
Sitta angemuiga mzee mwenzie Mwandosya katika kukaa kimya ingemsaidia sana. Hivi hajui kuwa ndani ya CCM huwa hawamtaki ila yeye anajishebedua tuu?
Lilianza lile la kutaka kuwa Spika wa JMT wakamwambia wanataka jinsia ya kike kama anataka afikirie cha kufanya. Likaja bunge la Katiba, hilo CCM walijua tokea mapema kuwa ni zigo zito na litaleta mparaganyiko ndani ya nchi. Wakasema zigo zito mpe Mnyamwezi Sitta ahangaike nalo.
Urais wakakata huko huko juu kwa juu, yeye bado anaona wenzake? Akae pembeni hayo mambo ya majibishano awaachie wakina Lusinde.
 
Ujinga mtupu ... Kesi yenye haijafunguliwa, Upelelezi huo anaufanya yeye? Malofa tumeamka, Hatudanganyiki tena ...
 
Back
Top Bottom