Sitta amjibu Sumaye kuhusu mabehewa mabovu

Sitta amjibu Sumaye kuhusu mabehewa mabovu

Sikuzote hajajibu anasubiri mpaka ukawa wawafungue macho wananchi?
amaechelewa sana najua hata mirad inyofunguliwa sasaiv ni fix tuu za uchaguzi
 
Tulitegemea pia angechukua maamuzi magumu sio kuja kutuhadaa na maneno ya asali.
 
Edward Lowasa awajibishwe, huyu ndo aliyehusika kwa kutoa maelekezo ya hayo mabehewa kukuu kununuliwa! Fisadi sana! Wala msimpe kura mpuuzeni!

hata mimi nashangaa kwa nini Mh Lowasa hayupo kwenye hiyo list hapo juu na wakati tunavyoaminishwa ni kwamba ufisadi kwenye hii nchi umesababishwa na Lowasa yani bila Mh Lowasa ufisadi ungekuwa hauko kwenye hili taifa
 
Alafu pia nashangaa kama hao wahusika wamefanya ufisadi wa kusababisha kupotea kwa mabilioni yote hayo ya pesa, kwanini Mh Sita asifanye nao mdahalo????????
 

​
WAZIRI wa Uchukuzi, Samwel Sitta, amemjibu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, baada ya kuituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa imewafumbia macho watendaji walioisababishia hasara nchi zaidi shilingi bilioni 220 kwenye ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.

Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.

Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.

Hata hivyo, Sitta ameongeza kuwa kamati hiyo ilibaini kampuni hiyo haikuwa na sifa na watendaji TRL walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa kitendo chao cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta mabehewa.

Viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu; Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosowile Ngosomiles; Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni, Jasper Kisiraga; na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
​
(NA DENIS MTIAMA/GPL)

Sita naye ni zero brain. Kila kampuni wanadeal nayo haina sifa!!!

Hata serikali ya kikwete haikuwa na sifa watatuambia tukiwabana sasa.
 
Hawa hawana mpango wa kumpeleka mtu Mahakamani,muda wote walikuwa wapi kusema kuwa wanafanya uchunguzi ukikamilika,wahusika watapelekwa Mahakamani.

Walisubiri mpaka Sumaye awalipue kipindi cha uchaguzi ndio waseme hayo wanayo yasema?hata kama kuna mtu atakayepelekwa Mahakamani vitakuwa ni vidagaa tu,mapapa hakuna hata mmoja atakayegusa Mahakamani na katika kundi la watu 32 la Magufuli sidhani kama wanakosekana.

Kweli asee walikuwa wanapita tu. Ni sehemu ya maisha kwa mujibu wao
 
....

Huyu Mu-Six tumueleweje?, he must have to be consistency Kama ni hivyo kwanini hao jamaa wa TRL nao asiwaalike wafanye naye mdahalo badala yake anawapeleka mahakamani? Kwani sheria za nchi hii zina double standard?

Mkuu kweli umeshachukulia kauli ya Sita kama kiwango cha kisheria? Mafisadi wanatakiwa kualikwa kwenye midahalo badala ya kupelekwa mahakamani? Ndio sheria mpya ya nchi yetu? Ha ha ha ha!

On a very serious note, kwa utu uzima aliofikia Mh. Sita anatakiwa kuacha hizo propaganda uchwara zifanywe na vijana zaidi kama Nape na Madelu. Yeye saa hizi, baada ya kuukosa urais na kutotaka kuhama chama, anatakiwa kuhangaikia kuingia kwenye safu za "elder statesmen" kama akina Salim, Malecela, n.k.
 
Kwenye wizi huu wote wako watu wa kwao na Mh. Mwakye, naona safari hii hakuna mchaga na mhaya hata mmoja hapo dili ni lazima ife tu.
 
Tulitegemea pia angechukua maamuzi magumu sio kuja kutuhadaa na maneno ya asali.
 
eti Bora kuendelea na CCM kuliko mabadiliko ... Kweli fedha Mwanaharamu ...
 
Back
Top Bottom